Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10588 articles
Browse latest View live

WERUWERU GOLDEN JUBILEE – ALUMNI MEETING

$
0
0
 Weruweru Golden Girls,
Please be advised that Alumni Meeting at Cine Club, Mikocheni B, on Sunday, September 1st, 2013 at 3:00pm.
 For registration and pledges please visit www.weruweru.mediart.co.tz
Let us all join together as we prepare for our Golden Jubilee
 “Kumanya, Kupenda, Huduma”

DOMITILA NJIKU SPECIAL NIGHT

$
0
0
Hakika ni usiku wa furaha sana kwa Binti Domitila Njiku ambapo amekutana na familia yake ndugu jamaa na marafiki pamoja na ndugu wa familia ya mumewe mtarajiwa katika chakula cha usiku cha kumuaga kabla ya ndoa yake. Tafrija hii ya aina yake inafanyika leo Agosti 29, 2013 katika Ukumbi wa Cassa ulipo Msasani kwa Nyerere jijini Dar es Salaam. Production by: MD Digital Company +255 717002303/+255 755 373999. WhatsAp: +255 788 207274.

 Domitila akikata keki ya Send Off  yake..
 Domitila akikabidhi keki kwa wakwe zake.
 Dada wa Bi Harusi, Joyce Njiku akiwa na rafiki yake Lilian Mkumbo a.k.a Bi harusi mtarajiwa.
 Sifa kubwa ya Biharusi Domitila ni tabasamu hatari ...
 Kwaito ipo kama kawa...
 Marafiki wa Bi harusi katika picha ya pamoja na Biharusi mtarajiwa.
Wasimamizi hawa maarufu sana mates.

PRESIDENT KIKWETE ARRIVES IN AUSTRIA ATTENDS UN-EUROPEAN COMMISSION'S HIGH LEVEL RETREAT IN AUSTRIA

$
0
0
President Jakaya Mrisho Kikwete is received by the Mayor of Salzburg, Mr Wilfred Haslauer at the Salsburg Airport in Austria on Thursday August 29, 2013 ahead of a High Level Retreat on “NEW IDEAS FOR A FAIR GLOBALISATION”. The retreat   is hosted and co-chaired by the President of the European Commission Mr Jose Manuel  Barroso and the UN Under-Secretary General for Humanitarian Affairs and Emergency Relief Coordinator, Ms Valerie Amos. 
The Tanzania flag flies alongside others of different countries at the Alpbach resort in Austria at the opening of the  High Level Retreat on “NEW IDEAS FOR A FAIR GLOBALISATION”. The retreat is hosted and co-chaired by the President of the European Commission Mr Jose Manuel  Barroso and the UN Under-Secretary General for Humanitarian Affairs and Emergency Relief Coordinator, Ms Valerie Amos. STATE HOUSE PHOTO

SBL YAUNGA MKONO KILIMO KWANZA

$
0
0
Wakulima wa shayiri katika kata ya Ngare Nairobi mkoani Kilimanjaro, wakikagua shayiri ya mkulima mwenzao ambaye alipata mbegu kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti. Kampuni hiyo iliwatembelea wakulima hao wa kanda ya kaskazini na  kujadili jinsi ya  kukuza kilimo cha zao hilo huku kampuni hiyo ikitatua matatizoyanayowakabili wakulima hao kwa kuwapatia pembejeo na kuwaahidi  kuwaletea mtaalam wa kupima udongo ili kujua ni mbolea gani dhabiti  itumike ili kupata mavuno yanayoridhisha..
Diwani wa kata ya Ngare Nairobi wilayani Siha,  mkoa wa Kilimanjaro akitoa maelekezo kwa wawakilishi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti ambao  ni Menaja mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Imani Lwinga(wa pili kushoto) pamoja na Meneja kilimo wa kampuni hiyo Shafii Mndeme(wapili kulia) wakati walipotembelea mashamba ya shayiri katika kata hiyo kwa lengo la kuwainua wakulima.
Menaja mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Imani Lwinga(kushoto) pamoja na Meneja kilimo wa kampuni hiyo Shafii Mndeme(kulia) wakikagua shayiri katika shamba la Bora Msaki mmoja ya wakulima wanaonufaika na mradi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti mkoani Kilimanjaro katika kata ya Ngare Nairobi wilayani Siha. Kampuni hiyo inaunga mkono kampeni ya Kilimo Kwanza kwa kuwapa mbegu na kuwahakikishia soko la kuridhisha wakulima wa shayiri kanda ya kaskazini.

