Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all articles
Browse latest Browse all 10768

SIMBA YAWAPELEKA OKWI, KIONGERA NDANDA FC NANGWANDA SIJAONA MTWARA

$
0
0


Na Fadha Kidevu Blog

WABABE wa Gormahia ya Kenya timu ya Simba Jumamosi ya wiki hii itapambana na wageni wa Ligi Kuu Ndanda FC,katika mchezo wa kirafiki utakao fanyika kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.



Simba iliyoibugiza Gor Mahia ya Kenya mabao 3-0,kwenye uwanja wa taifa Jumamosi iliyopita imeingia kambini leo Jumatatu kwenye Hoteli ya Shynovo kujiandaa na mchezo huo wa Jumamosi.



Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu,amesema timu hiyo kabla ya kwenda Mtwara itacheza mechi ya kirafiki Jumatano na Ijumaa itaondoka kwenda Mtwara kwa Ndege.



“Baada ya mchezo huo tutarudi Dar es Salaam kuendelea na kambi yetu tukijianda na mechi yetu ya kwanza dhidi ya ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambayo tutacheza uwanja wa taifa Dar es Salaam,”alisema Kaburu.

Simba inataraji kwenda huko ikiwa na kikosi chake kamili ikiwa ni pamoja na nyota wake Emmanuel Okwi akliyeidhinishwa rasmi kutikisa nyavu za timu pinzani kwenye Ligi Kuu Tanzania bara akiwa na wekundu hao wa msimbazi pamoja na Raphael Kiongera. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 10768

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>