
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea mkoani Ruvuma ambako alihudhuria mazishi ya Kada wa CCM na Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi Marehemu John Damiano Komba aliyefariki hivi karibuni, Chama cha Mapinduzi kilikuwa na maombolezo ya kitaifa ya siku tatu mpaka mazishi ya kiongozi huyo yalipofanyika jana yakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete.
Ndugu Abdulrahman Kinana ameanza ziara ya siku 9 mkoani Dodoma akianzia wilaya ya Mpwapwa kabla ya kuendelea na ziara hiyo katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.






