Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10864 articles
Browse latest View live

BLANCA MALITI AWINDA NA KUJISHINDIA MILIONI MOJA YA SERENGETO LAGER

$
0
0
Mshindi wa shilingi milioni moja wa shindani la Winda na Ushinde Bi. Blanca Maliti (katikati) mkazi wa mjini Morogoro akikabidhiwa mfano wa hundi na Meneja wa Mauzo wa Serengeti Breweries kanda ya kati Octavian Migire, kushoto kwake ni mama mdogo wa Blanca, Mwalimu Theresia Masashua kutoka Turiani, Bianca ni mshindi wa tatu kujishindia shilingi milioni moja katika promosheni hiyo ya Winda na Ushinde inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.
Mshindi wa shilingi milioni moja wa shindani la Winda na Ushinde Bi. Blanca Maliti (katikati) mkazi wa mjini Morogoro akifurahia mfano wa hundi pamoja na familia yake baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Mauzo wa Serengeti Breweries kanda ya kati Octavian Migire.
Mshindi wa shilingi milioni moja wa shindani la Winda na Ushinde Bi. Blanca Maliti (katikati) mkazi wa mjini Morogoro akifurahia pamoja na familia yake baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Mauzo wa Serengeti Breweries kanda ya kati Octavian Migire, kushoto kwake ni mama mdogo wa Blanca, Mwalimu Theresia Masashua kutoka Turiani, na Dada yake. Bianca ni mshindi wa tatu kujishindia shilingi milioni moja katika promosheni hiyo ya Winda na Ushinde inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.
Mshindi wa shilingi milioni moja wa shindani la Winda na Ushinde Bi. Blanca Maliti (katikati) mkazi wa mjini Morogoro akifurahia pamoja na familia yake baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Mauzo wa Serengeti Breweries kanda ya kati Octavian Migire, kushoto kwake ni mama mdogo wa Blanca, Mwalimu Theresia Masashua kutoka Turiani, na Dada yake. Bianca ni mshindi wa tatu kujishindia shilingi milioni moja katika promosheni hiyo ya Winda na Ushinde inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.

Airtel na UNESCO kuzindua radio jamii Karagwe Bukoba

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali UNESCO wanatarajia kuzindua radio jamii katika wilaya ya Karagwe mkoani Bukoba mwishoni mwa wiki hii
 
Uzinduzi huo unafatia ushirikiano kati ya Airtel na UNESCO katika mradi wa kusadia jamii na kufikisha mawasiliano ya radio sehemu ambazo zina changamoto za huduma za mawasiliano ya radio
 
Akiongea kuhusu uzinduzi huo ya Airtel Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano alisema  “ Mradi huu wa radio za jamii tunaufanya kwa kushirikiana na UNESCO kwa lengo la kuendeleza na kuboresha huduma za mawasiliano na kuwafikia wananchi wengi zaidi hususani wa maeneo ya vijijini.
 
Tumejipanga kufanya uzinduzi wa ushirikiano wetu na UNESCO na Radio ya FADECO Karagwe utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 19 julai 2013
 
Mgeni rasmi atakuwa ni mkuu wa mkoa wa Bukoba LutenFabian Masawe , pamoja na yeye tutakuwa na viongozi mbalimbali wa serikali watakaohuduria sherehe za uzinduzi huo
 
Tunaamii kwa kupitia radio hizi jamii itabadilika na kupata elimu zitakazosaidia kuleta maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu wananchi wengi wana pata habari mbalimbali zikiwemo za kibiashara, uchumi, kijamii na kisiasa.
 
Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Amin alisema “tunayo miradi mingi ya kusaidia jamii kujikwamua na hali ngumu za uchumi, kupata elimu bora, uongozi bora , kuachana na mila potofu na mengine mengi.  kwa kupitia mradi huu wa Radio tunaoshirikiana na wenzetu wa Airtel tumeshaona matunda na mafanikio mengi mpaka sasa, lengo letu ni kuhakikisha tunatatua changamoto zilizopo za kuwapata wananchi habari za ndani na nje ya nchi na kuwaunganisha na sehemu nyingine za nchi na Dunia.
 
Akiongea kuhusu uzinduzi wa Radio jamii Karagwe Mkurugenzi wa Radio ya FADECO Bw Joseph Sekiku alisema “Mpaka sasa vifaa na mitambo ya mawasiliano ya kisasa imeshafungwa na tuko katika hatua ya majaribio ambapo tumeshuhudia ufanisi mkubwa zaidi kulinganisha na awali kwani tumeweza kutanua wigo na kufikia vijiji vingi zaidi”.
 
nawashukuru sana Airtel na UNESCO kwa kutufikia na kuwawezesha kuendesha radio yetu kwa ufanisi zaidi. Radio ya FADECO ilizinduliwa toka mwaka 2007  na kuanza  kurusha matangazo yetu rasmi kwa vijiji vya karibu, changamoto tuliyokuwa nayo ni pamoja na kurusha matangazo yetu katika vijiji vilivyo mbali zaidi kutoka hapa radioni. Kwa kupitia mradi huu tumeweaza kuona mfanikio makubwa tayari, 
 
