Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10888 articles
Browse latest View live

Creditinfo Tanzania – the first fully licenced and operational credit reference bureau in Tanzania.

$
0
0


Creditinfo Tanzania Limited (CIT) received the licence to conduct credit reference business after satisfactorily met the conditions stipulated in the provisional licence that was granted by the Bank of Tanzania on October 2012 and demonstrated its readiness to commence business. This means that Creditinfo Tanzania, is the first company to receive a licence to operate a credit reference bureau in Tanzania issued under Section 48 of the Bank of Tanzania Act, 2006.

Subsequently, on 12thJune 2013, Creditinfo Tanzania started to provide services to public and various categories of business that are denominated under the Act as being eligible to provide credit information to a Credit Reference Databank. These include banks and non-bank financial institutions, savings and credit schemes, micro-finance companies, any other finance company that are licensed and supervised by the Bank of Tanzania. Similar services are available for subscriptions to all other credit providers, he added.


Speaking at the press conference today, Mr. Hakon Stefansson, on of the shareholders & Director Credit Bureau Expansion – Creditinfo Group said “Credit Reference Bureaus ensure responsible lending and borrowing, which is particularly important for the growing economies. Currently more than 45 banks have licenses issued by the Bank of Tanzania, and their successful development as well as successful development of country’s economy as a whole could be influenced by an adequate clients’ risk evaluation.  Credit reporting systems will improve credit risk and credit portfolio management, enhance financial supervision and financial sector stability and access to credit. We are delighted to have the opportunity to contribute to the Government of Tanzania’s efforts of creating sound financial infrastructures“. 

Mr. Davith Kahwa, Director– Creditinfo Tanzania said “We are also far advanced in negotiations with public information providers to access data that will allow us to develop value-added products. We anticipates that reliable, credible and accessible credit information will revolutionize the way credit decisions are made in Tanzania, facilitating effective risk management, quicker decisions and more accurate pricing of risks associated with credit decisions as well as reduced interest rates”
Persons who had difficulties accessing credit due to a lack of collateral will now be better positioned to do so provided they can demonstrate an excellent credit history and credit score. For the first time Tanzanians now can obtain a copy of their credit report” Mr Kahwa added 
The company will be investing heavily in training and the provision of technical oversight for the members of its user group, noting that a specialist in credit bureau systems and risk management will arrive in country in August to train our subscribers”
"Creditinfo Tanzania is committed to differentiating itself by focusing not just on the core business of individual and corporate credit information but also introduction of automated credit scoring software tools and developing value-added products from publicly accessible data sources, packaging them and making them easily accessible to users," Mr Stefanssonconcluded

WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE ZA KATA VYUO VIKUU WAMTAKA LOWASSA AWANIE URAIS 2015

$
0
0
Mbunge wa Monduli, ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu, Edward Lowasa, akisalimiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha UDOM waliotoka shule za sekondari za kata, wakati walipofika nyumbani kwake mkoani Dodoma kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia kielimu
Hamida Salum mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDOM, akizungumza kwenye hafla hiyo Juni 25, 2013
Mh. Lowasa katikati, Dkt. Mahanga (Kulia) na Parseko Korne wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao.
 
Na Father Kidevu Blog, Dodoma
Wanafunzi wa Chuo Kikuu ch DODOMA, maarufu kama UDOM, ambao walifika hapo wakitokea zile shule za makabwela (Shule za Kata), wamemtaka Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa, achukue fomu za kugombea urais 2015 muda utakapowadia.
 
Pia wameahidi kujichangisha fedha kwa ajili ya malipo ya fomu hizo endapo italazimika.

Kauli hiyo ya kwanza kutoka kwa makundi na watu wasiokuwemo ndani ya siasa, ilitolewa Jumatatu usiku nyumbani kwa Lowasa mjini Dodoma, wakati kundi nla wanafunzi hao walipofika kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia ikiwa ni matunda ya shule hizo, ambazo muasisi wake ni mbunge huyo wa Monduli.
 
“Mimi ninayofuraha kusimama hapa leo hii, nikiwa mtu tofauti, kwa maana ninayesoma elimu ya juu, baada ya kufanikiwa ,kuendelea na elimu ya sekondari kupitia shule za kata pale Kiluvya Dar es Salaam” anasema Hamida Salum ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza hapo UDOM.
 
“Wewe ni jembe, kama uliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kwa kipindi kifupi cha miaka 2, ninahakika unaweza kufanya men gi zaidi endapo utakuwa rais wan chi hii” mwanafunzi mwingine wa mwaka wa kwanza, Clementina Ophoro alisema, kwenye salamu za mwanafunzi mmoja mmoja wakati wa utoaji shukrani kwa Lowasa.
 
Lowasa wakati akiwa waziri mkuu wa Tanzania, kwenye mwanzoni mwa awamu ya n ne ya utawala wa rais Jakaya Kikwete, aliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kote nchini, ili kutoa nafasi zaidi za wanafunzi wa makabwela, walioishindwa kendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa madarasa.

Kwa sasa shule hizo zimekuwa zikibezwa na watu mbalimbali kwa maelezo kuwa hazina walimu wa kutosha na uhaba wa vifaa vya kufundishia ikiwemo vyumba vya maabara.
 
“Mimi ninawashangaa watu wanaosema kuwa eti shule za kata hazifai, kwa vile hazina walimu na vifaa. Haya maneno ni ya kupuuzwa, kwani binadamu hupaswi kukwepa changamoto za maisha” alisema mwanafunzi mwingine Victor Mafuru pia wa mwaka wa kwanza.
 
