Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10616 articles
Browse latest View live

Flaviana Matata aendelea kuitoa kimasomaso Tanzania, Afrika na Kimataifa

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
NYOTA ya mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata amezidi kung’ara baada ya kuingia katika orodha ya wanamitindo saba bora kwa upande kipato.
Kwa mujibu wa gazeti la biashara la kimataifa la Forbes kwa bara la Afrika (Forbes Africa) lililotolewa hivi karibuni, Flaviana ni mrembo pekee aliyeingia katika orodha hiyo kwa wanamitindo wa Afrika Mashariki na kuzidi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.
Katika orodha hiyo, mwanamitindo Maria Borges wa Angola ndiyo aliibuka namba moja na  wengine sita pamoja na Flaviana wakibaki kutoa ushindani mkubwa kwa mlimbwende huyo wa Angola.
Mbali ya Flaviana, wanamitindo wengine ambao wapo katika orodha hiyo ni Candice Swaenpoel, Katryn Kruger wote wakitokea Afrika Kusini, Ajak Deng, Grace Bol ( Sudan) na Liya Kebede wa Ethiopia,.
Flaviana Matata aliibuka katika jukwaa la kimataifa kama Miss Universe Tanzania mwaka 2007 na aliweka historia kwa kuingia 10 bora na baada ya kumaliza muda wake aliendelea na fani ya  uanamitindo Afrika kusini na baadaye alipata nafasi ya kufanya kazi Marekani na Ulaya katika makampuni makubwa ya uanamitindo ya Next Models International na sasa yuko Wilhelmina Models.
Akizungumza kutoka New York, Flaviana ameeleza kufurahia mafanikio haya hata hivyo ameongeza “Mpango wangu ni kuzidi kumweka Mungu mbele na kuhakikisha kuwa najitahidi kadri ya uwezo wangu na kuiletea sifa familia yangu na nchi yangu”.

Push Mobile kumwaga vitz 4, pikipiki 12 Serengeti Fiesta 2013

$
0
0
KAMPUNI ya Push Mobile Media Limited itatoa zawadi za magari aina ya Vitz manne (4) na pikipiki 12 kwa mashabiki mbali mbali watakaoshinda bahati nasibu maalum ya tamasha la Serengeti Fiesta linalotarajiwa kuzinduliwa Jumamosi mjini Kigoma.
Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa zawadi mbali ya magari na pikipiki, pia watatoa zawadi za fedha taslim (sh 100,000) kwa mashabiki hao ambao ili kushinda wanatakiwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 ili kuweza kushinda gari, pikipiki au fedha taslim na unaweza kushinda tiketi ya VIP kwa kutuma jina la msanii kwa mfano Diamond na kuacha nafasi na baadaye kuwema maoni yako kwenda namba hiyo hiyo.
Rodney alisema kuwa mbali ya kushinda tiketi, mshiriki atalipiwa tiketi ya ndege kuja Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki katika tamasha la fiesta la mwisho. Alisema kuwa wameamua kuweza zawadi hizo nono ili kunogesha zaidi tamasha hilo ambalo kwa kuwanufaisha mashabiki  wa muziki hapa nchini.
Aliongeza kuwa wamejipanga ili kuwashirikisha wananchi wote katika tamasha hilo kwani watatoa pia watazindua huduma mpya ijulikanayo kwa jina la Simu TV ambapo itamwezesha mashabiki kuona video mbali mbali za muziki na matukio mengine, kupata nyimbo mbali mbali, kupata taarifa mbali mbali ikiwa pamoja na za michezo kwa kupitia simu ya mkononi.
kuhusiana na zawadi za fedha, Rodney alisema kuwa zawadi hiyo itakuwa inatolewa kila siku kwa mashabiki watakaoshinda bahati nasibu hiyo. Alifafanua kuwa jumla ya sh milioni 80 zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili litakalodumu kwa kipindi cha miezi mitatu.

PONDA ALAZWA MUHIMBILI- POLISI WATOA TAMKO

$
0
0
 Sehemu ya kodonda katika bega la Sheikh Ponda baada ya kushinwa nyuzi.
  Katibu wa Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, akiwa katika Wodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akitibia jeraha alilopata jana akidaiwa kupigwa risasi mjini Morogoro.
 Sheikh Ponda akiwa hospitalini hapo na jeraha katika bega la mkono wa kulia.
Sheikh Ponda akiwa na msaidizi wake hospitalini hapo.
************************************
TAMKO LA JESHI LA POLISI KUHUSU SHEIKH PONDA ISSA PONDA

1.  MNAMO TAREHE 10, AGOSTI ,2013 MAJIRA YA SAA 8 MCHANA, MAENEO YA SHULE YA MSINGI KIWANJA CHA NDEGE MANISPAA YA MOROGORO,  KULIFANYIKA KONGAMANO LA BARAZA LA EID LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WAHADHILI MKOANI MOROGORO. DAKIKA KUMI KABLA YA KONGAMANO HILO KUMALIZIKA  ALIFIKA SHEKHE PONDA ISSA PONDA AMBAYE ALIZUNGUMZA KWA MUDA MFUPI.

