Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10735 articles
Browse latest View live

ESHE RASHINDI NDIYE REDD'S MISS MARA 2013

$
0
0
 Mshindi wa taji la Redd's Miss Mara 2013, Eshe Rashid akiwa katika picha ya pozi mara baada ya kuvikwa taji hilo hivi karibuni mjini Musoma mkoani Mara.
  Mshindi wa taji la Redd's Miss Mara 2013, Eshe Rashid (katikati) akiwa katika picha ya pozi mara baada ya kuvikwa taji hilo hivi karibuni mjini Musoma mkoani Mara.Kushoto ni Mshindi wa pili Amina Shabani pamoja na Mshindi wa tatu Marima Joseph. Washindi hawa watashiriki shindano la kumsaka mrem,bo wa Kanda ya Ziwa.

 Hatua ya tano bora waliingia warembo hawa.
 Huyu alikabidhi taji kwaniaba.
 wafanyakazi wa Barick Gold wakipiga picha na mshindi ambaye pia ni balozi wao.
 Wadhamini Barick Gold wakimvisha sasha Mshindi
Mwandaaji wa shindano hilo Godson Mkama akilamba picha na warembo hao.

MIAKA 13 YA LADY JAYDEE 'ANAKONDA' NI FUNIKA MBAYA

$
0
0

 Hivi ndivyo hali ilivyo ndani ya Ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam ambapo leo hii kuna bonge moja la show la Mwanadada mkongwe kwenye tasnia ya muziki hapa nchini,Lady Jay Dee ambaye anatimiza miaka 13 tangu alipoanza kazi yake ya muziki.katika show hii wanamuziki mbali mbali watapanda jukwaani aliwepo Mh. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
 Wadau mbali mbali wa muziki hapa nchini wapo ndani ya ukumbi huu hivi sasa kusuhudia show hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki.
 Ndani ni nyomi la hatari,lakini nje nako watu bado wanataka kuingia huku wengi wao wakisema kuwa "hata kama hakuna siti,sie tuko radhi kusimama ilimradi tumsapoti Dada yetu.
 Getini mambo yako namna hii.
 Foleni bado ni ndefu na watu bado wanazidi kuingia ukumbini hapa hivi sasa.
Burudani ya Utangulizi ikiendelea.

Kwa picha na video zaidi zitawajia baadae kidogo.

Miss Redds Iringa 2013 ni Neema Mality

$
0
0


Miss Redds Iringa 2013 Neema Mality akipozi na mshindi wa pili Lucy  George (kushoto), na mshindi wa tatu Lillian Samson baada ya kutwa taji hilo usiku huu. Picha na Francis Godwin

SHEREHE YA UWT KWA PLO ZAFANA DAR

$
0
0
 Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba akiwalaki Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead na Makamu Mwenyekiti wa POL Tayseer Khalid (mwanaume mwenye miwani) Khalid na ujumbe wake walipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, waliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Wanne Kushoto ni Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi.

 Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba (wapili kulia), akiwa na  Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead, Makamu Mwenyekiti wa PLO Tayseer Khalid, wakati ujumbe wa chama hicho ulipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, iliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi 

 Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO) Jihad Abu Zead akitazama bidhaa za kina mama wa UWT, ujumabe wa Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khali (kulia kwa Jihad), ulipowalisi. Wengine ni Mwenyeji wao, Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migoro na Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba.
 UNAONA WANAVYOWASHANGILIA! Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akimwambia Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO), Jehad Abu Zead, wakati ujumbe wa chama hicho ulipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, iliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto ni, Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid na Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba.
 Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) Jehad Abu Zead, akimpa kadi mwanachama mpya wa CCM, Mohamed Ali, katika sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba na Wanne ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Wasita niBalozi wa Palestina hapa nchini, Dk. Nasri Abujaisa
 Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba akimzadia nguo, Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead, wakati  cha Palestina (PLO) Jehad Abu Zead, akimpa kadi mwanachama mpya wa CCM, Mohamed Ali, katika sherehe maalum iliyoandaliwa na UWT leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza wakati sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Mamia ya wanachama wapya wa CCM ambao wengi wao ni vijana, wakiwa katika picha ya p0amoja na viongozi baada ya kupewa kadi zao katika sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Kinamama wakimwayamwaya wakati wa sherehe hiyo
 Wengine wakigaragara chini kwa furaha wakati wa sherehe hiyo
 Kikundi cha Vijana wa CCM cha Ilala wakionyesha umahiri wao wa kucheza sarakasi wakati wa sherehe hiyo
 Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi akimwekeza jambo, Mwenyekiti wake, Sophia Simba wakati wa sherehe hiyo
 Viongozi wote wa meza kuu wakiwaaga wananchi baada ya sherehe hiyo kufana
 Wana-UWT nao wakiwaaga viongozi kwa furaha
 Mjumbe wa Kamati Tandaji wa PLO, Jihad akionyesha zawadi aliyopewa na wanachama wa UWT katika sherehe hiyo. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba na Makamu Mwenyekiti wa PLO Tayseer Khalid
 Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba akizungumza wakati wa sherehe hiyo
 Jihad akizungumza wakati wa sherehe hiyo
 Vijana wanaoshiriki Miss Kanga Party ya Kibaha, wakisalimiana na wageni wa heshima kwenye sherehe hiyo.
 Wana-UWT wakiwa wamemzonga Jihad na hivyo Katibu Mkuu wa UWT Amina Makilagi kulazimika kutumia msuli kuwazuia, walipokuwa wakimshangilia kiongozi wakati akiondoka Uwanjani
Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba akiagana na Makamu Mwenyekiti wa PLO baada ya sherehe. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

WAWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE WASHEREKEA KUMALIZIKA KWA MASHINDANO HAYO.