Wanafunzi hao wa UDOM waliotoka kwenye shule za sekondari za kata, wameamua kuanzisha umoja wao kote nchini, ili kuendeleza ndoto za kuhakikisha kila mwanafunzi wa mtu masikini anapata elimu.
 
Kwa kuanzia wanafunzi hao wapatao 600, wameahidi kufundisha bure kwenye shule za umma, wawapo likizo baadaye mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.
 
Kwa upande wake, Lowasa ambaye alikuwa pamoja na naibu waziri wa kazi na ajira, Dkt. Makongoro Mahanga, mbunge wa Kigoma mjini, Peter Serukamba, na mkuu wa mkoa wa Singida, Parseko Kone, aliwapongeza wanafunzi hao kwa moyo wao wa shukrani na kuwataka wasikatishwe tama na maneno yanayotolewa juu ya ubora wa shule hizo, kwani yeye binafsi anajivunia juhudi zake kupitia sera za chama cha Mapinduzi, zimeweza an galau kutoa wanafunzi wengi kutoka shule hizo kujiunga na vyuo vikuu.

VOA KUKUTANA NA VIJANA WA MJINI DODOMA KATIKA PROGRAME YA JE NIFANYEJE?

$
0
0
Shirika la Utangazaji la Sauti ya Amerika Idhaa ya Kiswahili (VOA) ikishirikiana na USAID limeandaa mkutano mkubwa wa Vijana utakao fanyika kesho mjini Dodoma maarufu kama Je Nifanyeje?.


Washiriki wa mkutano huo ni vijana mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) pamoja na Vijana wengine wa mtaani Dodoma wamealikwa kuhudhuria.

Mtangazaji Mashuhuri  aliyejiunga na idhaa hiyo mwaka 2008 akitokea kituocha ITV na Redio One Sanday Shomari ndiye atakuwa akiongoza mkutano huo.


Wakizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari wa Bunge mjini Dodoma, Sande Shomari pamoja na Bi. Rose Mwakitwange (pichani juu) wamesema maandalizi  ya mkutano huo yamekamilika na mjadala wake utarushwa moja kwa moja na redio Mshirika ABM FM ya mjini Dodoma.


Aidha Bi Rose Mwakitwange ambaye aliwahi kuwa C.E.O wa New Habari Group amewataka wanahabari nchini kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuandishi na wazitumie katika kuelimisha umma na kujipatia kipato zaidi.

Mwakitwange amesema kuwa Wanahabari wana wajibu wa kuisaidia jamii kufahamu vitu vingi vinavyowatatizo hivyo Mwandishi wa Habari akitumia vyema taaluma yake ndiye mtu pekee anaeweza kujibu maswali hayo ya jamii katika nyanja mbalimbali kwa kuandika vitu kwa undani na umakini.

Pia amewataka waanahabari kujitokeza na kujiandikisha ili washiriki Mkutano wa Mafuta na Gesi maana utawawezesha kufahamu masuala mbalimbali na kuwapa mbinu za namna ya kuandika habari zihusuzo gesi na mafuta nchini.

KUMBUKUMBU ZA SIKU YA 40 YA MSIBA WA BABY SHANGAZI HOTEL MBEYA

$
0
0
FAMILIA YA ZAINABU ABEID ALLY (BABY SHANGAZI HOTELI) YA MBEYA INAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUMKUMBUKA MAMA YAO MPENDWA ALIYEFARIKI USIKU WA TAREHE 5-06-2013 KATIKA HOSPITALI YA RUFAA JIJINI MBEYA NA KUZIKWA SIKU YA ALHAMISI TAREHE 6.06.2013.

WATOTO WAKO POSTER, MABRUCK, ASHA, HAWA, HUSSEIN, HASIRA NA ABEID WANAUNGANA NA NDUGU NA JAMAA WALIOJITOLEA KWA HALI NA MALI KUHAKIKISHA MAMA YAO MPENDWA ANAPATA KILA AINA YA MSAADA ULIOKUWA UNAHITAJI MPAKA PALE MWENYEZI MUNGU ALIPOCHUKUA ROHO YAKE.

KUMBUKUMBU YA KUTIMIZA SIKU YA 40 BAADA YA KIFO CHA MAMA YETU INATARAJIWA KUFANYIKA NYUMBANI KWAKE MAREHEMU MBEYA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 6.07.2013 WOTE MNAKARIBISHWA.

MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI.
AHSANTENI SANA

WASHEHERESHAJI WALIPOTINGA BUNGENI DODOMA

$
0
0
 Mapema wiki hii Wanachama wa Chama cha Washereheshaji na watoa Huduma katika Shughuli mbalimbali nchini hasa Sherehe walifika Mjini Dodoma na kutembelea Bungeni na kujionea shughuli mbalimbali za Bunge. Father Kidevu Blog kupitia Kampuni yake ya MD Digital Company ambayo pia ni mtoa huduma ya Picha katika sherehe mbalimbali ilinasa taswira mbalimbali za wakali hao wa Kuongoza Shere na Misosi wakiwa Mjengoni.



 Wakiwa na Waziri wa Habari, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mkangara, Waziri, Prof.  Mark Mwandosya na Dk. John Magufuli
 Wakiwa wamevalia nadhifu kwa Batiki kwa akina mama na suti kali kwa wanaume walipiga picha ya pamoja.
 Magufuli akiwapa mkono baadhi yao.
 Akina mama walipiga yakwao...
 Wazee wa kazi nao hawakutaka kuikosa...