2. KONGAMANO HILO LILIFUNGWA  MAJIRA YA SAA 12:05 JIONI AMBAPO WATU WALIANZA KUTAWANYIKA, BAADHI YAO WAKIWA WAMEZINGIRA GARI DOGO ALILOKUWA AMEPANDA SHEKHE PONDA. BAADA YA KUTOKA KATIKA  ENEO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIZUIA GARI HILO KWA MBELE KWA NIA YA KUTAKA KUMKAMATA SHEKHE PONDA AMBAYE MPAKA SASA  ANATUHUMIWA KWA KOSA LA KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI SEHEMU MBALIMBALI HAPA NCHINI YENYE MLENGO WA KUSABABISHA UVUNJIVU WA AMANI.

3. BAAADA YA ASKARI KUTAKA KUMKAMATA, WAFUASI WAKE WALIZUIA UKAMATAJI HUO KWA KUWARUSHIA  MAWE ASKARI.  KUFUATIA PURUKUSHANI  HIYO, ASKARI WALIPIGA RISASI HEWANI KAMA ONYO LA KUWATAWANYA.

4. KATIKA VURUGU HIZO, WAFUASI HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA  MTUHUMIWA. HIVI SASA IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI AKITIBIWA JERAHA KATIKA BEGA LA MKONO WA KULIA LINALODAIWA ALILIPATA KATIKA PURUKUSHANI HIZO.

5. KUFUATIA TUKIO HILO, TIMU INAYOSHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA JUKWAA LA HAKI JINAI IKIONGOZWA NA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI  CP ISSAYA MNGULU IMEANZA KUFANYA UCHUNGUZI WA TUKIO HILO.

6. AIDHA, JESHI LA POLISI LINATOA  WITO KWA  WANANCHI KUWA WATULIVU WAKATI SUALA HILI LINASHUGHULIKIWA KISHERIA.

Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Tamasha la Afrika lafana Marekani

$
0
0
IMG_3439Nene Mtanzania aliyeongoza kamati ya maandalizi akijivunia kazi yake. IMG_3269Fashion ya mavazi ya Afrika. IMG_3282  IMG_3300  IMG_3326  IMG_3285  IMG_3337 
Kwa picha zaidi ungana na Sundayshomari.com

SHINING THE SPOTLIGHT ON FASHION DESIGNER LINDA BEZUIDENHOUT

$
0
0

Shining the Spotlight on Linda Bezuidenhout
Linda Bezuidenhout (LB) is a fashion designer who is based in Atlanta, USA. Linda has been involved in fashion industry for over 20 years, in Africa, Europe and the USA. The LB line is influenced by a wide range of world fashion, cultures and trends.

Linda comes from a Dutch-Tanzanian background and has been influenced with fashion since the age of 8 when she used to insist on designing her own holiday & special occasion clothes and have local tailors sew the dresses. As a teenager she lived in several different countries in Europe which developed her fashion vision and exposure.


 In her 20′s she moved back to Africa (Tanzania) and continued contributing to the fashion scene there as a top beautician with involvement in various beauty pageants in conjunction with some of the top African female singers such as M'bilia Bel & Vivic Motuwa. In her late 20′s she moved to USA and got involved in the men's world of fashion as well and owned several menswear stores in different malls in the US.

For more video and exclusive interviews go on www.swahilitv.blogspot.com

DAR LIVE YACHENGUA NA EXTRA BONGO, TOT IDD PILI

$
0
0
Ally Choki na mnenguaji wake wakionyesha ‘machejo’.Aziza Kimsi wa TOT Taarab akiimba.
Wanamuziki wa TOT wakiimba. Kiongozi wa Extra Bongo, Ally Choki, akiimba wimbo wa Mtenda Akitendewa.
Wanamuziki wa Extra Bongo wakiwa kazini.
Wanenguaji wa Extra Bongo wakijinafasi.
Naibu Mkurugenzi wa TOT, Gasper Tumaini akionyesha 'matindo' ukumbini.
MASHABIKI wa muziki jana walipata burudani ya kukata na shoka katika sikukuu ya Idd Pili kwenye Ukumbi wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam ambapo walichenguliwa vilivyo na bendi za Extra Bongo na TOT.
(NA ISSA MNALLY / GPL)

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAFANYA UZINDUZI WA MUONEKANO MPYA WA BIA YA KIBO.

$
0
0
 Meneja Miradi endelevu na uwajibikaji kampuni  ya bia ya Serengeti  Nandi Mwiyombela (Katikati), Meneja wa mauzo wa kanda ya kaskazini Patrick Kisaka (kushoto) na Attu Mynah (kulia) kutoka idara ya mipango wakionyesha mbele ya wasambazaji wa bia na waandishi wa habari aina mpya ya chupa yenye shingo ndefu ambayo bia ya Kibo Gold itapatikana kuanzia sasa, hafla hiyo ilifanyika katika kiwanda cha Serengeti Breweries kilichopo mjini Moshi.
 Meneja wa miradi endelevu na uwajibikaji Bi Nandi Mwiyombella akizungumza jambo mbele ya Wanahabari na wageni waalikwa kwenye hafla ya muonekano mpya wa bia ya Kibo Gold
Meneja wa kiwanda cha bia cha Serengeti cha njinpi Moshi Bw. Coleman Hanna (katikati) akibadilishana mawazo na meneja mauzo wa kanda ya kaskazini Bw. Patrick Kisaka (kulia) wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa bia ya Kibo Gold uliofanyika kiwandani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita. 
Msambazaji wa kwanza kabisa wa bia za Serengeti mkoa wa Kilimanjaro Mama Kisela, akipokea bia ya Kibo Gold yenye muonekano mpya na ladha ileile  kutoka kwa Attu Mynah wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa wa bia hiyo katika hafla fupi iliyofanyika katika kiwanda hicho wmwishoni mwa wiki.
******** 
 Kampuni ya bia ya Serengeti leo imezindua  muonekano mpya wa bia inayosherehekewa sana mkoani hapa, Kibo Gold.   Uzinduzi huu uliofanyika katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichopo Moshi, ulifikia kileleni kwa shughuli murua iliyoandaliwa na kampuni hii na kushuhudiwa na waandishi wa habari pamoja na wadau mbali mbali.    Bia hii ya Kibo sasa ina muonekano mpya wa chupa inayoashiria ubora wa kilichopo ndani.  Bia ni yenye ubora uleule wenye kiwango cha hali ya juu ila kwa chupa ya rangi ile ile iliyongarishwa na  shingo ndefu.

