Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk(kushoto) akiwa katika swala iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika msikiti wa msikiti wa Alsahaba ulioko eneo la Morombo jijini Arusha,ambapo aliwatembelea waumini hao na kutoa zawadi za tende.
**********
Waislamu kote nchini wametakiwa kujiandaa vyema na mwezi mtukufu wa Ramadhani unaotarajia kuanza hivi karibuni kwani kipindi hicho ni cha kufanya matendo mema na kuisaidia jamii hasa wahitaji.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa taasisi ya Islamic Foundation Bader Marei jana katika swala ya ijumaa iliyofanyika katika msikiti wa Alsahaba ulioko eneo la Morombo jijini hapa na kuhudhiriwa na Balozi wa falme la kiarabu nchini .
Bader huyo amesema kuwa kipindi cha Ramadhani ni kipindi cha kujitazama na kubadili mwenendo na kuwa watu wanaofaa katika jamii.
Akizungumza kwa niaba ya Ugeni huo wa Ubalozi wa falme hizo za kiarabu amesema kuwa ziara hiyo inalenga kuangalia changamoto za kijamii na kuangalia namna ya kuzitatua ambapo wamezindua visima 34 vya maji katika wilaya ya Ngorongoro.
Mbali na shughuli hizo pia wamegawa msaada wa tende kwa waislamu wote waliohudhuria katika swala hiyo ikiwa ni moja kati ya maandalizi ya Mwenzi huo mtukukufu.
Baadhi ya waumini walioshiriki katika swala hiyo Issa Tesha muuminI na Saidi Hamis muumini wameeleza kufurahishwa na ujio huo mkubwa ambao unashirikiana na jamii ya waislamu katika masuala mbali mbali ya kijamii na kidini.
“Tumefurahi kupata msaada wa tende kipindi cha Ramadhani upatikanaji wa tende huwa mgumu lakini sasa walau tuna tende tunashukuru sana “ Alisema Issa.Picha na Ferdinand Shayo wa jamiiblog.