Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10590 articles
Browse latest View live

SWAHILI RADIO KUANZA KURUSHA MATANGAZO HEWANI HIVI KARIBUNI KUTOKEA JIJINI WASHINGTON D.C. USA

$
0
0
Mkurugkenzi wa Swahili Radio Bwana Dickson Mkama (DMK) akiwa hewani wakati  wa majaribio
Mkurugenzi wa Swahili Radio Bwana Alex Kassuwi (King) akiwa hewani akifanya majaribio
Bwana DMK akiendelea na majaribio ya kipindi chake cha Entertainment
  Alex Kassuwi akiweka mitambo sawa wakati wa majaribio
 DMK akikamilisha taratibu za mwisho mwisho kuingia hewani
  Alex akifurahia baada ya mitambo kuonyesha mafanikio katika majaribio
 Wakurugenzi wa Swahili Radio Bwana Alex na DMK wakiendesha kipindi cha majaribio hewani

SWAHILI RADIO
Ni Radio iliyoanzishwa Jijini Washington DC USA na Kampuni ya "MMK MEDIA GROUP LLC " ambao wanamiliki Swahili Radio On Line,Swahili TV on Line,Swahilitv Blog, Swahili Magazine USA-AFRICA,na The Bridge Show ndani ya DCTV.
 
Radio hii pamoja na TV ziko kwenye majaribio kwa sasa na zitaanza kuwa hewani kwa watu wote kusikiliza na kuangalia punde muda wa majaribio utakapo malizika.Watanzania hao watatu wote kwa pamoja wanayofuraha kubwa kwa jinsi ambavyo majaribio ya kazi hizi yanavyoendelea na kwa kingereza wanasema THEY CAN'T WAIT TO BRING TO YOU WHAT YOU HAVE BEEN WAITING FOR.

"PROGRAMS ZA RADIO KWA KUANZIA"

*KIPINDI CHA BURUDANI NA MICHEZO DUNIANI*
*MAPENZI NA MAISHA*
*MAISHA UGHAIBUNI*
*HABARI ZA DUNIA*
*THE WEEKEND SPECIAL*

KWA HABARI ZAIDI TEMBELEA SWAHILITV.BLOGSPOT.COM

DKT. FENELLA AKUTANA NA WADAU WA FILAMU NA KUZUNGUMZA NAO.

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Waziri Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na Viongozi wa Steps (hawako pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake kwa mazungumzo juu ya maendeleo ya kazi za sanaa jijini Dar es Salaam.




Mtaalum Mshauri Bw. Sanctus Mtsimbe akiomuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt Fenella Mukangara (hayupo pichani) moja ya kazi yake  iliyopitia taratibu zote na ambayo hakimiliki ni yake mwenyewe.





Moja ya viongozi wa Steps Entertainment Bw. Jairaj Damodaran akifafanua jambo wakati wa kikao na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara.


Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamun Tanzania pamoja na Mkurugenzi wa Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko wakisikiliza majadiliano wakati wa mazungumzo kati ya Steps na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara jijini Dar es Salaam.
                                                            *********
Na Benedict Liwenga-MAELEZO
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara amekutana na wadau wa Kampuni ya Steps Entertainment  na kuzungumza nao juu ya maendeleo ya Tasnia ya Filamu nchini. Ujumbe huo wa Steps ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Dileshi Solanki .

Katika mazungumzo hayo Dkt. Fenella amegusia masuala ya uharamia katika  kazi za filamu nchini na kutia mkazo katika suala zima la maadili. Aidha Waziri ameeleza kuwa kuanza kwa urasimishwaji wa tasnia ya filamu na muziki unaoendelea kutekelezwa nchini kutasaidia sana kuondosha kazi zisizohalali. 

Aidha, Dkt. Fenella amewashauri wadau  wa tasnia ya filamu nchini washirikiane kikamilifu na Serikali katika kuendeleza na kukuza tasnia ya filamu na pia kuhakikisha wasanii wananufaika na jasho lao. Aidha ameeleza umuhimu wa kutoa elimu kwa wadau  na umma kwa ujumla juu ya fursa nyingi zilizopo katika tasnia.

Kwa upande mwingine Waziri Dkt. Fenella ameshauri pia kuwe na majumba maalum kwa ajili ya kuonyeshea sinema ambayo yatakuwa yanazipa kipaumbele filamu za kitanzania  pia amehamasisha wadau wa filamu kuanzisha majumba hayo na ambao tayari wameanzisha kutoa fursa hiyo ili kuziendeleza kazi za filamu za kitanzania.

“Kuwe na majumba ya kuonyeshea sinema ambayo yatakuwa yanazipa kipaumbele filamu za kitanzania”. Alisema Dkt. Fenella.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo alibainisha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la filamu zinazowasilishwa kwa ukaguzi na pia wadau wameanza kutumia stempu za TRA katika kazi za filamu na muziki ili kuzilinda kazi hizo. Stampu zilianza kutolewa tangu mwezi Januari mwaka huu .

Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mkuu Bw. Dileshi Solanki wa Kampuni ya Steps Entertainment ameiahidi Serikali kupitia Waziri wa Habari, Vijana na Utamaduni na Michezo Mhe Dkt Mukangara, kuendelea kuendeleza tasnia ya filamu kwa kushirikiana kikamilifu na serikali na kupiga vita uharamia dhidi ya filamu za kitanzania . Aidha wameiomba serikali kuendelea kuwajengea mazingira mazuri.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA BARRICK GOLD

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu Rais na mtendaji mkuu  wa African Barrick Gold Bwana Greg Hawkins na kufanya naye mazungumzo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais na mtendaji Mkuu wa African Barrick Gold Bwana Greg Hawkins(wapili kushoto) ikulu jijini Dar es Salaam leo.kushoto ni Afrisa mwandamizi wa African Barrick Gold Bwana Deo Mwanyika

WANAHABARI WAPEWA SOMO JUU YA MASWALA YA MAZINGIRA NA USAFIRI JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Mratibu wa Kongamano la siku moja kwa Wadau wa Habari na Mawasiliano hapa nchini,kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi,Prof. Msafiri Jackson akiwasilisha mada yake iliyohusu Uchafuzi wa Hewa pamoja na kelele,wakati wa Semina ya kuwafundisha Wanahabari namna ya kufikisha habari kwa jamii juu ya maswala ya Usafiri na Mazingira iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Semina ya siku moja kwa Wadau wa Habari na Mawasiliano hapa nchini,kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi,Prof. Msafiri Jackson akiwasilisha mada yake iliyohusu Uchafuzi wa Hewa pamoja na kelele,wakati wa Semina ya kuwafundisha Wanahabari namna ya kufikisha habari kwa jamii juu ya maswala ya Usafiri na Mazingira katika mtandao wa Kisayansi na Teknolojia iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa habari kutoka EATV,Sophia Mganya akiwasilisha Mada yake wakati wa semina hiyo ya kuwafundisha Wanahabari namna ya kufikisha habari kwa jamii juu ya maswala ya Usafiri na Mazingira katika mtandao wa Kisayansi na Teknolojia liyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wadau wa Maswala ya Habari na Mawasiliano wakifatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye Semina hiyo.

MOTO KUWAKA REDD'S MISS ILALA LEO

$
0
0
Mratibu wa Shindano la Redds Miss Tanzania Kanda ya Ilala 2013, Juma Mabakila (katikati waliokaa), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitangaza zawadi watakazopewa washindi wa shindano hilo litakalofanyika leo kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Dar es Salaam. Kutoka kushoto waliokaa ni Mkufunzi wa warembo hao Hafsa na William Malecela.

NGASA KUCHEZEA YANGA AKIMALIZA KIFUNGO CHA MECHI SITA

$
0
0
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga baada ya kukamilisha usajili wake.
 
Hata hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imebaini kuwa Ngasa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa na mkataba na Azam) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (sh. milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.
 
Kamati pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo.
 
Vilevile Kamati imepitia pingamizi zote zilizowasilishwa kuhusu usajili wa wachezaji, kukatiza mikataba ya wachezaji na kuzitaka klabu husika ziwe zimetatua masuala hayo hadi Alhamisi (Agosti 22 mwaka huu).
 
Kwa upande wa wachezaji wa kigeni, Kamati imeagiza wasiruhusiwe kucheza hadi watakapopata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) pamoja na vibali vya kufanya kazi nchini (work permits).
 
Kamati hiyo itakutana tena Ijumaa (Agosti 23 mwaka huu) ili kupata ripoti za pingamizi ilizoagiza ziwe zimefanyiwa kazi hadi Agosti 22 mwaka huu na kutoa uamuzi kwa pande ambazo hazikuafikiana.
 
UCHAGUZI TFF SASA KUFANYIKA OKTOBA 27
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuzingatia mamlaka iliyonayo katika kifungu cha 10(6) cha Kanuni za Uchaguzi za TFF inasogeza mbele tarehe ya uchaguzi wa TFF kutoka Oktoba 20 mpaka Oktoba 26 na 27 mwaka huu.
 
Sababu za kusogeza mbele uchaguzi ni kutokana na ukweli kuwa Oktoba 20 mwaka huu uongozi wa TFF utakuwa na shughuli nyingi za maandalizi ya mechi ya Simba na Yanga, na hivyo haitawezekana kusimamia shughuli za Mkutano Mkuu wa Uchaguzi kwa wakati mmoja na mchezo huo.
 
Siku ya mwisho ya kampeni itakuwa Oktoba 25 mwaka huu. Ukiondoa  mabadiliko hayo ya tarehe ya uchaguzi wa viongozi wa TFF, ratiba ya mchakato wa uchaguzi na itabaki kama ilivyotangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari Agosti 24 mwaka huu.
 
