Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Teknolojia mpya ya umeme jua ya gharama nafuu ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS). Katikati ni Paul Kiwele Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini,Mwisho ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Teknolojia mpya ya umeme jua ya gharama nafuu ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS) Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini Paul Kiwele katikati akizindua teknolojia hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam
Injinia Arnold Swai wa Kampuni ya Rex Energy akionyesha namna Teknolojia mpya ya umeme jua ya gharama nafuu ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS) inavyofanya kazi. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa na Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini Paul Kiwele.
Mwandishi wa habari kutoka kituo cha televisheni cha channel 10 Peter Shedrack akipokea zawadi ya solar mpya aina ya 3G+Solar Homes System (SHS) aliyojishindia wakati wa droo iliyochezeshwa kwenye uzinduzi wa teknolojia hiyo jijini Dar es Salaa. Anayemkabidhi ni Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini Paul Kiwele na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa.