“Tunagemea kuzindua rasmi ushirikiano wetu na UNESCO pamoja na Airtel siku Ijumaa hapa Karagwe. Nachukua fulsa kuwaalika wananchi wadau wa sekta za mawasiliano, viongozi mbalimbali kuhudhuria halfa hii ya uzinduzi na kusherehekea pamoja nasi mafanikio haya” aliongeza Sekiku
 
Mradi wa radio jamii umeanzishwa mwaka jana 2012 radio zaidi ya 10 katika maeneo mbalimbali ya nchi zitafaidika na mradi huu kama ilivyo katika Radio hii ya FADECO iliyopo wilaya ya Karagwe Bukoba

NISHATI KUINUA UCHUMI WA TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifafanua jambo wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba kiweka saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia, waliosimama kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa China hapa nchini Balozi Lu Youging na Rais wa Kampuni ya China Power Investment,  Lu Qizhou.
Mkurugenzi wa Tanesco, Felchesmi Mramba akibadilishana hati na Mwenyekiti wa Kampuni ya Uwekezaji ya CPI, Lu Quizhou baada ya kuingia mkataba wa uwekezaji wa nishati ya Umeme kutoka China. 
***********
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameendelea kusisitiza na kuwataka wakazi wa mkoa wa Mtwara kuelewa kuwa Gesi iliyopatikana katika mkoa huo ni kwa ajili ya Watanzania wote.
 
Akizungumza wakati akiwekeana makubaliano na kampuni ya uwekezaji wa nishati ya umeme kutoka China (CPI), Profesa Muhongo alisema kuwa hata kama wakazi wa mkoa huo watashindwa kuridhia uwekezaji wa nishati hiyo lakini gesi hiyo ni kwa maendeleo ya Watanzania wote.
 
Profesa Muhongo alisema kuwa makundi yanayopinga matumizi ya gesi hiyo yanapaswa kuweka hadharani mikakati yao kuliko wanavyofanya sasa kwa kupinga pasipo kutoa mipango yao.
 
Alisema inapaswa kufika mahali Watanzania wakagawanywa katika makundi mawili ikiwemo lile linalotaka maendeleo na linalopinga ili waweze kutengewa maeneo.
 
“Hatuwezi kuondoa umaskini kama tusipotumia gesi na raslimali tulizo nazo na hata hili tatizo linalolalamikiwa sasa la vijana kukosa ajira litapata ufumbuzi kama tutaweza kupanua uchumi wetu,” alisema.
 
Alisema kuwa Watanzania wanapaswa waache kulazimisha kufuata mawazo ya kupotosha.
 
“Tunataka uchumi ukue, tuwe na umeme wa uhakika na hata bajeti yetu kuondoka katika kuongeza bei katika bidhaa ndogo ndogo ili linaweza kufanikiwa kama tukiwa na umeme wa uhakika na kutumia gesi yetu,” alisema.
 
Aidha katika makubaliano hayo, Serikali imeingia makubaliano na kampuni hiyo kwa kuzalisha umeme wa megawati 600 katika eneo la Kinyerezi namba 3 lililopo jijini Dar es Salaam.
 
Alisema kuwa umeme huo utatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ifikapo mwaka 2014 mwishoni wataweza kuuza megawati 500 kwa nchi za nje zenye uhitaji wa nishati hiyo.
 
“Kupitia uzalishaji huo tunategemea mwaka 2016 tutaweza kuzalisha megawati 1500 za nyongeza  hatua hiyo itaweza kubadilisha uchumi wetu na kuwa na bajeti yenye uhakika zaidi,” alisema.

Profesa Muhongo alisema kuwa makubaliano hayo ambayo yanafanyika na Shirika la Umeme Nchi (Tanesco) na kampuni hiyo ya CPI utaweza kugharimu kiasi cha Dola milioni 300 hadi kukamilika.

RADIO 5 FM YAPONGEZA WAFANYAKAZI BORA

$
0
0
Mkurugenzi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis (kulia) akimkabidhi Pikipiki Mfanyakazi Bora wa Kituo hicho Semiyo Sonyo.
 **********
Mkurugenzi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis Amewataka watangazaji na wanahabari wanaofanya kazi katika vituo vya Radio na Televisheni hapa nchini kuzingatia weledi wa kitaaluma wanapofanya shughuli zao za kila siku ili kusaidia jamii ya kitanzania kukabiliana na changamoto katika kipindi hiki ambacho dunia inabebwa na utandawazi. 
Akikabidhi pikipiki kwa mtangazaji bora wa kipindi cha usiku cha LOVE CUTTS kinacho rushwa Radio 5 katika Hafla fupi iliyofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi Robert amesema vyombo vya habari vya kielectonic yaani Televisheni,Radio, na mitandao ya kijamii vinafikia watu kwa haraka zaidi na kwa unafuu wa gharama kuliko machapisho na kwamba vikitumika bila miiko ,weledi na kuzingatia kanuni za kitaaluma vinaweza kuwa sehemu ya tatizo badala ya kuwa vyombo vya kusukuma kasi ya maendeleo.
 
