Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all articles
Browse latest Browse all 10622

MBUNGE WA GEITA DONALD KEVIN MAX AFARIKI

$
0
0
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Geita (CCM) Mheshimiwa Donald Kevin Max (58)(picha) amefariki dunia. 

Kufuatia taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb) kwa Waheshimiwa Wabunge wote pamoja na umma kwa ujumla,  Mhe. Max amefariki dunia tarehe 23 Juni, 2015 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. 
Kwa mujibu wa taarifa hii, taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia kadri zitakavyopatikana ikiwa ni pamoja na ratiba ya Mazishi. 
 
“BWANA ametoa, BWANA ametwaa, Jina la BWANA  lihimidiwe.” Amina.

Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
DODOMA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 10622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>