AIRTEL YATOSHA ZIMEBAKI SIKU 5 KWA NYUMBA YA PILI

$
0
0
Airtel Yatosha inazidi kupamba moto. Zimebaki siku CHACHE SANA kwa wewe MTEJA wa Airtel kuibuka mshindi wa Nyumba ya kisasa ya Airtel Yatosha iliyojengwa na Shirika la nyumba la taifa (NHC) iliyopo maeneo ya kigamboni jijini Dar es saalam.

Meneja Uhusiano wa Airtel,Jackson Mmbando amesema “Siku ya Alhamisi tarehe 5 mwezi wa 9 ndio siku inayosubiriwa kwa hamu; ambapo tutapata mshindi wa nyumba ya pili ya promosheni ya Airtel Yatosha”

Wewe mteja wa Airtel Yatosha bado una nafasi ya kuibuka mshindi! Ni rahisi. Piga *149*99# sasa na ujiunge na kifurushi chochote cha SIKU, WIKI AU MWEZI cha Airtel Yatosha na moja kwa moja utaingia kwenye droo ya kushinda. Kumbuka, pia kuna Tsh milioni 1 kushindaniwa kila siku. Usilaze damu! Jiunge zaidid na Airtel Yatosha, uongeze nafasi zako zakushinda! Alidokeza bw, Mmbando

Airtel Yatosha. Na BADO!!
Meneja Uhusiano wa Airtel,Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari.

DK. MAHANGA ATEMBELEA VIWANDA, MASHAMBA YA CHAI NJOMBE

$
0
0
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,  Dk. Makongoro Mahanga (kulia) akioneshwa mitambo ya kuzalisha majani ya chai katika Kiwanda cha Chai cha Luponde, wilayani Njombe, alipofanya ziara ya kutembelea viwanda na mashamba ya chai  pamoja na kuzungumza na wafanyakazi. Kushoto ni Meneja wa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Antony Mwai.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,  Dk. Makongoro Mahanga akionja aina jibini (cheese) zinazozalishwa na Kiwanda cha Maziwa  cha CEFA Njombe, wilayani Njombe, alipotembelea kiwanda hicho hivi karibuni.
 Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (kushoto) akizungumza na Meneja Biashara wa Kiwanda cha Chai Luponde, Athanas Mwasamene alipotembelea hivi karibuni  shamba la majani ya chai-dawa (herbal tea) wilayani Njombe. Dk. Mahanga alifanya ziara wilayani humo ambapo alitembelea viwanda, mashamba ya chai pamoja na kuzungumza na wafanyakazi.
 Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Chai Luponde, wilayani Njombe,  Anthony Mwai (mbele) akimwonesha Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (katikati), shehena za chai-dawa (herbal tea) zinazozalishwa kiwandani hapo, tayari kusafirishwa kuuzwa nje ya nchi. Dk. Mahanga alifanya ziara wilayani humo ambapo alitembelea viwanda, mashamba ya chai pamoja na kuzungmza na wafanyakazi.

YAHAYA YA LADY JAY DEE YAMJAZA MAHELA LULU WAKATI WA UZINDUZI WA MY FOOLISH AGE.