Katika tafrija hiyo Mtangazaji Semio Sonyo amekabidhiwa pikipiki ikiwa ni sehemu ya motisha zinazo tolewa na kituo cha Radio five kwa wafanyakazi
wake waofanya vizuri katika majukumu yao.
Semio Sonyo akijaribu pikipiki aliyokabidhiwa na mkurugenzi wa Tan Communication Media,bwana Robert Francis

RAIS JK AFUTURU NA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasabahi baadhi ya watoto  yatima walioshiriki katika futari aliyoiandaa ikulu jijini Dar es Salaam leo.Watot yatima wanaolelewa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam walihudhuria futari hiyo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasabahi baadhi ya watoto  yatima walioshiriki katika futari aliyoiandaa ikulu jijini Dar es Salaam leo.Watot yatima wanaolelewa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam walihudhuria futari hiyo.
 Baadhi ya watoto hao wakihudumiwa futari.
 Baadhi ya watoto hao wakihudumiwa futari.
 Baadhi ya watoto  yatima wakishiriki katika futari iliyoandaliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni.
Baadhi ya watoto  yatima wakishiriki katika futari iliyoandaliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni.

MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZA WATANZANIA WAISHIO ABUJA NIGERIA, AONDOKA LEO KUREJEA TANZANIA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Watanzani ya waishio mjini Abuja, wakati alipokutana nao katika Makazi ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Nigeria, jana Julai 16, 2013 na kufanya nao mazungumzo. Makamu ameondoka leo mjini Abuja kurejea nchini Tanzania, baada ya kuhudhuria Mkutano wa 12 wa siku mbili wa Afrika uliokuwa ukijadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, Julai 15-16, 2013 mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika. Kushoto kwake ni mkewe, Mama Asha Bilal.
 Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, aliyemaliza muda wake, Siwajibu Baraka Siwajibu, akiwatambulisha baadhi ya Watanzania kwa makamu wa Rais, wakati alipofika kuzungumza nao katika Makazi ya Balozi wa Tanzania, Abuja Nigeria jana Julai 16, 2013. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal, na kutoka (Kulia) ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Mahadhi na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Fatma Rajabu.
  Baadhi ya watanzania waishio Abuja, wakimsikiliza Makamu, Dkt. Bilal, (hayupo pichani) wakati akizungumza nao.
  Baadhi ya watanzania waishio Abuja, wakimsikiliza Makamu, Dkt. Bilal, (hayupo pichani) wakati akizungumza nao.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Fatma Rajabu na Kaimu Balozi wa Tanzania, nchini Nigeria, aliyemaliza muda wake, Siwajibu Baraka Siwajibu, wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya watanzania waishio Abuja, baada ya makamu kufanya nao mazungumzo jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Fatma Rajabu, wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya watanzania waishio Abuja, baada ya makamu kufanya nao mazungumzo jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya watanzania waishio Abuja, baada ya makamu kufanya nao mazungumzo jana. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee,Salu Salatu, ambaye ni raia wa Nigeria aliyefanya kazi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria kwa muda wa Miaka 25 hadi sasa, baada ya Makamu kuzungumza na Watanzania waishio Abuja jana Julai 16, 2013. Makamu ameondoka leo mjini Abuja kurejea Tanzania baada ya kuhudhuria Mkutano wa 12 wa siku mbili wa Afrika uliokuwa ukijadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, Julai 15-16, 2013 mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.

DEAL MOJA

$
0
0
Fursa ingine kwa watu wote WANUNUZI NA WAUZAJI DUNIANI
Ni website ya kisasa yenye sifa za kimataifa www.dealmoja.com Yaap ni DEAL MOJA katika wavuti hii kuna mengi waeza fanya bila GHARAMA YOYOTEdealmoja_logogg
· TANGAZA BIASHARA YAKO KATIKA Category ya Business directory
· UZA AU NUNUA bidhaa kupitia wavuti hii
· KWA WALE WENYE BIASHARA AU HUDUMA ZA KUPANGISHA au KUUZA – Unaweza Tangaza kupitia wavuti hii BUREEEEEEE
Waweza jiuliza kwanini tunatumia lugha ya KIINGEREZA katika wavuti hii…. Sababu kubwa ni kuwa tunataka kwenda mbali … na hii itasaidia watanzania kufanya biashara na watu wote DUNIANI lugha kuu ikiwa ni KIINGEREZA.
Ni rahisi sana unajisajili kisha unaanza kurusha bidhaa zako katika website hii ya kisasa naya uhakika kabisa.
WAWEZA POST BIDHAA/HUDUMA
KUPITIA SIMU YAKO.

MAJEBELE KUZIKWA KESHO MAKABURI YA KINONDONI

$
0
0
MWILI  wa mwandishi mkongwe  David Michael Majebelle.  aliyefariki alfajiri ya Jumapili iliyopita unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam Julai 18

Kwa  mujibu wa taarifa rasmi ya familia iliyotolewa leo, mwili huo utaletwa  kutoka katika hospilai ya Mwananyamala  ulikohifadhiwa kisha kupelekwa nyumbani kwake eneo la Sinza  jirani na Lion Hotel   ambapo heshima za mwisho zitatolewa majira ya saa sita mchana kisha  kulepekekwa katika kanisa katoliki la Maria Mama wa Mwokozi  lililopo Sinza na baadaye saa tisa kupumzishwa katika makaburi ya Kinondoni.