Akiongea kwenye hafla hii Meneja wa miradi endelevu na uwajibikaji Bi Nandi Mwiyombella alisema bia hii ya Kibo Gold imekuwa ikitambulika kwa ubora na ladha nzuri kwa wateja.   “Kwa muonekano huu mpya wa chupa ya kisasa, tunaamini wateja wengi watavutiwa na kuipenda zaidi kwani ni muonekano unaokwenda na wakati.   Ubora wa bia hii, unakuwa dhahiri kweli kabisa ukizingatia kwamba inatengenezwa kwa maji yatiririkayo kutoka katika kilele cha juu kabisa cha mlima Kilimanjaro ambapo pia bia inazoa jina lake hili la ‘KIBO’, aliongeza Bi Nandi.

Kampuni ya bia Serengeti chini ya kampuni mama ya Diageo, inazingatia kanuni  na sheria zilizowekwa na kampuni hii kwenye ubora katika uzalishaji wa  bidhaa zote.  Muonekano wa bidhaa ni ule unaondena na soko za kimataifa na wa kuvutia.
 

Kampuni ya bia ya Serengeti  inatumia malighafi za kitanzania ili kuleta ubora halisi na vile vile kukuza uchumi wa Tanzania katika sekta ya kilimo. 

Kwa Mhariri:  Bia ya Kibo Gold ilirudishwa sokoni hapa Tanzania mwaka jana, 2012, mwezi wa sita baada ya kuwa haipo kwenye soko kadri ya miaka kumi.   Ni mojawapo ya bia zinazoongoza nyanda za kaskazini sasa hivi.  Bia hii inazalishwa katika kiwanda cha bia cha Serengeti cha Moshi na inasambazwa mkoani hapo na mikoa jirani, Arusha, Tanga, Manyara na Tanga kwa wingi.

Tafadhali kunywa kistaarabu.  Haiuzwi kwa walio chini ya miaka 18.

REDD’S MISS ILALA 2013 KUFANYIKA AGOSTI 16 GOLDEN JUBILEE DSM

$
0
0

 Warembo wanaotarajia kushiriki Redd’s Miss Ilala, wakiwa wamepozi wakati wa mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini.
Warembo wanaotarajia kushiriki Redd’s Miss Ilala, wakiwa wamepozi wakati wa mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini
Warembo wakiwa katika moja ya miondoko wakati wamazoezi
Mwalimu wa warembo hao, AKHSAS PETER akiwapanga vizuri kabla ya kupigwa picha na wandishi wa habari.
Warembo wakipita Mtaa wa Makunganya katikati ya Jiji la Dar es Salaam, wakitokea mazoezini katika Mgahawa wa Billicanas.
 Mwandishi Mwandamizi wa Habari za Michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula (kulia), akitoa maelezo kuhusu kazi za kila siku za waandishi wa habari kwa warembo wa wanaotarajia kushiriki mashindano ya Redd,s Miss Ilala walipotembelea chumba cha habari cha Jambo Leo
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL), Juma Pinto (aliyekaa kulia), akizungumza na warembo hao waliomtembelea ofisini kwake, Dar es Salaam. Aliyekaa katikati ni Mratibu wa mashindano hayo, Juma Mabakila. JCPL ni wachapishaji wa magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti, Dar Metro na jarida la Jambo Brand Tanzania.

WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA MONTAGE WASHEREHEKEA SIKUKUU YA EID NA WANAFUNZI YATIMA WA SHULE YA SEKONDARI YA WAMA - NAKAYAMA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Tanzania Teddy Mapunda  akiwagawia soda wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike  ambao ni yatima na wanaoishi  katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakati wa sherehe za sikuku ya Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo jana. Wafanyakazi wa kampuni hiyo  walisherehekea sikuu hiyo na  wanafunzi hao ili kuonyesha upendo.
Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Daud Nasibu akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike  ambao ni yatima na wanaoishi  katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama inayomilikiwa na taasisi hiyo wakati wa sherehe za Eid Mubarak ziliyofanyika shuleni hapo jana.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Montage ya jijini Dar es Salaam  wakiwahudumia chakula cha mchana wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike  ambao ni yatima na wanaoishi  katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani. Wafanyakazi wa kampuni hiyo waliamua kusherehekea sikukuu ya Eid Mubarak na wanafunzi hao jana  ili kuonyesha upendo
Wanafunzi  wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike  ambao ni yatima na wanaoishi  katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakila chakula cha mchana kilichoandaliwa na kampuni ya Montage Tanzania wakati wa sherehe za Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo jana.
Baadhi ya wanafunzi  wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike  ambao ni yatima na wanaoishi  katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakicheza mziki aina ya Kwaito  jana wakati wa sherehe za  Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo.

