
Wakulima pamoja na vijana kanda ya kaskazini wakiwa katika majadiliano mara baada ya kufanya ziara katika kituo cha Radio 5 nakuona namna inavyoendesha vipindi vyake katika maadhimisho siku ya radio duniani iliyofanyika 13/2/2015 jijini Arusha.

Mkuu wa vipindi vya radio 5 Mathew Philip akiteta jambo na mkulima aliyefika katika maadhimisho hayo.

Mtaalamu wa mnyororo wa dhamani kwenye mauzo ya kilimo kutoka Asasi isiyokuwa ya kiserikali la Farm Radio Bw.Terevael Aremu akizungumza katika maadhimisho hayo

Wafanyakazi wa kituo cha radio 5 wakiwa wanafurahia jambo

kushoto ni Mkuu wa vipindi vya Radio 5 Mathew Philip na Ashura Mohamed wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa sekondari walioshiriki katika maadhimisho hayo ya Radio duniani

Watangazaji mahiri wa kituo cha radio 5 wakiwa katika pozi Semio Sonyo kushoto,katikati Mwangaza Jumanne na Linus Kilembu

Kulia Hilda Kinabo na Semio Sonyo watangazaji wa Radio 5


Mkuu wa vipindi vya radio 5 Mathew Philip pamoja na Mtangazaji Linus Kilembu wakiwa katika majadiliano

Mtangazaji mahiri wa kituo cha Radio 5 Tonnie Kaisoi katika pozi
*******
Kituo cha Radio 5 chenao yake makuu jijini Arusha imeadhimisha siku ya Radio duniani kwa kuwakutanisha wakulima na vijana kanda ya kaskazini ikiwa nikuhamasisha vijana kujieleza namna Radio hiyo imesaidia katika kukuza uchumi,kijamii,kisiasa na kiutamaduni
Akizungumza na waandishi wahabari hivi karibuni Mkuu wa vipindi wa Radio 5 Bw.Mathew Philip alisema maadhimisho hayo yalidhaminiwa na kituo hicho pamoja na Farm Radio, ikiwa ni kuhadhimisha siku ya Radio duniani ambapo ilifanyika tarehe 13/2/2015 jijini Arusha
Bw.Mathew alisema kuwa wakulima pamoja navijana wa kanda ya kaskazini wakiwemo wanafunzi wa shule za sekondari,walipatana fursa ya kutembelea kituo hicho na kuona namna inavyoendesha vipindi vyake ikiwemo kipindi cha afya ya akili kwa vijana(Positive mood),Fahari yangu kipindi kinacho wagusa wakulima
Alitoa wito kwa Radio zingine kuwa na utaratibu wa kuhadhimisha siku hiyo kwa kuwa itasaidia kuongeza uaminifu mkubwa na wasikilizaji kwa ujumla
Kwa upande wake Mtaalamu wa mnyororo wa dhamani kwenye mauzo ya kilimo kutoka Asasi isiyokuwa ya kiserikali la Farm Radio Bw.Terevael Aremu alisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kusisitiza jamii kusikiliza radio hasa vipindi vya elimishi vinavyopatikana katika vituo vya radio hapa nchini na Afrika
Aidha alisema kuwa Jamii hasa wakulima wakisikiliza radio watapata elimu na taarifa mbalimbali za kile wanachokiitaji kwa wakati sahihi ikiwemo taarifa za hali ya hewa
(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)