$
0
0


UIMBAJI stadi wa Wibo wa YAHAYA wa Nguli wa muziki wa Kizaki kipya Lady Jay Dee umemjaza mahela Msanii wa Filamu aliyejizolea umaarufu kwa miaka ya hivi karibuni, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakati akiimba wimbo huo na Jide wakati wa uzinduzi wa Video yake mpya na yakwanza kusimama peke yake ya FOOLISH AGE.


Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya.


Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa.


“Jamanieee kumbe mziki unalipa ile mbaya yaani  nimeimba ubeti mmoja tu hapa ona hela kibao, kuanzia sasa na mimi nitaanza kuimba mziki”, alisikika Lulu akisenma huku akishangiliwa na mashabiki wake.

Uzinduzi wa fikamu hiyo ya kiswahili ambayo ina sub title ya Kiingereza na ambayo haipaswi kuangaliwa na watoto chini ya miaka 16, huku ikiwa imechezwa na wasanii maarufu na wakongwe  kama Elizabeth Michael mwenyewe, Diana Kimaro, Hashim Kambi, Ombeni Phiri na Mzee Jengua ulifanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Wasanii mbalimbali walihudhuria show hiyo usiku huu pale Mlimani City
 Lulu akizungumza machache mara baada ya Move yake hiyo kuoneshwa kwa mashabiki na wapenzi wa filamu Tanzania ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
 Wadau walifuatilia burudani...
 Jide akikamua jukwaani...
 Mama na mwanao ni kama chanda na Pete... huyo ni Natasha (kulia) na Bintiye Monalisa.
 .... Walitunzana tu kivyao vyao...

 noti alizo tuzwa Jide...

 Rich Rich akimwaga noti
 Wadau wakifuatilia uzinduzi huo wa Filamu.
 Furaha ilitawala

 Mwogozaji wa Filamu za Kibongo, Leah Mwendamseke nae alikuwepo kuangalia kazi hiyo ya Lulu.
 Waongoza Shughuli hiyo watangazaji wa Redio na TV Double G na mwana dada kutoka Times FM walikuwepo.

CHEKA AMSHINDA MMAREKANI PHILL WILLIAMS KWA POINT

$
0
0
Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kulia) akimuadhibu mpinzani wake Mmarekani, Phill Williams, wakaati wa pambano lao la raundi 12 la kuwania Ubingwa wa Dunia uzito wa Super Middle (WBF) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu. Katika pambano hilo Bondi Mtanzania Francis Cheka ameweza kumgalagaza kwa Pointi mpinzani wake na kutwaa ubingwa huo.
*******************
Na Mwandishi Wetu
HATA hivyo pambano hilo pamoja na yale ya utangulizi yaliingia dosari baada ya wachezaji kama Alfonce Mchumiatumbo, aliyekuwa akizichapa na Chupac Chipindi katika pambano lao la utangulizi la raundi sita, kugoma kupanda ulingoni kwa kile walichokuwa wakieleza mabondia hao kuwa wanahitaji kumaliziwa pesa zao za mkataba wa kucheza mechi hizo kabla ya kupanda ulingoni. 
Nao mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali, pia waligoma kupanda ulingoni wakishinikiza kumaliziwa pesa zao kwanza jambo ambalo lilifanya kuzua taflani ukumbini hapoa huku mapambano yakichelewa kuanza.
Ilipofika muda wa Cheka kupanda ulingoni pia alisikika mtangazaji akimuita muandaaji wa mapambano hayo ili kufika chumba alichokuwa Bondia mtanzania, Francis Cheka ili kumalizana naye mkwanja ili akubali kupanda ulingoni.
Alisikika Cheka akimuwakia muandaaji huyo kuwa, '' Nini Mmarekani hata angekuwa Mchina, nimalizie changu kwanza ili nipande ulingoni, ambalo pia lilichukua muda wa majadiliano hadi kuingiliwa kati na wadhamini na wadau wa ngumi waliotangaza kujikomiti kulipa pesa hizo wanazodai mabondia, ndipo mabondia hapo wakapanda ulingoni.