$
0
0
 Washindi wa Mashindano ya Guinness Football Challenge 2013 wakiwa kjatika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Epraimu Mafuru naMeneja wa bia ya Guinnes Davis Kambi wakati wa tafrija hiyo.
 Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephaim Mafuru nae akionesha kipaji chake mbele ya vijana hao.


 Meneja wa bia ya Guinness Davis Kambi (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru wakiwa katika picha na wadau wengine wa Guinness na wafanyakazi wa SBL.
 Ilikuwa ni furaha tu kwa kila mtu.
Wadau wa Guinness wakibadilishana mawili matatu wakati wa tafrija hiyo.
 Regina Gwae kutoka kampuni ya R & R Associate akizungumza jambo na mmoja wa washiriki wa mashindano ya Guinness Football Challenge
 Meneja wa bia ya Guinness Davis Kambi akilamba picha na mabalozi wa kinywaji hicho.
Baada ya kumalizika kwa mashindano ya Guinness Football Challenge yaliyokuwa yakiendeshwa na Kupitia kipindi maarufu cha  Guinness Football Challenge TV Show, hatimaye wawakilishi wa Tanzania katika mashindano hayo jana wamefanyiwa sherehe fupi katika Ukumbi wa Savannah Lounge Jijini Dar es Salaam na waandaji  na wadhamini wa shindano hilo Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwapongeza kwa hatua waliyofikia.

Yaliyokuwa yakifanyika Afrika Kusini hatimaye yalimalizika hivi karibuni huku timu ya Tanzania ikiishia katika hatua ya nusu fainali kwa nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Ghana, Cameroon, Kenya na Uganda zilizoshiriki mashindano hayo ukiwa ni msimu wa tatu.

Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na wanahabari iliwashuhudia vijana walioshiriki mashindano hayo wakiwa na nyuso za furaha na kulakiwa kwa shangwe na uongozi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti.

Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Savannah Lounge Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Moses Kebba ameipongeza timu hiyo kwa kufikia hatua nzuri ya mashindano hayo ambayo yalishirikisha timu mbalimbali za nchi zingine  za Afrika.

Alisema kwamba katika hatua hiyo ya nusu fainali waliofikia ni dhahiri vijana hao wamefanya kazi nzuri huku akivishukuru vyombo vya habari kwa kuwatangaza vyema wakati wa ushiriki wao kati mashindano hayo ya Guinnes Football Challenge.

Amesema kwamba katika mashindano hayo nchi kadhaa zilishiriki kama vile  Ghana, Cameroun, Kenya & Uganda, ambapo amekiri kwamba katika mashindano hayo kumekuwapo na ushindani mkubwa licha ya Tanzania kutoibuka na ushindi ilifanikiwa kufikia katika hatua ya nusu fainali.

Kwa upende wake Meneja wa bia ya Guinnes Davis kambi amesema kwamba  wataendelea kusaidia zaidi kuibua vipaji vya soka kupitia ushiriki huo ambao utaleta tija katika soka la Tanzania kwa kutangazika hatimaye kufanya vyema katika mashindano hayo ambayo yamekuwa na umaarufu mkubwa Afrika na sasa wataendelea kutafuta zaidi vipaji vitakavyoshiriki katika msimu ujao.


“Kila mmoja katika kampuni yetu ya SBL na watanzania wanayofuraha na nakuwapongeza Daniel Msekwa na  Mwalimu Akida,  kwa kufanya vizuri licha ya kushindwa kufika hatua ya fainali lakini kazi mlioifanya imeonekana na mmeweza kuiwakilisha vyem Tanzania katika mashindano ya Guinness Football Challenge”, Alisema Kambi

Katika fainali ya mashinado hayo yaliyoshirikisha pia timu za Uganda na Kenya timu ya Tanzania ya  GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE iliwakilishwa na Daniel Msekwa, Mwalimu Akida, Mohamed Kobembe, Gullam Sosha, Hamza Rashid,Lukwesa Kanakamfumu, Abubakari Mohamed, Kherry Sadallah, Simon Chimbo na Emmanuel Temu. 

Akizungumzia mashindano hayo Daniel Msekwa amesema: “Tumepata uzoefu mkubwa katika mashindano lakini kubwa ni kuhakikisha tunafanya mambo kulingana na mawasiliano ya kupata vipaji zaidi ambapo timu za Kenya na Uganda zilifanikiwa kufikia malengo mazuri lakini hayo yote ni changamoto kwetu.”

 “Tunaishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa sababu walifanya kila jitihada kipindi tupo Afrika Kusini kwenye mashindano na kuona utofauti wa nchi zingine kama Ghana na Cameroon,

WAFANYAKAZI WA BENKI YA BARCLAYS WATOA MSAADA KWA WATOTO MUHIMBILI HOSPITALI LEO

$
0
0
Mwanasheria wa Benki ya Barclays, Farija Ghilas akimkabidhi sehemu ya msaada waliotoa kwa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam jana, Sakina Hassani. Vitu vimetokana na michango ya wafanyakazi wanaofanyakazi katika benki hivyo.
 Wafanyakazi wa Benki ya Barclays wakitoa msaada wa vitu ,mbalimbali katika wodi ya watoto Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, vikiwemo sabuni, vyandaru, miswaki, vinywaji baridi pamoja na dawa za meno, vitu hivyo vimetokana na michango ya wafanyakazi  wa benki hiyo.
 Mwanasheria wa Benki ya Barclays, Farija Ghilas akimkabidhi sehemu ya msaada waliotoa kwa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, Sakina Hassani. Vitu hivyo vimetokana na michango ya wafanyakazi  wanaofanyakazi katika benki hivyo. 
 Rahma Said mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam akipokea sehemu ya msaada uliotolewa na wafanyakazi wanawake wa benki ya Barclays wakati walipofika kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika wodi ya watoto katika hospitali ta Taifa Muhimbili. Vitu vilivyokabidhiwa leo ni pamoja na sabuni, vyandaru, miswaki, vinywaji baridi pamoja na dawa za meno, vitu hivyo vimetokana na michango ya wafanyakazi  wa benki hiyo.

