Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10864 articles
Browse latest View live

WANASHERIA KUONGOZA KAMATI NYETI ZA TFF

$
0
0
JAJI Steven Ihema na wakili mwandamizi, Bi. Jesse Mguto wataongoza kamati muhimu za za maadili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zilizoundwa baada ya kufanya mabadiliko kwenye katiba ya Shirikisho hilo mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais wa TFF Leodegar C. Tenga alitangaza jana.

Shirikisho hilo pia limemteua Jaji Bernard Luanda kuongoza Kamati ya Rufaa za Uchaguzi wakati Profesa Mgongo Fimbo ataendelea kuongoza Kamati ya Rufaa za Nidhamu na Kamanda Mstaafu, Alfred Tibaigana akiendelea kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu.

Rais Tenga alisema hayo wakati alipoongea na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Utendaji, ambacho kikatiba kina jukumu la kuunda Kamati Ndogo za TFF na vyombo vya maamuzi.


“Tulitaka tuwe na watu solid (imara) na makini ambao watatuhakikishia tunakwenda vyema,” alisema Tenga akizungumzia uteuzi huo ambao unahitimisha mchakato wa mageuzi kwenye Shirikisho baada ya Uchaguzi Mkuu wa TFF uliopangwa kufanyika mwezi Februari kusimamishwa kutokana na baadhi ya wagombea kupinga kuenguliwa na baadaye kwenda FIFA.

Katika kumaliza tatizo hilo, FIFA ilituma ujumbe wake kusikiliza walalamikaji na watu wengine na baadaye kuagiza kuundwa kwa Kamati za Maadili na kufanyika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa TFF kwa ajili ya kuingiza vyombo hivyo kwenye katiba kabla ya kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa TFF.

“Tumezingatia pia maoni ya wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao walitaka kamati ziwe na majaji... lakini si rahisi kupata seating judges (majaji walio kazini) ndio maana tunawashukuru wale waliotuambia kuwa wako tayari kutusaidia.

“Tumetafuta majaji na mawakili waandamizi ambao tunaamini watatuhakikishia haki inatendeka na inaonekana inatendeka,” alisema Tenga na kuongeza kuwa pia walizingatia maombi ya wajumbe wengine watatu ambao walitaka kupumzika, akiwataja kuwa ni Deo Lyatto, Sylvester Faya na Idd Mtiginjollah.

Alisema kutokana na mfumo huo mpya, mambo yote yanayohusu masuala ya ndani ya uwanja sasa yatashughulikiwa na Kamati ya Nidhamu, wakati yale ya nje ya uwanja, ambayo yanawahusu viongozi na wanafamilia ya mpira wa miguu kwa ujumla, yatashughulikiwa na Kamati za Maadili.

Tenga alisema mabadiliko hayo pia yamegusa kamati nyingine mbili, yaani Kamati ya Nidhamu na Kamati ya Uchaguzi ambayo sasa itaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Zanzibar, Hamidu Mbwezeleni

Jaji Ihema ataongoza Kamati ya Rufaa za Maadili akisaidiwa na mwanasheria mwingine mwandamizi, Victoria Makani, huku Bi. Mguto, ambaye anakuwa mwanamke wa kwanza kuongoza vyombo vya vya maamuzi ataongoza Kamati ya Maadili akisaidiwa na makamu wake Francis Kabwe, ambaye Msajili wa Mahakama Kuu.

Katika uteuzi huo, baadhi ya wajumbe wamehamishwa kutoka kamati moja hadi nyingine. Mhe. Murtaza Mangungu, ambaye awali alikuwa Kamati ya Rufaa za Uchaguzi, sasa ataingia kwenye Kamati ya Rufaa za Maadili; Kamanda Mohamed Mpinga na Prof Madundo Mtambo wamehamishwa kutoka Kamati ya Rufaa za Uchaguzi kwenda Kamati ya Maadili.
Wajumbe wapya kwenye Kamati hizo ni pamoja na kocha wa zamani wa Taifa Stars na Reli ya Morogoro, Mshindo Msolla na Kamanda Mstaafu Jamal Rwambow wanaingia kwenye Kamati ya Nidhamu; mwanasheria maarufu Evodi Mmanda anaingia kwenye Kamati ya Maadili; mwanasheria mwandamizi Mustapha Kambona ambaye anaingia kwenye Kamati ya Nidhamu; Mhe. Mohamed Misanga ambaye anaingia kwenye Kamati ya Maadili na Kanali Iddi Kipingu, ambaye anasifika kwa kuendesha soka la vijana, anaingia kwenye Kamati ya Rufaa za Nidhamu.

Pia Mwanasheria Anne Steven Marealle anakuwa mjumbe kwenye Kamati ya Rufaa za Uchaguzi; Yohane Masale (Rufaa za Uchaguzi), Allen Kasamala (Rufaa za Uchaguzi);  Francis Kiwanga ambaye pia aningia kwenye Kamati ya Rufaa za Uchaguzi na mkufunzi wa FIFA, Henry Tandau ambaye anaingia kwenye Kamati ya Rufaa za Maadili.

Kamati ya Utendaji pia imefanya mabadiliko kwenye Kamati ya Waamuzi ambako mwenyekiti Said Nassoro na katibu Charles Ndagala wa Chama cha Waamuzi wanaingia kwenye kamati hiyo kushika nafasi ya Joan Minja na Riziki Majala.