Marehemu Majebele alizaliwa tarehe 03/05/1941 katika kijiji cha Ibiri, Wilaya ya Tabora Vijijini, Mkoa wa Tabora, akiwa mtoto wa tatu (3) wa familia ya watoto 10 wa Mzee Michael Kanyata Majebelle na Mama Theresia Malwa Majebelle ambao wote kwa sasa ni marehemu.

SHULE
Alisoma shule ya Msingi ya Bukene (1950) Puge, Wilaya ya Nzega, Mkoa wa Tabora tangu mwaka 1951, Baadaye katika Shule ya Kati (Middle School) ya Sikonge, Wilaya ya Sikonge, Mkoa wa Tabora, mwaka 1954 mpaka 1957.
 
Alijiunga na Tabora Boys School kwa masomo ya sekondari mwaka 1958 mpaka mwaka wa 1961.

Marehemu alikuwa mpenzi wa mpira wa miguu na aliwahi kushiriki kwenye mashindano ya SUNLIGHT CUP enzi zake.

KAZI
David aliajiriwa na kampuni ya Almasi ya Williamson Diamonds Ltd ya Mwadui, Shinyanga mwaka 1962 kama Public Relations Trainee. Mwaka 1963 alipelekwa Uingereza kusomea Stashahada ya Uandishi wa Habari/Upigaji Picha za Uandishi. 

Baada ya kuhitimu alibaki nchini humo kwenye Kampuni ya The Anglo American Corporation kupata uzoefu kable ya kurejea Mwadui kuendelea na kazi ya Afisa Uhusiano wa kampuni ya Williamson Diamonds Ltd hadi Septemba 1967 alipojiuzulu na kuajiriwa na Shirika la Ndege la Africa Mashariki (East African Airways) na kituo chake cha kwanza kikiwa ni Uwanja wa Kimataifa wa Embakasi – Nairobi. Oktoba 1971 alipewa uhamisho na kupelekwa London Uingereza kuwa mwakilishi wa Shirika hilo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa HEATHROW – London.

Julai 1974 alihamishwa kutoka Uingereza na kuletwa Tanzania kuwa Meneja Mauzo wa Kampuni Tanzu ya Shirika lililojulikana kwa jina la SIMBA AIR. Lilipovunjika Shirika la Ndege la Africa Mashariki (East African Airways)’

David Majebelle alijiunga na Shirika jipya la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) kama Meneja Mauzo. Mwaka 1978 aliacha kazi katika Shirika hilo na kujiunga na wamiliki wa magazeti ya AFRICA NEWS na baadaye NEW AFRICA mpaka mwaka wa 1990 kituo chake kikiwa Uingereza. Baada ya pale alianzisha Kampuni yake binafsi kwa jina la MEDIA ADVERTISING CO.Ltd iliyojihusisha na Uhusiano, Matangazo, Upigaji Picha ikiwemo za magazeti mbalimbali kama;

The Financial Times of London, New Africa African Business, Profit Magazine ,The African Review  na magazeti ya hapa nyumbani
Kadri umri wake ulivyokwenda aliandamwa na magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu. Ilibidi apunguze kasi ya kushughulikia Kampuni hiyo mpaka alipoifunga.

FAMILIA
David Michael Majebelle alifunga ndoa mwaka 1975. ameacha mke na watoto wane (4), wa kiume mmoja na wa kike watatu.

UMAUTI
Katika miaka miwili ya mwisho wa maisha yake, marehemu amekuwa akisumbuliwa na kisukari na shinikizo la damu. Jumatano iliyopita alifanyiwa vipimo huko hospitali ya Agha Khan ambako aligundulika kuwa amepata “multiple mild strokes”. Jumamosi kuamkia Jumapili iliyopita alifariki dunia.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina.

Raha ya milele umpe ee Bwana; na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani, Amina.

NBC YAZINDUA HUDUMA YA MIKOPO KWA WAFANYAKAZI WAAJIRIWA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa tatu kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mikopo ya Wafanyakazi Waajiriwa ya benki hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mikopo, Andrew Lyimo, Mkuu wa Huduma za Rejareja, Raymond Mutagahywa, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale na Kaimu Mkuu wa Hazina, Ivan Tarimo.  
 Mkuu wa Mikopo wa Benki ya NBC Tanzania, Andrew Lyimo (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mikopo ya Wafanyakazi Waajiriwa  jijini Dar es Salaam leo. Wengine kulia kwake ni Mkuu wa Huduma za Rejareja, Raymond Mutagahywa, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale. 
 Mkuu wa Huduma za Rejareja wa Benki ya NBC Tanzania, Raymond Mutagahywa (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mikopo ya Wafanyakazi Waajiriwa jijini Dar es Salaam leo. Wengine kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Bi. Mizinga Melu,  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Bi. Mwinda Kiula Mfugale na  Kaimu Mkuu wa Hazina wa NBC, Ivan Tarimo. 
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Bi. Mwinda Kiula Mfugale (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya waandishi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Mikopo kwa Wafanyakazi Waajiriwa ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.