Pia Kamati imeamua kuwa uchaguzi wa Bodi ya Ligi utabakia kuwa Oktoba 18 mwaka huu kama ilivyopangwa awali.
 
Kamati imesema inaamini wahusika wote watapokea vizuri mabadiliko hayo na inasikitika kwa usumbufu utakaosababishwa na mabadiliko hayo.

MISS TANZANIA BEAUTY PAGEANT USA KUFANYIKA DECEMBER WASHINGTON DC

$
0
0
  ANY INFOS FOR NOW CALL 202-830-8904

KONYAGI YAWAPIGA MSASA WAHARIRI JUU YA KUTHAMINI BIDHAA ZA NDANI

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (kushoto), akieleza mafanikio ya TDL ikiwa ni pamoja jinsi inavyolipa kodi serikalini ambapo kwa mwezi hulipa sh. bil. 7.  Mgwassa alikuwa akizelezea mafanikio hayo wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari ya kuwajengea uwezo wa kuthamini bidhaa za ndani leo kwenye Hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.Kulia ni mgeni rasmi katika semina hiyo, Mbunge wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Tanzania, Mussa Zungu.

 Mgeni rasmi katika semina hiyo, Mbunge wa Jimbo la Ilala ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu, akitoa pongezi kwa Mkurugenzi wa TDL, David Mgwassa kwa kukipatia mafanikio makubwa kiwanda hicho.
 Mkurugenzi wa Masoko wa TDL, Joseph Chibehe 9kulia) akielezea mbele ya wahariri, historia ya kinywaji cha Konyagi.
 Baadhi ya wahari walioalikwa kwenye semina hiyo, wakisikiliza kwa makini wakati Chibehe aielezea historia ya TDL.
 Seheumu ya wahariri wa vyombo vya habari waliohudhuria semina hiyo
 Baadhi ya wahari walioalikwa kwenye semina hiyo, wakisikiliza kwa makini wakati Chibehe aielezea historia ya TDL.
 Picha juu na chini ni baadhi ya wahariri na wanahabari wakiwa katika semina hiyo iliyoandaliwa na TDL.

 Mgeni rasmi, Mussa Zungu 9katikati waliokaa) akiwa na MD wa TDL , Mgwassa, Mkurugenzi wa Masoko, Chibehe katika picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya habari nchini.
 MD wa TDL, Mgwassa (katikati) akimuaga Mussa Zungu. Kulia ni Chibehe.
Baadhi ya wahariri walioalikwa kwenye semina hiyo, wakisikiliza kwa makini wakati Chibehe aielezea historia ya TDL. PICHA  ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

UNGA WAKAMATWA HONG KONG NDANI YA CHUMA CHA MASHINE

$
0
0
Wakati vita ya kupambana na wafanya biashara wa dawa za kulevya nchini Tanzania ikisha kasi kwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harison Mwakyembe kuweka bayana majina ya Wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JNIA walio husika katika zoezi la kufaulisha mabegi 9 yaliyo na dawa za kulevya kwenda Afrika Kusini,Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na heroin ikiwa ndani ya mashine
Waziri Mwakyembe aliwataja watu hao leo ambao ni maofisa usalama, Polisi na mbeba mizigo wa uwanja huo wa Ndege wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere.

Lakini hayo yakitokea nchini Tanzania kwa Waziri wa Uchukuzu kula kiapo cha wanaolidhalilisha jina la baba wa Taifa kupitisha madawa ya kulevya.

Kwa mara nyingine jana tarehe 15/8/2013, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.

Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za hongkong (167,500 us dollars)

Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.

Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni kifungo cha maisha na faini ya dola milioni 5 za hongkong.

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WAOMBOLEZA KIFO CHA KATIBU MKUU IKULU MSTAAFU ABEL MWAISUMO.

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuomboleza na kufariji wafiwa  kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu, Abel Mwaisumo, aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay  Dar es Salaam.
Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo  kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu, Abel Mwaisumo, aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo huku Mama Salma Kikwete akisubiri zamu yake wakati walipokwenda kuomboleza na kufariji wafiwa  kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu, Abel Mwaisumo, aliyefariki juzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay Dar es Salaam.
Mama Salma Kikwete akifariji wafiwa wakati yeye na Rais Kikwete walipokwenda kuomboleza na kutoa pole kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu, Abel Mwaisumo,aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wengine wakiomboleza na kufariji wafiwa  katika  msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu, Marehemu, Abel Mwaisumo, aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu, Abel Mwaisumo, aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay Dar es Salaam>(PICHA NA IKULU).