Wajumbe wa Kamati hizo ni kama ifuatavyo:
Kamati ya Rufaa za Maadili ni Jaji Steven Ihema (mwenyekiti), Victoria Makani (m/mwenyekiti), Mhe. Mohamed Misanga, Henry Tandau na Mhe. Murtaza Mangungu.

Kamati ya Maadili: Bi Jesse Mguto (mwenyekiti), Francis Kabwe (m/mwenyekiti), ACP Mohamed Mpinga, Prof. Madundo Mtambo, na Evod Mmanda.

Kamati ya Rufaa za Nidhamu: Prof. Mgongo Fimbo, Ong’wanuhama Kibuta (m/mwenyekiti), Kanali Mstaafu Idd Kipingu, Dk. Mshindo Msolla, ACP Jamal Rwambow.

Kamati ya Nidhamu: Kamanda Mstaafu Alfred Tibaigana (mwenyekiti), Mustafa Kambona (m/mwenyekiti), Azzan Zungu, Yussu Nzowa na Mohamed Msomali.

Kamati ya Rufaa za Uchaguzi: Jaji Bernard Luanda (mwenyekiti), Francis Kiwanga (m/mwenyekiti), A. Steven Semu, Yohane Masalla na Allen Kasamala.

Kamati ya Uchaguzi: Hamidu Mbwezeleni (mwenyekiti), Moses Kaluwa (m/mwenyekiti), Mustafa Siani, Hassan Dyamwale na Kitwana Manara.

Kamati ya Waamuzi: Kapteni Mstaafu Stanley Lugenge (mwenyekiti), Omar Kasinde (m/mwenyekiti), Said Nassoro, Charles Ndagala na Mohamed Nyama.


MAELEZO WAADHIMISHA MIAK 95 YA MANDELA KWA KKULA KEKI

$
0
0
 Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Maelezo, Anna Itenda akikata keki ya maadhimisho ya miaka 95 ya Rais wa Kwanza Mzawa wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ambaye  ametimika miaka 95 tangu kuzaliwa kwake. Keki hiyo iliandaliwa na Wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo. Keki hiyo ililiwa na waandishi wengi waliokuwapo Maelezo leo.

 Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Maelezo, Anna Itenda akikata keki ya maadhimisho ya miaka 95 ya Rais wa Kwanza Mzawa wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ambaye leo ametimika miaka 95 tangu kuzaliwa kwake. Keki hiyo iliandaliwa na Wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo.
 Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Maelezo, Anna Itenda akikata keki ya maadhimisho ya miaka 95 ya Rais wa Kwanza Mzawa wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ambaye leo ametimika miaka 95 tangu kuzaliwa kwake. Keki hiyo iliandaliwa na Wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo.
 Anna Itenda akimlisha keki mmoja wa Maofisa wa idara ya Habari.
Keki hiyo ya Mandela.

SAMSUNG YAJA NA E-WARANT KUEPUKA BIDHAA FEKI

$
0
0
Meneja mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Samsung,Sryvester Manyara (kushoto)  akimkabidhi simu,Mwandishi wa Gazeti la Habari Leo,Theopister Nzanzugwanko mara baada ya kushinda kwenye droo ya wanahabari kwa simu mpya ya Galaxy Star.Katikati ni Oditor wa bidhaa za Samsung,Sadic Abbas.
Meneja mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Samsung,Sryvester Manyara (kushoto)  akimkabidhi simu,Mwandishi wa Gazeti la Majira,Charles Lucas mara baada ya kushinda kwenye droo ya wanahabari kwa simu mpya ya Galaxy Star.Katikati ni Oditor wa bidhaa za Samsung,Sadic Abbas.
Meneja mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Samsung,Sryvester Manyara (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa kuchezesha droo ya kila mwezi kwa wateja walionunua bidhaa za kampuni hiyo iliyochezeshwa Dar es Salaam jana.Kutoka kushoto ni Meneja wa Tawi la Samsung Quality Center, Jafari Adam,Mwakilishi wa Bahati na sibu ya Taifa,Mrisho Milao na Oditor wa bidhaa za Samsung,Sadic Abbas.
Meneja mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Samsung,Sryvester Manyara (wa pili kulia) akimpigia simu mshindi wa TV ya Samsung nchi 32 wakati wa kucheza droo kwa wateja wa kila mwezi wa bidhaa za kampuni hiyo,ambapo  mkazi wa Dar es Saalaam, Goodluck Mumvuri alijishindia.Kutoka kulia ni Kutoka kushoto ni Meneja wa Tawi la Samsung Quality Center, Jafari Adam,Mwakilishi wa Bahati na sibu ya Taifa,Mrisho Milao na Oditor wa bidhaa za Samsung,Sadic Abbas.
Meneja mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Samsung,Sryvester Manyara (katikati)  na Oditor wa bidhaa za Samsung,Sadic Abbas wakionyesha simu mpya za Galaxy Star ambazo ziligawiwa kwa wanahabari kwa njia ya kuchezesha droo ya bahati na sibu.Kushoto ni Mwakilishi wa Bahati na sibu ya Taifa,Mrisho Milao.

CHRISTABELLA MSANGI SPECIAL NIGHT ILIVYOFANA USIKU WA KUAMKIA LEO

$
0
0
Biharusi Mtarajiwa, Christabella Msangi akipunga mkono kusalimia wageni waalikwa katika tafrija yake ya kukata na shoka iliyofanyika ukumbi wa Lion Hotel Sinza jijini Dar es Salaam usiku wa Julai 18, 2013 sambamba na Siku ya Kimataifa ya Mandela.

