




Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema kuwa tume hiyo haiendeshwi na rimonti kwani ni chombo kinachojitegemea katika kufanya shughuli zake hivyo amewaasa wananchi na wanasiasa kuondoa fikra potofu juu ya tume hiyo.
Pia Jaji Lubuva ameongeza kuwa tume hiyo haifanyi kazi kwa kushinikizwa na mtu yeyote Yule badala yake wanafanya kazi kutimiza jukumu walilopewa kitaifa.
Aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati akitambulisha mfumo mpya wa kuboresha daftari la kupigia kura kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voter Registration (BVR) ,ambapo alisema kuwa teknolojia hiyo itaanza kutumika mwezi Agusti mwaka huu katika shughuli za uboreshaji wa daftari la wapiga kura
Aidha alisema kuwa mfumo huo utaleta maboresho na utasaidia kuwepo kwa daftari la kura linaloeleweka na lisilo na mashaka.
Pia aliongeza kuwa siku 14 za wananchi kufika katika vituo vya kupigia kura kuboresha taarifa zao na kuandikisha wapiga kura wapya ambao hawaklupata fursa hiyo na kuwa zoezi hili litawahusu Watanzania wote.
Kuhusiana na matukio ya mabomu yanayojitokeza hususani Mkoa wa Arusha alisema kuwa ulinzi utaimarishwa ili kuwapa fursa wananchi kujitokeza kupiga kura kwa usalama
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela amesema kuwa maboresho hayo yatasaidia ushiriki mpana wa wananchi katika kutimiza haki zao za kidemokrasia na kikatiba za kupiga kura hivyo amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika zoezi hilo
.(Pamela Mollel jamiiblog)
.(Pamela Mollel jamiiblog)