MKUTANO WA JE NIFANYEJE WA VOA DODOMA

$
0
0
DSC03460 
Dr. Mary Mwanjelwa mbunge wa Mbeya (viti maalum) mgeni rasmi katika wa mkutano wa Je Nifanyeje ulioandaliwa na VOA kwa ushirikiano na USAID akifungua rasmi mkutano huo wa vijana katika ukumbi wa African Dreamer Dodoma Jumatano.
DSC03455Katika meza kuu kutoka kushoto ni Mariam Salum Msahaba (Zanzbar), Josephine Johnson Genzabuke (Kigoma),Ritta Motto Kabati (Iringa), Faida Mohamed Bakari (Kusini Pemba) IMG_2784Washiriki wa "Town Hall meeting". IMG_2770Washiriki wakifuatilia mkutano. IMG_2777Washiriki wakiwa na mgeni rasmi. IMG_2788Mshiriki Sebastian ambaye ni mwanafunzi wa CBE akitoa pointi. IMG_2776Washiriki wa mkutano huo kushoto Panelist Dr.Ilyu Mohamed na Advocate Jp mshauri wa EABTM. IMG_2778Kutoka kushoto Mariam Salum Msahaba (Zanzbar),Faida Mohamed Bakari (Kusini Pemba),Dr. Mary Mwanjelwa Mbeya, Rose Mwakitwange,Ritta Motto Kabati (Iringa) na Rais wa wanafunzi wa CBE Dodoma. IMG_2796Nikitoa saini kwa washiriki wa semina. IMG_2805Timu ya Je Nifanyeje Tanzania kutoka kushoto Adeodatus Kakorozya, Mwanaharusi Pongwa na Mensiah . IMG_2790Washiriki wa mkutano wakiwa kwenye majadiliano. IMG_2799Wasaa wa kung'aa na baadhi ya washiriki wa mkutano wanafunzi wa CBE Dodoma. Kwa picha zaidi bofya
IMG_2798 
 IMG_2816

BUNGENI DODOMA

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Ilala, jijini Dar es Salaam, na mmoja wa Wenyeviti wa Bunge, Mussa Zungu Azzan akiongoza kikao cha Bunge
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kutoka Mkoani Arusha, Catherine Magige akiwa Bungeni mjini Dodoma Juni 26,2013.
 Mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kingwangalla (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa CCM nchi za SADC, Kelvin Nyamori (katikati) na Mbunge wa Kisesa, Luhanga Mpina, nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.

 Mbunge wa Viti Maalu, Faida Mohamed Bakar akizungumza jambo na Mbunge wa Tandahimba, Juma Njwayo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.
Mbunge wa Viti Maalum, Faida Mohamed Bakar akifurahia jambo na Wabunge wenzake  Juma Njwayo wa Jimbo la Tandahimba, na Dk. Hamisi Kingwangala wa Nzega(kushoto) nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.
 Wapigapicha za Habari wakiwa kazini Bungeni
 Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Josephine Gezabuke (kulia) nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana. Kushoto ni Waziri wa Makamu wa Rais, Mazingira, Dk. Terezya Huvisa.
 Wabunge wakitoka Bungeni jana

MSHINDI WA DROO YA PILI KAMPENI YA WINDA NA USHINDE ATANGAZWA.

$
0
0
 
 Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo (wa pili kulia) akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde  Mwl.Michael Valerian Mbuya katika mkutano na wana habari uliofanyika jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni Meneja mauzo  wa Push Mobile Rugambo Rodney, kulia kwake ni Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Humudi Abdul Hussen(wa kwanza kushoto).
 Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo(katikati) akiongea na wana habari wakati wa kumtangaza mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde katika mkutano uliofanyikajana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam. 
 Wakihakiki namba za simu za mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde iliofanyika jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti, wa kwanza kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo, Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko(katikati) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu Humudi Abdul Hussen(kushoto).

*************
Mshindi asherekea kitita cha 1,000,000 huku akiwapongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa promosheni hiyo. 

25 Juni 2013, kampuni ya bia ya Serengeti imetangaza mshindi wa pili wa kampeni ya Winda na Ushinde ambae amejinyakulia kitita cha milioni moja baada ya kuchezesha droo yake ya pili. Droo hiyo ilichezeshwa katika ofisi za kiwanda hicho jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mhakiki kutoka katika bodi ya uchezeshaji promosheni bwana Humud Abdul Hussein.

Baada ya kupokea Michael Varelian Mbuya (29) ambae ni mwalimu wa sekondari kutoka Tabata Dar es salaam alionesha furaha yake na kubaki bumbuwazi kwa furaha. “Nina furaha isiyokifani kuwa mshindi wa promosheni hii ya Winda na Ushinde kutoka katika kampuni ya bia Serengeti na ntaitumia kufungua duka kwani ni ndoto yangu kubwa. Na najivunia kuitumia bia ya serengeti kwani ndio bia niipendayo na nawapongeza sana kampuni ya Serengeti kwa kuanzisha mashindayo haya na mpaka sasa nimeshajishindia bia nyingi pamoja na bia taslimu” alisema mshindi huyo.

Akiongelea promosheni hii meneja wa kinywaji cha Serengeti Mr.  Allan Chonjo alisema “promosheni hii ni ya kipekee na mpaka sasa watu 110,000 wameshajishindia bia za bure na pesa taslimu ambazo ni shilingi 10,000 na100, 000/= na droo ya kwanza ilichezeshwa mwezi uliopita huku mshindi kutoka Moshi akiondoka na kitita cha milioni moja, pia promosheni hii inampa fursa mshindi kununua kile anachokitaka baada ya kujishindia fedha taslimu kwani tunaamini baadhi ya wateja wetu wana ndoto nyingi sana za mafanikio ila tatizo huwa ni pesa ili kitimiza ndoto zao.

