
*****
Kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha,imeibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza katika Sekta ya Mawasiliano na habari baada ya kushindanishwa na makampuni mengeni katika maonyesho ya nane nane kwa ukanda wa kaskazini yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya themi jijini Arusha
Akiongelea ushindi huo jana,Meneja masoko wa kampuni hiyo Bi,Sarah Keiya alisema kuwa chanzo cha ushindi huo ni kutokana na timu nzuri aliyonayo ndiyo iliyopelekea wao kuibuka kidedea kwa kuwa wamekuwa wakifanya kazi kwa umoja na mshikamano wa hali ya juu
"Najivunia timu yangu ya nguvu kwa kweli sisi wafanyakazi wa Redio 5 tunashirikiana sana na tunafanyakazi kwa ushirikiano pia ,nawapongerza sana na Tunamshukuru Mungu kwa kufanukisha ushindi wetu"alisema Keiya
Pia Meneja huyo alimpongeza mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw.Robert Francis kwa kuwawezesha kwa hali na mali kufanikisha utendaji wao walipokuwa katika maonyesho hayo ya nane nane.
Pia Meneja huyo alimpongeza mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw.Robert Francis kwa kuwawezesha kwa hali na mali kufanikisha utendaji wao walipokuwa katika maonyesho hayo ya nane nane.