Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all articles
Browse latest Browse all 10595

MAXIMO APATA AHUENI BAADA YA OSCAR JOSHUA KUANZA KUJIFUA

$
0
0


Na Fadher Kidevu Blog
KOCHA wa Yanga, Marcio Maximo  ameanza kupata ahueni baada ya beki wa kushoto Oscar Joshua kuanza mazoezi mepesi mepesi leo kufuatia kuumia nyama za paja kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Wakati Maximo akifurahia kurejea uwanjani kwa beki huyo vinara wa ligi hiyo Azam wamepata pigo baada ya beki wake tegemezi David Mwantika,kuumia kifundo cha mguu na kulazimika kuukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Prisons.

Joshua aliyekosa mchezo wa Jumapili dhidi ya Prisons aliumia nyama za paja kwenye mchezo wa awali dhidi ya Mtibwa Sugar wakati Mwantika ameumia Jumamosi iliyopita wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Hali hiyo imewafanya makocha wa timu hizo mbili Maximo na Joseph Omog kuwa katika hali tofauti hasa ukizingatia ugumu uliopo kwenye ligi ya msimu huu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 10595

Trending Articles