Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10720 articles
Browse latest View live

USHIRIKI DARFUR MIKONONI MWA SERIKALI- TENGA

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amesema kuwa ushiriki wa klabu za Tanzania kwenye mashindano ya Kombe la Kagame yaliyopangwa kufanyika kwenye miji ya Darfur Kaskazini na Gordofan Kusini nchini Sudan unategemea tamko la Serikali ambayo kwa sasa inafanya tathmini ya hali ya usalama.

Tenga, ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF, alisema tayari TFF na Serikali zimeshafanya mazungumzo, na Serikali imepewa taarifa zote muhimu kuhusu mashindano kwa ujumla, malazi ya klabu za Tanzania, uhakika wa usalama, usafiri wa ndani na mambo mengine muhimu hivyo kwa sasa Serikali inatathmini taarifa hizo kabla ya kutoa tamko.

“Masuala ya usalama yako nje ya uwezo wa CECAFA. Kwa hiyo, kama Serikali itabaini kuwa hali usalama ya huko si nzuri, hatutaziruhusu na kama ikiona hali ni nzuri, itaruhusu,” alisema Tenga.

“Jukumu la CECAFA (Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu vya Nchi za Afrika Mashariki na Kati) ni kuandaa mashindano na kupata uhakika wa usalama kutoka nchi mwenyeji.
“Kama tukipata uhakika huo wa usalama, mashindano yanafanyika. Lakini nchi moja moja zinayo haki ya kuhoji usalama kwa kuwa ni wajibu wa Serikali hizo kujali maisha ya wananchi wake.”

Tenga alisema kuwa mashindano hayo yalikuwa yafanyike Ethiopia, lakini katika dakika za mwisho nchi hiyo iliomba isiandae mashindano hayo hadi mwakani na ndipo Sudan ilipojitokeza kuokoa mashindano hayo.

Alisema wakati wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) uliofanyika Mauritius, CECAFA iliitisha mkutano mkuu wa dharura na kupewa taarifa ya maandalizi ya mashindano hayo kutoka uongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Sudan na wanachama wakaridhia baada ya kuhakikishiwa usalama.

“Hivyo nchi wanachama wa CECAFA zimeridhia kushiriki baada ya kuhakikishiwa usalama, lakini kwa kuwa Waziri wetu ameonyesha wasiwasi kuhusu usalama wa Darfur, hatuna la kufanya zaidi ya kumsikiliza. Ni kauli ya kiongozi anayeonekana kuwajibika na ni lazima tusubiri tamko la Serikali,” alisema Tenga.

“Lakini napenda kuishukuru Serikali ya Sudan kwa uamuzi huo kwa sababu kuandaa mashindano hayo si kitu kidogo. Tayari Katibu Mkuu wa CECAFA (Nicholas Musonye) ameshakwenda kwenye maeneo hayo na kukaa wiki nzima akikagua viwanja na hoteli zitakazotumika na kuridhika nazo,” alisema.

Alisema watu wasipotoshe tamko la Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alilolitoa Bungeni kuhusu ushiriki wa timu zetu Darfur.

“Mhe. Membe alisema Serikali itafanya uchunguzi ijihakikishie kuwa hali ya usalama ni nzuri… alisema Serikali haitakubali kuruhusu raia wake kwenda Darfur wakati hali ya usalama si nzuri,” alisema Tenga.

“Kwa maana hiyo, na baada ya TFF kuipa Serikali taarifa zote muhimu kuhusu hali itakavyokuwa wakati wa mashindano, sasa tunasubiri tamko la Serikali. Na hii ni kawaida kabisa kwa kuwa hata hapa tunapoaandaa mashindano, ni lazima kwanza tupata uhakika wa usalama kutoka serikalini ndipo tuziite timu.”

Alifafanua kuwa si jukumu la CECAFA kuamua mashindano yafanyike mji gani na kwamba chama cha nchi mwenyeji ndicho kinachoamua mashindano yafanyike mji gani.

“Sasa kwa suala la Sudan, magavana wa majimbo hayo mawili ya Darfur Kaskazini na Gordofan Kusini waliomba kwa chama chao mashindano hayo yafanyike kwenye miji hiyo na Serikali ya Sudan ikaihakikishia CECAFA usalama,” alisema.

“Sasa ikitokea Serikali yetu ikasema hali si nzuri, hatutaziruhusu timu zetu ziende kwa sababu masuala ya usalama yako nje ya CECAFA.”

TAIFA STARS SASA INAJITOSHELEZA- TENGA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeishukuru Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kuiwezesha timu ya taifa, Taifa Stars kuondokana na matatizo na kuwaomba Watanzania kuiombea timu ili ifanye vizuri katika mechi yake ya kesho (Juni 8 mwaka huu) dhidi ya Morocco mjini Marrakech.

Stars, ambayo inashika nafasi ya pili kwenye kundi lake la mashindano ya awali ya Kombe la Dunia ikiwa nyuma ya Ivory Coast kwa tofauti ya pointi moja, inacheza na Morocco katika mechi ya nne itakayofanyika Marrakech baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mechi ya kwanza iliyofanyika Dar es Salaam mwezi Machi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisema kuwa tangu kuanza kwa udhamini, TFF haijawahi kupata udhamini mkubwa kama wa Kilimanjaro Premium Lager ambayo imeingia mkataba wa miaka mitano wa kuidhamini Stars wenye thamani ya dola milioni 10 za Marekani.

“Katika kipindi chote hiki hatujawahi kupata udhamini ambao umekidhi mahitaji yote ya timu kama huu wa TBL,” alisema Tenga kwenye mkutano na waandishi uliofanyika kwenye ofisi za TFF.

