






Namelok akimkabidhi msaada wa blanketi kwa mratibu wa kituo cha watoto walemavu Monduli Mireile Kapilima katikati ni Katibu wa UWT Mkoa wa Arusha Stamili Dendegu




Na Pamela Mollel,Monduli
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Arusha Namelok Sokoine ameitaka jamii kujitolea kuwasaidia watoto walemavu wanaolelewa katika kituo cha huduma ya walemavu cha kanisa katoliki jimbo kuu Arusha kwa kuwa wazazi wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu
Alisema hayo jana wilayani Monduli wakati akikabidhi misaada mbalimbali huku akiungwa mkono na wanawake wenzake waliomsindikiza kuwaona watoto wenye ulemavu wa viungo na utindio wa ubongo
Namelok alisema kuwa kuna baadhi ya wazazi ambao hawana uwezo wa kumudu kulipa shilingi 1500 kwa siku hivyo ni vyema jamii ikaguswa kuwasaidia watu wenye uhitaji
“Zipo familia zinatumia zaidi ya shilingi 1500 kwa siku kila mmoja akijitolea itasaidai kwakuwa kwa mwezi ni shilingi elfu 45000 kwa mtoto mmoja”alisema Namelok
Pia mbunge huyo alitoa shukrani zake kwa Mbunge wa jimbo hilo Edward Lowassa kwa kuweza kutoa eneo hilo na kujengwa kituo chenye uwezo wa wawahudumia watoto 52.
Misaada aliyokabidhi Mbunge huyo ni pamoja na Blanket 50, shuka,unga,mchele,sabuni, sukari na mafuta
Mratibu wa kituo hicho Mineile Kapilima alisema kituo hicho kimekuwa kikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ufadhili wa kudumu hivyo mahitaji ya kituo kuongezeka siku hadi siku kwa kuwa awali kituo kilikuwa kunauwezo wa kulaza wototo 30 lakini kwa sasa wanafika hadi 52
“ukosefu wa chakula,matibabu,nguo,hatuna ufadhili wa kudumu kwa kuwa wazazi wengi hawana hawana uwezo”alisema Kapilima