 Poa zawadi ya mafuta mama.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays, Neema Sengo akizungumza na waandishi wa habari baada kutembelea wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam na kwafariji watoto walolazwa katika wodi hiyo na kuwabidhi vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, miswaki, vyandarua, mafuta, pamoja na vinywaji baridi kwa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam, leo. 

NAPE: PUUZENI VITISHO VYA CHADEMA KAPIGENI KURA KWA AMANI

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg.Nape Nnauye amewataka wananchi kwenye kata zinazofanya uchaguzi mdogo kesho kupuuza alivyoviita vitimbi vya Chadema na wafuasi wao badala yake wajitokeze kwa wingi kushiriki kwenye upigaji wa kura kwa amani na utulivu.
Nape ameyasema hayo jijini Arusha jana wakati alipokuwa anajibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua tathimini ya kampeni na jinsi CCM ilivyojipanga kwenye uchaguzi mdogo katika kata mbalimbali nchini.

Nape alisema kwa ujumla wake kampeni zimekwenda vizuri karibu katika kila kata ukiacha matukio kadhaa machache ya vurugu ambayo alidai yamekuwa yakiratibiwa na Chadema na wafuasi wao baada ya kuvuta bangi na kunywesha vijana wao viroba.

"nimekuwa Arusha kwa siku mbili tatu, hakuna mashaka kuwa Arusha wamechoshwa na vurugu za Chadema , baada ya kuhangaishwa kwa miaka mitatu na vurugu za Chadema wameamua sasa kurudisha utulivu na heshima ya jiji la Arusha, hivyo nawapongeza sana" alisema Nape.

" ni kweli hata mie nimesikia wenzetu baada ya kuona maji ya shingo wameamua kutumia vitisho kujaribu kutisha watu hasa kina mama na wazee wasiende kupiga kura, lakini nawahakikishia CCM tumejipanga kuwalinda waende kupiga kura kwa amani na utulivu. Isitoshe taarifa tulizoziapata zinaonyesha serikali imejipanga vizuri sana kulinda amani na utulivu, hivyo tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura bila hofu" alisisitiza Nape.

Aidha Nape alidai kwa taarifa walizonazo wanamatumaini kuwa kata zote 25 zinazofanya uchaguzi mdogo CCM itashinda kwani wanaamini kuwa wananchi wana imani kubwa na CCM na kuwa vitimbi vinavyofanywa na wapinzani nchini vimewachefua sana wananchi.

Itakumbukwa kuwa chaguzi ndogo nchini zinafanyika kwenye kata 25 kufuatia kata hizo kuwa wazi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo vifo na baadhi kuhama au kufukuzwa vyama vyao vya siasa.

Ushindani mkubwa ulitegemewa sana jijini Arusha ambapo kuna kata nne zinafanya ucahguzi mdogo kufuatia Chadema kuwafukuza madiwani wake. Hata hivyo hali jijini Arusha inaonyesha Chadema kulemewa sana kiasi cha kuwa na uwezekano wa kupoteza kata zote ambazo walikuwa wakizimiliki mwanzoni.

TAZAMA VIDEO YA SHOW YA THE FINEST YA MWANA FA HAPA

$
0
0
 Linah, Mwana FA Na Maua On Stage @ Makumbusho Ya Taifa Dar Es Salaam.
 Wahudhuriaji wa "The Finest" Kama Zamani wakiwa wanaenjoy burudani classic kutoka kwa Mwana FA.
IMG_7288
Mwana FA akiwasili katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam huku akiwa amevalia suti matata iliyotengenezwa na mbunifu wa mavazi anayekuja kwa kasi nchini Sheria Ngowi.

IMG_7336
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA akikamua jukwaani wakati wa Show ya Kijanja ya The Finest iliyorindima usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar. Nyuma yake ni Msanii Linah aliyeshirikishwa kwenye nyimbo ya YALAITI aliyoimba na Mwana FA akisubiri kutumbuiza.
IMG_7422 
IMG_7361
Msanii wa muziki wa Bongo Flava nchini Ben Paul akisindikiza kutoa burudani wakati wa show ya Mwana FA iliyopewa jina la “The Finest”. Wasanii wote walionekana nadhifu kwa kuvaa masuti ya gharama.
IMG_7357
Kutoka (kulia) ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe, akiwa na Mbunge wa Bumbuli (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba, wakiwa ni miongoni mwa mashabiki wa Mwana FA, waliohudhulia shoo hiyo. Kushoto ni Mtangazaji wa Clouds FM, Gerald Hando.
IMG_7427
Mashabiki wa Mwana FA, wakimshangilia Superstar wao wakati akitoa burudani.
IMG_7430
 Wema Sepetu na Kidate wake nao walikuwepo kwenye show ya wajanja.
Fa 7
Mashabi wa Mwana FA wakionekana kukongwa mioyo yao wakati wa show iliyobeba jina la  “THE FINEST”…Na kweli ilikuwa The Finest kama inavyoonekana pichani.
IMG_7330
Watu weweeeeeeeeeee…..ukumbi ulirindima Shangwe za mashabiki wa Mwana FA.
IMG_7418
Mwana FA akiendelea kuwapa raha mashabiki wake.
IMG_7399
Wadau wakishow love nje ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI KUAGA MWILI WA MAREHEMU TIMOTH APIYO KARIMJEE LEO