WASHINDI WA PROMOSHENI YA AIRTEL YATOSHA WA WIKI WAPATIKANA

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando akionyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) jinsi droo ya Airtel Yatosha inavyochagua mshindi wa kila siku wakati wa droo ya kwanza ya   promosheni hiyo ya Yatosha iliyotoa jumla ya washindi 7 toka mikoa mbalimbali, katikati anaefuatilia droo hiyo ni  Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao na Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakwanza kulia. Droo ya Airtel Yatosha imetoa jumla ya ashindi 7 ambapo kila mmoja amejishindia shilingi milioni moja.
Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando akiongea na moja ya washindi wa promosheni ya Airtel yatosha mara baada ya kuibuka mshindi katika droo ya wiki ya kwanza inavyochagua mshindi wa kila siku wakati wa droo ya kwanza ya   promosheni hiyo ya Yatosha iliyotoa jumla ya washindi 7 toka mikoa mbalimbali, katikati anaefuatilia droo hiyo ni  Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao na Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakwanza kulia. Droo ya Airtel Yatosha imetoa jumla ya ashindi 7 ambapo kila mmoja amejishindia shilingi milioni moja.

DSE YAUNGANA NA KAMPUNI ZA MCL NA KPMG KATIKA MRADI WA TOP 100 KUZITAMBUA KAMPUNI BORA

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Moremi Marwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana juu ya DSE kuungana na kampuni Mwananchi Communication Limited (MCL) na Kampuni ya KPMG kufadhili mradi ujulikanao kama Tanzania Top 100 wenye lengo la kuzitambua kampuni bora zenye mafanikio nchini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Moremi Marwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana juu ya DSE kuungana na kampuni Mwananchi Communication Limited (MCL) na Kampuni ya KPMG kufadhili mradi ujulikanao kama Tanzania Top 100 wenye lengo la kuzitambua kampuni bora zenye mafanikio nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Tido Mhando.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Moremi Marwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana juu ya DSE kuungana na kampuni Mwananchi Communication Limited (MCL) na Kampuni ya KPMG kufadhili mradi ujulikanao kama Tanzania Top 100 wenye lengo la kuzitambua kampuni bora zenye mafanikio nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Tido Mhando.

NIMR WAZUNGUMZIA UTAFITI WA DAWA ZA ASILI KWA MATUMIZI YA BINADAMU

$
0
0
Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk. Julius Masaga(kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, juu ya shughuli za taasisi za utafiti na uendelezaji wa tiba asili kwa ajili ya matumizi ya binadamu. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa NIMR, Coletha Njelekela na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Zamaradi Kawawa.

HAPPY BIRTHDAY 95 MZEE NELSON MANDELA

$
0
0
“Happy birthday Mzee Madiba.” Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, leo ametimiza umri wa miaka 95, pia anatimiza siku ya 40 tangu alipolazwa katika Hospitali ya Medclinic, Pretoria kwa ajili ya matibabu.

Nelson Rolihlahla Mandela, alizaliwa Julai 18, 1918 katika Kijiji cha Mvezo, eneo la Mthatha, Transkei Mkoa wa Eastern Cape na ametumia zaidi ya asilimia 70 ya maisha yake akipigania haki na usawa wa wananchi wa Afrika Kusini.

Maadhimisho ya miaka 95 tangu kuzaliwa kwa Mandela yanabeba uzito mkubwa kuliko maadhimisho mengine yaliyotangulia kwani kwa siku 40, wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa katika wasiwasi mkubwa hasa kutokana na kuzorota kwa afya ya kiongozi huyo.

Mandela alilazwa katika hospitali hiyo Juni 8, mwaka huu akiugua magonjwa ya figo na afya yake imeelezwa kuwa ni mbaya.


Leo, Rais Jacob Zuma atawaongoza mamilioni ya wananchi wa Afrika Kusini katika maadhimisho ya nne ya kimataifa ya ‘Siku ya Mandela’ ambayo yanakwenda sambamba na siku yake hiyo ya kuzaliwa.

Tangu kulazwa kwa Mandela huko Pretoria, Rais Zuma amekuwa akiwahimiza wananchi wake wajiandae kusherehekea miaka 95 ya Mandela akiwatia moyo wale waliokuwa na wasiwasi kwamba Madiba asingeweza kuifikia leo kutokana na matatizo ya kiafya.

Siku ya Mandela huadhimishwa kuenzi kazi za kiongozi huyo alizozifanya kwa miaka 67 akiutumikia umma wa wananchi wa Afrika Kusini, zikiwamo vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na hatimaye kuwa Rais wa kwanza mzalendo kwa miaka mitano, kisha kustaafu.

Pia ‘Mandela Day’ hutumika kukumbuka kampeni yake dhidi ya ubaguzi wa rangi na utetezi wa haki za binadamu maarufu kwa jina la “46664”, ambayo ni namba ya utambulisho aliyoitumia alipokuwa mfungwa katika Gereza la Visiwa vya Robben.

Dakika 67 za Mandela
Kwa maana ya Siku ya Mandela ambayo pia imeidhinishwa na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, wananchi wa Afrika Kusini wanatumia dakika 67 kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni hatua ya kuenzi kile wanachokiita ‘kazi za mtu aliyejitoa maisha yake kwa ajili ya kupigania haki na utu’.