MASHINDANO YA MIJADALA YA SHULE ZA SEKONDARI MWANZA KUANZA SEPT. 2.

$
0
0
Mkurugenzi wa Stopper Entertainment, Mursin Mambo, akifafanua jambo kuhusiana na Mashindano ya Shule za Sekondari.
 
Mashindano ya Mijadala kwa shule za sekondari mkoani Mwanza (Interschools Debate Competition), yanatarajiwa kuanza septemba 02 mwaka huu.
 
Akizungumza katika semina elekezi, iliyowakutanisha baadhi ya walimu wa mijadala kutoka katika  shule mbalimbali za sekondari mkoani Mwanza, mkurugenzi wa Stoppers Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo, Bwana Mukhsin Mambo, amesema jumla ya shule 32 kutoka mkoani Mwanza, zitashiriki katika shindano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika mkoani humo na Tanzania kwa ujumla.
 
Mambo, amesema shindano hilo pia litaonyeshwa kwenye moja ya runinga hapa nchini kuwapa fursa watazamaji kushuhudia vipaji vya wanafunzi katika kujieleza mbele ya jamii.
 
Amesema nia na madhumuni ya shjindano hilo, mbali na kuondoka na kitita cha zawadi kwa washindi lakini pia ni njia mojawapo ya kuinua kiwango cha elimu hapa nchini kwa wanafunzi kupata nafasi ya kujieleza mbele za watu, kufanya utafiti kutokana na mada itakayowekwa mezani, kuweka mahusiano mema dhidi ya wanafunzi na kujenga kizazi kipya katika nyanja ya elimu kupitia mfumo wa mijadala.
 
Miongoni mwa shule zitakazoshiriki shindano hilo ni pamojana Nsumba sekondari, Nganza Sekondari, Butimba sekondari, St. Joseph Girls Sekondari, Buswelu Sekondari, New Hellen Sekondari, Hill crest Sekondari, Bismark Sekondari.

RADIO 5 WAIBUKA WASHINDI WA KWANZA MAONYESHO YA NANENANE KANDA YA KASKAZINI.

$
0
0
 Wafanyakazi  wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 kushoto ni Semio Sonyo ,Sarah Keiya meneja masoko,katikati ni David Rwenyagira na Deo Gee wakifurahia  kikombe cha ushindi ambapo jana waliibuka washindi wa kwanza kwenye maonyesho ya 20 ya Nane nane kwa kanda ya kaskazini,yaliyofanyika katika viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha.
Meneja masoko wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio5 Sarah Keiya pamoja na Dadiv Rwenyagira wakiwa wameshikilia kikombe mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza maonyesho ya 20,ya nane nane kwa kanda ya kaskazini yaliyofanyika katika viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha.

AIRTEL YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WAKE

$
0
0
Kulia  ni Meneja wa Duka la Airtel Mako makuu Bi, Happy John  akiwa na mshindi wa zawadi ya shilingi milioni moja kwa wiki  hii  Bw, Rakesh Mawji  akihesabu pesa zake mara baada ya kuzitoa kupitia huduma ya Airtel Money. Hafla ya makabidhiano na mshindi huyo ilifanyika katika ofisi za Airtel jiji ni Dar es salaam.

Kulia  ni Meneja uhusiano wa Airtel Bw jackson Mmbando akiwa akimpongeza mume wa mshindi wa wiki hii Bw, Hassan Abdalah mara baada ya mke wake (kati) Bi Mwajuma kukabidhiwa zawadi yake shilingi milioni moja na kuitoa kupitia huduma ya Airtel Money Hafla ya makabidhiano namshindi huyo ilifanyika katika ofisi za Airtel jijini Dar es salaam.
Kati ni Mwalim steven Maguru akionyesha pesa yake kwa furaha kiasi cha shilingi laki moja aliyotoa kupitia Airtel money mara baaada ya kushinda milioni moja na kupokea yote kupitia Airtel Money. Kulia ni mshindi mwingine wa wiki hii Bw, Rakesh Mawji na kushoto ni meneja Uhusiano wa Airtel bw, jackson Mmbando mara baada ya kukutana na washindi hao makao makuu ya Airtel jijini dar es salaam.

SHINDANO LA VIPAJI LA REDD'S MISS ILALA 2013 LEO

$
0
0
Warembo wanaotarajia kushiriki Redd’s Miss Ilala Talent hii leo, wakiwa wamepozi wakati wa mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini.
**********
KATIKA Kuelekea Redds Miss Ilala Ijumaa, leo kutakuwa na shindano la kumtafuta mrembo mwenye kipaji (Talent) itakayofanyika katika mgahawa wa City Sports and Lounge uliopo katikati ya jiji.
Mratibu  wa shindano hilo, Juma Mabakila  alisema kuwa maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza kuwa warembo wote 14 wamejipanga kuonesha vipaji vyao ipasavyo.
Mabakila alisema mshindi wa talent atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Ijumaa ijayo  katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower ulipo katikati ya jiji.
Mratibu huyo wa Ilala alisema mbali ya burudani hiyo, pia watatumia nafasi hiyo kuuza ticket za VIP ambazo ni chache kwa watu maalum, lakini kutakuwa na bahati nasibu itakayotoa pasi za bure za kusingia katika onesho la Ijumaa.
Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya Ilala maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.
“Tumejipanga vizuri kuonesha shoo nzuri kuanzia hii ya telent na ile kubwa Ijumaa, kutakuwa na vitu tofauti na ilivyokuwa mwaka jana, kweli mambo yanakwenda vizuri,” alisema  Mabakila.
Mashindano ya Redd's Miss Ilala yamedhaminiwa na Redd's Original,magazeti ya Jambo Leo, Tanzania Daima,Smile, CXC Safaris, Blog ya wananchi, Fredito na Dodoma wine.

