![]() |
Katibu msaidizi wa CCM Iringa mjini akipokea fomu ya balozi Augustino Mahiga anayeomba kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini leo |
Balozi Mahiga akirejesha fomu za ubunge jimbo la Iringa mjini leo
Balozi Mahiga akisalimiana na mgombea mwenzake Michael Mlowe (kulia)
Balozi Mahiga akiweka sahihi kitabu cha wageni leo
Na Matukiodaima BLOG
ALIYEKUWA mmoja kati ya wagombea zaidi ya 40 wa wagombea wa nafasi ya urais Balozi mstaafu Augustino Mahiga amejitokeza kuchukua na kurejesha fomu wa ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) huku akijihakikishia kuwa ndie anayestahili kumpokea ubunge aliyemaliza muda wake mchungaji Peter Msigwa (Chadema)
Balozi Mahiga alieleza kuwa yeye baada ya kustaafu nafasi ya ubalozi moja kati ya ndoto yake ni kuendelea kuwatumikia wananchi kwa ngazi ya ubunge ama udiwani kazi ambayo anaamini ataifanya kwa uadilifu mkubwa kama alivyofanya katika nafasi ya ubalozi wa Tanzania katika nchi mbali mbali .