RAIS KIKWETE APOKELEWA NA RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI KWA FURAHA LEO

$
0
0
Rais Joyce Banda wa Malawi akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amuda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lilongwe tayari kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC leo

MABINGWA BONANZA LA SERENGETI FIESTA WAPATIKANA KIGOMA

$
0
0
Nahodha wa timu ya mashabiki wa Arsenal mkoani Kigoma Samweli Balina akipokea kombe la ushindi na kitita cha fedha taslimu laki tatu kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba baada ya kuibuka washindi katika bonanza la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza lililofanyika siku ya ijumaa jioni katika uwanja wa Kawawa uliopo Ujiji,  anayeshuhudia kulia ni meneja wa biashara wa kanda ya ziwa kutoka kampuni ya bia ya Serengeti  Bw. Octavian Migire, na Katibu wa Chama cha soka mkoani Kigoma Bw. Mrisho Bukuku, Bonanza hilo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager. Timu za mashabiki zilizoshiriki bonanza hilo ni Chelsea, Liverpool, Real Madrid, Barcelona, Bayern Munich, AC Milan.



Nahodha wa timu ya mashabiki wa Manchester United mkoani Kigoma akipokea kombe la ushindi wa pili na kitita cha fedha taslimu laki mbili kutoka kwa meneja wa biashara kanda ya ziwa kutoka kampuni ya bia ya Serengeti  Bw. Octavian Migire anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba baada ya kuibuka washindi wa pili katika bonanza la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza lililofanyika siku ya ijumaa jioni katika uwanja wa Kawawa uliopo Ujiji,  , na Katibu wa Chama cha soka mkoani Kigoma Bw. Mrisho Bukuku (mwenye Kaunda suti), Bonanza hilo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager. Timu za mashabiki zilizoshiriki bonanza hilo ni Chelsea, Liverpool, Real Madrid, Barcelona, Bayern Munich, AC Milan.



Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Yanga, Said Sued “Scud” wa pili kulia waliosimama akiwa katika picha ya pamoja na mashabiki wenzake wa timu ya Arsenal ya Uingereza katika bonanza la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza lililofanyika katika uwanja wa Kawawa uliopo Ujiji mjini Kigoma. Kushoto kwake ni Mchezaji bora wa bonanza hilo Mawazo Said. Arsenal waliibuka washindi na kujinyakulia kitita cha shilingi laki tatu. Timu za mashabiki zilizoshiriki bonanza hilo ni Chelsea, Liverpool, Real Madrid, Barcelona, Bayern Munich, AC Milan.

DORICE MOLLEL NDIYE REDD’S MISS ILALA 2013

$
0
0


Redds Miss Ilala  Dorice Mollel (katikati) akipozi na washindi wenzake. Kutoka kulia ni mshindi wa pili Alice Isaac na mshindi wa tatu Clara Bayo.
  *************
Mwandishi Wetu
Miss Tabata  Dorice Mollel  (22) usiku wa kuamkia jana aliwashinda warembo wengine 13 kushinda Redds Miss Ilala 2013 katika shindano iliyofanyika kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Dar es Salaam.

Dorice alimrithi Noela Michael ambaye alishinda taji hilo mwaka jana pia akitokea Tabata.

Dorice alizawadiwa 1.5milioni/-, na mshindi wa pili Alice Isaac (Dar City Centre) alipata 1milioni /-.


Mshindi wa tatu katika shindamo hilo ni Clara Bayo (Dar City Centre) ambaye  alizawadiwa 700,000/-. Mshindi wanne Pendo Lema (Tabata) alizawadiwa 400,000/- na watano  Shamim Mohamed alipata 300,000/-.

Mrembo Juanita Kabunga kutoka Tabata alizawadiwa 500,000/- baada ya kushinda Miss Talent na Kabula Kibogoti pia kutoka Tabata alishinda taji la Miss Rio and Spa na kuzawadiwa 200,000/- na ajira ya kudumu kwenye kampuni hiyo.

Warembo waliosalia kila moja alipata kifuta jasho cha 200,000/-.
Warembo hao ni Clara Paul, Anna Johnson, Irene Mwelolo, Rehema Mpanda,  Martha Gewe, Diana Joachim, Natasha Mohamed,  Kazumbe Mussa, Kabula Kibogoti na Juanita Kabunga.

UDHAMINI WA CASTLE LAGER KWA FC BARCELONA KUINUFAISHA TANZANIA

$
0
0


Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwenye mkutano na waandishi wa habari kutangaza udhamini wa Castle Lager kwa klabu ya FC Barcelona  ya nchini Hispania, (kushoto) ni  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kushilla Thomas.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kushilla Thomas (kushoto), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kutangaza udhamini wa Castle Lager kwa klabu ya FC Barcelona  ya nchini Hispania, kulia ni Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo. 

                                                                                               *******
Baada ya kutangazwa kwa udhamini wa miaka mitatu wa bia ya Castle Lager kwa moja ya FC Barcelona, moja ya klabu maarufu zaidi duniani, leo hii udhamini huo unazinduliwa rasmi hapa Tanzania.  huu unafanyika.

Udhamini huu unaifanya Castle Lager kuwa Bia rasmi ya FC Barcelona barani Afrika hususani hapa Tanzania na nchi nyingine 10 barani Afrika ambapo Castle Lager itakuwa kinywaji rasmi pia kwenye shughuli zote za klabu ya FC Barcelona katika nchi hizi. 

