Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na aliyekuwa Mbunge wa Ulanga Mashariki, Celine Kombani (56),amefariki dunia hii leo nchini India .
Kombani alipitishwa na Chama cha Mapinduzi kutetea jimbo lake la Ulanga Mashariki na alipita bila kupingwa katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga.
Father Kidevu Blog inatoa pole kwa watanzania wote, Ndugu, Jamaa na Marafiki. R.I.P C. KOMBANI
Father Kidevu Blog inatoa pole kwa watanzania wote, Ndugu, Jamaa na Marafiki. R.I.P C. KOMBANI