Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akipokea mashuka 150 kutoka kwa Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya ya jamii CHF yaliyotolewa na mfuko huo kwa wilaya ya Kilwa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya NHIF uliofanyika katika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi, Katikati ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa mkoani Lindi Bi Fortunata Raymond.
Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi wilaya ni Kilwa. Baadhi ya akina mama wakishindana kukuna nazi ambapo baada ya kumaliza zoezi hilo waliunganiswa katika huduma za CHF. Baadhi ya madaktari wakisubiri kuanza kutoa huduma katika uzinduzi huo. Wananchi wakipima uzito.