Dakika hizo 67 zinawakilisha idadi kama hiyo ya miaka ambayo Mandela alitumika, hivyo Waafrika Kusini watakuwa wakitoa msaada na huduma kwa jamii iwe ni kwa watoto yatima au watu wengine ambao ni wahitaji katika jamii.

Kituo cha Kumbukumbu ya Mandela kimewataka wananchi kuungana na kuonyesha ushirikiano wao kwa Mandela kwa kutumia dakika 67 za muda wao kuzisaidia jamii zao ili kumuenzi kiongozi huyo ambaye ni alama ya dunia.

Nchini Tanzania napo jamii imeombwa kufanya matukio kama hayo ya kuisaidia jamii hasa wasio jiweza na watoto yatima kumuenzi kwa vitendo Baba wa Taifa la Afrika Kusini mzee Madiba.

Ofisi za UN Tanzania kushirikiana na Ubalozi wa Afrika Kusini na Waafrika Kusini waishio Tanzania wameaanda maadhimisho hayo yatakayo fanyika kituo cha Yatima cha St Teresa’s Children’s Home kilichopo Mburahati, Kigogo Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 mchana hii leo. 

Wananchi walio na vitu mbalimbali kama nguo, vyakula, madaftari, vitabu na vitu mbalimbali kwaajili ya kusaidia yatima hao wameombwa waje navyo pamoja na hivyo, shughuli za usafi zitafanyika kituoni hapo. 

WANAHABARI WATEMBELEA MRADI WA URANIUM WA MANRTA TANZANIA,NAMTUMBO MKOANI RUVUMA

$
0
0
 Afisa wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania inayoshughulika na Mradi wa Uchimbaji Madini aina ya Uranium,uliopo kwenye Kijiji Mkuju,Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma,Fredrick Kriel akitoa mada ya maswala ya Usalama Mgodini wakati wa Semina fupi kwa Baadhi ya Wanahabari waliofanikiwa kutembelea Mradi huo uliopo pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seluu na kufahamu mambo mbali mbali juu ya Madini hayo ya Uraniuam.
Afisa wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel akionyesha moja ya mambo muhimu na yanayotakiwa kuzingatiwa kwa mtu yeyote awapo Mgodini.
Meneja Mkuu wa Maswala ya Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Cornelis Van Den Berg akifafanua jambo kuhusu mradi huo wa Madini ya aina ya Uranium wakati wa semina fupi na baadhi ya Wanahabari walioweza kutembelea Mgodi huo leo,na kuweza kujionea na kufahamu mambo mbali mbali juu ya Mgodi huo.
Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Palangyo akielezea namna Kampuni yake inavyoweza kutoa kipaumbele katika kusaidia jamii inayouzunguka mradi huko.
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wahusika wa Mradi huo.Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda ambaye ameambatana na wanahabari hao,na wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Palangyo.
Sehemu ya Mandhali ya Mahema ya maofisi ya Kampuni hiyo wakati huu wa Utafiti wa Madini ya aina ya Uranium.
Wanahabari hao wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wasimamizi wa Mradi huo.
Afisa wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel akitoa maelezo ya namna mambo yanavyokuwa pindi wawapo kazini.Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda na kushoto ni Mwanalibeneke Othman Michuzi wakisikiliza kwa umakini.

TIGO KUWEZESHA WATEJA WAKE KUMILIKI BIASHARA

$
0
0
 Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, akionyesha ufunguo wa Bajaji kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Uendeshaji wa Fair Deal auto-dealers, Bw. Anil Dewan kama ishara ya uzinduzi ya promosheni mpya ya “Miliki Biashara Yako” ambayo itawawezesha wateja wake kiuchumi kupitia Bajaji 60 zitakazoshindaniwa kwa muda wa miezi miwili, ambapo kila siku mteja atashinda Bajaji moja.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga akionyesha alama ya dole ndani ya Bajaji moja kati ya 60 zitakazoshindaniwa kwa kuongeza salio ya Tsh 1000 tu kwa siku. Mteja wa Tigo anaweza kuongeza salio mara nyingi awezavyo ili kujiongezea nafasi zaidi ya kushinda.

 Meneja Mbunifu wa Ofa za Tigo Suleiman Bushagama (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu promosheni mpya ya “Miliki Biashara Yako.” Pembeni yake ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, Meneja Mauzo Bw. Israel Gadiel  na Mkurugenzi Mkuu wa Uendeshaji Bw. Anil Dewan wote kutoka Fair Deal auto dealers wasambazaji wa Bajaj nchini Tanzania.   
Kutoka kulia Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Uendeshaji, Anil Dewan na Meneja Bidhaa Khalid Saifullah kutoka Fair Deal auto-dealers, wasambazaji wa Bajaj nchini Tanzania.
Moja kati ya Bajaji 60 ambazo zimeanza kushindaniwa leo katika promosheni ya “Miliki Biashara Yako” kutoka Tigo kwa kuongeza salio ya Tsh 1000 tu kwa siku. Mteja wa Tigo anaweza kuongeza salio mara nyingi awezavyo ili kujiongezea nafasi zaidi ya kushinda. Kila Bajaji ina thamani ya Tsh 6,700,000 na Tigo imechukua jukumu la kulipia leseni ya barabara (road license) na bima ya Bajaji tayari kwa mteja atakayeshinda kuja kuichukua na kuanzisha biashara yake mara moja.