Lengo la kampuni yetu ni kuendeleza umoja na mshikamano  na wateja wetu kwa kuutambua na kuuthamini mchango wa wateja wetu kwani wao ni muhimili mkubwa katika kukuza na kuendeleza bai yetu ya Serengeti. Na sasa kampuni ya Serengeti inachezesha promosheni hii kutimiza azma yake ya kuinua uchumi wa wateja wao kama sehemu ya shukrani kwa wateja wake.
Ni wakati wako ndugu mteja kushiriki mara nyingi uwezavyo na kuhakikisha unajishindia zaidi ya milioni saba. Ili kushiriki unatakiwa kufungua chini ya kizibo cha bia ya Serengeti na utakuta namba maalumu na unatakiwa kuituma kwenda namba 15317 na utapokea majibu.
Tafadhari kunywa kistaarabu na ni maalum kwa 18+

KWI KWI MTANDAO WA FULLSHANGWE INASHUGHULIKIWA

$
0
0
WADAU WA MTANDAO WETU WA FULLSHANGWE TUNAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA KUANZIA LEO KUTOKANA NA MTANDAO WETU KUTOKUWA HEWANI KUTOKANA NA SABABU ZILIZO NJE YA UWEZO WETU HATA HIVYO WATAAAMU WETU WANAFANYA KILA LIWEZEKANALO ILI TUWEZE KUREJEA WAKATI WOWOTE
TUNATUMIA NAFASI HII PIA KUWAOMBA RADHI WADHAMINI WETU NMB, NBC SBL, NHIF NA WILNA INTERNATIONAL TUNAOMBA MTUVUMILIE WAKATI TUNASHUGHULIKIA TATIZO HILO.

RAIS MAHINDA WA SRILANKA ATUA NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
Rais Wa Sri Lanka Me.Mahinda Rajapaksa akikagua gwaride la heshima liliandaliwa na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.
 Mtoto Faith Warioba nayesoma katika shule ya awali ya Montessori jijini Dar es Salaam akimlaki kwa maua Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi nchini huku Rais Dkt.Jakaya Kikwete akishuhudia.

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuweasili nchini  kwa ziara ya kikazi leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
 Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa akisalimia na Msaidi wa Rais Masuala ya Kidiplomasia Balozi Liberata Mulamula wakati Rais Kikwete alipokuwa akiwatambulisha baadhi ya viongozi na wasaidizi wake kwa mgeni wake muda mfupi baaday kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa wakipokea heshima za urais muda mfupi baada ya mgeni huyo kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Sri Lanka wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za utamaduni vilivyokuwa vikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa shamrashamra za kumpokea mgeni huyo wakati alipowasili leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini

TAMASHA LA TIGO KABANG KUFANYIKA JIJINI MWANZA

$
0
0
 Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litakalofanyika siku ya jumapili hii bure kabisa katika viwanja vya  CCM Kirumba jijini Mwanza, kushoto msanii Diamond Platnumz na kulia msanii Madee ambao watatoa shoo siku hiyo na wasanii wengine. 
 Msanii wa bongo flava Diamond Platnumz akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni yake Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga. 
 Msanii Madee akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni yake ni Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga na Diamond Platnumz . 
 Msanii Richie Mavoko akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili kulia kwake ni Msanii Madee, meneja wa Tigo Bw. William Mpinga na Diamond Platnumz.

REDD'S MISS TEMEKE 2013 KUFANYIKA JUNI 5, TCC CLUB

$
0
0
Warembo wanao wania Taji la Redd's Miss Temeke 2013, kutoka kushoto walio simamaMargreth Olotu, Narietha Boniface, Latifa Mohamed, Mutesa George, Naima Ramadhan, Margreth Gerald, Mey Karume, Esther Muswa, Aksaritha Vedustus na Svtlona Nyameyo CHINI, Irenej Rajab, Darlin Mmary, Stella Mngazija na Hyness Oscar. Wakipiga picha ya pamoja baada ya mazoezi yao jijini Dar es Salaam leo.

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA BUNGENI DODOMA

$
0
0

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wapili kushkto) akizungumza na Wabunge kutoka kulia, John Cheyo Bariadi Mashariki (UDP), James Mbatia wa kuteuliwa  (NCCR Mageuzi) na Mansoor Shanif Hiran  mbunge wa Kwimba (CCM) nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.Kushoto ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama.

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama nje ya Ukumbi wa Bunge mjini DodomaJuni 27,2013.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akisalimiana na Mkurugenzi wa Masama Promotion, Alex Msama nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Juni 27,2013.


Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla (kulia) akifurahia jambo na Mbunge wa Mbeya Mjini na Waziri Kivuli wa Wizara hiyo kutoka Kambi ya Upinzani Bungeni, Joseph Mbilinyi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk.Terezya Huvisa akisisitiza jambo wakati akiongea na wapigapicha za Habari nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo. Mazungumzo makubwa yalikuwa juu ya Usafi hasa jiji la Dar es Salaam. Dk. Huvisa alisema jiji sasa litakuwa safi na tayari mkakati wao umekutana na ziara ya Rais Obama wa Marekani hivyo utakuwa endelevu
 Waziri Kivuli wa Maji na Umwagiliaji, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Sabreena Hamza Sungura akizungumza na Mbunge Mwenzake nje ya ukumbi wa Bunge.
Mbunge wa Mafia ambaye pia ni Kamishna wa Skauti Tanzania, Abdulkarim Shah, akizungumza na vijana wa Skauti Mkoa wa Dodoma waliotembelea Bungeni jana kujifunza shughuli mbalimbali.