“Udhamini utaleta manufaa mengi kwa wanywaji wa Castle Lager na mashabiki wa FC Barcelona nchini Tanzania kupitia promosheni mbalimbali na hii itaongeza umaarufu wa timu hii hapa Tanzania na barani Afrika kwa ujumla,” alisema Kushilla Thomas, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania. 

Hii ni mara ya kwanza kwa FC Barcelona kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya Kiafrika jambo ambalo litawafungulia milango mashabiki wa FC Barcelona nchini Tanzania na nchi nyingine barani kuweza kupata bidhaa, matukio ya kukumbukwa na nafasi za kushinda safari safari ya kwenda Barcelona Hispania kuitembelea klabu. 

“Tumefurahi kusaini mkataba na Castle Lager, chapa inayofahamika dunia nzima. Tunafanana mila na desturi na Castle Lager na sote tuna historia ya miaka zaidi ya 100. Pia kama tulivyo sisi Barcelona, bia ya Castle Lager ina mapenzi makubwa kwaa mpira wa miguu pamoja na mashabiki barani Afrika,” alisema Javier Faus, Makamu wa Rais wa Barcelona anayeshughulikia Uchumi.

Castle Lager imekuwa ikijihusisha na na mpira wa miguu barani Afrika kwa muda wa miaka 85 ambapo hivi sasa inadhamini ligi za soka katika nchi za Zimbabwe, Swaziland na Lesotho. Pia Castle Lager ni mdhamini wa mashindano ya COSAFA yanayofanyika Kusini mwa Afrika na CECAFA yanayofanyika Afrika Mashariki. 

Kutokana na mpira wa Ulaya kupata umaarufu mkubwa na mashabiki barani Afrika, Castle Lager kwa miaka mingi imekuwa mdhamini wa matangazo ya mashindano mbalimbali ya mpira na kuwapatia mashabiki nafasi ya kuangalia mechi za Klabu bingwa Ulaya, ligi kuu ya Uingerereza na ligi kuu ya Hispania kupitia luninga.

Watumiaji wa CASTLE Lager pamoja na mashabiki wa FC Barcelona hapa Tanzania sasa watarajie mambo makubwa kwani udhamini huu utawaletea mambo mengi ya kusisimua. 


MASWALI NA MAJIBU KWA MKURUGENZI WA MASOKO WA TBL, BI. KUSHILLA THOMAS

1. Je Ushirikiano huu unahusu nini?
Ushirikiano huu unaifanya, Castle Lager kuwa Bia rasmi Ya Afrika inayodhamini FC Barcelona.Castle ni bia  bingwa ya Afrika ambayo inajitahidi kusimamia na kuendeleza ukamilifu/ubora wake wakati FC Barcelona ni timu bingwa ambayo daima inalenga kufikia mafanikio zaidi. Huu ni ushirikiano imara na ni matokeo ya mapenzi yetu kwenye soka

2. Unajisikiaje kuhusiana na ushirikiano huu?
Nina msisimko mkubwa kuhusiana na ushirikiano huu na FC Barcelona  na Nina furaha kusema kwamba ushirikiano huu utaimarisha uhusiano kati ya Castle Lager na wateja wake wa Afrika ambao ni mashabiki wazuri wa timu hii ambayo inaangaliwa na kufuatiliwa na wapenzi wa soka duniani kote.

3. Castle itafaidika vipi na ushirikiano huu?
Kupitia ushirikiano huu, Castle Lager itakuwa ni bia pekee Afrika yenye haki za kipekee kutumia  Nembo ya FC Barcelona, rangi, na picha za wachezaji katika mawasiliano ya bidhaa ya Castle kama vile matangazo ya aina zote nk. Tunaamini kwamba ushirikiano huu Utajenga uhusiano kati ya FC Barcelona na watumiaji wa bia ya Castle Lager.  Aidha kutakuwa na shughuli mbalimbali zinazohusu kuendeleza mpira Tanzania zikiendelea  na maeneo mengine ya Afrika inakopatikana bia ya Castle.

Bia ya Castle inatambuliwa kama mdhamini Mkuu wa mpira wa miguu na matukio mengine mengi ya michezo Afrika na kimataifa. Ushirikiano huu kati ya  Barca / Castle ni kilele cha mafanikio ya udhamini wa michezo.

4. Ina maana gani kwa mashabiki wa soka na watumiaji/wateja wa CASTLE katika
Nchi yako?

Tunataka kuhakikisha kwamba tunaimarisha undugu huu katika soka la Tanzania na hasa mashabiki wa FC Barcelona ambao ni sehemu ya ushirikiano huu wa kusisimua. Maelezo zaidi yatafafanuliwa wakati wa uzinduzi wa kitaifa jijini Dar es Salaam tarehe 17 Agosti na wapenzi wa soka wa Tanzania watashiriki katika mfululizo wa shughuli za soka za kikanda / kanda ambazo ni za kuhamasisha. Kutakuwa na shughuli za kijamii, kuwazawadia mashabiki wetu waaminifu wa Castle/Barca.  Kupitia ushirikiano huu Castle Lager itahakikisha kila shabiki anafurahia wakati kamili

5. Je Ushirikiano huo utakuwa na manufaa chanya kwenye jamii Nchini  kwako?.

Hakika, Mashabiki wa Barcelona Tanzania na jamii zao kuna mengi ya kusuburia, Castle Lager ina mipango mikubwa ya kuifikia jamii kwa maendeleo kwenye mikoa zaidi ya nane nchini. 