MAJEBELE AZIKWA

$
0
0
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamelibeba sanduku lililohiofadhi mwili wa Marehemu David Majebele wakienda kuzika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam leo. Majebele ni miongoni mwa waandishi wa Habari wakongwe wa Tanzania waliokuwa wakifanya vyema katika tasnia yao kitaifa na kimataifa.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa makaburini wakati wa mazishi ya Mzee David Michael Majebele.

 Baadhi ya watoto wa Marehemu wakiwa makaburini.
 Wanafamilia ya Majebele wakiwa na simanzi wakati wa kukamilisha safari ya mwisho ya ndugu yao.
MWILI  wa mwandishi mkongwe  David Michael Majebelle.  aliyefariki alfajiri ya Jumapili iliyopita umezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam.

Kabla ya mazishi hayo ulipelekwa nyumbani kwake eneo la Sinza  jirani na Lion Hotel   ambapo heshima za mwisho zilitolewa majira ya saa sita mchana kisha  kulepekekwa katika kanisa katoliki la Maria Mama wa Mwokozi  lililopo Sinza na baadaye  makaburi ya Kinondoni.


Marehemu Majebele alizaliwa tarehe 03/05/1941 katika kijiji cha Ibiri, Wilaya ya Tabora Vijijini, Mkoa wa Tabora, akiwa mtoto wa tatu (3) wa familia ya watoto 10 wa Mzee Michael Kanyata Majebelle na Mama Theresia Malwa Majebelle ambao wote kwa sasa ni marehemu.

WAFANYAKAZI AIRTEL DAR LEO WAKO MITAANI KUTOA SOMO JINSI YA KUJIUNGA NA AIRTEL YATOSHA!

$
0
0
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi, Adriana Lyamba akijipanga na mmoja wa afisa mauzo wa Airtel wa Dar es salaam Bi, Violet Kajubili muda mfupi kabla ya wafanyakazi wote  kuelekea katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar esa salaam kuonana na wateja ili kutoa huduma mbalimbali ikiwemo  kuwaelimisha wateja wao jinsi ya kutumia huduma ya Airtel yatosha na promosheni ya shinda nyumba 3.

Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba  LEO amesema Airtel imefanya zoezi  la kuingia mtaani jijini dar es salaam na
wafanyakazi wao wote wa ofisi kuu jijini Dar es salaam kwa lengo la
kuhakikisha kuwa kila mteja anafaham jinsi ya kufaidika na huduma zao
zote ikiwemo ya Airtel Yatosha, ambapo mteja hujiunga kwa kupiga
*149*99# Kisha kuchagua kifurushi nafuu cha  SIKU WIKI AU MWEZI ili

kuongea kwa gharama nafuu kwenda mtandao wowote nchini Tanzania
 Meneja Uhusiano wa Airtel jackson mmbando akibadilishana mawazo na Maafisa mauzo wa Airtel  wa mkoa wa Dar es Salaam leo wakati wafanyakazi hao wakijipanga kuingia mtaaani kukutana na wateja wao na kuwaelekeza jinsi ya kujiunga na huduma ya Airtel Yatosha SHINDA  NYUMBA 3
 
 Baadhi ya maofisa na viongozi wa Timu Airtel Yatosha  wakiendelea kupeana maelekezo jinsi ya kwend a kuingia sokoni kwenye kila mtaa jijini Dar es salaam ili kuwapa somo la AIRTEL YATOSHA shinda nyumba tatu.

Wananchi Sasa Kupata Taarifa za Huduma za RITA kwa ‘Sms’ , Tovuti na Mitandao ya Kijamii

$
0
0
Naibu Waziri Angellah Jasmine Kairuki akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi. 
 **********
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umezindua huduma mpya za kidijitali zinazowawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi kupata huduma za RITA kwa kutumia simu zao na hivyo kupunguza gharama.

RITA, ambayo ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria, imezindua huduma hizo jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Julai 18, 2013) ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki.

Huduma za Simu Kupitia ‘sms’
Kwa wateja wa RITA wenye simu za mkononi na ambao wangependa kupata taarifa mbalimbali kuhusu huduma zetu bila kufika katika ofisi zetu, watapaswa kutoa namba zao za simu za mkononi , namba hizo zitaingizwa katika Kanzi ya RITA (RITA Database) na hivyo RITA kuweza kuwasiliana na wateja kwa njia ya simu kila panapohitajika.

Baada ya namba hio kuingizwa katika Kanzi (Database), RITA itakuwa inawasiliana na mhusika moja kwa moja kwa ujumbe mfupi wa maandishi (sms) popote alipo kwa kumpa taarifa za huduma zetu na kujibu maswali yake bila ya yeye kufika katika ofisi za RITA.