WAJUMBE WA KAMATI YA UHURU MARATHON WATAJWA

$
0
0
Waziri wa habari,Vijana,utamaduni na michezo Dr Fenella Mukangara akitangaza majina ya wanakamati aliowateuwa kuratibu mbio za uhuru mwaka huu nchini,Dkt Mukangara amewataja wajumbe hao kuwa ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq  (Mwenyekiti) na  Wajumbe wengine katika kamati hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, Naibu Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda na Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa. Wengine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Intellectuals, Innocent Melleck, Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), Gabriel Nderumaki, George Kavishe kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mhariri Mtendaji wa Uhuru, Jossiah Mfungo na Habib Gunze wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
 Mratibu wa mbio za uhuru nchini Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari juu ya mipango mbalimbali ya mbio za uhuru nchini ,Kulia ni Waziri wa habari,Vijana,utamaduni na michezo Dr Fenella Mukangara ambapo waziri amewateuwa wajumbe kumi watakaoratibu mbio hizo mwaka huu. 
Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali nchini wakiwa katika chumba cha mikutano cha wizara ya habari tayari kumsikiliza Mheshimiwa waziri atangaze kamati hiyo.
***********
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mukangara jana alitangaza wajumbe watakaosimamia mbio za Uhuru Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Dk. Fenella alisema wajumbe wa kamati hiyo itakayokuwa na watu 10 itakuwa na jukumu la kuhakikisha mbio hizo zinafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
 
Kamati hiyo inatarajiwa kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq huku ikiwa na wajumbe wengine kutoka katika sekta mbalimbali nchini.

Wajumbe wengine katika kamati hiyo iliyoundwa na waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, Naibu Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda na Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa.

Wengine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Intellectuals, Innocent Melleck, Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), Gabriel Nderumaki, George Kavishe kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mhariri Mtendaji wa Uhuru, Jossiah Mfungo na Habib Gunze WA Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Waziri Fenella alisema mbio hizo zitakuwa zimegawanyika katika sehemu nne kukiwa na mbio ndefu za kilomita 42, mbio za kati kilomita 21, mbio za kujifurahisha kilomita 5 na mbio fupi ambazo ni maalumu kwa viongozi zikiwa za kilomita 3.

“Mbio hizi zina lengo kuu la kuimarisha umoja, upendo, mshikamano na amani kwa Taifa letu. Tunategemea Watanzania wengi, ikiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, wanafunzi wa ngazi mbalimbalio na wananchi kwa ujumla wataungana na kushiriki mbio hizi,” alisema.
Naye Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema wazo kubwa la kuanzisha mbio hizo ilikuwa ni kutaka kuwakumbusha Watanzania kuuenzi umoja, amani, mshikamano ulipo pamoja na uhuru wetu.

Mratibu huyo alisema, mpaka sasa wanariadha zaidi ya 300 kutoka nje ya Tanzania wameomba kushiriki mbio hizo za aina yake hapa nchini.
“Sisi kama vijana tukaona kuna haja ya kufanya kitu cha kuwakumbusha Watanzania wenzetu kwani tunatakiwa kudumisha urithi wa amani, mshikamano na uhuru wetu tulioachiwa na mababu zetu,” alisema.

Melleck alisema mbali na mbio hizo kufanyika siku hiyo, pia kutakuwa na tamasha kubwa la burudani litakalofanyika katika Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaam ikiwa ni mkesha wa kusubiri siku ya Uhuru.

Mbali na hayo Waziri Fenella naye alizitaka taasisi mbalimbali kuhakikisha wanazidhamini mbio hizo kwani zina manufaa kiubwa kwa taifa.

CREDITINFO GLOBAL FORUM, PRAGUE, 18TH& 19TH SEPTEMBER 2013

$
0
0
Credit info is proud to present its first official Global Forum, to be hosted in the beautiful city of Prague. 
The Conference will bring together a number of influential specialists, practitioners and providers within the Credit Industry. It will present an excellent opportunity for these experts to share ideas about the challenges and best practice worldwide.

Amongst the speakers are representatives from Paypal, Societe Generale Group,International Finance Corporation (IFC), Bank of Georgia as well as Credit Bureaus in 4 continents.

Creditinfo greatly appreciates the contributions of its speakers who will be delivering informative and comprehensive presentations focussing on the following key areas:


1.    The major challenges when setting up a Credit Bureau
2.    Innovative data sources to enhance traditional credit bureau data
3.    How to overcome concerns with data acquisition
4.    How to ensure data quality in an imperfect world
5.    The use of credit reports when making a credit decision
6.    Development of Data Roadmap with Lenders working together with Credit Bureaus
7.    In an on-line world how best to use data for identification and fraud prevention
8.    Implementing credit bureau scorecards
9.    The usage of Credit Bureau data to better manage your portfolio
10.  Using blended data and scorecards to make better SMEs decision
11.  Support strategic direction by Benchmarking your portfolio against the market
12.  Psychographic profiling, does it have a role in credit granting?