$
0
0
 Jeneza lililohofadhi Mwili wa Mzee Timothy Apiyo aliyewahi kuwa Katibu wa Ikulu na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya awamu ya pili likiwa viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam hii leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mblele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, marehemu, Timoth Apiyo, aliyefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo Juni 15, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa maziko

 Asha-Rose Migiro, akipita kutoa heshima zake za mwisho mblele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, marehemu, Timoth Apiyo, aliyefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo Juni 15, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa maziko
 Jaji Mstaafu, Joseph Sinde Warioba na Mkewe wakipita kutoa heshima zake za mwisho mblele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, marehemu, Timoth Apiyo, aliyefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo Juni 15, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa maziko
 Viongozi mbalimbali waliohudhuria kuaga Mwili wa Mzee Timothy Apiyo wakiwa viwanja vya Karimjee.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia baada ya kutoa heshima za mwisho mblele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, marehemu, Timoth Apiyo, aliyefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo Juni 15, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa maziko.


HAPPYNESS WATIMANYWA NDIE MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI

$
0
0
Mshindi wa taji la Redds Miss Kanda ya Kati Happiness Watimanywa (Katikati) akiwa na nyuso ya furaha mara baada ya kamati ya majaji kumtangaza mshindi katika kinyanganyiro kilichoshirikisha walimbwendwe 12 kutoka Mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma Wa Kwa Kwanza kulia Ni Mshindi wa Tatu Jackline huku Mshindi wa Pili ni  ( Wa kwanza Kushoto) Sabrina Juma Kutoka Mkoani Tabora
Jaji Mkuu wa Shindano ya Kumsaka Mloimbwende wa Kanda ya Kati Mh Hashim Lundenga Akipungia mikono watanzania waliofika kushuhudia mlimbwende wa Kanda ya kati anapatikana
Mshiriki wa Kinyanganyiro Cha Redds Miss Kanda ya Kati Hawa Nyange akijitambulisha
 Mmoja wa Washiriki wa Kinyanganyiro Cha Kumtafuta Mlimbwende wa Kanda ya kati akijitambulisha mbele ya hadhara
 Muda wa Kuonyesha Vipaji ukawadia
 Mavazi ya Ubunifu
 Walimbwende walioingia hatua Ya Tano Bora
 Wadau wa Miss Tabora wakifuatilia shindano kwa ukaribu kabisa
Mratibu na mwandaaji wa Redds Miss Kanda ya Kati akitoa Maneno huku pembeni yake ni Mgeni Rasmi (katikati) Mh John Komba akiwa na baadhi ya wabunge wenzake kutoka Zanzibar
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Amin akicheza na mmoja wa mashabiki wake ambaye alikua akiigiza kama Linah jana wakati wa shindano la kumtafuta Redds Miss Kanda ya Kati
Mmoja wa mashabiki wakimtunza Mwanamziki wa Kizazi kipya Amin wakati alipokuwa akitoa Burudani Jana katika Kinyanganyiro Cha Kumtafuta Mlimbwende wa Kanda ya Kati
Baadhi ya wadau waliojitokeza kwenye kushuhudia Shindano la Redds Miss Kanda ya Kati lililofanyika Usiku wa Kuamkia Leo Katika Ukumbi wa Kilimani Mkoani Dodoma.Picha Na Josephat Lukaza Wa Lukaza Blog

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 16 2013

MLIPUKO WA BOMU ARUSHA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Arusha
KUTOKANA na mlipuko wa kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu, uchaguzi wa Kata nne jijini Arusha uliopangwa kufanyika leo umeahirishwa na kupangwa tena kufanyika Juni 30 mwaka huu.

Uchaguzi huo umeahirishwa huku mlipuko wa jana ambao ulitokea wakati Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maeendeleo (Chadema), Freeman Mbowe anafunga mkutano wake, ulisababisha kuzuka kwa taharuki kubwa katika mkutano huo wa kampeni.

Watu kadhaa wamehofiwa kufa katika mlipuko huo, ambao umezidi kuomnyesha kuwa hali ya amani kataika Taifa hili la Tanzania inazidi kutoweka.

Mwandishi wetu jijini Arusha, aliiambia Handeni Kwetu kuwa uchaguzi huo umeahirishwa. Bado tunafuatilia kwa kina mtifuano huo sambamba na hali za majeruhi na waliopoteza maisha.

Mlipuko huo ulitokea na kuleta wasiwasi mkubwa katika kazi za kijamii, kama vile mikutano na makongamano pale yanapohusisha watu wengi na kuleta hofu kubwa.

JK Mgeni rasmi mechi ya wakuu wa wilaya na wabunge

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mechi ya hisani itakayowakutanisha waheshimiwa wabunge na Wakuu wa wilaya, itakayopigwa Juni 29, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
 
Mechi hiyo itatanguliwa na ile ya Juni 22 mjini Dodoma, ambapo huko mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambapo lengo la mechi hizo ni kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya albino, huku kukipangwa kuwa na burudani za kila aina, sambamba na wasanii watakaoamua kuungana na serikali juu ya uchangiaji huo.
 