Tunataka kuhakikisha kwamba tunaimarisha undugu huu katika soka la Tanzania na hasa      mashabiki wa FC Barcelona ambao ni sehemu ya ushirikiano huu wa kusisimua. Maelezo  zaidi yatafafanuliwa wakati wa uzinduzi wa kitaifa jijini Dar es Salaam tarehe 17 Agosti na wapenzi wa soka wa Tanzania watashiriki katika mfululizo wa shughuli za soka za kikanda /  kanda ambazo ni za kuhamasisha. Kutakuwa na shughuli za kijamii kuwazawadia mashabiki wetu waaminifu wa Castle/Barca.  Kupitia ushirikiano huu Castle Lager itahakikisha kila shabiki anafurahia.

CLOUDS MEDIA WATOA DARASA KWA WANA KIGOMA JUU YA FURSA ZILIZOPO MKOANI HUMO

$
0
0
Mkuu mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu,Mh Issa Machibya akizungumza machache wakati wa ufunguzi wa Semina ya Fursa kwa vijana zinazopatikana ndani ya mkoa wa Kigoma na kwingineko,mapema leo asubuhi.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group ambao ndio waratibu wa tamasha kubwa la burudani hapa nchini la Fiesta 2013,imehudhuriwa na vijana mbalimbali kutoka kila pembe ya mkoa huo wakiwemo na wasanii mbalimbali maarufu kutoka jijini Dar,ambao wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo jioni ya leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.Aidha katika Semina hiyo ya Fursa,baadhi ya vijana wengi walionekana kuvutiwa kwa kiasi kikubwa kwa yaliyokuwa yakizungumziwa,ikiwemo suala la ujasiliamali.
 Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akimkaribisha mgeni rasmi wa semina hiyo,Mh Issa Machibya mapema leo asubuhi,kwenye ukumbi wa Kibo Peak,uliopo Kigoma mjini,kulia kwake ni msanii mahiri wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto ambae pia likuwa ni mmoja wa watoa mada kuhusiana na suala zima la Fursa.Semina hiyo imewashirikisha wadau mbalimbali,wakiwemo NSSF,Wasanii wa Bongofleva,wakazi  wajasiliamali mbalimbali ndani ya mji wa Kigoma.
 Pichani juu ni baadhi ya Wasanii wa Bongofleva na wadau wengine wakiwemo wakazi wa Kigoma wakisiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo kuhusiana na fursa mbalimbali. 
 Sehemu ya Meza kuu ikishangilia jambo,kutoka kushoto ni Kaimu Meneja wa NSSF mkoani Kigoma,Bwa.Said Abdallah,Mkuu wa Wilaya ya Uvinza ambae alikaimu pia nafasi ya Mkuu wa wilaya ya Kigoma mjini,Mh.Khadija Nyembo,Mkuu wa Mkoa,Mh.Issa Machibya,Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji kutoka  Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,Msanii Mrisho Mpoto (haonekani) pamoja na msanii wa muziki wa kizazi kipya,ajulikanae kwa jina la kisanii AY.
 Baadhi ya Wasanii wa bongofleva ambao wanatarajiwa kutumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,wakitambulishwa kwa wakazi wa Kigoma,wakati wa kuanza kwa semina ya Fursa iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Kibo Peak mjini humo.
 Mkali wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya wakazi mbalimbali wa mji wa kigoma,alipokuwa akiielezea mada mojawapo iliyohusiana na fursa mbalimbali zilizomo ndani ya mji huo na wakazi wake.
Baadhi akina mama walioshiriki semina hiyo wakijadiliana jambo huku wakinukuu baadhi vipengele vilivyowagusa kwa namna moja ama nyingine.
Baadhi ya Wasanii wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo,kushoto ni Mwana FA,Sheta,Joe Makini.
  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza mbele ya umati wa vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye semina ya Fursa,mapema leo asubuhi.Mutahaba aliwafungua vijana wa mji huo kwa kuzichambua mada mbalimbali zilizohusu Fursa ndani ya mkoa wao,ikiwemo nini maana ya fursa,kishindo cha fursa pamoja na mada nyingine iliyohusu Fursa katika kuongeza thamani.
 Baadhi ya vijana mbalimbali kutoka ndani ya mkoa wa Kigoma wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi kwenye ukumbi wa Kibo Peak.
 Kaimu Meneja wa NSSF mkoani Kigoma,Bwa.Said Abdallah akifafanua Fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya shirika la NSSF,zikiwemo za kujiunga na shirika hilo kurahisisha upatikanaji wa mikopo,matibabu na mambo mengine mbalimbali,aidha Bwa,Said amewataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha na shirika la NSSF ambako wanaweza kunufaika na huduma mbalimbali na zenye uhakika.
 Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya na mfanyabiashara,Ambwene Yesaya a.k.a AY akitoa ushuhuda wake na mifano mbalimbali  katika Semina ya Fursa,kuhusiana na fursa alizozipata na kuzifanyia kazi,na kumpelekea mafanikio aliyonayo mpaka sasa,AY amewataka vijana kutokuwa na moyo wa kukata tamaa haraka katika mambo yao wayafanyayo na pia kujali suala la muda katika mambo yao wayanayojishughulisha nayo. 
Mratibu Mkuu wa Semina ya Fursa,ambaye pia ni Mtangazaji wa Clouds FM,Gerald Hando akitoa utaratibu wa ushiriki kwa wadau mbalimbali waliojitokeza kwa wingi mapema leo asubuhi kwenye ukumbi wa Kibo Peak.Semina hiyo ilioonesha mafanikio makubwa kwa wakazi wa Kigoma,iliwakutanisha Wadau mbalimbali wakiwemo NSSF;Lake Oil,Wasanii wa Bongofleva na wengine wengi . Picha zote na Michuzjr-Kigoma.