Reynir Grétarsson, CEOCreditinfo, is a firm believer that “Information is the lifeblood of the modern economy.” He advises that “Creditinfo will always be an innovatortaking the initiative in the development of new services and processes in the Credit Bureau industry. We continue to strive to enrich business performances and consumers lives by converting data to intelligent decisions. 
Through our partnership programmes and Global Forums, we are able to develop & improve on financial infrastructures for the benefit of the overall economy, whilst facilitating access to (affordable) credit, increasing financial inclusion and lowering interest rates.
Creditinfo’s strategy continues to be direct, fast and flexible thanks to a growing, experienced and professional worldwide team who are continually creating& developing credit risk and information solutions to meet current market demands.
For more information and registration:

PPF WAZUNGUMZIA SHUGHULI ZAO

$
0
0
UTANGULIZI
Mfuko wa Pensheni wa PPF  ni Mfuko mkongwe hapa nchini, ulianzishwa mwaka 1978 kwa Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa PPF Sura na. 372kwa madhumuni ya kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendena na hayo kwa wafanyakazi wote walio katika sekta rasmi na zisizo rasmi.

majukumu ya mfuko

PPF ina majukumu yafuatayo:-
kuandikisha wanachama,
kukusanya michango,
kuwekeza michango inayokusanywa na
kulipa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa wanachama wake.

WIGO WA UANACHAMA
Mfuko unaandikisha wanachama kutoka katika sekta zote za uchumi mashirika ya umma, makampuni binafsi, waliojiajiri wenyewe na sekta isiyo rasmi

Mafao ya PPF: Mfuko wa PPF una mafao saba baadhi ya mafao ambayo Mfuko unatoa ni
Mafao ya Pensheni ambapo hutolewa pale ambapo mwanachama anapokuwa amechangia kwa kipindi cha miaka 10 au zaidi na amefikia umri kustaafu yaani miaka 55 mpaka 60.Na awe ameondoka kwenye ajira.


Mpaka sasa PPF ina wastaafu  wapatao 25,896 na tunalipa kila mwezi Billioni 3.7
Hii ni kwa mafao ya uzeeni tu mnaweza kuona jinsi tunavyosaidia kuondoa umaskini na kukuza uchumi wa nchi.

Mafao ya Ugonjwa
 Hutolewa pale ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa ameondoka kazini kwa sababu za ugonjwa na imedhibitishwa na Daktari kwamba kweli hawezi kufanya kazi tena

Mafao ya Elimu:
Hutolewa pale ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa amefariki dunia baada ya kuchangia kwa muda wa miaka 3 au zaidi.

Fao hili hutolewa kwa watoto wa mwanachama wasiozidi 4 kwa kulipia gharama ya elimu ya chekechea mpaka kidato cha nne.

Kwa kutambua umuhimu wa elimu kuanzia mwakani 2014 Mfuko unaongeza muda wa kuwasomesha watoto mpaka kidato cha sita.
Tunalipa mmoja kwa mmoja kwenye shule za watoto wanachama

UWEKEZAJI
Jukumu linginge kubwa ni kuwekeza; Mfuko wa PPF unawekeza kwa mujibu wa sera ya uwekezaji sambamba na mwongozo wa uwekezaji wa SSRA na BOT.  Baadhi ya sehemu Mfuko unawekeza katika Majengo kama vile ofisi mfano PPF Tower,PPF Plaza Mwanza,vile vile wekeza kwenye hoteli,nyumba za kupanga vile vile tume tumeshiriki kwenye ujenzi wa vyuo vikuu kama vile UDOM-kwenye chuo cha Mifumo ya Komputa na chuo kikuu cha sayansi na Teknologia Nelson Mandela kilichopo Mkoani Arusha.

Tumeshiriki kwenye uwekezaji katika sekta ya Kilimo Kagera Sugar, 21st Century kiwanda cha Nguo Morogoro Uwekezaji mwingine ni kwenye Mikopo ya Saccos kwa wanachama wetu ambapo PPF unakopesha wanachama kwenye maeneo ya Kazi ambapo inasaidia kukuza uchumi

MAFANIKIO YA MFUKO
Mfuko umetimiza miaka 35 mwaka huu na ulianza kwa mtaji wa shilingi million 50 mwaka 1992.lakini Mfuko unaendelea vizuri kwa kuwa na uwezo wa kulipa mafao kwa wakati bila kulazimika kuuza vitega uchumi au kukopa mahali popote

Kwa upande wa thamani ya Mfuko:
Mfuko umeendelea kukua mwaka hadi mwaka ambapo kwa sasa thamani ya Mfuko ni shilingi trillion 1.3 ukilinganisha na mwaka jana 2012 Desemba ambapo thamani ya Mfuko ilikuwa trillion 1.09

IDADI YA WANACHAMA
Mfuko umeendelea kukua kwa upande wa uanachama ambapo hadi kufikia mwezi Juni 2013, tulikuwa na jumla ya wanachama 224,193 ukilinganisha na wanachama 203,981 kwa mwezi Desemba 2012

Matumizi ya mifumo ya habari:
Mfuko umefanikiwa sana katika nyanja ya teknolojia kwa kuweza kulipa mafao kwa kutumia mtandao, hivyo kulipa kwa wakati.