Kupata Taarifa fupi ya ‘sms’ kuhusu Usajili wa Vizazi na Vifo
Kuanzia sasa, mteja wa RITA mwenye simu ya mkononi na anayetaka kujua kwa ufupi namna ya kusajii matukio kama vizazi na vifo, anaweza kutuma neno RITA kwenda namba 15584(gharama ya sms Tsh 200 tu) na atapokea mwongozo utakaomwezesha kujua utaratibu wa kusajili kizazi au kifo kilichotokea hospitali na kwengine.

Kupata Taarifa fupi kuhusu ombi la cheti cha kuzaliwa
Aidha, RITA imeanzisha huduma ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (sms) ili kuwawezesha wateja kupata ‘sms’ pindi maombi yao waliyowasilisha RITA kuhusu huduma mbalimbali yanapokua yamekamilika. Maombi haya ni kama yale ya vyeti vya kuzaliwa baada ya kujaza fomu na kufanya malipo stahiki.

Anachotakiwa kufanya mteja wa RITA mwenye simu ya mkononi ni kutuma neno CHETI kwenda namba 15584 na atapokea ujumbe mfupi (sms) utakaomjulisha kama cheti chake kiko tayari ama bado. Wateja wanaopaswa kutuma ujumbe huu ni wale ambao wamekamilisha taratibu zote ikiwemo kujaza fomu na kufanya malipo stahiki.

Aidha, kwa wale wateja ambao hawatatuma ujumbe na namba zao za simu zipo katika Kanzi (Database) ya RITA, watatumiwa ujumbe mfupi kuwa vyeti vyao vipo tayari ili wavichukue mara baada ya vyeti hivyo kuchapwa.

Huduma za RITA kupitia ‘Tovuti na Mitandao ya Kijamii”
Tunataka kuwa karibu zaidi na kushirikiana na umma, kwa kutumia tovuti, mitandao ya kijamii na simu za mkononi kama njia ya kuwasiliana na kusambaza taarifa muhimu kwa wananchi.

Kutokana na ongezeko la watumiaji wa intaneti, mitandao ya kijamii na simu za mkononi, RITA iko tayari kwenda sambamba na mabadiliko hayo na kutoa jukwaa la mawasiliano baina yetu na wananchi. Tovuti, mitandao ya kijamii na simu za mkononi ni njia rahisi ya kuweza kuwafikia wananchi wetu walioko ndani na nje ya Nchi kwa kutoa taarifa muhimu na kuwajibu maswali mbalimbali kuhusu huduma zetu. Kupata huduma hizi wa watumiaji wa intaneti ni rahisi:

Huduma hizi zina lengo la kupunguza gharama na usumbufu
Ni matumaini ya RITA kuwa matumizi ya huduma hizi yatasogeza huduma zetu karibu zaidi na wananchi wote, walio ndani na nje ya nchi. Aidha, huduma hizi zitapunguza usumbufu na gharama za kusafiri hadi katika ofisi za RITA kwa ajili ya kupata taarifa au majibu ya maswali . Pia, huduma hizi zitawapa fursa wananchi na wateja wa RITA kuwasilisha maoni au malalamiko yao kwa urahisi kupitia mitandao ya kidijitali.

LOWASSA AMFAGILIA RAIS KIKWETE

$
0
0
Na Swahili TV
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa  Edward Lowassa, amemsifia Rais  Jakaya Kikwete kuwa ameweza kuifanya Tanzania kupata heshima  katika ulingo wa kimataifa, aliyasema hayo wakati akihojiwa na Swahili TV jijini Washington DC.

Alisema kitendo cha Rais wa Marekani  Bwana Barack Obama kuja nchini naviongozi mbalimbali wa mataifa makubwa  kumeonyesha Rais Kikwete  anakubalika.

“Ni hivi karibuni  tu  Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu wa Marekani  George W.Bush  walikuwa nchini Tanzania, hii inaonyesha kuwa Tanzania iko juu katika medani za kimataifa” alisema Mheshimiwa Lowassa.


Mheshimiwa Lowassa ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi, aliongeza kwa kusema, Rais  Kikwete anastahili pongezi sana kwa hilo kwani sio rahisi kwa viongozi wa mataifa makubwa kutembelea nchi zingine  labda kama mko juu sana katika medani za kimataifa.

Pia alisema  Rais Kikwete amekuwa akihusishwa  na utatuzi au ushauri wa kutatua matatizo mbalimbali ya nchi zingine na pia ameanza kuishirikisha Tanzania katika usimamizi wa amani katika nchi mbalimbali.

Tanzania iliweka historia hivi karibuni kwa maraisi wawili wa Marekani kukutana  katika nchi moja kwa wakati mmoja,  Rais Barack Obama na George W.Bush walikutana jijini Dar es Salaam mwezi huu.

kwa habari zaidi tembelea Swahili TV Blog 

LOWASSA AFANYAMAHOJIANO VOA

$
0
0
IMG_3081 
Khadija Riyami wa VOA akifanya mahojiano na Mh.Edward Lowassa hotelini kwake The Willard Washington Dc. Ambapo pamoja na mambo mengine katika mahojiano hayo alikanusha yale baadhi waliodai kuhamishia siasa zake kwenye nyumba za ibada. Kusikiliza matangazo hayo ya VOA bofya hapa chini. 
Viewing all 10864 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>