Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (Pwani.kushoto)akimkabidhi msaada wa sanduku la vifaa vya kupimia macho Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Mbenjamin Majoya kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambapo wanafunzi hao watapata huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.hafa hiyo ilifanyika hivi wilayani 002mkuranga mkoa wa Pwani.
Matroni wa haospitali ya wiraya ya Mkuranga Mkuranga Rosemary Magombola akisoma moja ya maneno kwenye kibao maarumucha kupimia macho mara baada ya kukabidhiwa msaada huona taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden kwa ajili ya wanafunzi wa shuleza msingi 122 .Kulia ni Mratibu wa taifa wa huduma za macho Dkt.Nkundwa Mwakyusa (kushoto) Mratibu wa mradi huo kwa watoto wa shule za msingi toka taasisis ya ya Brien Holden Vision Institute Eden ,Rebecca Kasika.
Afisa maendeleo ya jamii ya mji wa kibaha mkoa wa pwani akikabidhiwa na Mashine ya kupimia macho na Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi wa msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi wa Wilaya hiyo ya Kibaha ambao watanufaika na huduma hiyo ya upimaji macho pamoja na matibabu bure
Wafanyakazi wa hospitali ya Kibaha kitengo cha macho wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa ya Brien Holden Vision Institute Eden,mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4.
***********
NA MWANDISHI WETU
TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision imetoa msaada wa vifaa vya kupimia macho wa zaidi ya sh milioni 11.4 kwa Wilaya za Mkuranga na Kibaha ziliyopo mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msada huo ,Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Benjamin Majoya alisema msaada huo utasaidia katika kupandisha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi katika Wilaya hiyo kutokana na idadi ya watoro darasani kupungua kuanzia mwaka huu.
Alisema kupungua kwa idadi ya wanafunzi watoro kutakwenda sambamba na kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi watakaojiunga na elimu yasekondari mwaka ujao.
Majoya alisema msaada uliotolewa na Taasisi hiyo umekuja kwa wakati mwafaka kwa wakati amabo ulikuwa ukihitajika hivyo mbali ya kuwasaidia wanafunzi wa shule za msingi lakini pia utawasaidia wananchi wote wa Wilaya hiyo.
Alibainisha kuwa msaada huo unaojumuisha mashine zote za kupimia macho pamoja kutengenezea miwani za aina mbalimbali utasaidia kuondoa tatizo la uoni hafifu ambalo hapo awali wazazi walikuwa na imani potofu kwamba huenda watoto wao wamerogwa .
Akielezea ukubwa wa tatizo hilo ,alisema kuwa uoni hafifu umekuwa sababu ya mwanafunzi kutokufanya vizuri kitaaluma kutokana na kuugua mara kwa mara hivyo kusababisha utoro.
“Tunaishukuru sana Taasisi ya BrienHolden Vision kwa msaada waliotupatia na tunaahidi kuutumia kwaajili ya wananchi ,na ifahamikie kwamba hii itabaki kuwa mali ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ’”alihitimisha Majoya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Eden Mashayo alisema lengo la Taasisi yake ni kuwajengea uwezo wa kuona wanafunzi pamoja na walimu lakini pia kutoa mafunzo kwaajili ya walimu ili waweze kuwapima wanafunzi wapate huduma stahiki ili kuondokana na tatizo hilo..
Mashayo aliahidi ushirikiano baina ya Taasisi yake ,Wizara ya Afya,Wilaya ya mkuranga na kwa kuleta mtaalamu wa masuala ya macho kila mwezi mara mbili ambaye atakuwa akiwahudumia wakazi wa eneo hilo ili kuondokana na tatizo la uoni hafifu ambalo litapungua kwa asilimia 10 .
Kwa upande wake Mkuu wa Mratibu wa huduma za macho Taifa kutoka Wizara ya Afya Dk Nkundwe Mwakyusa alisema kuwa mradi huo unaosaidia shule za Msingi bagamoyo na Kibaha umeshahudumia shule 121 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili utahudumia shule 116 .
Akizungumzia changamoto zinazowakabili alisema kuwa huduma hizo hazipewi kipaumbele kwasababu serikali inajua tu kunawafadhili .
Hata hivyo alibainisha kuwa ili kutatuua changamoto hizo na kuifanya jamii iwe na uelewa sahihi juu ya magonjwa ya macho mikakati iliyopo huenda mambo yakabadilika na mwaka huu jamii itaanza kupata taarifa sahihi kuhusu magonjwa ya macho.
Naye daktari Mtalamu wa macho Gilbert Massawe wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga na Afisa Maendeleo ya jamii mji wa kibaha Leah Rwanji waliishukuru Wizara ya Afya sambamba na Taasisi ya
Brien Holden Vision kwa msaada wao na kubainisha kuwa utasaidia kupunguza idadi ya utoro kwa wanafunzi kwa asilimia 10.