Vile vile Mfuko umepunguza matumizi ya karatasi yaani ‘paper work’ kwa kurahisisha malipo kwa wanachama na kwa upande wa watoa huduma tunatumia  mfumo wa ‘E-banking’ yaani pesa zinatumwa moja kwa moja kwenye akaunti ya mhusika.

Kupitia mifumo ya kisasa ya PPF, mwanachama anaweza kupata taarifa zake za michango, dai au pensheni kwa mstaafu kupitia simu ya kiganjani au tovuti ya Mfuko ambayo ni www.ppftz.org
Mwanachama anaandika neno michango anaacha nafasi anaweka namba ya   uanachama na kutuma kwenye namba 15553.

Si hivyo tu , bali hata mwajiri anaweza kupata taarifa za michango ya wafanyakazi wake akiwa katika sehemu yake ya kazi bila kwenda katika ofisi za PPF hii inaokoa muda na pia kuongeza uhakika wa uwasilishwaji wa michango ya wanachama.

Kwa kutambua umuhimu wa matumizi ya mifumo ya habari mwaka huu 2013 katika wiki ya Hifadhi ya Jamii, Mfuko wa Pensheni wa PPF ulitunukiwa hati ya  utambuzi kama Mfuko bora kwenye matumizi ya Mifumo ya habari. Hati hiyo ilitolewa na Mhe. Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,kwa kuwa Mfuko bora katika Nyanja ya mifumo ya habari kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwenye kutoa huduma mbalimbali.

Utoaji wa Mikopo ya SACCOS
PPF ni waanzilishi wa mikopo ya SACCOS tulianza kutoa mikopo ya saccos mwaka 2004.
Tunatoa mikopo hii kupitia SACCOS za wanachama wetu zilizopo kwenye maeneo yao ya kazi.
Mpaka sasa tumeshatoa zaidi ya Billioni 56 kwenye SACCOS 46

Tuzo katika Utawala bora
Kwa kutambua uwazi katika uendeshaji wa Mfuko Umoja Mifuko ya hifadhi ya Jamii Duniani (issa) uliweza kutupatia Tuzo katika utawala bora kwa kuendesha shughuli mbali mbali kwa uwazi kama vile mikutano ya wanachama na wadau PPF huu ni mwaka wa 23 tuna desturi ya kukutana na wanachama na wadau wetu.
Hati safi kutoka kwa CAG kwa kuwa na mahesabu yaliyo safi
Uwekezaji ni mzuri ambapo tumewekeza katika sehemu mbalimbali kama vile hoteli za kitalii mfano East African Hotel Arusha na Gold Crest Mwanza ambapo watalii wengi wanafika hivyo inasaidia kwenye ukuaji wa Uchumi.

Tumewekeza kwenye ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa ajili ya kuwauzia wanachama wetu.PPF imekuwa Mfuko wa kwanza kwa kuanzisha miradi ya nyumba za bei nafuu.
Tulijenga nyumba 580 Kiseke Mwanza na tuliziuza kwa bei nafuu ya kati ya  shilingi millioni 16 mpaka million 33. Zoezi hili ni endelevu kwa mikoa mingine

Fao la Elimu:
PPF imekuwa Mfuko wa kwanza kuwa na Fao la elimu kwa watoto wa wanachama wetu.Ambapo lilianza kutolewa mwaka 2003 ambapo tangu tuanze kwasomesha kiasi cha shilingi billion 3.6

LENGO
Katika Mpango mkakati wa Mfuko kwa kipindi cha miaka 3 (2013-2015) baadhi ya malengo ya Mfuko ni kama ifuatavyo:
Thamani ya Mfuko ni kukua kutoka trillion 1.09 Desemba 2012 na kufikia trillion 2 ifikapo  Desemba 2015 Na Idadi ya wanachama kuongezeka kutoka wanachama 203,981 Desemba 2012 kufikia laki 4 Desemba 2015. Lengo kuongeza mara mbili thamani ya Mfuko

Mwisho kabisa ningependa kuwashukuru wanachama na wadau wote wa Mfuko kwa Mchango Mkubwa Mliotupa Hivyo tunaomba tuendelee kushirikiana kwa kuendelea kuwa wanachama wa PPF na wale ambao bado hamjajiunga na PPF tunaomba mjiunge ili muweze kuwa na uhakika wa maisha yenu ya sasa na baadaye.

RAIS KIKWETE AMTHIBITISHA ADAM MAYINGU KUWA MKURUGENZI MKUU WA PSPF

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Adam H. Mayingu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).
Taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam jana, Jumanne, Agosti 13, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi unaanzia Juni 8, mwaka huu, 2013.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mayingu alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wa PSPF.
Bwana Mayingu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bibi Hawa Mmanga ambaye amestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
 
14 Agosti, 2013

JK APATA JEZI NAMABA 10 YA BARCELONA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Kushilla Thomas akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete jezi iliyosainiwa na wachezaji wote wa timu ya FC Barcelona Ikulu jijini Dar es salaam jana ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuendeleza soka na ikiwa ishara ya kutambua ushirikiano wa kihistoria kati ya Castle Lager na FC Barcelona uliosainiwa hivi karibuni huko Camp Nou Hispania. Wanaotazama ni Meneja Mauzo wa TBL Kanda ya Kusini James Bokella (wa kwanza kulia) na Meneja Masoko wa TBL Bi. Natalia Celani (wa pili kulia). Na kushoto ni Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo na Aggrey Marealle, Mkurugenzi wa Executive Solutions washauri wa mahusiano wa TBL.
 wakiwa katika picha ya kumbukumbu mara baada ya makabidhiano.
Jezi hii sasa iliwekwa katika Fremu maalum ambayo itawekwa ukutani.