Chritabella anataraji kufunga ndoa Julai 20, 2013 na Bwana Norbert Kinyaia kanisa Katoliki Parokia ya Segerea jijini Dar es Salaam.

Production by: MD Digital Company - +255 755 373 999 au +255 717 002 303 WatsApp - +255 788207274.

Bi Harusi mtarajiwa Chritabella akiwa na mpambe wake Mrs Eliflorida Mbazi.
Bi harusi mtarajiwa, Christabella akikata keki yake.
 Huyu ndiye kijana Mtanashati, Norbert Kinyaiya ambaye ama kwa hakika alikuwa akimyima usingizi Bi. Christabella na akaamua kuwaambia wazazi wake yupo tayari sasa kuambatana nae na Mungu akijalia Jumamosi Julai 20, 2013 watapata Baraka za Mungu kuwa mwili mmoja na kuambatana vyema kila mmoja akiachana na wazazi wake.
 Mama Msangi akilamba picha na Binti zake.
 Mzee Msangi nae akipiga picha na vito vya thamani kutoka katika uzao wake.
 Hii sasa ndio familia kamili ya Mzee Msangi ikiwa katika picha ya pamoja.
 Kakaz na dadaz wa Bi harusi wakimwagia mafweza Christabella.
 Mambo yalipendeza hapa ni mashangazi wakipaa vyao huku wakiangalia kwa namna tafrija inavyoenda.
 wacha weeeeeeeeee...!!! Raha ya sherehe ni kucheza na kupiga menu! hapa mambo yalinoga.
 Wengine walishindwa kusimama lakini walionesha umahiri wao hapo hapo vitini walipoketi.
Waalikwa ....
Pozi zilikuwepo kupata taswira za kuvutia....
 Wageni waalikwa mbalimbali walikuwepo Ukumbini hapo...
 hapana chezea familia ya Msangi wewe.
 Christabella anaolewa uchagani na hapa akipata staili ya uchezaji wa watani zake.. kwa kushikana mikono ili wasije fanyiana ndivyo sivyo watu wakakosa nauri.
Yap! Yap huu nao ni mmoja ya uchezaji ...

BALOZI MULA MULA APOKELEWA KWA SHANGWE WASHINGTON DC

$
0
0
IMG_3118Mama Balozi Liberata Mula mula akipokelewa na mama Munanka baada ya kukutana na kujitambulisha kwa rais Obama huko White house alhamisi. Balozi Mula mula alitoa shukrani za dhati kwa mabalozi wenzake waliofika kumpongeza pamoja na Mh.EL mbunge wa Monduli na watanzania wote waliokuwapo kwa kuhudhuria hafla hiyo. Pamoja na mambo mengine alieleza pia kushangazwa kwake na kufurahishwa na mapokezi yasiyo na makuu yalio ya kifamilia zaidi aliyopewa huko White house na Rais Barack Obama na familia yake alipowasilisha hati zake za utambulisho siku ya alhamisi Julai 18.IMG_3168Mama Balozi Mula mula akiwa na mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa bunge la Tanzania na mbunge wa Monduli Edward Lowassa. IMG_3143Mchungaji Shideko akifungua kwa sala. IMG_3125Mc wa shughuli hiyo Mindi Kasiga na afisa habari ubalozini akitoa utaratibu. IMG_3164Mama Munanka akiwa na Raymond Maro. IMG_3153Mama Munanka akiitambulisha familia yake. IMG_3145 Balozi wa Rwanda nchini Marekani Prof.Mathilde Mukantabana akisikiliza kwa makini.
IMG_3178Shamis akiwa na balozi wa Burundi nchini Marekani.Kwa taarifa zaidi bofya www.sundayshomari.com

RORBERT KINYAIA NA CHRISTABELLA MSANGI WALIVYOMEREMETA

$
0
0
 Maharusi Norbert Kinyaiya na mkewe kipenzi Christabella Msangi wakiwa wenyew furaha baada ya kufunga ndoa yao takatifu leo Julai 20, 2013 katika kanisa Katoliki Parokia ya Seregerea jijini Dar es Salaam na kufuatiwa na tafrija kubwa katika ukumbi wa Maua Ubungo Extrenal.
 
Production by: MD Digital Company:
Mob: +255 373999;+255 717002303; Whatsapp:+255 788 207274
Maharusi wakicheza ngoma za kichaga.
Wapambe wa maharusi wakifuatilia matukio kwa furaha
Baadhi ya wanandugu wa maharusi wakiwa ukumbini
Mashangazi wa Biharusi wakiwa ukumbini
Ndugu wa Bwana harusi wakiwa ukumbini
Hapa ni mwendo wa kulishana ndafu
Wageni mbalimbali waalikwa.

