Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all articles
Browse latest Browse all 10588

MASAU BWIRE HUYOOOOO DARAJA LA KWANZA MSIMU UJAO

$
0
0
Huyu ni Mwalimu Massau Bwire msemaji wa timu ya Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani ambaye anaweza kushika rekodi ya msemaji wa klabu zilizoshiriki Ligi kuu msimu huu aliye na maneno mengi na majigambo ya kutosha wakati timu yake ikichuana na timu kubwa hasa simba na Yanga.

Leo timu yake imekula kichapo kutoka kwa Standa United.

Hivi karibuni alijitapa vilivyo wakati wa mchezo dhidi ya Yanga kuwa timu yake itatoka na ushindi mnono lakini iliambulia kichapo cha mbwa mwizi.

Bwire ambaye kitaaluma ni Mwandishi wa habari na Mwalimu anashika nafasi hiyo akiwaacha wasemaje wengine kama Haji Manara wa Simba, Tobias Kifaru wa Mtibwa na Jerry Muro wa Yanga. 

Ruvu Shooting imeungana na Polisi Moro kushuka daraja. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 10588

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>