Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenela Mukangala yuko nchini China katika ziara ya kuangalia maendeleo ya Sekta ya Utangazaji na kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Utangazaji kati ya Tanzania na China.
Katika ziara hiyo ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba Nkinga, Mkurugenzi Mkuu wa TBC Bw. Clement Mshana na Mkurugenzi wa Utangazaji TCRA Bwana Habbi Gunze.