EAC yazindua utafiti wa uelewa wa raia kuhusu mtangamano

$
0
0
Na Mwandishi wa EANA
Arusha, Julai 21,2013(EANA) -  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dk Richard Sezibera ameelezea umuhimu wa kuifanya jumuiya hiyo kuwa yenye msisimko zaidi na ya kuvutia.
‘’Jumuiya yetu (EAC) inatakiwa kuwa ya manufaa, yenye ufanisi, msisimko na ya kuvutia kuwawezesha wana Afrika Mashariki kupata kilichobora kutoka kwake,” alisema katika makao makuu ya jumuiya hiyo Jijini Arusha, Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA) linaripoti.
 Dr Sezibera alikuwa anazindua utafiti juu ya uelewa wa raia wa Afrika Mashariki kuhusu mtangamano wa Jumuiya hiyo, unaofanywa kwa ushirikiano baina ya EAC na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Ujerumani (GIZ) katika nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo.
 Halfla hiyo ya muda mfupi alihudhuriwa na Timu ya Watafiti na  maafisa waandamizi wa GIZ, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na EAC.
 Utafiti huo utakaofanywa katika nchi wanachama ambazo ni Burundi,Kenya,Rwanda, Tanzania na Uganda utachukua mwezi mmoja na unatarajiwa kumalizika Agosti 24.
 Utafuti huo utafanyika kwa njia ya madodoso ya kwenye mtandao na kwa mahojiano ya moja kwa moja katika maeneo maalum yatakayochagulia kwenye majiji na miji ya mipakani. 
 “Utafiti huo unatarajiwa kutupatia mwanga juu ya namna ya watu wanavyoiona EAC, wanaifahmu vizuri kiasi gani,jinsi wanavyozifahamu nembo za EAC na jinsi wavyoitathmini utendaji wake ,” aliongeza.
 Kwa mujibu wa taarifa ya EAC, kubwa zaidi katika utafiti huo ni kutathmini jinsi taarifa zinavyowafikia walengwa na jinsi inavyoeleweka na raia wa Afrika Mashariki na namna gani ya kuweza kusonga mbele.
 Dk Sezibera alizipongeza juhudi hizo za utafiti, akisema zipo katika uhalisia wa kutaka kuileta jumuiya hiyo karibu zaidi na walengwa.
 Mkuu wa Mawasiliano na Masuala ya Umma wa EAC, Owora Richard Othieno alisema kuwa mradi huo unalenga kubaini kama ndoto za mtangamano za wana Afrika Mashariki zinaendana na matakwa ya Mkataba wa EAC.

MAMBO YA CARNIVAL 2013 MAREKANI

$
0
0
400749_10200413813003381_332493024_nMaandamano yakiwa yamechanganya kama mdundiko.13248_10200413822683623_340761968_nMdau Charles Kaiza akiwakilisha kwenye Carnival 2013 huko Baltimore Maryland. 969928_10200413809243287_1170790526_n1069172_10200413810843327_358761529_n178998_10200413820243562_2037111565_n945719_10200413816523469_1426623641_n988632_10200413824043657_1824575750_nKwa picha zaidi bofya Sundayshomari.com

KAMPUNI YA GREEN WASTE PRO YAKABIDHI NDOO 16 ZA RANGI KATIKA SHULE YA BUNGE NA KUFANYIA USAFI MAZINGIRA YA SHULE HIYO

$
0
0
IMG_9383 
Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph (katikati) pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo na wanafunzi na walimu wakifanya usafi katika mazingira ya shule ya msingi Bunge ikiwa ni sehemu ya ratiba wanazozifanya kila mwaka za utaratibu wa kuweka mazingira ya manispaa ya Ilala katika hali ya usafi ikizingatiwa ni katika kati ya jiji la Dar es Salaam.
IMG_9402
Mkusanyaji wa Mapato wa kampuni hiyo Bw. Almachlus Rwakatale akikabidhi jumla ya ndoo 16 za rangi kwa Mkuu wa mazingira katika Shule ya Msingi ya Bunge ya jijini Dar es Salaam Mwl. Frida Madanganya. Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph.
IMG_9368
Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph na Mkusanyaji wa Mapato wa kampuni hiyo Bw. Almachlus Rwakatale wakishirikiana na uongozi wa shule ya msingi Bunge katika zoezi la upandaji miti kwenye maeneo mbalimbali yanayoizunguka shule hiyo.
IMG_9376
Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph na Mkuu wa mazingira katika Shule ya Msingi ya Bunge ya jijini Dar es Salaam Mwl. Frida Madanganya wakishirikiana kumwagilia maji moja ya miti waliyopanda katika shule hiyo kuhamasisha utunzaji wa mazingira.
IMG_9380
Zoezi la usafi likiendelea kwa kushirikiana na Walimu pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
IMG_9390
Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na ratiba wanazozifanya kila mwaka za utaratibu wa kuweka mazingira ya manispaa ya Ilala katika hali ya usafi ikizingatiwa ni katikati ya jiji la Dar es Salaam na safari hii wametoa ndoo 16 za rangi katika Shule msingi Bunge.

RAIS DK.SHEIN, AFUTARISHA CHOKOCHO PEMBA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) pamoja na Viongozi na wananchi na  waumini wa Dini ya Kiislamu wa Chokocho jimbo la Mkanyageni Mkoa wa  Kusini Pemba,wakijumuika katika chakula cha futari aliyoiandaa katika  Kijiji hicho jana
 Baadhi ya Wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa  Chokocho Jimbo la Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika chakula cha futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Skuli ya Chokocho jana.
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,(katikati)  akijumuika na Wanawake wa Chokocho Jimbo la Mkanyageni Mkoa wa Kusini  Pemba, katika futari aliyowaalika viwanja vya Skuli ya Chokocho  jana.(kushoto) Mkuu wa wilaya ya Chake chake Mwanajuma Majid
 Baadhi ya akina mama wa Chokocho Jimbo la Mkanyageni Mkoa  wa Kusini Pemba, wakiwa katika chakula cha Futari katika Mwezi mtukufu  wa Ramadhan,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa Skuli ya  Chokocho Pemba jana.
Ustadh Yussuf Ali, akitoa neon la shukurani kwa niaba  ya Wananchi na Waislamu wa Chokocho Jimbo la Mkanyageni jana,mbele ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali  Mohamed Shein,baada ya futari aliyowaandalia katika viwanja vya Skuli  ya Chokocho jana.

