Redd's Miss Tanzania, Brigitte Alfred (katikati) akiwa sambamba na Mshindi wa Pili wa Taji hilo Eugenia Fabian (kushoto) na Edna Sylvester wakati warembo hao walipo twaa nafasi tatu za juu za Redd's Miss Tanzania 2012. Leo warembo hao wote wanavua mataji yao ya vitongoji.
****** ******
Na Father Kidevu Blog.
Wakati shindano la Redd's Miss Tanzania 2013 likizidi kushika kasi kwa vitongi vingi na mikoa kumalizia mashindano yao na kubaki Ngazi ya Kanda na Taifa leo kivumbi kina waka kwa warembo kadhaa kuchuana vikali kuwavua mataji washindi wa tatu bora ya Miss tanzania 2012.
Hapo Sinza warembo 12 watapanda jukwaani kuwania taji la kitongoji hicho linaloshikiliwa na Redd's Miss Tanzania 2012 Brigite Alfred analishikilia.
Huko Mara napo kutakuwa na mchuano mkali kwa warembo 12 nao kupanda jukwaani kuwania taji linaloshikiliwa na Redd's Miss Tanzania namba 2, Eugen Fabian.
Ndani ya jiji la Dar es Salaam tena kutakuwa na patashika ya sketi kuchanika pale katika Kitongoji cha Kigamboni City ambapo warembo wengine 12 watawania taji la kitongoji hicho linaloshikiliwa na Redd's Miss tanzania namba tatu Edna Sylvesta.