Turn off for: Swahili

Madaktari bingwa kutoka India

Daktari bingwa kutoka India katika hospitali ya Apollo Abhijit Singh akizungumza jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha katika kituo cha MMC Health

Wagonjwa wakiwa wanapatiwa vipimo mbalimbali

Atul Behll ambaye pia ni daktari bingwa kutoka India akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari

Mgonjwa aliyekuja kupata huduma akiwa anasaidiwa na wahudumu wa kituo hicho

Wagonjwa wakiwa wanasubiria kupata huduma

Mmiliki wa mtandao wa http://jamiiblog.co.tz Pamela Mollel akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari bingwa kutoka India
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kazini
MADAKTARI bingwa kutoka hospitali ya SPS Apollo iliyopo Ludhiana nchini India wamewasili nchini na kuanza kutoa huduma ya ushauri bure kwa magonjwa makubwa ambayo yamekuwa yakiwasumbua watu wengi na kuwalazimu kwenda kutibiwa nchini India.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kutoa huduma kwawanawake (MMC) ambapo ushauri huo unatolewa, Mratibu wa Kambi hiyo ya matibabu Arusha, Austin Makani alisema kuwa , madaktari bingwa hao wanatoa ushauri kwa wagonjwa wenye matatizo ya Figo , Moyo, tumbo, saratani, mishipa ya fahamu, uti wa mgongo, upasuaji wa kawaida na wa
kupunguza uzito.
Austin alisema kuwa, ujio wa madaktari hao watano kutoka nchiniIndia umeratibiwa na kituo cha kutoa huduma kwa wanawake (MMC) kwa kushirikiana na hospitali ya SPS Apollo iliyopo Ludhiana nchini India na wamefikia hatua hiyo baada ya kugundua kuwa wagonjwa wengi wanaoenda kutibiwa nchini India wanasumbuliwa na magonjwa hayo.
Alisema kuwa, uwepo wa madaktari hao bingwa kwa siku tatu utasaidiasana wananchi wa jiji la Arusha kufika na kupewa ushauri bure juu ya magonjwa yanayowasumbua na hivyo kuokoa gharama ya kusafiri hadi nchini India kufuata huduma hizo.
‘hapa sisi wanachofanya madaktari hawa bingwa ni kusikiliza wagonjwana baada ya kupata maelezo wanapata ushauri bure wa kwenda kupima kulingana na ugonjwa alionao na baada ya kurudisha majibu ndipo tunamwandikia dawa ya kutumia na kama ugonjwa wake unahitaji kutibiwa India tunampunguzia gharama kidogo ya kwenda kutibiwa India ‘alisema
Austin.
Alisema kuwa, uwepo wa kambi hiyo ya matibabu jijini Arusha unatoafursa pia kwa wagonjwa waliokuwa wakatibiwe nchini India kutokana na magonjwa yanayowasumbua na kuweza kupata ushauri wa haraka na wakti mwingine kuepuka gharama za kusafiri.
Wakizungumza katika kituo hicho, Madaktari hao bingwa ,Abhijit Singhna Atul Behll kutoka hospitali ya SPS Apollo India walisema kuwa ,changamoto kubwa iliyopo katika nchi za kiafrika ni watu wengi kutokuwa na utamaduni wa kwenda kupima afya zao ,hivyo aliwataka
wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kufika kwa wiki ili kupataushauri juu ya afya zao.
Walisema kuwa,nchini India kuna watanzania wengi wanaopata matibabu kutokana na magonjwa yaliyotajwa ,hivyo wakaona kuna umuhimu mkubwa kwa wao kuwafikia na kuweza kutoa ushauri bure na hatimaye kupunguza gharama za kwenda nchini India.