Mashindano ya kusoma Quran tukufu kitaifa yamalizika

$
0
0

Msomaji wa Quran tukufu katika mashindano ya kitaifa, Seif Salim Said ambaye ni mremavu wa macho akisoma wakati wa fainali zake leo.

Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya kitaifa ya kuhifadhi Quran tukufu yamemalizika leo, huku walemavu wa viungo wakiwa kivutio cha aina yake, kwa kuonyesha maajabu.
Walioshangiliwa na hata kuwatoa machozi watazamaji walikuwa ni Ummy Kuluthumu Swaleh Saidi kutoka Pemba, ambaye hakuwa na miguu wala mikono pamoja na  Seif Salim Said ambaye ni mlemavu wa kuona na kusikia, waliweza kusoma vizuri bila kubabaika huku wakiwapita hata wale waliokuwa na viungo kamili.
 
Mashindano hayo yalimalizika jana Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo yalihusisha washiriki 72 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
 
Walemavu hao pamoja na wengine sita, walizawadiwa fedha taslim  pamoja na fimbo za kuwawezesha kutembea.
 
Nafasi ya mshindi wa kwanza kwa wavulana ilikwenda kwa Abdul Hamid na msichana alikuwa Suria Ally Bakari ambao kwa pamoja walipewa  Bajaji na fedha taslim sh. 500,000.
 
Washindi wa mashindano hayo yaliyoandaliwa na Eshe Sururu Foundation, yaligawanywa katika makundi matano, kwa upande wanawake na wanaume, huku washindi  wengine wakiondoka na pikipiki, baiskeli, vyereheni na fedha taslim.
 
Katibu wa kamati ya maandalizi, Issah Ramadhan Mohamed alisema kuwa madhumuni ya kuandaa mashindano hayo ni kuibua ari kwa vijana wa kiislam waweze kusoma Quran Tukufu  kwa mustakabali wa maisha mema.
 
Alisema yalishirikisha wasichana 38 na wavulana 34 ambapo kila upande alitoka mshindi wa kwanza hadi wa tatu na yaligawanywa kwa ngazi tano ikiwemo kuhifadhi Juzuu 20,10, tano na tatu.

DK.THOMAS LUTUO NA NURU LWAMBANO WALIVYO IAGA KLABU YA MAKAPERA TANZANIA

$
0
0

Maharusi Dk. Thomas Lutuo na Nuru Lwambano wakiwa ni wenye furaha dakika chache baada ya kuvishana pete za ndoa katika Kanisa Katoliki Parokia ya St. Peters Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Ndoa hiyo ilifungwa Julai 20, 2013 na Paroko Msaidizi wa Kanisa Hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tumaini Media, Father. Paulo Haulo na baade maharusi hao waliungana n wanafamilia katika tafrija iliyofanyika Mwika Hall Sinza. 

Production: MD Digital Company:- Mob: +255 373 999; +255 717002303 Whatsapp: +255 788 207274.


 Bi Harusi akiwa na msimamizi wake kabla ya kwenda kanisani.
 Maharusi wakisubiri kufungishwa ndoa yao takatifu.
 Wasimamizi wakiwa kanisani
 Wazazi pamoja na ndugu jamaa na marafiki wakiwa kanisani
 Ndugu Jamaa na marafiki wakiwa Kanisani wakati wa Ibada ya Ndoa
 Nuru akimvisha Pete Mumewe Dk. Thomas
 Father Paulo Haule akimpa Sakrament Bi Harusi Nuru.
 Father Paulo Haule akimlisha Sakrament takatifu Dk. Thomas
 Wanakwaya wakiwa Kanisani wakiimba wakati wa Ibada ya Ndoa.
  Maharusi wakuiweka saini vyeti vyao vya ndoa.
 Jamani tumehitimu urafiki, uchumba na sasa ni WANANDOA... na hivi ndio vyeti vyeti vya kuthibitisha hilo.
 Wapambe wakiingia ukumbi wa Mwika Sinza Makaburini tayari kwa kuanza tafrija.
 Maharusi hao nao wakiingia ukumbini
 Wanafamilia walijipanga kuwapokea kwa shangwe.
 Picha ya pamoja ya Kamati ya Maandalizi.
 Mwenyekiti wa Kamati akikabidhi zawadi ambayo ni Stakabadhi ya kuweka hela Benki zaidi ya Milioni 2.
 Wakisubiri maelekezo ya MC wa Shughuli hiyo Godwin Gondwe
 Bwana Harusi Dk. Thomas akitambulisha mkewe na familia yake kwa ujumla.
 Bi Harusi Nuru akitambulisha familia yake
 Maharusi wakikata keki
 Ulishanaji wa keki ulikuwa ni wa staili yao. Na licha ya kuwa Bi harusi alikuwa mfupi lakini zoezi lilipendeza sana.
 Dk. Thomas akikabidhi keki kwa wakwe zake...
 Ni heshima tu na hakuna la ziada... Bi harusi Nuru akikabidhi keki kwa wakwe zake.
 Mvinyo wa kupongezana ulifunguliwa na Kanali Mstaafu wa Jeshi.
..... Mungu atutangulie katika ndoa yetu hii
 heri na fanaka ilitoka kila kona
 Watu weeeeeeeee.... dada huyo ameolewa dada huyo...ameolewa...
 Mpango mzima na hii ndio sherehe ya ndoa
 Maharusi wakiweka salio la uhai sawa.
 Ilikuwa ni furaha hadi raha kwa maharusi.
 Zawadi na Pongezi zilitolewa kwa maharusi.
 Wazazi nao walitoa pongezi
 Wazazi walipewa zawadi kwa malezi mema...
Hapo sasa... hii ngoma we acha tu KWAITO ilipigwa vilivyo...

