Mkurugenzi wa kampuni ya BIMO Media , Bertha Ismail akisoma risala katika ufunguzi wa maadhimisho ya ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015 yaliyokuwa yakitimua vumbi katika uwanja wa Stedium jijini Arushaambapo pia yataambatana na mashindano ya kila mwaka ya kielimu ya uandishi wa insha,makala pamoja na uchoraji picha juu ya masuala ya utalii kwa wanafunzi wa shule za msingi 25 zilizopo Arusha yaliyoandaliwa na kampuni ya BIMO Media
Mgeni rasmi ambaye Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat M.Ntabindi akisalimiana na wachezaji kabla ya mechi ya TIMU ya Maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha na timu ya AFC Arusha katikaufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015.
Watoto wenye chini ya umri wa miaka 13 wakifanyiwa mahojiano ,aliyeshika maiki ni mmiliki wa jamiiblog Bi.Pamela Mollel*************
TIMU ya Maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha inayoshiriki ligi daraja lakwanza imeshindwa kuonyesha makali mbele ya wadogo zao timu ya AFC Arusha inayoshiriki ligi daraja la pili baada ya kutoka suluhu ya bao 1-1 katika ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015.
Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Sheikh AmrI Abeid ,uliiwashuhudia maafande hao wa Oljoro wakianza kucheka na nyavu za AFC baada ya kujipatitia bao lake kupitia kwa mchezaji Swalehe Idd alilofunga kwa njia ya Penalti mnamo dakika ya 58, iliyosababishwa na mabeki wa timu pinzani kunawa mpira katika eneo la hatari.
SOMA ZAIDI>>>FK MATUKIO