Aidha katika pambano la raundi 10 la mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali la kuwania Ubingwa wa WBF wa Afrika, Thomas Mashali ameweza kumshinda kwa pointi 2 tu mpinzani wake Mada Maugo na kutwaa Mkanda huo wa ubingwa wa WBF wa Afrika.
Na katika pambano la Utito wa Juu la utangulizi la Raundi sita kati ya Bondia Alfonce Mchumiatumbo na Chupac Chipindi, Mchumiatumbo amemchapa kwa KO mpinzani wake katika raundi ya tano, baada Chupac kunyoosha mikono juu kuashiria na wasaidizi wake kutupa taulo ulingoni kuashiria kushindwa kumalizia mchezo huo.  
 Waziri wa Habari, Fenella Mukangara (katikati) akipozi na mabondia Phill na Cheka, ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa pambano hilo la kimataifa.
 Waziri wa Habari, Fenella Mukangara (wa pili kushoto) akimvisha Mknda wa Ubingwa wa Dunia wa WBF Bondia Francis Cheka baada ya kumchapa kwa Pointi mpinzani wake Mmarekani, Phill Williams, katika pambano lao la raundi 12 lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu.
 Mashabiki wa Cheka wakifurahi na kumbeba baada ya kutangazwa mshindi.
 Bondia Mmarekani Phill Williams (kulia) akichapana na Francis Cheka wa Tanzania katika pambano lao lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
 Mabondia hao wakiliana Timing.......
 Cheka (kulia) na Phill wakichapana......
 Cheka (kulia) na Phill,wakiendelea kuchapana 
We subiri inakuja hiyooooo
 Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofurika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kumshuhudia Cheka akimchakza Mmarekani.
  Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofurika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kumshuhudia Cheka akimchakza Mmarekani.
 Baadhi ya wageni waalikwa walioshuhudia mchezo huo.
Bondia Mada Maugo (kulia) akimwadhibu mpinzani wake, Thomas 
Mashari kwa konde zito wakati wa pambano lao la raundi 10 la kuwania ubingwa wa Dunia wa WBF, ambapo Mashali ameibuka mshindi kwa 
Pointi dhidi ya Maugo. SOURCRE: Sufiani Mafoto Blog.


BAILEYS YADHAMINI ONESHO LA MAVAZI LA NECHA LA MBUNIFU DANIELA RAYMOND

$
0
0
 Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia kinywaji chake cha Baileys imedhamini onesho la Mavazi lijulikanalo kama NECHA la mbunifu wa mavazi Daniela Raymond. Onyesho hilo lilifanyika ktik kituo cha Utamaduni wa watu wa Kamara.


















RAIS JAKAYA KIKWETE APOKEWA NA GWARIDE LA SUNGUSUNGU WA AUSTRIA

$
0
0
 Taswira za askari wa jadi wa jimbo la Tyrol huko Alpbach nchini Austia wakiingia kwa gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima ya Rais Jakaya Kikwete aliye katika mkutano wa Kamisheni ya Ulaya mjini humo. Historia ya askari hawa, wanaojulikana kama Schuetzenkompanie, inakwenda miaka ya 1810 wakati wa vita na watu wa Bavaria. Soma historia yao BOFYA HAPA
 Sungusungu hao wakiendelea kuwasili
 Kila mmoja ana gobole lililotengenezwa kienyeji
 Watoto kwa wakubwa wamevutiwa na Sungusungu hao
 Gwaride rasmi
 Mdau anajiunga na Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Austria Mhe Heinz Fischer (katikati), Rais wa Kamisheni ya Ulaya Mhe Jose Manuel Barroso (wa pili kushoto), Rais wa Mkutano wa Alpbach Dr Franz Fischer (kushoto) pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandala

REDD'S MISS TANZANIA PHOTOGENIC 2013 KUJULIKANA LEO

$
0
0
WASHIRIKI wa shindano la Redd's Miss Tanzania leo watapata fursa ya kumjua mrembo wa kwanza kuingia katika hatua ya Nusu fainali ya Shindano la Redd's Miss Tanzania 2013 wakati mrembo mmoja kati ya wanyange hao 30 atakapotajwa mshindi wa Miss Photogenic 2013.