 Wabunge ni wachache bungeni maana imesalia siku moja kwa Bunge kuahirishwa...
 Mbunge wa Viti Maalum, Paulin Gekul akisoma ratiba ya Shughuli za Bunge Juni 27,2013.
 Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu Azzan (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Iddi Mohamed Azzan wakiwa Bungeni Dodoma.
 Halima Mdee Mbunge wa Jimbo la Kawe akigeuka kuzungumza na Wabunge wenzake wa CHADEMA Bungeni.
 Mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee  (kushoto) na Mbunge wa viti Maluum, Paulin Gekul wakiwa Bungeni. Nyuma ni Mbunge wa Viti Maalu, Chiku Abwao.

 Wabunge mbalimbali wa CHADEMA wakiwa Bungeni
Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) Mbunge wa Viti Maalum, Lediana Chilolo (katikati) na Mbunge wa Uzini Mohamed Seif Khatib wakiwa nje ya Ukumbi wa Bunge.

MTEMVU AUNGURUMA TMK

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (aliyevaa miwani katikati), akifuatwa na wananchi baada ya kumaliza mkutano wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni.

 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akimsikiliza Mweka Hazina wa Kikundi cha Kuweka na Kukopa (VICOBA), Anjela Ndigula ambaye alipokea sh. 50,000 alizotoa msaada kwa Muya Thabit ili ajiunge na kikundi hicho, baada ya kuambiwa hana haki hivyo anashindwa kulipia pango. Msaada huo aliutoa katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni.
 Muya Thabit akicheza kwa furaha baada Mbunge Mtemvu kumsaidia fedha za kujiunga na vicoba
 Diwani wa Kata ya Temeke, Khamis Nsombo, akiwazawadia fedha wasanii wa kikundi cha Msimamo

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akikizawadia fedha kikundi cha sanaa cha Msimamo kilichokuwa kinatumbuiza katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni. Pia aliahidi kukipatia kikundi hicho sh. 500,000 za kununulia vifaa zikiwemo ngoma.
 Mtemvu akiangalia wakati msanii wa Msimamo akicheza ngoma
                             Wasanii wakicheza ngoma ya Lizombe ya asili ya Mkoa wa Ruvuma
                                             Msanii akichangamsha mkutano huo
                         Mtemvu akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Temeke, Khamis Nsombo
                                              Nsombo akiteremka kutoka jukwaani baada ya kuhutubia
                                                       Mtemvu akiwasalimia wananchi
                           Muya Thabit akiomba fedha kwa Mbunge Mtemvu ili alipe pango
                                    Wananchi wakiuliza maswali kwa Mbunge wao Mtemvu




Kilimanjaro: Taifa Stars bado ina nafasi nzuri

$
0
0
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager akikabidhi zawadi maalumu kwa mchezaji wa Timu ya Taifa, Shomari Kapombe,  Jijini Dar es Salaam wakati wa chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wa Taifa Stars. Zawadi kama hizo zilikabidhiwa kwa wachezaji wote na benchi la ufundi.
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager akikabidhi zawadi maalumu kwa Nahodha wa Timu ya Taifa, Juma Kaseja Jijini Dar es Salaam wakati wa chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wa Taifa Stars. Zawadi kama hizo zilikabidhiwa kwa wachezaji wote na benchi la ufundi.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager akikabidhi zawadi maalumu kwa mchezaji wa Timu ya Taifa, Salum Abubakar,  Jijini Dar es Salaam wakati wa chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wa Taifa Stars. Zawadi kama hizo zilikabidhiwa kwa wachezaji wote na benchi la ufundi.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager akikabidhi zawadi maalumu kwa mchezaji wa Timu ya Taifa, John Bocco,  Jijini Dar es Salaam wakati wa chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wa Taifa Stars. Zawadi kama hizo zilikabidhiwa kwa wachezaji wote na benchi la ufundi.
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager akikabidhi zawadi maalumu kwa mchezaji wa Timu ya Taifa, Nardil Haroub (Cannavaro),  Jijini Dar es Salaam wakati wa chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wa Taifa Stars. Zawadi kama hizo zilikabidhiwa kwa wachezaji wote na benchi la ufundi.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager akikabidhi zawadi maalumu kwa Kocha wa Timu ya Taifa, Kim Poulsen, Jijini Dar es Salaam wakati wa chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wa Taifa Stars. Zawadi kama hizo zilikabidhiwa kwa wachezaji wote na benchi la ufundi.
**************
 
Wadhamini wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Kilimanjaro Premium Lager, wamewataka watanzania kutokata tamaa licha ya Taifa Stars kutofuvu kucheza Fainali za Kombe la Dunia Brazil mwakani kwani timu imeonesha uwezo wa hali ya juu mpaka sasa.
 
Ombi hilo lilitolewa na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe wakati alipowaandalia Taifa Stars chakula cha jioni katika hoteli ya Tansoma ikiwa ni utaratibu wa wadhamini hao kama njia ya kuwakaribisha wachezaji kambini.
 
Alisema bado kuna mashindano mengine kama CHAN na AFCON ambayo wana imani Taifa Stars itafuzu na kwuweka historia.
 
Aliwaasa wachezaji kuhakikisha wanashinda mechi dhidi ya Uganda haa nyumbani na pia watakapoenda Uganda baadaye mwezi huu katika mechi ya kuwania kufuzu mashindano ya CHAN mwakani nchini Afrika Kusini.
 
