Promosheni ya Bia ya Asili ya NZAGAMBA iliyozinduliwa tarehe 13 Agosti jijini Mwanza inafikia Kilele mwishoni mwa wiki ijayo ambapo Zawadi kubwa ya Ng’ombe Dume watatu watakabidhiwa kwa washindi.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili Meneja mauzo wa Bia ya Nzagamba Bw. Peter Mwambenja alisema; Tunafurahi kuona kuwa wananchi, hasa wapenzi wa Bia hii ya Nzagamba wameshiriki kwa kiasi kikubwa katika promosheni hii ya aina yake. Sasa tunaelekea mwisho wa promosheni yetu na tunategemea kutoa Zawadi ya Ng’ombe Dume watatu kwa washindi kama tulivyoahidi. Ng’ombe hao watatolewa kuanzia Ijumaa ya wiki ijayo hadi siku ya jumapili kama ifuatavyo;
Ijumaa, tarehe 25 Septemba – Mwanza, katika kiwanja cha Mkapa kilichopo KISESA
Jumamosi, tarehe 26 Septemba – Bariadi, katika kiwanja cha MALAMBO na
Jumapili, tarehe 27 Septemba ni Geita, katika viwanja vya Nyankumbu
Katika kila eneo lililotajwa hapo juu tutatoa Zawadi ya Ng’ombe mmoja kwa mshindi, hivyo kukamilisha idadi ya ng’ombe watatu kwa maeneo yote matatu.
Maandalizi yote ya sherehe za kukabidhi Zawadi hizo yamekamilika na tunategemea kuanza sherehe hizo saa nane mchana kwa kila eneo. Alisema Mwambenja.
Nao wananchi walioshiriki promosheni hiyo wameonesha wazi kufurahishwa na jinsi promosheni ilivyoendeshwa na wanasubiri Zawadi ya ng’ombe kwa hamu kubwa. Hii ni mara ya kwanza mimi kuona mtu anashinda Zawadi ya Ng’ombe kwenye promosheni. Kwa kweli huu ni ubunifu wa hali ya juu na wa kupongezwa. Tunasubiri kwa hamu siku hizo zifike ili washindi warudi nyumbani na Ng’ombe wa Zawadi. Alisema mmoja wa washiriki mjini Mwanza.
Bwana Mwambenja aliwasisitiza walioshiriki katika promosheni hii kujitokeza kwa wingi katika maeneo yaliyotajwa kuja kushuhudia washindi wakikabidhiwa Zawadi, ambapo pia kutakuwa na burudani mbalimbali kwa wananchi Bia ya Nzagamba inatengenezwa na Kampuni ya Nzagamba iliyopo jijini Mwanza na kusambazwa katika mikoa ya kanda ya ziwa. Kampuni ya Nzagamba iko chini ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).