“Lakini katika mwaka mmoja uliopita (tangu TBL ianze kudhamini) hatujawahi kushindwa kuisafirisha timu; kushindwa kulipa posho za wachezaji; kutanguliza watu wetu kwenda nje kuiandalia timu sehemu nzuri; kuzilipia tiketi za ndege timu tunazocheza nazo mechi za kirafiki na hata kuzilipia ada ya kucheza mechi (appearance fee).

“Posho za wachezaji zimepanda kwa karibu mara mbili na ndio maana leo wachezaji wanaijali timu yao. Yote haya ni kutokana na udhamini huu. Watu wanasema usione vinaelea….”

Tenga alisema kuwa udhamini huo ndio sasa umeanza kuzaa matunda na timu inafanya vizuri ikiwa ni pamoja na kuwa na maandalizi ya muda mrefu.

“Sasa tunawaomba Watanzania waiombee timu na tunawashukuru wale waliokwenda Morocco kuishangilia kwa kuwa vijana wetu wanapata nguvu pale wanapoona kuna watu wako nyuma yao,” alisema Tenga.

Rais huyo wa TFF pia alisifu kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kuiita timu Ikulu na kuongea na kula na wachezaji, akisema kitendo hicho kitasaidia kuongeza hamasa kwenye timu.

Naye Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kampuni yake itaendelea kuwa bega kwa bega na TFF na kwamba uhusiano baina ya pande hizo mbili umeimarika na utaendelea kuimarika.

Katika mkutano huo, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilikabidhi fulana maalum kwa ajili ya mashabiki ambao wamekwenda Morocco kuishangilia timu.

Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu alisema tayari fulana 250 zimegawiwa kwa mashabiki walioko Morocco na nyingine zilitarajiwa kusafirishwa jana.

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAAHIDI KUENDELEZA UDHAMINI TAMASHA LA BULABO

$
0
0
Kiongozi wa kikundi cha Basesilia Bujora, akionyesha umahiri wake wa kucheza na nyoka katika siku ya mwisho wa tamasha hilo ambapo kikundi chake kiliibuka washindi wa siku hiyo, Tamasha hilo lililodumu kwa takribani wiki nzima lilivutia maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza  lilidhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.
 Wasukuma kucheza na nyoka ni asili yao na hapa ni moja ya burudabni za nyoka zikiendelea.
Umati wa wakazi wa Wilaya ya Magu wakifuatilia kwa makini ngoma za jadi kutoka kabila la wasukuma ‘Bulabo’ katika kiwanja cha Kisesa. Tamasha hilo lililodumu kwa takribani wiki nzima lilivutia maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza  lilidhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.

Kwa shangwe kubwa maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Magu jijini Mwanza wamekuwa wakishuhudia burudani ya ngoma za asili za kabila la wasukuma ’Bulabo’ ambalo limemalizika siku ya Jumapili jioni katika uwanja wa Kisesa jijini Mwanza. Katika sherehe hizo za kiutamaduni vikundi ishirini na nane kutoka makabila ya wasukuma  vilishiriki na kuzifanya sherehe hizo zivutie zaidi. Kampuni ya bia ya Serengeti imeahidi kuendelea kudhamini tamasha la ngoma za kabila la wasukuma ’Bulabo’ ambazo ni maalum kwa ajili ya kusheherekea sikukuu za mavuno kila mwaka.

``Tunayofuraha kubwa kwa mara nyingine tena kuona tumeweza kuungana na wenzetu wa kabila la wasukuma katika kipindi cha wiki moja sasa na kusherehekea furaha yao baada ya mavuno huku wakiendelea kuzienzi tamaduni zao. Ni kwa mara ya nane sasa tumekuwa tukidhamini sherehe hizi za bulabo na tunaahidi kuendelea kudhamini kwani sherehe hizi zina mchango mkubwa kwa wasukuma na taifa kwa ujumla”. Alisema jaji Mark Bomani mwenyekiti wa kampuni ya bia ya serengeti.

Kampuni ya bia ya Serengeti imekuwa ikidhamini tamasha hilo kwa takribani mwaka wa nane sasa,ambapo waandaaji wameishukuru kampuni hiyo kwa kuwezesha na kufanikisha tamasha hilo, ”Napenda kutoa shukrani zetu kwa kampuni ya bia ya Serengeti ambayo imekuwa mdhamini wetu kwa muda mrefu sasa inafika miaka minane, tumekuwa nao bega kwa bega na hasa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Mheshimiwa Mark Bomani ambae pia ni mlezi wetu hapa Bujora” alisema Padri Mhoja, muandaaji wa tamasha hilo.

Naye mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magu  Mheshimiwa Jacquieline Liana, ameipongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa kudhamini tamasha hilo na kuomba wadau wengine kujitokeza kudhamini kama wenzao wa kampuni ya bia ya Serengeti wanavyofanya, pia aliwaasa vijana kuacha tabia za kunywa pombe wakati wa kazi na badala yake wafanye kazi kwa bidii ili waje kusheherekea sherehe hizi za Bulabo mwakani.

 Katika sherehe hizo za Bulabo vikundi vilivyoshiriki vilishindana kwa mtindo wa mtoano ambapo vikundi viwili vikiwa katika pande mbili tofauti za uwanja vikitenganishwa na bendera nyekundu, huku majaji wakiangalia ni kundi lipi lenye umati mkubwa hivyo ni kuashiria kuwa mwenye watu wengi zaidi ndiye mwenye mvuto zaidi na hapo kutangazwa mshindi. Kigezo kingine kichokuwa kikiwafanya washiriki waongeze jitihada katika kucheza na kujikuta wakiwapa raha zaidi watazamaji ni kile cha kundi linaloshindwa kutakiwa kutoa elfu thelathini katika laki mbili ambazo zilikuwa zikitolewa kwa kila kundi na kumpa mshindi.