“Tumeshindwa kufuzu kwenda Brazil basi twende Afrika Kusini mwakani,” alisema Bw. Kavishe.
Alisema wao kama wadhamini wamefarajika kuona jinsi Timu ya Taifa imepiga hatua tangu waanze kuidhamini mwaka jana.
 
“Vilabu vya  Simba na Yanga zilikuwa na nguvu sana na moja ya dhamira zetu kama wadhamini ilikuwa ni kuinua kiwango cha Taifa Stars na kufanya watanzania warudishe imani kwa timu yao na sote ni mashuhuda kwani katika mechi ya kwanza kabisa mwaka jana uwanja ulikuwa na watu 10,000 tu lakini katika mechi dhidi ya Ivory Coast hivi majuzi uwanja ulijaa kabisa,” alisema.
 
Meneja huyo pia alitumia nafasi hiyo kutoa zawadi maalumu kwa wachezaji hao ambazo ni pamoja na DVD zilizorekodiwa maelezo (profiles) za kila mchezaji, kazi ambayo ilifanywa kitaalamu kwa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager.
 
Wachezaji wataweza kutumia kazi hizi kwenye mitandao ili waweze kujulikana vizuri ndani na nje ya nchi.
 
“Tulisema tunaijenga timu na timu inajengwa na wachezaji na ndio maana tumeamua kufanya kazi kama hizi ambazo zitapandisha hadhi ya wachezaji,” alisema huku akitoa wito kwa vilabu kutosita kuaruhusu wachezaji wakati wanaitwa kurekodi kazi kama hizo.
 
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa, Kim Poulsen aliwashukuru wadhamini na kusema, “Kwa kweli mumekuwa zaidi ya wachamini maana ushirikiano mliioonesha ni wa hali ya juu.”
 
Alisema wachezaji wana ari kubwa sana kwani matunzo wanayopata sasa hivi ni ya hali ya juu na wote wanalenga kupata mafanikio.
 
Taifa Stars iko kambini kuanzia Julai 4 mwaka huu ikijiandaa na mechi dhidi ya Uganda Jumamosi hii na mechi ya marudiano itapigwa wiki mbili zijazo Mjini Kampala ili kuwania kufuzu katika mashindano ya CHAN.

MFANYA BIASHARA NDOGONDOGO ATANGAZWA MSHINDI WA DROO YA TATU YA WINDA NA USHINDE YA BIA YA SERENGETI

$
0
0
Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo(katikati) akiongea na wana habari wakati wa kumtangaza mshindi wa droo ya tatu ya Winda na Ushinde ambaye ni Bi Blanca Mariki, katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jana jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na wadau wengine wa droo hiyo Meneja mauzo  wa Push Mobile Rugambo Rodney(kulia) na Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko (kushoto).

********
Kampuni ya bia ya Serengeti imetangaza mshindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya Winda na Ushinde ambae amejinyakulia kitita cha milioni moja baada ya kuchezesha droo yake ya tatu na ya mwisho. Droo hiyo ilichezeshwa katika ofisi za kiwanda hicho jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mhakiki  kutoka katika bodi yamichezo ya Bahati Nasibu.



 
Baada ya kupokea simu Blanca Mordest Mariki(30) anayefanya biashara ndogo ndogo kutoka Morogoro alionesha furaha yake na kubaki bumbuwazi kwa furaha. “Nimefurahi sana kuwa mshindi wa promosheni hii ya Winda na Ushinde kutoka katika kampuni ya Bia ya Serengeti.
 
 Na najivunia kuitumia bia ya serengeti kwani ndio bia niipendayo na nawapongeza sana kampuni ya Serengeti kwa kuanzisha mashindayo haya” Pamoja na ushindi huu mkubwa nimeshajishindia bia za bure za Serengeti mara mbili, pamoja na hela taslimu shilingi 10,000 mara nne ambazo huwa natumiwa kupitia njia ya simu”. Alisema mshindi huyo.
Akiongelea promosheni hii meneja wa kinywaji cha bia ya Serengeti Allan Chonjo alisema “promosheni hii ni ya kipekee na mpaka sasa watanzania wengi wameshajishindia bia za bure na pesa taslimu ambazo ni shilingi 10,000 na100,000/=  na pia washindi wetu wakubwa wa droo ya kwanza na ya pili walijishindia milioni moja kila mmoja.
 
Mshindi wa droo ya kwanza alitoka Kilimanjaro na mshindi wa pili alitoka Dar es Salaam na wote waliipongeza sana kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuwasaidia wateja kwani wameinua uchumi wao kupitia ushindi wao wa promosheni hii”.
“Lengo la kampuni yetu ni kuendeleza umoja na mshikamano  na wateja wetu kwa kuutambua na kuuthamini mchango wao kwani wao ni muhimili mkubwa katika kukuza na kuendeleza bia yetu ya Serengeti.
Promosheni hii inaendelea mpaka mwisho wa mwezi Julai na kumalizika kwa promosheni ya Winda na Ushinde ni mwanzo wa mengine mengi yanayotolewa na kampuni ya bia ya Serengeti kwa ajili ya wateja wetu”. Aliongeza meneja huyo.
 Tafadhari kunywa kistaarabu na ni maalum kwa 18+

TANGAZO LA MSIBA WA HUMPHREY GEORGE LUPENZA-MUME WA LEAH SAMIKE

$
0
0
Mpigapicha na Mhazini wa Cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) , LEAH SAMIKE anawatangazia kifo cha mume wake Bwana HUMPHREY GEORGE LUPENZA aliyekuwa Mkurugenzi Mtedaji wa Lucky  Construction  Limited, (pichani) kilichotokea leo Saa 10: 55 alfajiri katika Hospitali ya Hindu Mandal Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu tokea Jumapili.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Marehemu, Kipunguni B -Ukonga Moshi Bar. Jirani na Kanisa la Pentekoste (Kanisa la Mabati).

Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzako.

Marehemu ameacha Mke Leah William Samike na watoto 5 ambao ni Maximillian-Samike, Mary -Maria Clara, George, Harrison na Jane-Fatuma.  

Tuungane na familia ya Marehemu katika kuipa faraja.

Humphrey akiwa na Mkewe Leah Samike siku ya harusi yao mara baada ya kula kiapo chao cha ndoa cha kuishi pamoja milele hadi kifo kitakapowatenganisha.

MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMINA.  

Article 21

$
0
0

 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Bi. Selina Agustine Mwita, kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Wajumbe wawili na Mwenyekiti, wa Baraza hilo, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya Ndugu Jamaa na marafiki, na wafanyakazi wa Tume ya Maadili waliohudhuria hafla hiyo.
 Rais Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na walioapishwa kwa kumbukumbu.
Rais Kikwete, akiagana na watoto wa mmoja wa walioapishwa Bi. Selina Agustine (katikati yao) baada ya picha ya pamoja.

ZEE TOWN SOJAZ WAJA NA CHINJA CHINJA YA HIPHOP

$
0
0
Wasanii wanao unda kundi la ZEETOWN SOJAZ King Pozza (kulia) na Kira Kirami wakiwa katika pozi.
 
WASANII wawili wanao unda kundi la mzijki wa kizazi kipya la Hiphop linalojulikana kama Zee town Sojaz  kutoka visiwani Zanzibar wameachia kibao chao cha kwanza kinachokwenda kwa jina la Chinjachinja.
Wasanii hao Joseph Mwingira 'King Pozza na Omari Ali 'Kira Kirami wameuambia mtandao huu kuwa wimbo huo wameufanyia kazi visiwani humo katika studio ya Jupitor chjini ya mwaandaji Aloneym.
Vijana hao ambao wamesema wamepania vikali kushika anga za Hip Hop visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wapo mbioni kupakua albam ya nyimbo zao kadhaa ila kwa sasa wanaupa nafasi wimbo wao huo kufanya kazi kwanza.
 "Tuna mapango wa kutoa albam ila si hivi sasa tunaupa nafasi wimbo wetu huu wa chinjachinja kufanya vyema sokoni ndipo tutoe albam", alisema Mwingira.

LOWASSA AWASEMEA WAZEE

$
0
0

 Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa akizungumza wakati wa majadilino yaliyohusu namna ya kuingiza  suala la wazee katika ajenda mpya za Maendeleo baada ya mwaka 2015.
 
Mkutano huo ulioambatana na chakula cha mchana ulifanyika  siku ya Jumatano hapa Makao Makuu ya  Umoja wa Mataifa na ulioandaliwa na United Nations Foundation kwa kushirikiana na  Mashirika mengine ya Kimataifa.   katika mchango wake, Mhe. Lowassa amesisitiza umuhimu wa   ubia kati ya serikali na  sekta binafsi katika kuzikabili changamoto za ongezeko la idadi ya  wazee  duniani.
 
Inasemekana miaka michache ijayo  idadi ya wazee duniani itazidi idadi ya watoto wadogo chini ya miaka mitano.  Pamoja na Mhe. Lowassa wengine waliochangia majadiliano hayo ni   Bi. Ann Pawliczko kutoka UNFPA wa pili kutoka  kushoto, Bw. Jack T. Watters kutoka Pfizer, Bw. Paul Ong HelpAge International, Bw. Sharig Khoja kutoka United Nations Foundation, aliyeketi karibu na Mhe. Lowassa ni Bi. Jane Barratt aliyeratibu majadiliano hayo.
 Sehemu ya  washiriki wa majadiliano hayo wakiwamo pia Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa
 Mhe. Lowassa akipeana  mkono na mmoja wa waandaji wa majadiliano hayo kuhusu Wazee, takwimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la  Idadi ya Watu ( UNFPA) zinazonyesha kwamba mwaka 1950  idadi ya wazee  duniani waliokuwa na  miaka 60 au kuzidi ilikuwa milioni 205, 2012 idadi hiyo iliongezeka hadi kufikia 810 milioni. Inakadiriwa kwamba idadi hiyo itaongezeka hadi kufikia  Bilioni 1 si zaidi ya miaka   kumi ijayo na ifikapo mwaka 2050  idadi ya wazee   wenye umri wa miaka 60 na kuendelea itafikia bilioni 2.  Aidha duniani kote wanawake ndio wanaokadiriwa kuishi umri mrefu zaidi kuliko wanaume.
 Mhe. Edward Lowassa akibadilishana mawazo na Balozi wa Zimbabwe katika Umoja wa Mataifa, Bw. Chitsaka   Chipaziwa
 