MAKUMBUSHO WAFUZU MAFUNZO YA ULINZI SHIRIKISHI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana(kulia) akimkabidhi cheti, Mtendaji wa Kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni , Husna Nando wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ulinzi shirikishi  Dar es Salaam jana.Picha na Michael Machellah.
Mhitimu wa mafunzo ya Ulinzi shirikishi kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni ,Ally Vumbi(kushoto)akipiga saluti kwa Mkuu wa Wilaya, Jordan Rugimbana mara baada ya kutunukiwa cheti baada ya kumaliza mafunzo ya ulinzi shirikishi Dar es Salaam jana.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani Mkuu wa mafunzo ya Ulinzi Shirikishi Kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni, Koplo Ibrahim Omari wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ulinzi shirikishi Dar es Salaam jana.
 


Mkuu wa mafunzo ya Ulinzi Shirikishi Kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni, Koplo Ibrahim Omari akitoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya Jordan Rugimbana kwa kupisha zoezi la kutoa mafunzo ya ulinzi shirikishi kuwa la Wilaya nzima wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ulinzi shirikishi Dar es Salam jana.



Baadhi ya Polisi jamii wa Barabara ya Kilwa,wakiwa kwenye gwaride na mbwa waliopewa mafunzo maalumu ya ulinzi shirikishi wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ulinzi shirikishi wa Kata ya Makumbusho Mwananyamala Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.


MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,Jordan Rugimbana ametoa muda wa miezi mitatu,Kata zote za Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ziwe zimeshaanzisha vikundi vya Ulinzi shirikishi na kiongozi yeyote atakaekaidi agizo hilo basi anashiriana na wahalifu.
Rugimbana aliyasema haya wakati wa hafla ya kukabidhi Vyeti kwa wahitimu wa 40 waliofuzu mafunzo ya ulinzi shirikishi kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo pia ametoa fursa ya baadhi ya wahitimu kwenda Polisi Kilwa Road kupata elimu ya kutumia Mbwa katikka kazi ya ulinzi shirikishi baada ya kuvutiwa na vijana wa Polisi jamii walioonyesha gwaride pamoja na mbwa katika hafla hiyo.
Alisema Rugimbana,”Nendeni mkafanye kazi na mtakapo pata kikwazo niambieni niko tayari kudili na mtu wa yeyote,kafanyeni kazi kwa ufasaha muipe sifa Kata ya Makumbusho na Wilaya nzima ya Kinondoni kwa kumaliza kabisha swala la uhalifu,madawa ya kulevya  pamoja na usafi wa mazingira”.
Rugimbana alisema kuanzia sasa mtu yeyete atakayekamatwa kwa uchafuzi wa mazingira faini ni fedha taslimu shilingi 50,000/= na hiyo pesa ni ya kwako wewe uliyemkamata.
 Aidha Mkuu wa Wilaya alichangia mfuko wa Polisi jamii Kata ya Makumbusho kiasi cha Shilingi 1,000,000/= pamoja na kuwa mlezi wa Polisi jamii wa Wilaya nzima.
Akitoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya,Diwani wa Kata ya Makumbusho, Ally Haroub aliwaomba wakazi wa makumbusho kutoa ushirikiano katika swala la ulinzi shirikishi ili kupunguza uhalifu, madawa ya kulevya na swala la mazingira kwa kutoa tofauti zao za kidini,kabila wala umri kwani kipindupindu hakichagui dini ,kabila wa la Kiongozi.
Mafunzo ya wahitimu ya vijana wa ulinzi shirikishi yametumia muda wa miezi miwili chini ya Koplo Ibrahim Omary kutoka kituo cha Polisi Ostarbay yenye madhumuni ya kuunganisha polisi na jamii ili kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano katika kuondoa kero za uhalifu,kutatua matatizo ya uhalifu na kuondoa hofu ya usalama wa jamii husika.
Wakisoma risala wahitimu hao kuwa mafunzo waliyopata ni huduma bora kwa wateja,ukakamavu,dhana ya polisi jamii,nidhamu,ukamataji salama wa mhalifu,uwasilishaji taarifa,sheria ndogo nogo za ulinzi,usafi na mazingira na pia walipata nafasi ya kutembelea kikosi cha mbwa na farasi.
Mwisho walizindua mfuko wa Ulinzi shirikishi ambao kila mwananchi atakayeguswa na huduma yao achangie ambayo ni 03201000035 Dar es Salaam Commuty Bank Tawi la Magomeni.

TRAFIKI FEKI ADAKWA AKILA VICHWA TABATA

$
0
0

 Askari Bandia wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliyekamatwa leo mchana maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya sare zake mara baara ya kukamatwa. Askari huyu feki amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa juu yake.
Afande huyo akiwa chini ya ulinzi wa Polisi mara baada ya kukamatwa mchana wa leo akila vichwa maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam.Askari huyu feki amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa juu yake.
Afande huyo akiwa Kituo cha Polisi Stakishari. Source: MICHUZI MEDIA
Viewing all 10616 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>