Washindi katika ngoma hizo zilizodumu kwa takribani wiki moja ni Nghomi Lukala, Kanigini Hindiya, Kibola Shitungulu, Bagehu Lukala, Mayokagose, Kinasa Ncheye, Nyamuitabungagwa Mnkoti, Mabeshi Lukwaja, Nyeyewaza, Shigulu Dema, Bulolo Shokolo, Seleleko na Basesilia Bujora aliyemalizia siku ya Jumapili baada ya mpinzani wake kuingia mitini.

AUNT EZEKIEL AKUTANA NA BODI YA FILAMU.

$
0
0
WASANII wa filamu nchini wameshauriwa kuwasilisha miswada ya filamu kwa Bodi ya Filamu ilkaguliwe na kupewa kibali kama unafaa,umefata sheria na haujakiuka maadili ya sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza pamoja na kanuni zake.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fissoo wakati wa kikao na mtengenezaji wa filamu Aunt Ezekiel kuhusiana na kazi yake mpya ijulikanayo kama Scola.

Katibu huyo amefafanua kuwa kuna umuhimu wa wasanii kufata sheria  na taratibu za filamu kabla ya kuanza kutengeneza na kuzitoa filamu zao ambapo sheria inawataka kuwasilisha  miswada (script) Bodi ya filamu ili ukaguliwe na kupewa idhini yakuendelea na kazi hiyo.

“Wasanii mnatakiwa kuzingatia sheria na kuwasilisha script ili zikaguliwe na kupata ruhusa kwa mujibu na taratibu za sheria kabla ya kuanza kutengeneza filamu kwa sababu sheria Na 4 ya mwaka 1976 ya Filamu na Michezo ya Kuigiza pamoja na kanuni zake zinataka wasanii kutotoa au kutengeneza filamu kabla ya kupeleka mswada(script ) kwa Bodi.

Aidha Katibu huyo amefafanua kuwa wasanii wanapotengeneza picha kupitia script ambazo hazijakaguliwa kuna uwezekano mkubwa wakuwepo sehemu ambazo zinakiuka maadili ya mtanzania,ikiwepo uvaaji wa mavazi mafupi yaliyopitiliza kwa waigizaji wanawake,lugha mbaya na baadhi ya vitendo vingine visivyofaa kuoneshwa kwa umma.

Bi Fissoo amesema kuwa Bodi imepewa mamlaka kwa mujibu wa Shetia kuzuia filamu hizo ambazo hazijakaguliwa ,na kama msanii hajafuata sheria atapata hasara kutokana na gharama ambazo atakuwa ametumia na endapo filamu hiyo itafutwa, jambo a,balo Bodi isingelipenda liwakute wadau wake.

Kwa upande wake Msanii wa Filamu za Kiswahili Aunty Ezekiel ameomba radhi kwa kutoleta script yake ya filamu hiyo mpya ya SCOLA Bodi ya Filamu na ameahidi kurekebisha baadhi ya vipengele kama alivyoelekezwa na Bodi hiyo kwani vitu hivyo vinaweza kurekebishika.

Aunty Ezekiel amefurahishwa sana na kuishurukuru Bodi ya Filamu Tanzania kwa kufanya majadiliano mazuri juu ya filamu yake kwa kubaini mapungufu yaliyopo na ameahidi kuyafanyia kazi ili kuboresha filamu hiyo na pia amewaasa wasanii wengine wote kuwa na imani na Bodi ya Filamu na kutokuwa na dhana tofauti juu ya Bodi hiyo.
Aunty Ezekiel ni msanii aliyetengeneza filamu nyingi hapa nchini ambazo zinasambazwa na Kampuni ya Steps Entertainment iliyopo hapa nchini.

WAKAZI WA DAR NA MWANZA WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUMEZA DAWA

$
0
0
 Dk. Mwelecele Malecela-Mkurugenzi wa NIMR


Hussein Makame –MAELEZO

SERIKALI imewaomba wananchi wa mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza wenye umri kuanzia miaka mitano na kuendelea kujitokeza kwa wingi katika zoezi la umezaji wa dawa za Matende na  Mabusha(Ngirimaji),na Kichocho litakalofanyika kuanzia Juni 22 hadi na Agosti mwaka huu.

Wito huo umetolewa na Afisa Mradi wa   Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele (NTD), Bernad Kilembe katika mafunzo kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari juu ya mpango huo yaliyofanyika ofisi za NIMR  jijini Dar es Salaam leo.

Alisema zoezi hilo linatarajiwa kufanyika katika majiji  hayo  kuanzia Juni 22  hadi 26 mwaka huu na litakuwahusisha wakazi wote wa maeneo hayo, ambapo watameza dawa za ALBENDAZOLE na MECTIZAN kwa Dar es Salaam na PRAZIQUANTEL kwa Mwanza.

Alisema zoezi hilo litafanyika katika vituo 1500 vilivyoko jijini Dar es Salaam ambapo kwa upande wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano watameza dawa ya PRAZIQUANTEL kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa kichocho.

Alivitaja vituo hivyo kuwa ni shule za msingi, vituo vya mabasi,sokoni, magerezani, taasisi mbalimbali, maofisini na kambi za jeshi.

Alisisitiza kuwa kwa upande wa watoto wanatakiwa wameze dawa ya PRAZIQUANTEL masaa mawili baada ya kula, ambapo kwa mkoa wa Mwanza zoezi litahusisha umezaji wa dawa hiyo kwenye shule za msingi kwa watoto wenye umri wa kwenda shule za msingi mwezi wa Agosti, mwaka huu.