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa timu hiyo ya wakuu wa wilaya, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kuwa huku mheshimiwa rais akiwa mgeni rasmi, ila wamejipanga imara kwa ajili ya kuwaonyesha kazi wabunge, ambao baadhi yao wameanza kujigamba dhidi ya mechi hiyo ya aina yake.
Alisema kuwa Watanzania wote watakaopata fursa ya kuhudhuria kwenye mechi hizo wataaburudika kwa kiasi kikubwa, huku wakiamini kuwa licha ya wakuu wa wilaya wengi kuwa mikoani, ila wana nguvu na ari ya kushinda mbele ya wabunge.
 
“Tupo imara na tutaanza mazoezi yetu kesho Jumatatu kwa kukutanisha wakuu wa wilaya wote waliokuwa kwenye timu hii, huku barua za kuwaombea mialiko kutoka kwa Wakuu wa Mikoa tayari zimeshafika kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili.
 
“Katika mechi hizi, mwamuzi wa kati atakuwa atakuwa Reginald Mengi, ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, huku waamuzi wa pembeni wakiwa ni IGP Said Mwema na Stephen Wassira, ambapo wote watashiriki katika mchezo huu,” alisema.
 
Aliwataja Wakuu wa wilaya waliotwa kwenye uundwaji wa kikosi hicho kuwa ni pamoja na Venas Mwamoto (Kibondo), Ramadhan Maneno (Kigoma), Norman Sigara (Mbeya), Krispin Meela (Rungwe), Benson Mpesya (Kahama), Deodatus Kinanilo (Chunya), Herman Kapufyi (Same), Francis Isaac ( Chemba), Wilson Mkambaku (Kishapu), Yahya Nawanda (Iramba), Elibariki Kingu (Igunga), Festo Kiswaga (Nanyumbu), Paza Mwamlima (Mpanda), Abdallah Ulega (Kilwa), Seleman Mzee (Kwimba), John Mongela (Arusha), Konstantin Kanyasu (Ngara), Paulo Mzindakaya (Busega), Mrisho Gambo (Korogwe), Muhingo Rweyemamu (handeni), Cristofa Magala( Newala), Erasto Sima (Bariadi), Jordan Rugimbana (Kinondoni), Joseph Mkirikiti (Songea), Ngemela Rubinga (Mpanda) nay eye mwenyewe anayotokea wwilaya ya Handeni, ambaye pia ni msemaji wa timu hiyo.
 
Aidha, Muhingo alitaja kikosi cha wanawake kuwa kinaongozwa na Beth Mkwasa (Bahi), Sarah Dumba (Njombe), Josephine Mapiro (Makete), Hafsa Mtasiwa (Pangani), Mboni Mgaza (Mkinga), Halima Dendegu (Tanga), Queen Mlozi (Singida), Angelina Mabula (Butiama), Merry Tesha (Ukerewe), Christina Mndeme (Hanang), Anna Magoha (Urambo) Jacqueline Liana ( Magu).

HUU NDIO UZALENDO WA KWELI

REDD'S MISS MOROGORO 2013 NI DIANA LAIZER

$
0
0

 Redd's Miss Morogoro 2013, Diana Laizer (katikati) akipozi na mshindi wa pili, Sabra lsmail (kushoto) na mshindi wa tatu Muzne Abduly.


TAIFA STARS VS IVORY COAST TAIFA LEO

$
0
0
 Beki wa kati wa Taifa Stars, Kelvin Yondan akijaribu kumdhibiti Kalow Salomon wa Ivory Coast huku mlinda mlango Juma Kaseja akiruka kukamata mpira miguuni kwa Kalow na Eraston Nyoni na Frank Domayo wa Tanzania wakisogea kuongeza nguvuwakati timu hizo mbili zilipokutana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika mchezo wa marudiano wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia Brazil 2014 nchini Brazil. Ivory Coast ilishinda 4-2.

 Kikosi cha kwanza cha Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambacho kilishuka dimbani dhidi ya Ivory Coast Jana.  Mstari wa nyuma walio simama kutoa kushoto ni Mbwana Samata, Erasto Nyoni, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu, Kevin yondani na Nahodha Juma Kaseja. Mbele kutoka kushoto-Nadir Haroub 'canavaro', Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Salum Abubakar na Shomari Kapombe.

Kikosi cha kwanza cha Ivory Coast walio simam kutoka kushoto ni, Kalow Salomon, Serey Geoffroy, Bamba Souleman, Traore Lacia, Yaya Toure na Gosso Gosso Jean -Jacques. Msari wa mbele kushoto-Yao Gervals, Aurier Alain,  Nahodha Zokara Didier, Barry Boubacar na Boka Arthur.
 Mbwana Samatta akiwatoka washambuliaji wa timu ya Taifa ya Ivory Coasta waliokuwa wamezengea lango la Timu ya Taifa Taifa Stars.


Aliyekuwa Kocha wa wekundu wa Msimbazi Simba, Mfaransa Patrick Liewigakipita jukwaani mbele ya wafanyakazi wa NSSF. Mfaransa huyu amerithiwa mikoba yake na Kocha Mzawa Abdalh King Kibaden Mputa aliyewahi kuichezea timu hiyo na kuinoa kwa mara kadhaa.
 Timu za Simba na Yanga ambao ni timu kubwa na zilizo na upinzani mkali leo zilionesha uzalendo wao kwa kuunganisha mabango yao na kuishangilia timu ya Taifa.
 Mdau wa father Kidevu Blog, John Mapinduzi nae alikuwepo uwanjani.
 Hapa ilikuwa ni Msuli tu baina ya Shomary Kapombe (20 mgongoni ) na Aurier Alain.
 Mwamuzi wa mchezo wa leo kati ya taifa Stars ya Tanzania na Ivory Coast Mehdi Abid kutoka Algeria akimwamuru Mchezaji Yaya Toure wa Ivory Cost kuacha kulia lia bali aende akacheze mpira.
 Shomary Kapombe akilia kwa maumivu baada ya kuumua mguu.
 Wachezaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta (10) na Thomas Ulimwengu (11) wakiwa katika heka heka za kutafuta mpira.
Ubao wa Matokeo ulisomeka hivi ..
  
