DC Mufindi Evarita Kalalu
Na matukiodaima.co.tz
SERIKALI wilayani Mufindi mkoani Iringa imeipongeza shule binafsi ya Southern Highlands Mafinga kwa kuongoza kiwilaya na kuwa shule ya 8 kimkoa katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka 2014 .
Akitoa pongezi hizo hizo mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu alisema kuwa shule hiyo imeendelea kuipa heshima kubwa wilaya ya Mufindi
" Kilichofanywa na shule hii ya Southern Highalnds ni heshima kubwa kwa shule yenyewe ila ni heshima ya wilaya nzima mkoa na hata taifa katika kuonyesha uwezo mzuri wa walimu na watumishi wote wa shule hiyo ......amini huu ni mfano mzuri kwa shule nyingine kuiga kwani baadhi ya shule binafsi badala ya kupanda katika ufaulu zimeendelea kushuka huku shule hii yenyewe ikizidi kufanya vema...kweli nawapongeza sana walimu na uongozi mzima wa Southern Highalnds kwa matokeo mazuri"

Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya aliwataka walimu wa shule zote wilayani Mufindi kuendelea na moyo wa kujituma katika ufundishaji ili kuzidi kuongeza kasi ya ufaulu katika shule zote za msingi na sekondari ndani ya wilaya hiyo.
Alisema kuwa sifa na ubora wa elimu inayoendelea kutolewa katika shule hiyo ya Southren Highalnds Mafinga inatokana na umakini na mkurugenzi wake Bi Mary Mungai ambae amepata kuwa afisa elimu katika wilaya hiyo na wilaya nyingine nchini .
"Anachokifanya mkurugenzi wa shule hii ni kuendelea kuonyesha umakini wake katika taaluma na ingekuwa si vema kama shule hiyo ingeendelea kufanya vibaya ila katika kuhakikisha kuwa wazazi wanaopeleka watoto wao hapo hawajapotea ni baada ya kuendeleza ufaulu mzuri zaidi"
Kalalu aliwataka wazazi wa wanafunzi waliofaulu katika shule hiyo na wengine wote kuhakikisha wanajiandaa kuwapeleka watoto wao sekondari muda utakapofika badala ya kuwaacha watoto hao kukaa majumbani ama kwenda mijini kufanya kazi za ndani na uzululaji.