Akizungumzia ugonjwa Matende na Mabusha,Kilembe alisema maambukizi ya magonjwa hayo na kichochco yameenea karibu nchi nzima ambapo alisema tatizo hilo lipo kwa kiwango cha kuanzia asilimia 1 hadi 69.

Akizungumzia zoezi hilo, Afisa Mradi wa NTD, Dk.Edward Kirumbi aliwataka wananchi wa majiji hayo kuondoa hofu juu ya dawa hizo kwa kuwa hazina athari huku akikanusha uvumi kuwa ukipasuliwa ngirimaji utakufa au itaathiri nguvu za kiume.

Naye Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Neema Rusaibamayila aliwataka wahariri hao kufikisha ujumbe kwa jamii na kuwahamasiaha wananchi kuhudhuria kwenye zoezi hilo.

Mpango huo unahusisha udhibiti wa magonjwa matano ,ambayo ni Matende na Mabusha(Ngirimaji), Magonjwa mengine ni Usubi, Trakoma na Minyoo ya Tumbo.

 Alisema  ugonjwa wa  Matende na Mabusha husababishwa na minyoo midogo,huenezwa na mbu aina ya Culex na Anopheles, wakati ugonjwa wa kichocho husababishwa na minyoo jamii ya Schistosoma.

MWENYEKITI WA CCM JAKAYA KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KUPOKEA RASIMU YA KATIBA MPYA

$
0
0
 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiongoza kikao cha Maalum ya CCM 'Kamati Kuu' kilichokutana jana usiku mjini Dodoma kwa ajili ya kuipokea Rasimu ya Katiba mpya, iliyosomwa hivi karibuni.
 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana jana tarehe 10/06/2013 chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya kupokea rasimu ya katiba mpya.

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana jana tarehe 10/06/2013 chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya kupokea rasimu ya katiba mpya.

Kamati Kuu inaipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi nzuri na kukamilisha kazi kwa wakati.

Kamati Kuu imepokea rasimu hiyo na kuelekeza kuwa; Kwa kuwa rasimu hii ni ya kwanza ambayo inapelekwa kujadiliwa tena kwa wananchi kupitia mabaraza mbalimbali ya katiba baada ya kuisha kwa hatua ya kutoa maoni.

 Kamati Kuu imekiagiza Chama kijipange kuijadili rasimu hiyo ndani ya Chama kama baraza la kitaasisi la katiba na kuwataka wanachama na wapenzi wa CCM wajitokeze kwa wingi na kushiriki kwenye mabaraza haya.

Ushiriki huu wa CCM baada ya kupokea rasimu umekusudia kushirikisha wanachama wetu kwenye ngazi ya tawi, wilaya, mkoa na Taifa.

Lakini pia Jumuiya za CCM zimekusudia kushiriki kama mabaraza ya Katiba na hivyo kuongeza ushiriki wa wanachama na wapenzi wa CCM katika mchakato huu.

CCM kama baraza la katiba la kitaasisi litaipitia rasimu iliyowasilishwa kifungu kwa kifungu na kwa kuzingatia maoni ya CCM yaliyotolewa mwanzoni kabisa mwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba, wanachama wetu watashiriki kutoa maoni yao.

Pamoja na kazi nzuri ya Tume ya Mabadiliko ya katiba, Kamati Kuu inaiomba Tume hiyo kueleza vizuri mchakato mzima kutoka rasimu ya kwanza mpaka rasimu ya mwisho ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi juu ya mchakato mzima hasa baada ya rasimu ya kwanza kutoka.

Kamati Kuu inawasihi Watanzania kushiriki tena kwenye kutoa maoni kupitia mabaraza ya katiba kwa rasimu ya kwanza, bunge maalum la katiba kwa rasimu ya pili na kupitia kura ya maoni kwa rasimu ya tatu, kwa amani,utulivu na kuvumiliana ili mwisho wa siku tupate Katiba nzuri ya nchi yetu kwa masilahi ya Watanzania walio wengi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Moses Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo mchana kuhusu kikao hicho cha Kamati Kuu ya CCM, kilichokutana jana usiku.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, waliohudhuria kikao hicho jana usiku.
 Sehemu ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao wengi wao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba, akiperuzi 'mambo flani' katika simu yake ya mkononi, wakati akiwa ukumbini humo kwenye Kikao cha Kamati Kuu kilichokutana jana usiku.

LWAKATARE WA CHADEMA ATOKA KWA ZAMANA

$
0
0
Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Wilfred Lwakatare akizungumza na wanahabari baada ya kutoka kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam baada ya kupewa dhamana jana. Kulia ni mmoja wa mawakili wake, Profesa Abdallah Safari.
Lwakatare akizungumza jambo kabla ya kuondoka
Lwakatare akilakiwa na wafuasi na wanachama wa chma hicho.

RAIS KIKWETE AAPISHA MABALOZI WAWILI DODOMA LEO

$
0
0
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha  Mhe Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (kuli) , anayekuwa balozi wa Tanzania nchini China. 
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha  Mhe Anthony Cheche (kushoto) anayekuwa Balozi wa Tanzania katika Congo DRC.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakiwa na mabalozi wapya walioapishwa leo Juni 11, 2013 katika Ikulu Ndogo Dodoma. Mabalozi hao ni Mhe Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (kuli) , anayekuwa balozi wa Tanzania nchini China na Mhe Anthony Cheche (kushoto) anayekuwa Balozi wa Tanzania katika Congo DRC.
 
