Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all articles
Browse latest Browse all 10609

DK. STERGOMENA TAX WA TANZANIA AWA KATIBU MTENDAJI WA SADC

$
0
0
Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamemteua Dkt. Stergomena Tax wa Tanzania kuwa Katibu Mtendaji mpya wa Jumuia hiyo.

 Wakuu hao wamemteua Dkt. Tax jioni ya leo, Jumamosi, Agosti 17, 2013, mwishoni mwa kikao chao cha siku ya kwanza cha mkutano wa 33 wa wakuu hao unaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Bingu wa Mutharika kwenye mji mkuu wa Malawi wa Lilongwe.

Uteuzi huo unafuatia mapendekezo ya Baraza la Mawaziri wa SADC ambao walifanya tathmini ya wagombea wawili wa nafasi hiyo ambako Dkt. Tax alipatiwa wastani wa alama 79 wakati mgombea mwingine wa nafasi hiyo, MheshimiwaPeter G. Sinon, Waziri wa Serikali ya Shelisheli alipata alama 72.

Dkt. Tax ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki anachukua nafasi ya Dkt. Tomaz Augusto Salamao wa Mozambique ambaye amemaliza muda wake baada ya kutumikia nafasi hiyo kwa miaka minane.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 10609

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>