Shindano hilo no moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao ambapo washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusufainali ya shindano hilo litakalo fanyika baadae mwezi ujao.

Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model, Miss Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.

Akizungumza na Father Kidevu Blog hii leo, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga 'Uncle' amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha na wanahabari wazoefu wa masuala ya urembo Tanzania watakaa na kuchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.

Mshindi anataraji kutangazwa leo jioni katika hoteli ya Giraffe Ocean View na kujipatia tiketi hiyo.

Taji la Redd's Miss Tanania Photogenic  linashikiliwa na Mrembo Lucy Stephano aliyelitwaa mwaka 2012. Wafuatao ndio warembo watakao wania taji hilo hii leo.

 ESHYA RASHID
JANETH AWET
 HAPPINESS WATIMANYWA
CLARA BAYO
DORICE MOLLEL
 LATIFA MOHAMED
SALSHA ISDORY
 PRISCA PAUL
 LUCY TOMEKA
SEVERINA LWINGA
 SABRINA JUMA
 MIRIAM MANYANGA
LINA ALLAN
 LUCY JAMES

GLORY STEPHEN
 NEEMA SHAYO
 ALICE ISAACK
 SARAH PAUL
 PHILLIOS LEMI

NANCY MOSHI
 JACLINE LUVANDA
 DIANA LAIZER
 LUCY CHARLES
 SVETLANA NYAMEYO

NARIETHA BONIFACE
 MARY CHEMPONDA
 NICE JACK HERMAN
ANASTAZIA DONALD
 NEEMA MALITI
ELIZABETH PERTY

WERUWERU GOLDEN JUBILEE – ALUMNI MEETING

$
0
0
                    WERUWERU GOLDEN JUBILEE – ALUMNI MEETING
Weruweru Golden Girls,
Please be advised that the Alumni Meeting will be held on Sunday, September 1st, 2013 at 3:00pm at Cine Club,Mikocheni. All Weruweru Girls are urged and are Welcome to attend this Important Strategizing Meeting for our Golden Jubilee Celebrations preps.
 For registration and pledges please visit www.weruweru.mediart.co.tz
Let us all join together as we prepare for our Golden Jubilee
“Kumanya, Kupenda, Huduma”

MTWARA WAPOKEA KWA SHANGWE SEMINA YA FURSA KWA VIJANA

$
0
0
Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume  akizungumza mapema leo kwenye semin ya FURSA iliyofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia ni Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo.Semina hiyo inaratibiwa na Clouds Media Group na kufadhiriwa na NSSF,Lake Oil,Zantel,MaxMalipo na wengineo imewashirikisha wadau mbalimbali wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
  Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakifuatilia kwa makini  yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa kwa Vijana iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa  Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo,Mh.Yahya alizunguma mengi zikiwemo fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Mtwara na Singida namna ya kuzifanyia kazi katika suala zima la kujikwamua na maisha. 
Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba  akihitimisha semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo mchana,ndani ya ukumbi wa ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia kwake ni Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume pamoja na Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi.Semina ya Fursa kwa vijana tayari imekwishafanyika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na sasa Mtwara.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPO.COM