Ras Inocent Nganywagwa nae alikuwepo uwanjani hapo kushuhudia mchezo huo na alipoa badaa ya kutulizwa na Ivory Coast.
 Hakika ni huzuni kwa kila aliye ipenda Taifa Stars...
LICHA ya kufungwa goli 4-2 na Ivory Coast hii leo katika uwanja wake wa nyumbani Timu ya Taifa ya Tanzania imeonesha kandanda safi na lakuvutia ambalo lilikuwa likiwatoa jasho wakali hao wa soka bara afrika.

Ivory Coast ikishusha dimbani wachezaji wake wote wakali wanaosakata soka la kulipwa Ulaya wakiongozwa na Yaya Toure walishikwa na butwaa pale Amri Kiemba alipo pachika bao la kwanza katika dakika ya kwanza ya mchezo huo ulioujazwa watu uwanja wa taifa jijini Dar esa Salaam.

Ingawaje Tanzania inakosa nafasi ya kufuzi fainali za kombe la Dunia 2014 huko Brazil lakini kikosi hicho kinacho nolewa na Kim Poulsen kinaonesha sasa kuiva na kuimarika hivyo kuleta matumaini makubwa zaidi kwa watanzania katika michuano ya AFCON.

Ushindi wa leo wa Ivory Coast inaifanya timu hiyo namba moja Bara Afrika kufikisha pointi 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote katika kundi hilo na sasa itasubiri kucheza na mmoja wa washindi wengine wa makundi mengine tisa ili kuwania kwenda Brazil mwakani.

Tanzania inabaki na pointi zake sita, huu ukiwa mchezo wa kwanza kufungwa nyumbani katika kampeni hizi na Morocco bila kuhusisha matokeo yake na Gambia, ina pointi tano ikishika mkia wa kundi.  

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mehdi Abid aliyesaidiwa na Hamza Hammou, Bauabdallah Omar wote kutoka Algeria, hadi mapumziko Ivory Coast tayari walikuwa mbele kwa mabao 3-2.

Stars ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao na kuzitumia vyema nyasi za |uwanja wa taifa na kugeuza machinjio ya Tembo wa Teranga mfungaji akiwa ni Amri Kiemba dakika ya kwanza tu aliyepokea pasi ya Mbwana Samatta kufuatia mpira wa kurushwa na Erasto Edward Nyoni kusababisha kizazaa cha piga ni kupige langoni mwa Ivory Coast.

Ivory Coast walishtuka na kujitambua kuwa wapo katika eneo hatari na  dakika ya 15 kupitia kwa Lacina Traore ilisawazisha goli hilo baada ya mabeki wa Stars kuzembea kuokoa huku Mkali wa Man City, Yaya Toure akafunga la pili kwa mpira wa adhabu dakika ya 23, nje kidogo ya eneo la hatari.

Bao hilo lilitokana na wachezaji wa Stars kupanga ukuta wao vibaya na kumpoteza maboya kipa wao, Juma Kaseja aliyeruka bila matumaini kuufuata mpira huo.

Stars walinoa tena kisu chao na kukaza kamba zao vyema kisha kumuweka sawa Tembo wa Teranga na kufanikiwa kupachika bao la kusawazisha kupitia mchezaji wa Kimataifa anaesakata kabumbu huko Congo DRC katika Klabu tajiri ya TP Mazembe, Thomas Ulimwengu hii ikiwa ni kunako dakika ya  35 baada ya kazi nzuri ya Shomary Kapombe.

Hata hivyo, Ivory Coast wakapata penalti rahisi baada ya Gervinho kujiangusha wakati anakabiliana na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kumpa nafasi Yaya Toure mkuachia mkwaju ambao licha ya Kaseja Kuucheza kwa mguu lakini uliingia wavuni dakika ya 43.

Kipindi cha pili Stars ilikianza vizuri na kushambulia mara nyingi langoni mwa Ivory Coast, lakini wakaishia kukosa mabao ya wazi.

Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mdenmark, Kim Poulsen dakika ya 85 baada ya Shomari Kapombe kuumia na kutoka nje na kumuingiza Hamis Mcha  na kumtoa kiungo Mwinyi Kazimoto na kumuingiza mshambuliaji Vincent Barnabas yaliigharimu Tanzania kwa kufungwa bao la nne na kupotea kabisa mchezoni.

Baada ya kutoka Kazimoto, aliyetekeleza majukumu yake vizuri leo, Ivory Coast wakatawala sehemu ya kiungo na kutengeneza bao la nne lililofungwa na Bonny Wilfred akitokea benchi dakika ya 88.

Pamoja na kufungwa, Stars ilicheza soka safi ya kuvutia na mabao yote yalitokana na makosa – na si kuzidiwa uwezo. 

Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe/Khamis Mcha dk 85, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto/Vincent Barnabas dk 87, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Amri Kiemba.

Ivory Coast; Boubakar Barry, Arthur Boca, Didier Zakora, Solomon Kalou/Sio Giovanni, Gervais Yao, Jean Jarques Gosso Gosso, Alain Aurier, Lacina Traore/Bonny Wilfred, Yaya Toure, Geoffrey Serey na Suleiman Bamba/Nori Koffi Christian.