RAIS KIKWETE NA MAKAMU WAKE WAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA ASKARI WALIOKUFA DARFUR

$
0
0
 Majeneza yenye miili yakiwa eneo la tukio tayari kuagwa.
 Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Rais na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Makamu na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, akiwafariji wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnard Mengi, akiwa na baadhi ya viongozi, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Majeneza yenye miili ya Askari wa kulinda Amani, wa jeshi la Ulinzi la Tanzania, waliokufa huko Darfur Julai 13, 2013, wakati wa zoezi la kuagwa miili hiyo lililofanyika leo kwenye Uwanja wa Wizara ya Ulinzi, Upanga jijini Dar.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Bilal, na viongozi wengine wakiwa katika shughuli hiyo ya kuagwa miili ya askari hao leo kwenye Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga Dar es Salaam. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakati wakiwa katika shughuli hiyo ya kuaga miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla. Kulia ni Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa zoezi hilo.
 Mkuu wa Majeshi,Jenerali Davis Mwamunyange, akizungumza wakati wa zoezi hilo.
 Baadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa miili hiyo.
 Baadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa miili hiyo.
 Baadhi ya Askari pia wakiwa na nyuso za huzuni.PICHA NA OMR.

MSHINDI WA KWANZA WA NYUMBA YA YATOSHA KUPATIKANA MWISHO WA MWEZI HUU

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa shirika la nyumba la Taifa Bw, Yahaya Charahani akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati ambapo waandishi hao walitembelea eneo la kibada wilaya ya Temeke kujionea Nyumba 3 zinazoshindaniwa katika promosheni ya Airtel Yatosha. Nyumba hizi zimenunuliwa na Airtel toka shirika la nyumba la taifa kwaajili ya promosheni ya AIRTEL shinda Nyumba.kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati ambapo waandishi hao walitembelea eneo la kibada wilaya ya Temeke kujionea Nyumba 3 zinazoshindaniwa katika promosheni ya Airtel Yatosha. Nyumba hizi zimenunuliwa na Airtel toka shirika la nyumba la taifa kwaajili ya promosheni ya AIRTEL shinda Nyumba 3.
Mwishoni mwa wiki hii Shirika la nyumba la taifa limewathibitishia watanzania kwamba tayari nyumba tatu zinazoshindaniwa katika promosheni ya airtel yatosha zimekamilika na tayari mafundi wanafanya matengenezo ya mwisho tayari kwa kukabidhiwa kwa washindi hao.
**********
Afisa Uhusiano wa NHC YAHAYA CHARAHANI amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati ambapo wanahabari toka vyombo mbali mbali walitembelea nyumba hizo kujionea jinsi mradi unavyokwenda “nyumba hizi tatu zenye thaman ya shilingi milioni 194 zimekamilika na pindi washindi watakapotangazwa wataweza kuhamia katika nyumba hizi mara moja tu.

Amesema nyumba hizo ambazo ni za kisasa zitakidhi mahitaji ya wengi kwani ujenzi wake umezingatia mahitaji ya familia kubwa. Nyumba hizi zina vyumba vitatu vya kulala, jiko, sebule nzuri pamoja na sehemu ya nje iliyonakishiwa kwa umakini ili kuipa nyumba mvuto wa hali ya juu. Aliongeza bw, CHARAHANI Pia alibainisha kuwa wateja wa kampuni ya airtel wanaweza kuzitembelea nyumba hizo na kujionea wenyewe kiwango cha ubora wa nyumba hizo.

“Hizi nyumba ziko wilaya ya Temeke eneo la kibada karibu kabisa na Tuangoma ambapo hadi kufika katika nyumba hizi ni umbali wa kilomita 2 tu kutoka kituo cha basi kilipo, eneo ambalo linafikika na linamakazi mzuri sana” alimalizia kwa kusema Bw, CHARAHANI.

Nae Meneja Uhusiano wa Airtel JACKSON MMBANDO amewataka watanzania kuendelea kutumia mtandao wa airtel hususani huduma ya yatosha kwa kupiga *149*99# na kuchagua vifurushi vinavyowatosha ili kujihakikishia nafasi ya kushinda nyumba hizo.

Amesema airtel imedhamilia kutatua matatizo ya wateja wake kwa kutoa huduma nafuu na bora kuliko mtandao wowote lakini pia promosheni hiyo ya YATOSHA inalenga kubadilisha maisha ya watanzania hasa wale wanaotumia mtandao wa airtel Amesema katika promosheni hiyo jumla ya shilling million 284 zitatumika kuwazadia wateja wa kampuni hiyo ambapo milioni 194 zitanunua nymba hizo 3 toka shirika la nyumba na kiasi kinachobaki kwa siku 90 Airtel itatoa milioni moja kwa mshindi mmoja kila siku.

KAMPUNI YA ISERE SPORTS YASAIDIA VIFAA TIMU YA FRESH NIGA YA KILWA MASOKO

$
0
0

Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya Isere Sports inayoshuhulika na uagizaji na uuzaji wa vifaa vya michezo,Abbas Isere (kulia) akimkabidhi jezi Katibu Mipango wa timu ya Fresh Niga ya Kilwa Masoko ,Maulid Mtika maarufu Milulu zenye thamani ya Sh. 350,000.
 