MAKEKE COLLECTION YAZIDI KUNOGA

$
0
0
Hii ni kampuni mpya mitindo ambayo imeanza kupamba moto toka mwishoni mwa mwaka jana chini ya designer  JOCKTAN WA MAKEKE AFRIKA pamoja na SCHOLASTICA WA MAKEKE AFRIKA na kutwaa umaarufu wa kutosha kutokana na kazi  zake kutokea kuwakuna sana wapenzi wengi wa mitindo nchini Tanzania na hata nje pia, Mitindo hio ya ki – makeke  inazidi kuchanja mbuga kwa spidi ya ajabu kwani ina mahadhi ya mwafrika halisi  na  cha kushangaza zaidi ni kwamba makeke afrika koleksheni imezidi kuboresha muonekano wake na kuwa wa mvuto zaidi  na wamezidi kuboresha huduma kwa wateja wao, hawa jamaa pia ndio waanzilishi wa mitindo ya ki – makeke na show ya Rangi Rangi za Makeke(RRM) Fashion wikend ambayo imefanya vizuri sana na kupokelewa vzuri na mashabikiwa mitindo Tanzania

UMOJA WA VIJANA WAPATA KATIBU MKUU MPYA

$
0
0
Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake Martin Shigela akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ndugu Mboni Muhita kabla ya kuanza kwa kikao cha wajumbe wa baraza la Umoja wa Vijana katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.


Mtela Mwampamba akiwasili kwenye uwanja wa CCM Afisi Kuu za CCM Zanzibar tayari kuhudhuria kikao cha Baraza Kuu la Vijana Taifa.

Mjumbe wa Baraza la Vijana Taifa  Antony Mavunde akisaliminiana na Mjumbe wa Baraza kutoka Jumuiya ya Wazazi William Malecela nje ya jengo la Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Vijana Taifa.
Wajumbe wa Baraza la Vijana wakicheza ngoma ya Boso yenye asili ya Kusini Pemba, kabla ya kuanza kikao cha Baraza Kuu la Vijana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Balozi Seif Idd akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar ambapo Makamu wa Pili wa Rais ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi.
Viongozi Wakuu wa CCM wakiomba Dua mbele ya kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Vijana la CCM Taifa.


January Makamba akizungumza na Wajumbe wa Baraza laVijana wa CCM kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Emmanuel Nchimbi akitoa salaam kwa wajumbe wa Baraza kuu la Vijana Taifa kabla kuanza kwa kikao cha Baraza Kuu la Vijana wa CCM
Mjumbe wa Kamati Kuu Mohamed Seif Khatibu akiwasalimu wajumbe wa Kikao Cha Baraza Kuu la Vijana la Taifa kwenye ukumbi wa mikutano CCM Zanzibar.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Sadifa Juma Hamisi akisoma risala kabla ya kumkaribisha Balozi Seif Idd kufungua kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana.


Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Idd akitoa hotuba ya kufungua kikao cha Baraza Kuu la CCM Vijana leo 1/9/2013 katika ukumbi wa mkutano wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.



Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixtus Mapunda akizungumza kwa mara ya kwanza na wajumbe wa Baraza la Vijana wa CCM .

 Meza Kuu ikiwa na Katibu Mkuu mpya aliyechaguliwa Sixtus Mapunda wakati wa kikao cha Baraza la Vijana kilichofanyika Zanzibar.
Wajumbe wa Mkutano wa Baraza kuu la CCM wakiserebuka baada ya kuidhinisha kuwa Sixtus Mapunda ndiye Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkubatia Katibu Mkuu wa umoja wa vijana aliyemaliza muda wake Ndugu Martin Shigela,kulia niKatibu Mkuu mpya wa UVCCM akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai .

AIRTEL YAPATA MKURUGENZI MPYA WA IT

$
0
0
 
Airtel Tanzania inatangaza uteuzi wa Bw. Frank Filman kuwa mkurugenzi wa kitengo cha teknolojia ya IT aliyechukua nafasi hiyo rasmi kuanzia sasa

Filman ambaye ni mtanzania alianza kazi Airtel akiwa kama munagalizi wa system (system Admistrator) na baadaye alipanda cheo na kuwa Meneja wa Mradi wa Technolojia ya IT. Kutoka mwaka 2007 mpaka 2009, alikuwa Meneja wa kitengo hicho nchini Ghana ambapo alisimamia na kutoa mchango mkubwa  uzinduzi wa mtandao wa Airtel  nchini Ghana.