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu  na Makamu wa Rais DktbMohamed Gharib Bilal pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Makatibu wakuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

WAALGERIA KUCHEZESHA TAIFA STARS, IVORY COAST

$
0
0
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeteua waamuzi kutoka Algeria kuchezesha mechi kati ya Taifa Stars na Ivory Coast itakayofanyika Jumapili saa 9 alasiri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi hao watakaochezesha mechi hiyo ya kundi C kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil wataongozwa na Charef Mehdi Abid atakayepuliza filimbi. Atasaidiwa na Hamza Hammou na Bouabdallah Omari wakati mezani atakuwa Sofiane Bousseter.

Abdi na wezake wanatarajiwa kutua nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 12 asubuhi kwa ndege ya EgyptAir. Mtathmini wa waamuzi ni Athanase Nkubito kutoka Rwanda ambaye atatua nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya RwandAir.

Kamishna wa mechi hiyo ni Bernard Mfubusa kutoka nchini Burundi ambapo atawasili nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 3.35 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways. Maofisa wote hao wa mechi hiyo watarejea makwao Jumatatu (Juni 17 mwaka huu).

HATUA YA TATU RCL KUCHEZWA JUMAMOSI
Mechi za kwanza za hatua ya tatu ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao zitachezwa Jumamosi (Juni 15 mwaka huu) wakati za marudiano zitachezwa Jumatano ya Juni 19 mwaka huu.


Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo (Juni 11 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kupitia ripoti za michezo iliyopita na kufanya uamuzi mbalimbali ikiwemo mechi ya marudiano kati ya Mpwapwa Stars na Machava FC ambayo haikuchezwa.

Machava FC ambayo ilishinda mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Moshi kwa mabao 2-0 inaendelea katika hatua ya tatu kwa vile haikuhusika katika kukwamisha mchezo wa marudiano uliopangwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kiliuhamishia mchezo huo kwenye Uwanja wa Mgambo mjini Mpwapwa kinyume na maelekezo ya Kamati ya Mashindano ya TFF. Kamati katika kikao chake cha awali iliekeleza kuwa mechi zote za RCL zitachezwa makao makuu ya mikoa isipokuwa kwa Morogoro ambapo timu ya Techfort FC iliruhusiwa kutumia Uwanja wa CCM Mkamba mjini Ifakara.

Hivyo timu nane zilizofuzu kucheza raundi hiyo ni Friends Rangers ya Dar es Salaam, Kariakoo ya Lindi, Katavi Warriors ya Katavi, Kimondo SC ya Mbeya, Machava ya Kilimanjaro, Njombe Mji ya Njombe, Polisi Jamii ya Mara na Stand United FC ya Shinyanga.

Wakati timu nyingine zimefuzu kwa kushinda mechi zao za raundi ya mbili, Njombe Mji imeingia hatua hiyo kwa kuwa timu yenye uwiano mdogo wa kufungwa (best looser) katika hatua ya pili.

Katika hatua hiyo mechi ni ifuatavyo; Kariakoo vs Friends Rangers, Machava FC vs Stand United FC, Polisi Jamii vs Katavi Warriors, na Kimondo SC vs Njombe Mji. Timu zilizoanza kutajwa ndizo zinazoanzia nyumbani.

Vilevile Kamati ya Mashindano imeagiza Kamishna wa mechi ya marudiano kati ya Mpwapwa Stars vs Machava FC, Mwijage Rugakingira wa Tanga ambaye alikwenda Uwanja wa Mgambo badala ya Uwanja wa Jamhuri kinyume na maelekezo ya TFF aondolewe kwenye orodha ya makamishna.

Pia waamuzi wa mechi hiyo ambao nao walikwenda Mpwapwa badala ya Dodoma Mjini wamepelekwa Kamati ya Waamuzi ya TFF kwa ajili ya kuchukuliwa hatua kutokana na tukio hilo.

Kamati ya Mashindano imekumbusha kuwa RCL ni mashindano yanayosimamiwa na TFF, hivyo maelekezo yoyote kuhusiana na mashindano hayo pia yatatoka TFF na si mahali pengine popote. Hivyo, msimamizi wa kituoa hana mamlaka ya kubadili uwanja.

Hatua ya nne ya RCL itachezwa kati ya Juni 23 na 23 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 29 na 30 mwaka huu.

BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AFUNGUA MKUTANO WA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA TANAPA MKOANI IRINGA

$
0
0
1aWaziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akifungua mkutano wa Shirika la Hifadhi za Mbuga za Taifa TANAPA na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Wajibu wa vyombo vya habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za taifa unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo Ofisi za Manispaa ya Iringa.

 Balozi Kagasheki amewaasa wahariri wa vyombo vya habari kujadiliana kwa undani suala zima la kukomesha ujangili na jukumu la wanahabari katika mkakati huo wakishirikiana na serikali kwa ujumla kupitia taasisi za ulinzi katika mbuga za wanyama, amewataka wahariri kuwa wabunifu kwa kuandika makala na habari za kiuchunguzi ili kuibua mbinu hizo chafu na majangili ili kutokomeza ujangili huo na kupata ufumbuzi kamili wa changamoto hizo za ujangili.

