Rama Salim (kushoto) akiwania mpira na Emmanuel Okwi wa Simba.
Na Fadher Kidevu Blog
KIUNGO wa Coastal Union Mkenya Rama Salim amesema yeye ni zaidi ya Haruna Niyonzima na Pierre Kwizera wanaochezea klabu kongwe za Simba na Yanga
Rama Salim amesema licha ya nyota hao kutoka nchi za Burundi na Rwanda kuwa na majina makubwa lakini wanamchango mdogo kwa timu hizo tofauti na uwezo wao wanapokuwa uwanjani
“Pengine majina yao yanatokana na ukubwa wa timu wanazochezea lakini uwanjani hawana tofauti nanigumu kushindana na mimi kwa sababu nimewaacha mbali na kazi yangu inaonekana ndani ya timu.
Rama Salim amejiunga na Coastal msimu huu akitokea Gor Mahia ya Kenya na tayari ameifungia timu hiyo bao moja katika mechi dhidi ya Simba ambapo tiu hizo zilitoka sare ya 2-2 kwenye mechi ya ufunguzi ya msimu huu uwanja wa taifa Dar es Salaam.