
Mjane wa aliyekuwa msanii wa muziki Mzee Gurumo akikabidhiwa hundi ya shilingi milioni mbili na afisa mahusiano wa NSSF Juma Kintu.
Shirikisho la Muziki Tanzania, ‘SHIMUTA’ likishirikiana na NSSF wamemkabidhi mjane wa msanii wa muziki, Mzee Muhidin Maalim Gurumo shilingi milioni mbili kama ahadi yao waliyoitoa kipindi cha nyuma.
Akizungumza na waandishi wa habari ndani ukumbi wa Benjamini Mkapa Towers, Rais wa shirikisho la muziki, Addo November amesema walimuaidi mjane huyo kumpatia Bajaj ili iweze kumsaidia kimaisha.
“Hapo mwanzo tulimwaidi mjane tutamnunulia Bajaj ili iweze kumsaidia katika maisha yake,” alisema. “Leo tumetimiza hili tukishirikiana na wadau wetu NSSF. Tumefanikisha kutimiza ahadi kwa kumkabidhi mjane cheki ya milioni mbili. Tumeona tumkabidhi pesa mwenyewe ili ajue kama ataenda kununua Bajaj au pengine anahitaji mahitaji mengine. Kwahiyo tumeona pesa inaweza kumsaidia zaidi.”
Naye mjane wa GuRumo alilishukuru shirikisho la muziki pamoja NSSF ambao wameona umuhimu wa kumsaidia katika kipindi hicho kigumu.
“Nawashuku wote, nalishukuru shirikisho la muziki pamoja na mfuko wa jamii NSSF kwa kuniondoa na ukiwa,” alisema.

Rais wa shirikisho la muziki Ado November akizungumza na waandishi wa habari

Mjane mzee Gurumo

Mjane wa Gurumo akipokea hundi

Mmoja kati ya wasanii wakongwe wa muziki wa band akizungumza