 Ameongeza kwamba wizara yake iko tayari kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wahariri na wadau mbalimbali yatakayofanikisha kupata ufumbuzi wa kutokomeza kabisa ujangili katika mbuga na pia amejiwekea utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari kila mwezi atakutana na vyombo vya habari ili kuzungumza na wanahabari kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo.
2aWahariri mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki wakati akifungua mkutano huo.3aWahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa makini katika kusikiliza wakati Waziri Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika mkutano huo.4aBalozi Khamis Kagasheki akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano huo kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo mjini Iringa5aMkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Waziri wa Malisiali na Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki.
1 Waziri wa Malisili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma wakati akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Siasa na Kilimo mkoani Iringa ambako mkutano wa Wahariri wa vyombo vya habari na Shirika la Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA unafanyika. 3Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Ardhi Mazingira Ndugu James Lembeli akiingia kwenye ukumbi wa mkutano huku akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi kushoto.4Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki wa pili kutoka kulia akiwa katika mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Mazingira Ndugu James Lembeli na kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma.5Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki katikati akiwa katika mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya Ardhi na Mazingira Ndugu James Lembeli na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma6Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akizungumza katika mkutano huo huku Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki wa pili kutoka kushoto akisikiliza, wengine ni Ndugu James Lembeli Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Mazingira na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma.7Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya Ardhi na Mazingira Ndugu James Lembeli akizungumza katika mkutano huo huku waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akisikiliza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma.8Mkurugenzi wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akizungumza katika mkutano huo kukaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo unafofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo mjini IringaPICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE- IRINGA

USIKOSE IJUMAA HII NYUMBANI LOUNGE MIAKA 13 YA LADY JAYDEE KATIKA MUSIC

REDD'S MISS TANGA 2013 KUFANYIKA JUNI 22,MKWAKWANI

$
0
0
WAREMBO wanaowania shindano la kumtafuta mlimbwende wa mkoa wa Tanga Redd's Miss Tanga 2013 wakiwa katika pozi mara baada ya kumalizika mazoezi yao kwenye ukumbi wa Lavida Loca jijini Tanga,ambapo shindano linatarajiwa kufanyika June 22 mwaka huu katika uwanja wa mkwakwani mjini Tanga.

LILIAN SOTI ATWAA TAJI LA REDD'S MISS KIGOMA 2013

$
0
0
Mrembo wa mkoa kigoma kwa mwaka 2013 Lilian Soti (aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Faidha Hamisi (kulia) na mshindi wa tatu Hapiness Arbogast (kushoto) muda mfupi baada ya shindano hilo.

MKUTANO WA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA TANAPA WAENDELEA MKOANI IRINGA

$
0
0
1Mkurugenzi wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Allan Kijazi akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa washiriki wa mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na TANAPA unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo mjini Iringa ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, Maada mbalimbali zinawasilishwa leo ikiwa ni pamoja na Masuala ya Utalii ndani ya hifadhi, Miradi ya ujirani mwema na Ulinzi katika mbuga.2Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Mubnge wa jimbo la Iringa mjini Mchunagji Peter Msigwa akitoa mada katika mkutano huo wakati wa majadiliano kuhusu utalii katika hifadhi za TANAPA kulia ni Mkurugenzi wa Tanapa na Kushoto ni Dr. Ayoub Rioba na mstari wa nyuma kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Mzingira na Maliasili Ndugu James Lembeli na kushoto ni Meneja uhusiano wa TANAPA Bw. Pascal Shelutete.
3Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Mzingira na Maliasili Ndugu James Lembeli akizungumza katika mkutano huo unaoendelea mjini Iringa leo4Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Mzingira na Maliasili Ndugu James Lembeli akisisitiza jambo wakati akichangia mada katika mkutano huo unaoendelea leo.5Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima Ndugu Charles Misango akiuliza swali katika mkutano huo6Dr. Ayoub Rioba akiendesha majadiliano katika mkutano huo7Mwandishi wa habari Antonio Nugas kutoka Radio Clouds kushoto akiwa pamoja na washiriki wengine katika mkutano huo.8Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali za mkutano huo.9Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali za mkutano huo.10Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali za mkutano huo. Picha na Fullshangwe Blog.

KILI MUSIC AWARDS WINNERS TOUR 2013 HIYOOO INAKUJA ULIPO

$
0
0
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Kili Music Tour 2013 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kala Jeramiah na Nasssib Abdalah 'Diamond'. 
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdalah akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya wasanii kwenye mikoa 8, ambapo jumla ya wasanii 24 watashiriki.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Kala Jeramiah akizungumzia ziara ya wasanii.
 Chazi Baba akitoa vionjo vya moja ya nyimbo zake. 
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akiteta jambo na, Diamond na Chaz Baba wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu Kili Music Tour 2013.
Profesa J akiwashukuru wale wote waliompigia kura pamoja na kuwasihi wasanii tutokata tamaa na kujipanga vizuri katika tuzo za mwakani ili waje kung'ara.

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YATUNUKUIWA CHETI NA SHIRIKA LA VIWANGO LA KIMATAIFA (ISO)

$
0
0
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Mark Taylor (katikati) na  Meneja viwango wa SBL,  Paul Kitambi wakionesha cheti walichotunukiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa(ISO) kwa wana habari katika ofisi za kiwanda hicho cha SBL jijini Dar es Salaam jana.Kulia ni Meneja mawasiliano ya ndani wa SBL, Imani Lwinga.
Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Kitambi, akizungumza na wana habari, kuhusu kutunukiwa cheti 9001:2008 na shirika la viwango la kimataifa (ISO) baada ya kukidhi vigezo vya shirika la Det Norske Veritas (DNV) linaloaminika kimataifa katika kutoa huduma za ukaguzi na uhakiki wa utendaji wa viongozi na wafanyakazi katika makampuni, mkutano huo ulifanyika jana katika ofisi za Kiwanda cha bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Taylor .
 Meneja mawasiliano ya ndani wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Imani Lwinga akizungumza jambo katika mkutano na wana habari jana jijini Dar es Salaam.
Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Kitambi akiwa amebeba cheti walichotunukiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa(ISO) mara baada ya kumaliza mkutano na wanahabari jana jijini Dar es Salaam.