YANGA YAILAMBA AZAM 1-0 NGAO YA JAMII HII LEO

$
0
0
BAO pekee la kiungo Salum Abdul Telela jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC na kutwaa Ngao ya Jamii.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Oden Mbaga, aliyesaidiwa na Hamisi Chang’walu na Omar Kambangwa wote wa Dar es Salaam, hadi mapumziko Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Yanga ilipata bao hilo mapema tu dakika ya pili, mfungaji kiungo Salum Abdula Telela aliyeunganisha pasi ya Didier Kavumbangu.

Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea kucheza vizuri na kukosa mabao zaidi, huku sifa zaidi akistahili kipa chipukizi Aishi Manula.

Dakika ya 67 Telela alikarbia kufunga tena baada ya kuunganishia nje krosi nzuri ya Haruna Niyonzima.

Dakika ya 81 Niyonzima alikaribia kufunga mwenyewe kwa mpira wa adhabu, lakini shuti lake liligonga mwamba wa juu na kudondokea chini kabla ya beki Aggrey Morris kuondosha katika hatari.

Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’/Deo Munishi ‘Dida’ dk15, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Mbuyu Twite dk15, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Salum Telela, Jerry Tegete/Hussein Javu68, Didier Kavumbangu na Haruna Niyonzima.

Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni/Joackins Atudo dk46, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Himid Mao, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’/Gaudence Mwaikimba dk74, Kipre Balou/Ibrahim Mwaipopo dk62 na Khamis Mcha. SOURCE: BIN ZUBERI BLOG.

WAKAZI WA KIGOMA WALIPOKEA KWA KISHINDO TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013

$
0
0
Pichani ni msanii wa bongofleva aJulikanae kwa jina la Shilole na madansa wake wakiwachengua vilivyo wakazi wa Kigoma,waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia kwenye jukwaa la tamasha la Serengeti Fiesta 2013,usiku huu kwenu uwanja wa Lake Tanganyika.
 Sehemu ya umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu wakiburudika na Wasanii wa Serengeti Fiesta 2013
 Burudani ya kutosha kabisa
 Hapatoshi ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu.
 Mwanamuziki mahiri wa muziki wa Dansi,Christian Bella akikamua jukwaani usiku huu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,mkaoni Kigoma ambapo watu wamefurika ile mbaya.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cassim Mganga akiimba jukwaani mbele ya maelfu ya wakazi wa Kigoma ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.
 Sehemu ya umati wa watu waliofurika ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu
 Msaniii anekuja kwa kasi kwenye miondoko ya Hip Hop,Stamina akikamua jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Kigoma waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta
 Ni Shangwe tu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma usiku huu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea
 Yaani hapatoshi kabisa,wakazi wa Kigoma wamecharuka na burudani murua kabisa ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rachael kutoka THT,akionesha umahiri wake wa kutumbuiza jukwaani usiku kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Washabiki wa tamasha la Fiesta wakifuatilia kwa makini yanayojiri usiku huu ndani y uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Wadau nao wamejitokeza kwa wingi
Peter Msechu na densa wake wakikamua vilivyo usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.