NAPE AITEKA DONGOBESH NA BASHNET

$
0
0
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa kata ya Dongo besh na kuwaambia wakati ndio huu kwa wao kuchagua kiongozi atakaye wafaa kwa kuleta maendeleo yao.
 Umati mkubwa wa wakazi wa Dongo besh wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kwenye mkutano wa kuhitimisha kampeni za udiwani zilizofanyika Dongobesh.
 Mgombea wa udiwani wa Dongo besh, Joseph almaarufu Cheng Lee akihutubia wakazi wa eneo hilo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsikiliza mkazi wa  Dongo besh aliyeamua kurudisha kadi ya Chadema  na kurejeaa CCM,baada ya kuelewa yale aliyokuwa akihutubia Nape.
 Mtoto huyu hakuwa nyuma kufuatilia mkutano wa kampeni za udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Dongo besh.
 Wakazi wa Dongo besh wakiwa juu ya mti kabisa kusikiliza sera za CCM.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye akipata mapokezi ya kichama alipowasili kwenye kata ya Dongo besh.
 Wazee wa kimila wakifanya ibada ya kimila kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni za Udiwani Dongo besh.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki kucheza ngoma ya wenyeji wa Dongo besh mara baada ya kumaliza kuhutubia na kufunga kampeni za kugombea kiti cha udiwani.


BASHNET
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu ( Uwekezaji na Uwewezeshaji) Dk. Marry Nagu.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na Mbunge wa Babati Vijijini  , ndugu Jitu Soni .


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa Nape Nnauye akisalimiana na mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa Bashnet wwakati wa kuhitimisha mikutano ya kampeni za udiwani.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa kiti cha udiwani kwa tiket ya CCM, Ndugu Nicodemus Gwandu.


 Mbunge wa Babati Vijijini, Jitu Soni akiwa pamoaja na wananchi wa jimbo lake wakati wa mkutano.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimjulia hali mama mzazi wa Laurent Tara.

Montage Ltd na Serena Hoteli wala chakula cha Mchana na Watoto waishio kwenye mazingira magumu

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Montage Ltd,Teddy Mapunda akisaidia kuwapatia Watoto vinywaji wakati wa hafla fupi ya Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Hoteli ya Serena pamoja na Kampuni ya Montage,kwa Watoto wainshio katika Mazingira Magumu wa Kituo cha Pasada,Kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam.Hii ilikuwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
 Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Hoteli ya Serena,Seraphin Lusala (kulia) akiwa sambamba na Meneja Mkuu Msaidizi wa Hoteli hiyo,Daniel Sambai wakisaidiana kuwapatia Watoto vinywaji wakati wa hafla fupi ya Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Hoteli ya Serena pamoja na Kampuni ya Montage,kwa Watoto wainshio katika Mazingira Magumu wa Kituo cha Pasada,Kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam.Hii ilikuwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
 Kazi ikiendelea.
 Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Hoteli ya Serena,Seraphin Lusala akizungumza machache wakati wa hafla hiyo,iliyofanyika kwenye ukumbi wa Maquee uliopo ndani ya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
  Watoto wakipata chakula.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hoteli ya Serena.Picha na Othman Michuzi.

Mara waweka historia kwa kuchangia damu nyingi

$
0
0
Na Craig Ferla ,  Mara
Kuokoa maisha ya maelfu ya mama zetu na watoto wetu wachanga Tanzania inawezekana! Kwa pamoja tunaweza kabisa kubuni mbinu mpya za kufanikisha yale ambayo awali tuliyaona kama hayawezekaniki… Hivi sasa ninapoandika makala hii, benki ya damu ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) Kanda ya Ziwa imefurika, huku maandalizi ya kuongeza uwezo wa taasisi hii kupokea damu nyingi kwa mpigo yakiendelea, na hii ni kutokana na mwitikio mkubwa wa wakazi wa wilaya zote za mkoa wa Mara kujitokeza kwa makundi makubwa kujitolea damu kwa hiari! Mwitikio huo wa shamra shamra za maadhimisho ya Siku ya Mchangiaji Damu Duniani ambayo kitaifa yanafanyika Mkoani Mara bila shaka yoyote, umetokana na ujumbe wa wahamasisha jamii, kuwashawishi wakazi wa Mara kutoa‘zawadi ya maisha,’hasa hasa ili kuokoa akina mama na watoto.

Mama Ye!ni kampeni inayohimiza wanajamii kuchukua hatua kuokoa maisha ya maelfu ya mama zetu na watoto wachanga wa Tanzania. Hii ni kampeni inayoongeza msisitizo wa Kampeni ya kimataifa ya Kupunguza Vifo vitokanavyo na Uzazi Barani Afrika (CARMMA) iliyozinduliwa Novemba 2011 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete. Kwa pamoja tumeazimia kuona kuwa ‘Mama asife wakati analeta uhai.’
Kuna ambao watajiuliza kuna uhusiano gani kati ya uhai wa akina mama na uchangiaji damu, na ni kwa niniMama Ye!imeungana na NBTS na mamlaka za Mkoa wa Mara kwa ajili ya maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Mchangia Damu Duniani? Kwa mtazamo wangu, jibu ni rahisi. Takwimu za Tanzania kwa kutumia makadirio ya Shirika la Afya Duniani zinakadiria kuwa 80% ya damu inayokusanywa hutumika kwa watoto pamoja na akina mama wenye matatizo yatokanayo na ujauzito. 

Inakadiriwa kuwa kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua  ndicho chanzo kikuu cha vifo vya wanawake wajawazito, na husababisha kifo kimoja kati ya kila vifo vitatu hadi vitano vya akina mama wajawazito nchini Tanzania.

