
Hafla hiyo ilifana kwa kiwango cha hali ya juu na iliyomfanya Zari kulia jukwaani kwa furaha kutokana na alivyopokelewa na watanzania huku wakiita Wifi, Wifi!!, Kila aliyehudhuria katika hafla hiyo alionekana akiwa amevalia mavazi meupe na mwenye furaha. Lakini pia hata mimi pamoja na kwamba nilienda kuripoti matukio ya hafla hiyo ilibidi nifuate utaratibu kwa kugonga vitu vyeupe kama wengine ili nisije nikaharibu shughuli ya watu.
Nilifurahia sana hafla hiyo kama walivyofurahia mashabiki wengine wa Diamond na nitamkubali siku zote kwa kazi yake nzuri anayoifanya kimuziki akiiweka Tanzania juu katika ramani ya muziki Afrika na Duniani “Viva Diamond, Viva Zari” Asanteni.


Ilikuwa Full Burudani kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Picha zaidi: FULLSHANGWE BLOG