FOOLISH AGE YA LULU KUZINDULIWA MWISHO WA MWEZI HUU NDANI YA MLIMANI CITY

$
0
0

 Msaani mwenye kipaji cha Hali ya juu nchini na Mwenye umri mdogo Elizabeth Michael "LULU"anatarajia kuzindua filamu yake ya Kwanza tokea alipotoka Gerezani, Filamu hii iitwayo FOOLISH AGE ikiwa imetengezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited itazinduliwa Mnamo tarehe 30 August 2013 Katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam. Filamu hiyo inayoelezea Maisha ya LULU ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu kutokana na Kutengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited Katika Uzinduzi huo wa Filamu hiyo ya Lulu Wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi Band anatarajiwa kushusha bonge moja la burudani ya kufa mtu. 
Kupitia mtandao wa kijamii wa Lulu aliyejaaliwa kuwa na kipaji cha kuigiza na mwenye mvuto mbele ya runinga aliandika "Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu....!!!ninafuraha ya kuwafahamisha kuwa TAREHE 30/8/2013 ndio siku nitakayozindua movie yangu mpya iitwayo FOOLISH AGE....Hatimaye narudi kazini!!!!Uzinduzi utafanyika katika ukumbi wa MLIMANI CITY....kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa muziki....na pia LADY JAY DEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo pia!!!nahitaji support ya mashabiki wote wa LULU na mashabiki wa BONGO MOVIE.....♥♥♥♥!!!#PROINPROMOTERS"
Baada ya uzinduzi wa Filamu hii nakala zitaendelea kuuzwa katika maduka yote ya Filamu nchini na Filamu hii imetengenezwa na itakuwa inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited
Usikose uzinduzi Huu utakaofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City tarehe 30 August 2013

MBOWE AWATAKA WATANZANIA KUJADILI RASIMU YA KATIBA NA KUTOA MAONI VYEMA.

$
0
0
 IMG_2579
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh. Freeman Mbowe akihutubia wakazi wa wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza mwishoni mwa juma kwenye mkutano wa hadhara.
IMG_2543
Helikopta maalum iliyowabeba viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh. Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika walipowasili eneo la Mnada Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kufanya mkutano wa hadhara wilayani humo mwishoni mwa Juma.
 
IMG_2610
Mwananchi wa Geita ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akitoa maoni yake ya Rasimu ya Katiba Mpya mbele umati wa wafuasi wa Chadema na wakazi wa wilaya hiyo ambapo wengi wao wametaka Ushuru wa Masoko ufutwe pamoja na baadhi ya kinamama kulalamikia shida ya Maji kwenye Wilaya hiyo na Mh.Mbowe aliwaasa kutumia Mabaraza ya CHADEMA kuwasilisha maoni yao wakati wa mkutano wa hadhara.(Picha na Zainul Mzige waDewji Blog).
IMG_2604
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika akiteta jambo na mmoja wa viongozi wa Chadema wilayani Sengerema Hemedi Sabula wakati wa mkutano huo wa hadhara.
 
Na. Mwandishi wetu.
Mwenyekiti wa Chama cha Domekrasia na maendeleo (CHADEMA) Mh.FREEMAN MBOWE amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kujadili Rasimu ya Katiba mpya ili ipatikane Katiba itakayokidhi haja ya Watanzania.
 
Amesema hayo alipokuwa akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Sengerema mkoani waMwanza alipokuwa kwenye ziara ya kichama kuhamasisha wanachama wa chama hicho kuunga mkono kuwepo na Serikali tatu ndani ya Jumuiya ya Muungano wa Tanzania.
 
Amesema kuwepo Serikali tatu siyo mzigo kama Chama cha Mapinduzi (ccm) kinavyosema ila tunataka kuwepo serikali ya Tanganyika na Zanzibari na ile ya muungano ili kuleta usawa ndani ya Muungano huo.
 
Pia amesema kuwa Lugha ya Kiingereza na Kiswahili ipatiwe kipaumbele kufundishwa kuanzia daraja la awali hadi Chuo Kikuu ili kuwajengea Watanzania kufahamu Lugha ya Kiingereza vema na kupata ajira kwa urahisi.

Picnic ya wana DMV yafana

$
0
0
IMG_3637Kushoto Hellena Nyerere akiwa mama Kimolo mwenyekiti wa UWT-DMV , mdau na Julia Nyerere katika Picnic ya wana DMV iliyofanyika huko Wheaton Md mwishoni mwa juma. IMG_3624Kushoto mwenyekiti wa CCM DMV Bw.George Sebo akifuatiwa na Mama Kimolo na Katibu wa CCM-DMV Bw.Yakub Kinyemi. IMG_3659Makamu rais wa jumuiya ya Watanzania DMV Bw.Raymond akijipongeza. IMG_3663Bi.Grace Sebo mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya CCM DMV na dada Asha Hariz wa tano ladies wakijaza mapendekezo yao ya marekebisho ya katiba. IMG_3641Fomu ya marekebisho ya katiba kwa upande wa Marekani ilivyo. IMG_3613Mfugo ulikuwa wa kutosha. IMG_3618Bi.Grace Sebo akiwa na Elinita Mhando Shomari mtoto Rose Shomari. IMG_3651Brigedia General Maganga mwmbata wa kijeshi Washington Dc akiwa na Abbas akifuatiwa na Emanuel Muganda na Fella.Kwa picha zaidi ungana na sundayshomari.com
Viewing all 10590 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>