 Aidha kuna uhaba mkubwa wa damu kwenye hospitali zetu—huku ikikadiriwa kuwa ni theluthi moja tu ya chupa 450,000 za damu zinazohitajika nchini kila mwaka ndizo zinazokusanywa. Ni wazi kabisa kuwa wapo akina mama wetu wanaovuja damu nyingi baada ya kujifungua wanaofariki kutokana na uhaba wa damu kwenye vituo vya tiba. 

Iwapo watavuja damu nyingi baada ya kujifungua, wanawake wanaweza kuhitaji kuongezewa damu ili kuwaokoa. Kama damu itakuwepo katika vituo vya tiba, basi akina mama hao wataokolewa. Vile vile, kama akina mama wengi wataokolewa basi watoto wachanga wengi nao wataokolewa, na hii ni kutokana na uhusiano wa karibu kati ya uhai wa watoto wachanga na ule wa mama zao.


Na la muhimu zaidi kwaMama Ye!– kuchangia damu ni kitendo kinachobeba maana nzito na cha kuonekana, ambacho kinaweza kufanywa na mtu yeyote yule ili kushiriki kuokoa maisha ya mama zetu. Ni maamuzi yanayotokana na dhamira ya mtu kuchangia damu. 

Na kama dhamira hiyo ya kuchangia damu inatokana na nia ya kuokoa maisha ya akina mama, basi inaweza kuwa chachu kwa mtu huyo huyo kuchukua hatua nyingine ambazo zinaweza kutendwa na kila mtu ili kuwaokoa akina mama na watoto wetu wachanga. 

Kwa mfano, kuwahimiza akina mama wajawazito kuhudhuria kliniki japo mara nne; kuwawezesha akina mama kujifungulia katika vituo vya tiba ambapo kuna mhudumu mwenye ujuzi kwa kuwaandalia usafiri au kuwaangalia watoto wao pale nyumbani; na kuwafuatilia viongozi katika jamii na kujua ni hatua gani zinachukuliwa kuhakikisha uwepo wa huduma na ubora wa huduma hizo kwa akina mama na watoto wachanga.
  
Mara Oyee!!Mmetoa ujumbe wa kishindo katika wiki mbili zilizopita, kutoa matumaini kwa uhai wa mama zetu na watoto wachanga!! NBTS imethibitisha kuwa ukusanyaji wa damu katika sherehe za kitaifa kama hizi umevuka kiwango kilichokuwa kimezoeleka!! Zaidi ya watu 1,250 wamechangia damu katika sherehe za wilayani Bunda, Butiama, Serengeti, Tarime na Rorya wiki iliyopita. 

Wiki hii wakazi wa Manispaa ya Musoma nao pia wamejitokeza kwa makundi makubwa—Jumla ya wakazi 500 wamechangia damu katika siku mbili tu zilizopita, na wakati huo huo wakitoa ahadi zao na wito kwa wanajamii wengine kuchukua hatua mbalimbali kuokoa maisha ya akina mama na watoto wachanga mkoani Mara. 

Na kwa hakika tangu maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Mchangiaji Damu Dunani ya mwaka huu yaanze katikati ya Aprili, zaidi ya chupa 5,000 za damu zimekusanywa mkoani Mara. Tembelea ukurasa wetu wafacebookkuona picha za jinsi Mkoa wa Mara ulivyoweka historia mwaka huu katika shamra shamra za Siku ya Mchangiaji Damu Duniani, nchini Tanzania!!

MRISHO MPOTO NA BENDI YA MJOMBA BAND KUFANYA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA

$
0
0
1Msanii wa ngoma za asili na Mkurugenzi wa bendi ya Mjomba Band Mrisho Mpoto akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kinondoni Mkwajuni wakati alipotangaza kuhusu kundi lake kuanza kampeni kubwa ya kuhamasisha wananchi kuhusu usafi wa mazingira mijini na vijijini kwa kunawa mikono na sabuni, kujenga na kutumia vyoo bora na kuboresha mzingira kwa ujumla ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia walengwa kwa kubadili tabia na njia mbadala za mawasiliano kuhusu elimu hiyo, Upatikanaji wa maji safi na salama na usafi wa mazingira bado ni tatizo kubwa kwa watanzania walio wengi. 

Mwaka 2010 aslimia 9 tu ya wananchi waishio vijijini na asilimia 22 ya wananchi waishio mijini waliweza kupata huduma bora za usafi wa mazingira. kati ya sababu zingine , ni watu kutozingatia faida za usafi wa mazingira Katika k kampeni hiyo Mrisho Mpoto na kundi lake la mjomba Bandi wanashirikiana kwa pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, kushoto ni Mariam Mahamudu Afisa Afya, Mazingira Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii , Kampeni hiyo itaanza na mikoa ya Dodoma, Mara, Njombe, Rukwa na Tanga kabla ya kuendelea mikoa mingine.
2Mariam Mahamudu Afisa Afya, Mazingira Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii akizungumza katika mkutano huo kuzungumzia kuhusu kampeni hiyo, kulia ni Mrisho Mpoto Mkurugenzi wa Mjomba Band.3Kundi zima la mjomba band likiwa katika mazoezi makali katika makao makuu ya kundi hilo Kinondoni Mkwajuni.5Wakionyesha vitu vyao katika mazoezi hayo4Mrosho Mpoto akiimba katika mazoezi hayo ili kujiweka sawa kwa ajili ya kampeni hiyo kulia ni msanii wa kundi hilo anayejulikana kama Mbagala na katikati ni Mwimbaji wa kundi hilo Ismail.
Viewing all 10735 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>