
Msanii wa muziki wa kizazi kipya "Bongo Flava, Shilole na wacheza show wake, wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka msanii mwenzao wa Bongo Flava, Mez B, mzaliwa wa Dodoma, wakati wa bonanza lililoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Februari 20, 2015. Bonanza hilo lilipambwa na michezo mbalimbali kama vile, soka, netibole, voliboli na muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiongozwa na balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto wa Mjomba band. Wasanii wengine ni pamoja na Chege na Temba na Mr. Blue. Mez B, ni mzaliwa wa mkoa wa Dodoma, ambaye alifariki leo saa tano kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma, alikokuwa akipatiwa matibabu. Anatarajiwa kuzikwa Jumatatu ijayo Februari 23.

Chege(kulia) na Temba

Wanachuo na watu wengine wakipagawishwa na muziki uliokuwa ukiungurumishwa kwenye bonanza hilo

Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, (wapili kulia) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, wakwanza kulia, wakati akitoa nasaha kwa timu mbili za soka kutoka vyuo vikuu mkoani Dodoma

Maafisa wa juu wa PSPF, wakipasha misuli. Hata hivyo hawakuingian uwanjani kusakata kabumbu kutokana na muda kuwa mchache

Mchezaji wa timu ya Nertiboli ya chuo cha fedha CBE mkoani Dodoma, akiruka juu kumzuia mchezaji mwenzake kutoka UDOM.