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Vifaa vya michezo, Isere Sports imetoa jezi seti moja yenye thamani ya sh. 350,000 kwa timu ya Fresh Niga ya Kilwa Masoko inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu wilaya ya Kilwa.

 Katibu Mipango wa timu ya Fresh Niga, Maulid Mtika akipokea jezi hizo jana alisema msaada huo ni mfano wa kuigwa na wafanyabiashara wengine wenye uwezo wa kusaidia kuibua vipaji vya vijana kwenye soka.

Mtika ambaye ni maarufu kwa jina la Milulu alisema imefika wakati Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litafute njia ili lishuke mpaka ngazi ya wilaya kujua matatizo yanawakabili timu ili kutafuta vipaji vya wachezaji watakaochukua nafasi ya waliopo Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).

'Tunao vijana wenye vipaji vya kucheza soka kufikia ngazi ya timu ya taifa, kinachowanyima nafasi ya kuonekana ni vifaa vya michezo tunaomba TFF ishuke mpaka ngazi ya wilaya kuwasaidia vijana kukuza vipaji.

Alitoa wito kwa wadau wa michezo kujitokeza kusaidia timu ambazo hazina wafadhili lakini kuna vijana ambao wako tayari kuonesha vipaji vyao.

 Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Isere alisema jana kuwa msaada huo ameutoa ili kukuza vipaji vya soka katika wilaya hiyo ambao wanahitaji misaada kama hiyo ili kuendeleza vipaji.

MFUMO MPYA WA USAJILI WA VIZAZI NA VIFO KUPITIA MKAKATI WA USAJILI WA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO WAZINDULIWA JIJINI MBEYA LEO

$
0
0
Mgeni Rasmi,  Naibu Waziri wa katiba na Sheria,Mh, Angellah Kairuki akimkabidhi mmoja wa akina mama aliyejitambulisha kwa jina la Fides Samson akikabidhiwa cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake mwenye umri chini ya miaka 5,mara baada ya kuzindua mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,mkoani Mbeya.Mpango huo umefadhiriwa na mashirika mbalimbali likwemo shirika la UNICEF,DFTDA (iliyokuwa CIDA Canada zamani) pamoja na Shirika la Wafanyakazi la kujitolea (VSO).
 
 
Picha ya pamoja mara baad ya  kuuzinduliwa mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 bure jijini Mbeya,hafla hiyo inayoratibiwa na RITA,imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,mkoani Mbeya.Mpango huo umefadhiriwa na mashirika mbalimbali likwemo shirika la UNICEF,DFTDA (iliyokuwa CIDA Canada zamani) pamoja na Shirika la Wafanyakazi la kujitolea (VSO).
 Naibu Waziri wa katiba na Sheria,Mh, Angellah Kairuki akizindua mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,mkoani Mbeya,kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Philip Saliboko na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini,Dkt.Norman Sigalla na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya Ushauri RITA,Bwa.Vincent Mrisho na wageni mbambali wakilishuhudia tukio hilo adhimu kabisa.Shughuli nzima inaratibiwa na RITA.
 Baadhi ya akina mama wakiwa na vyeti vya kuzawaliwa vya watoto wao wanye zaidi ya wiki mbili tangu kuzaliwa kwao,mara baada ya kabidhiwa leo na Mgeni Rasmi,  Naibu Waziri wa katiba na Sheria,Mh, Angellah Kairuki mara baada ya kuuzindua mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 bure jijini Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,mkoani Mbeya.Mpango huo umefadhiriwa na mashirika mbalimbali likwemo shirika la UNICEF,DFTDA (iliyokuwa CIDA Canada zamani) pamoja na Shirika la Wafanyakazi la kujitolea (VSO).
 Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa katiba na Sheria,Mh, Angellah Kairuki akizungumza mbele ya wakazi wa mji wa Mbeya (hawapo pichani) mapema leo wakati alipokuwa akizindua mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,jijini Mbeya.
 Baadhi ya Wakazi wa jijini Mbeya wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa Ruanda Nzovwe mapema leo wakati  wa uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,jijini Mbeya.
Mwakilishi Mkazi wa shirika la UNICEF hapa nchini,Dkt.Jamal Gulaid  Mgeni akizungumza mbele ya wakazi wa mji wa Mbeya (hawapo pichani) mapema leo wakati alipokuwa akizindua mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,jijini Mbeya.
 Baadhi ya akina mama na watoto wao wakifuatilia kwa makini yalikuwa yakijiri kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,hafla hiyo inayoratibiwa na RITA imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,jijini Mbeya.
 Baadhi ya  Wageni waalikwa na wawakilishi kutoka mashirika mbalimbali ya Kimataifa wakifuatilia  uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,jijini Mbeya.
 Mwenyekiti wa bodi ya Ushauri RITA,Bwa.Vincent Mrisho akifafanua jambo kwa Baadhi ya Wakazi wa jijini la Mbeya  (hawapo pichani) kuhusiana na uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,jijini Mbeya.Aidha Bwa.Mrisho aliongeza kuwa mkakati huo hauwalengi watoto walio chini ya miaka mitano tu bali ni sehemu ya mfumo mpya wenye lengo la kuwapa nafasi wananchi  walio zaidi ya miaka mitano kujisajili na kupata vyeti vya kuzaliwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini,Dkt.Norman Sigalla (pichani kati) akiwa na Mgeni Rasmi pichani kushoto,Naibu Waziri wa katiba na Sheria,Mh, Angellah Kairuki mara alipokuwa akiwasili kwenye uwanja wa Ruanda Nzovwe jijini Mbeya kwa ajili ya kuuzindua mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 bure jijini Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,mkoani Mbeya.Mpango huo umefadhiriwa na mashirika mbalimbali likwemo shirika la UNICEF,DFTDA (iliyokuwa CIDA Canada zamani) pamoja na Shirika la Wafanyakazi la kujitolea (VSO).Picha na Michuzi Media Group-Mbeya. 