Na Mwandishi Maalum
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa ( Mb) amesisitiza haja na umuhimu wa kuwapo kwa  ubia kati ya serikali na sekta binafsi katika kuzikabili changamoto zinazotokana na ongezeko  kubwa la idadi ya wazee.
“ Maisha Zaidi ya miaka 60   hayapashwi kuwa ya utegemezi, unyonge,  kutojiweza au  kutokuwa na  matumaini.   Wazee bado na wanao mchango  mkubwa  ndani ya  jumuiya,  jamii,   na  familia zao ili mradi tu wawezeshwe”.
Na kwa sababu hiyo anasema Mhe, Lowassa, juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali   katika  nchi zilizoendelea na zinazoendelea  Tanzania ikiwamo za utoaji wa huduma za msingi kama vile  Afya , pensheni na uwezeshwaji zinapashwa kuchagizwa na sekta binafsi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, na  Waziri Mkuu  Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa(Mb ), ameyasema hayo siku ya jumatano hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wakati aliposhiriki  majadiliano  kuhusu namna gani suala la  Wazee linavyoweza kuingizwa katika ajenda za maendeleo baada ya mwaka 2015.
Majadiliano hayo  yaliandaliwa na   United Nations Foundation kwa ubia na International Federation of Ageing,   Help Age International,  AARP, Global Coalition on Aging, mHealth Alliance na Pfizer
“Kama  kundi hili la  wazee likiwezeshwa na kusaidiwa ipasavyo , linaweza kuipatia jamii soko jipya,  ujasiriamali,  utoaji wa maamuzi, utoaji wa huduma na  utalaamu  anuai katika maeneo ya sayansi, teknolojia na  upatanishi” anasema  Lowassa
Na kuongeza, ili hayo yote na mengine mengi yaweze kufanikiwa panahitajika  bajeti ya kutosha  kwa ajili ya kundi hilo la jamii ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya  pensheni, huduma za afya ambazo zitakidhi mahitaji ya wazee, huduma za kisaikolojia na huduma za ulinzi jamii,.
Hata hivyo anasema, inasikitisha kwamba, katika nchi nyingi za Afrika na nyinginezo hata zile zilizoendelea bado  haziwezi kutoa huduma za uhakika na zenye viwango vya kukidhi mahitajio ya wazee.
“Mara nyingi huduma kwaajili ya wazee inabidi zishindane na huduma za makundi mengine kama vile  ongezeko la vijana wasiokuwa na ajira,  upunguzaji wa  vifo vya watoto wachanga na wanawake wajawazito. Hata hivyo pamoja na changamoto zote hizi za vipaumbele hatuwezi kuendelea na utaratibu  huu wa kuchagua. Lazima tutumie maandalizi ya  ajenda za maendeleo baada ya 2015 kuwahudumia wazee” anasisitiza Lowassa.
Akasema Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kujikumbusha na kujifunza kwa kosa la kutoingiza suala la Wazee katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs) yanayoelekea ukingoni,  kwa  kuhakikisha kwamba Wazee wanaingizwa katika   malengo mapya ya maendeleo baada ya 2015 kwa kuwa ni suala ambalo haliepukiki
Akizungumzia hatua mbalimbali zinazochuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwahudumia wazee, Mhe. Lowassa anasema kama ilivyo kwa  nchi nyingine, Tanzania nayo inakabiliwa na ongezeko la idadi ya wazee.
Kwa mfano, amesema asilimia 4.5 ya idadi ya watu, ni watu walio na  umri wa miaka 65  wastani  wa juu zaidi  kuliko ule wa asilimia 3.6  Afrika  Kusini mwa Jangwa la  Sahara.
“ Asilimia 80 ya  watu hawa wanaishi vijijini na maisha yao yanategemea kilimo. Serikali  inajitahidi kadri iwezavyo kutoa huduma za msingi kwa kundi hilo  ingawa pia, na kama ilivyo kwa nchi nyingine, tunakabiliwa na changamoto nyingi kukidhi mahitaji yote ya wazee”. Akabainisha
Akatumia pia fursa hiyo kuyashukuru mashirika ya kimataifa kama vile Help Age International ambalo limekuwa likiendesha shughuli zake nchi nchi  tangu mwaka 1993.
Akatoa mfano kwa kusema  Shirika hilo,  mwezi  Juni mwaka huu kwa kushirikia na Pfizer limezindua mpango wa miaka miwili  wa kupunguza athari zitokanazo na  magonjwa yasiyoambukiza (NCD) ambayo yamekuwa yakiwaathiri wazee.
Akasema  utoaji wa huduma hiyo unakwenda sambamba na    juhudi za serikali katika kukabiliana na  magonjwa hayo.
Akatoa wito kwa mashirika mengine kuiga mfano huo na kwamba serikali itakuwa tayari kushirikiano nayo,
Takwimu kutoka  Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu ( UNFPA) zinaonyesha kwamba,  katika kila sekunde watu wawili duniani wanaadhimisha miaka 60 ya kuzaliwa kwao, na kwa mwaka   karibu watu milioni 58 wanaadhimisha miaka 60 ya kuzaliwa.
Aidha katika kila watu nane,  mmoja ana miaka 60 au zaidi na makadirio yanaonyesha kwamba ifikapo mwaka  2050 katika kila watu  watano mmoja atakuwa na miaka 60 au zaidi.
Ongezeko la  idadi ya wazee duniani linachangiwa na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na  ongezeko la umri wa kuishi ambapo katika nchi 33  raia wao wanaishi zaidi ya miaka 80 wakati miaka mitano iliyopita nchi ambazo  umri wa kuishi  ulifika miaka 80 zilikuwa 19 tu.
Utafiti zaidi unaonyesha , umri wa kuishi  utaongezea  hadi kufikia miaka 90 au hata miaka 100. Japani  kwa sasa ndiyo inasemekana  kuongoza kwa  kuwa na asilimia 30 ya wazee lakini ifikipo mwaka 2050  nchi 64 zitaungana na Japani kwa kuwa na  asilimia 30 au zaidi ya wazee.
Viewing all 10888 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>