Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuashiria uzindizi wa ujenzi wa Ofisi za Mahaka ya Afrika uliofanyika leo katika kijiji cha Lakilaki kilichopo Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Wengine pichani Rais wa Mahakama ya Afrika,Jaji Theodor Meron (kushoto), Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman (wapili kushoto), pamoja na viongozi wengine mbalimbali.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Rais wa Mahakama ya Afrika,Jaji Theodor Meron kuzindua ujenzi wa Ofisi za Mahaka ya Afrika uliofanyika leo katika kijiji cha Lakilaki kilichopo Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Meero Contractors LTD Jeremiah Ayo (kushoto),akiwa katika sherehe ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa ofisi za mahakama ya Afrika iliyofanyika Lakilaki Arumeru,Arusha. Kampuni ya Meero ndio wanaojenga barabara yenye urefu wa 1.30 km kwa kiwango cha lami.
Baadhi ya maofisa na mafundi wakiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Meero Contractors LTD Jeremiah Ayo wa (wa nne kulia)akishuhudia sherehe ya kuweka jiwe la msingi ofisi za Mahakama ya Afrika iliyofanyika katika eneo la Lakilaki Arumeru , mjini Arusha leo.