BALOZI LUMBANGA AWA MWENYEKITI WA BODI YA PPRA

$
0
0
NA JENNIFER CHAMILA- MAELEZO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amemteua Balozi Matern Lumbanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Manunuzi Serikalini ( PPRA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari  na  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya PPRA   Laurent Shirima imeeleza kwamba uteuzi huo , umeanza  rasmi kuanzia  Juni 20 ,mwaka huu ambapo Balozi Lumbanga amechukua  nafasi ya Dk.  Enos Bukuku aliyemaliza muda wake katika uongozi huo.
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Balozi Lumbanga ni mchumi kitaaluma,ana Shahada ya kwanza ya Uchumi ambayo ameipata katika Chuo Kikuu cha Dares salaam(UDSM).
Pia ana Shahada ya Uzamili pamoja na Shahada ya Uzamivu katika masuala ya Mahusiano ya Kimataifa taaluma aliyoipata  chuo cha Geneva School of Dipmacy and International Relations, Switzerland.
Balozi Lumbanga ameitumikia Serikali ya Tanzania katika nyazifa mbalimbali tangu mwaka 1972,mwaka 1995 aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi nafasi alioishika hadi mwaka 2006 alipoteuliwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) nchini Geneva.Amestaafu utumishi wa umma  Julai mwaka jana (2012).
 
Balozi Lumbanga amekuwa Mwenyekiti wa tatu wa bodi  ya PPRA tangu ilipoanzishwa mwaka 2005 ambapo Mwenyekiti wa kwanza alikuwa Bw.Philemon Luhajo na kufuatiwa na Dk.Bukuku.

BARCLAYS BANK TANZANIA YAIPATIA MILIONI 120 TAASISI YA NKWAMIRA KUSAIDIA VIJANA

$
0
0
 Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamaniya shilingi Milioni 120 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Nkwamira, Nooreen Mazalla (kulia) kwaajili ya kusaidia vijana waishio mtaani bila elimu au kazi, makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Dar es salaam jana. Wengine pichani ni Meneja Miradi wa Nkwamira, Alice Mwiru pamoja na Mtaalam wa masula ya Ufundi, David Bavo.

 Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Kavishe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi  hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 120 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Nkwamira Sustainable life Trust, Nooreen Mazalla (kulia) kwaajili ya kusaidia vijana waishio mtaani bila elimu au kazi. Kushoto ni Meneja Miradi wa Nkwamira, Alice Mwiru .
 Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Kavishe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya mpango huo ambao utawashirikisha vijana 60 kutoka Dar es Salaam na 40 kutoka Morogoro.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Nkwamira Sustainable life Trust, Nooreen Mazalla akieleza kuwa msaada huo kutoka Barclays Benki Tanzania kwaajili ya kuendeleza vijana ni mkubwa na utaenda mbali sana kuwasaidia vijana hao, na kuahidi kuuendeleza na kupata vijana hao hadi watakapo patikana washindi wawili. 
Barclays kupitia mpango wa kusaidia jamii unangalia vijana waishio mitaani wasiokuwa na uwezo wa kujiendeleza kielimu au kupata kazi kutokana na kutokuwa na elimu.  Aidha Noreen Mazalla amesema kuwa vijana watakaofaidika katika mpango huo ni wale walio na umri kati ya miaka 15 - 35 ambao watapata nafasi ya kujiendele\za kwa kuwapatia mafunzo ambayo yatagusa mada za kuendesha biashara zao pamoja na mafunzo ya kifedha.

KAULI YA BALOZI LIBERATA MULAMULA

$
0
0

Na Swahili TV
Mhe. Balozi Liberata Mulamula ametoa kauli ya kuwaunganisha watanzania wote, amesema kamwe hatoruhusu tofauti na makundi katika jamii za kitanzania. Ameyazungumza hayo katika papo kwa hapo ya Swahili TV.

AGONGWA NA GARI NA KUFA PAPO HAPO DAR ES SALAAM HII LEO.

$
0
0
 Mkazi wa Dar es Salaam ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja leo amefikwa na umauti baada ya kugongwa na gari aina ya Nissan ambalo linafanya shughuli za kubeba abiria kati ya Gongo la Mboto na Kariakoo jijini Dar es Salaam namba za usajili T 288 AZB na namba ya njia ni S 264D.
 
Kwa mujibu wa mashuhuda wameiambia Father Kidevu Blog kuwa, marehemu aligongwa na gari wakati akijaribu kuvuka barabara ya Nyerere eneo la Mtava karibu na Quality Centre leo asubuhi.
 Askari Polisi wakijadiliana jambo wakati wakifanya taratibu za kuondoa mwili wa marehemu eneo la tukio.
 Daladala hilo T 288AZB ambalo limemgonga mkazi huyo ambaye baadhi ya watu walitambua kuwa anaishi maeneo ya Buguruni Relini.
 Askari akiuliza endapo marehemu huyo aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 45 na 50 anatambulika na yeyote.
Mwili wa marehemu ukiondolewa eneo la tukio.
Viewing all 10864 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>