REDD'S MISS KINONDONI 2013 WATEMBELEA WAGONJWA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MWANANYAMALA

$
0
0
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (katikati) akiwa na mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Ssebo wakitoa maelekezo kwa warembo mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiwagawia warembo vifaa kwa ajili ya kujikinga na vumbi mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
Warembo wajielekezana namna ya kuvaa vifaa vya kujikinga na vumbi kabla hawajaanza zoezi la kufanya usafi.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiwa na mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Ssebo wakiwaongoza warembo mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
 Mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Ssebo akiwaongoza warembo kuchukua vifaa kwa ajili ya kuanza zoezi la kufanya usafi.
 
Warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013 wakiwa katika zoezi la kufanya usafi.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiongea na vyombo vya habari. 
Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2012/13 ambaye alitokea Redd'd Miss Kinondoni 2012 akiongea na vyombo vya habari.
  Mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Ssebo akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika zoezi la kufanya usafi.
Bw. Ssebo alisema kuwa mchakato wa kumtafuta Redd's Miss Kinondoni umeanza kwa kishindo ambapo warembo hao ambao walishaanza kambi tokea mwishoni mwa wiki iliyopita jana waliweza kutembelea hospitali ya Mwananyamala  na kufanya usafi.
Warembo hao ambao wanajumuisha vitongoji vya Dar Indian Ocean, Sinza na Ubungo baada ya kufanya usafi hospitalini hapo walijionea hali mbaya iliyokuwepo pale na kuamua kufanya harambee ya kuchangisha hela kwa ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds).
Harambee hiyo imepangwa kufanyika siku ya alhamis tarehe 13, katika ukumbi wa Ambassador kuanzia saa moja jioni huku mgeni rasmi akiwa ni meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda.
Warembo hao leo watafanya usafi hospitali ya Sinza na kutembelea mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi.
Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim Blog 'FATHER KIDEVU BLOG', SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog, DjChoka Blog na Kajunason Blog.

JAJI BOMANI ASHAURI KUPIGWA KURA ILI KUABAINI MFUMO WA MUUNGANO

$
0
0
NA BELINDA KWEKA – MAELEZO, DSJ
MWANASHERIA  Mkuu wa Serikali  mstaafu, Jaji Mack Bomani ametoa wito wa kupingwa kwa kura ya maoni kwa wakazi wa Tanzania Visiwani ili kuona kama wanahitaji mfumo gani wa Muungano kabla ya kuendelea na mchakato wa sasa wa rasimu ya Katiba  mpya .

Akizungumza na  waandishi wa  habari leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari –MAELEZO , Jaji Mack   Bomani  alisema  anaipongeza tume ya Jaji  Joseph   Warioba kwa kazi nzuri na pia kwa mapendekezo yake juu ya  Muungano  wa Tanzania.

Kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo  Jaji  Bomani  alitoa historia fupi juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo ameeleza kuwa muungano huo ulipendekezwa na hayati Sheikh Abeid  Amani  Karume na hayati Mwalimu  Julius  Nyerere, ambao walikutana mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari, mwaka 1964.


Jaji Bomani   aliongeza  hayati  Karume  alipendelea nchi mbili kuungana  na kuwa  nchi moja , lakini hayati  Nyerere  alisita  kidogo  kwa kuogopa kwamba ingeonekana Zanzibar imemezwa na Tanganyika na pengine kuleta maasi Zanzibar hivyo kupendekeza kuundwa mfumo wa muda mfupi wakati mfumo wa kudumu ukifanyiwa kazi.

 “Suala la Muungano  ndilo  suala kubwa kuliko yote katika  mchakato  wa Katiba mpya.  Niliwahi kuto ushauri nao ni kwamba ifanyike kura ya maoni ya wananchi hasa Zanzibar  kama wanautaka muungano au la na kama wanautaka uwe muungano  wa mfumo gani ? Mpaka sasa maoni ambayo yanasikika ni maoni ya viongozi mara Zanzibar ijitoe kwenye muungano mara tuwe na muungano wa mkataba,” alisema  Jaji Bomani.

Akijibu maswali aliyoulizwa  na waandishi wa habari ,Jaji Mack Bomani amesema katika uundwaji wa Serikali tatu anaamini utaweza kumaliza migogoro inayojitokeza mara kwa mara hasa upande wa Zanzibar kuogopa kumezwa.

“Woga  wa gharama za mfumo wa Serikali tatu hauna msingi.Inategemea Serikali hizo unazifanya vipi.ipo mifano mingi mno duniani ya miungano ya mfumo mbalimbali,” alisisitiza.

Pia ameongezea kuwa kama kutaundwa Serikali tatu basi iwe Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano.

Akiongezea kuhusu katiba mpya amesema “kwa maoni yangu si lazima kazi hii ya katiba iishe kabla ya 2015, tupate muda wa kutosha ili tuweze kupata katiba ya kueleweka na kukubalika na kila mtu”.

MKUTANO WA WADAU WA UHAMASISHAJI WANANCHI KUJIUNGA NA NHIF,CHF NA TIKA WAFANA PWANI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza, akihutubia katika mkutano wa wadau wa kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Biama ya Afya mkoani Pwani leo.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk. Mohammed Hashim 9kulia) akimshukuru Mkuu wa Mko wa Pwani, Mwantumu Mahiza kufungua mkutano wa wadau wa mkoa huo wa kujadili uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko huo, leo mjini Kibaha. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano huo
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akielezea mikakati mbalimbali ya kuboresha mfuko huo nchini
Mratibu wa NHIF Mkoa wa Pwani,Andrew Mwilungu akiwakaribisha wadau kwenye mkutano huo muhimu wa uboreshaji sekta ya afya kwa wananchi kujiunga NHIF,CHF pamoja na TIKA mkoani
Humba akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza kwa nasaha zake alizozitoa wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa wadau ambao ulihudhuriwa na watendaji wakuu wa kutoka wailaya zote za mkoa huo wakiwemo na wabunge.
Mbunge wa Kibiti, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Pwani, Abdul Marombwa akitoa shukrani kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa hotuba yake pamoja na ujio wa NHIF  mkoani humo.
Baadhi ya wakuu wa wilaya za Mkoa wa Pwani, wakiwa katika mkutano huo. Kutoka kulia ni, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Ahmed Kipozi na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu
Baadhi ya watendaji wa wilaya za mkoa wa Pwani wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya wadau wakihudhuria mkutano huo.
 Mmoja wa wadau wa mkutano huo akihudumiwa na maofisa wa NHIF
Viongozi wa NHIF, CHF wakiwa pamoja na wadau kwenye mkutano huo
 Ofisa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NHIF, Grace Kisinga (kulia) akiratibu mkutano huo. Kutoka kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Hamis Mdee na Mratibu wa NHIF Mkoa wa Pwani, Andrew Mwilungu.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NHIF, Eugen Mikongoti, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo

TUZO ZA FILAMU ZA STEPS KUFANYIKA JUMAMOSI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya usambazaji wa filamu Tanzania ya Steps Entertainment limited Jumamosi  itatoa tuzo kwa wasanii, Watayarishaji, Waongozaji, na wadau mbalimbali waliopo katika tasnia ya filamu Tanzania.
Mratibu wa tuzo hizo, Carlos Johns Silondwa alisema kuwa tuzo hizo zitafanyika kwenye ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza na zitawahusisha zaidi wasanii wanaofanya kazi na kampuni yao tu.
Silondwa alisema kuwa kutakuwa na vipengele nane ikiwa pamoja na Filamu Bora ya Mwaka, Kampuni iliyotengeneza filabu bora, msanii anayependwa na watu ndani na nje ya mwisho, msanii bora chipukizi, muigizaji bora wa kike, muigizaji bora wa kiume, muongozaji bora wa filamu na mwandishi bora wa filamu.
Silondwa alisema kuwa wameandaa tuzo hizo kwa lengo la kuanzisha tuzo hizo ni kuleta ushindani na kukubali mchango wa wasanii, watayarishaji na wadau wote kampuni inatumia fursa hii ya kuwatambua na kujali mchango wa wasanii katika ukuzaji wa filamu nchini Tuzo ni kichocheo kitakacholeta ushindani unaoweza kujenga tasnia ya filamu na kujenga ajira kwa jamii kubwa.
Alisema kuwa tuzo hizo zimezingatia michango mbalimbali kutoka kwa wadau mbalimbali ambao wamekuwa mbele katika kutangaza tasnia ya filamu ndani na nje ya nchi kupitia njia mbalimbali, pia kutakuwa na tuzo za heshima kwa waliotangulia kuitambulisha tasnia ya filam u Tanzania.
“Tunaamini kuwa tuzo zitakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza tasnia ya filamu kuongeza ushindani katika kutengeneza filamu Bora, hadithi nzuri zinazoelimisha, kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania lugha ambayo imekuwa ikukua kila siku kwa kupitia filamu za kitanzania zinazopenyeza na kuvuka mipaka ya nchi,” alisema Silondwa.
Alisema kuwa wanaarajia kuwa na Tuzo kubwa zitakazoshirikisha wadau wote kwa baadae, na kuwa ni moja kati ya moja ya kampuni wadhamini wa tuzo zenye mlengo wa kimataifa, mwaka huu kampuni imeandaa tuzo hizo pasipo kuwatumia wadhamini wa nje ya kampuni ikipata udhamini kwa kampuni ya Steps Solar pekee.

Museveni awapongeza Mwalimu Nyerere,Karume

$
0
0
 Na Mtuwa Salira,EANA
Arusha, Juni 12,2013 (EANA)--Rais Yoweri Museveni wa Uganda (pichani juu) amewaelezea viongozi waanzilishi wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Shekhe Abeid Karume kuwa walikuwa viongozi wenye muono wa hali juu katika Afrika Mashariki walioacha ubinafsi wa mamlaka ya nchi zao na kuunganisha watu wao kwa lengo la kuwa na umoja imara.

 ''Viongozi hao wanastahili kutambuliwa kwa maamuzi yao ya busara ya kuunganisha Tanganyika na Zanzibar kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,'' Rais Museveni aliwaambia wajumbe wa semina ya mahusiano ya wabunge mjini Entebe, Uganda mwishoni mwa wiki.


 Hatua hiyo ya kishujaa na ya kupongezwa haina budi kuigwa na nchi wananchama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), aliongeza, Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA) linaripoti.
 
Nyerere alistaafu urais mwaka 1985 na kufariki mjini London Uingereza Oktoba 14, 1999 akiwa na umri wa miaka 77. Shekhe Karume (67) aliuawa Aprili 1972 mjini Zanzibar.

Rais Muveni alikuwa anahutubia semina ya siku mbili yenye kauli mbiu : ''Kukuza soko lenye misingi ya watu wa Afrika Mashariki.''  

''Huku ikiwa na idadi ya watu milioni 140, Afrika Mashariki ina soko kubwa ambalo linaweza kuvutia kwa urahisi wawekezaji ambao wanaweza kujenga viwanda katika kanda hii,'' Museveni alitoa maoni yake juu ya kauli mbio hiyo, kwa mujibu wa gazeti la Monitor la nchini Uganda.

Aliongeza: ''Ubaguzi unaotokana na tofauti za kikabila na dini zinapingana na matakwa ya wote, wazalishaji na wafanyabishara.''

Alitoa changamoto kwamba kuunganishwa kwa Afrika Mashariki ilikuwa '' ni lazima kwa kuwa watu katika kanda hiyo walikuwa tayari wameunganishwa kwa utamaduni na lugha zao.''
Viewing all 10720 articles
Browse latest View live