Mwishoni mwa mwaka 2009 Filman alirejea Tanzania akiwa kama Meneja wa Huduma za kimtandao  (Network service Manager ) za Airtel Tanzania.

Baadaye alijiunga na kitengo cha mauzo na kama meneja wa Techonologia na biashara na huko aliweza kuchangia ongezeko la mapato kwa kiasi kikubwa hadi kufikia 100%  kwa mienzi 12 tu.

Katika miaka yake 12 na Airtel, Filman amefanya kazi miaka miwiliAirtel Ghana na zaidi ya miaka tisa akiwa na Airtel Tanzania.

Akizungumzia juu ya uteuzi huo, Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso alisema "Uteuzi wa Filman kuwa Mkurugenzi wa kitengo cha Teknolojia ya IT ni ushahidi wa dhamira ya Airtel Tanzania
kuendeleza, kulea na kukuza vipaji vya wafanyakazi wake ndani ya nchi. Sisi tunayo furaha kubwa kuona Watanzania wanachukua majukumu makubwa katika moja ya makampuni yanayokuwa kwa kasi na nyeti kama hii.

Teknolojia ya IT ni msingi muhimu wa mafanikio katika mawasiliano ya simu kwa sababu huduma zetu mbalimbali ikiwa ni pamoja na  huduma za kifedha yaani Airtel Money na  internet zinategemea teknolojia hiyo."

Aliendelea kwa kusema Kampuni imemteua Bw. Filman ikiwa na uhakika kwamba ataifanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa kabisa.

"Tunaamini Bw. Filman atafanya vyema kazi yake kutokana na uzoefu alionao lakini vilevile Airtel itaendeleza dhamira yake kuwaendeleza na kuwawezesha wafanyakazi wengine kushika nyazifa kama hizi nchini na kwenye nchi nyingine za Afrika na Asia ambapo Airtel inafanya biashara. pia Airtel tutaendelea kuwapa mafunzo wafanyakazi wetu ambayo yatawafanya wawe kwenye viwango vya kimataifa" Alisema Bw. Golaso.

Akizungumzia uteuzi wake Filman alisema, "Nimekuwa nikitamani kupata nafasi hii na nilijua siku moja naweza nikaipata na ninayofuraha kupata wadhifa huu Airtel Tanzania . kwa miaka mingi nimepitia mafunzo mbalimbali, na nina uzoefu nilioupata nchini Ghana pamoja na nchi nyingine Airtel inayofanya biashara. Hivyo niko tayari na nimejiandaa vyema kukabiliana na changamoto zote katika utendaji wa kazi hii na kuhakikisha natoa huduma zenye ubora kwa watanzania."

Airtel tunamini wafanyakazi ndio nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko ya kitamaduni , kasi ya kazi na kibiashara.  Airtel imewekeza katika kukuza uwezo wa wafanyakazi na kutoa nafasi ya kukuza fani ndani ya kampuni. Mafunzo ya ujuzi daima imekuwa ni mikakati yetu inayoendana sambamba na ujuzi unaohitajika kimataifa alisema bw Sunil Colaso mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania

Airtel imeweza kutoa mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi wake ili kuhakikisha wafanyakazi wa Airtel wanatoa huduma bora za kitaalamu kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kumekuwa na fursa ambazo zimekuwa zikitolewa kwa wafanyakazi wa Airtel Tanzania katika vitengo vya masoko, Mauzo, IT, pamoja na kuwa na mfumo wa kuwapeleka baadhi ya wafanyakazi wake nchi tofauti kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwa kufanya kazi kwa mienzi 6 hadi 18 katika Airtel Afrika na India.

Mauzo, masoko na huduma kwa Wateja kupitia Chuo Kikuu cha Centum .Airtel pia imekuwa ikiendesha mafunzo kwa ajili ya wafanyakazi wa Ambapo wafanyakazi wamekuwa wakipewa ujuzi na maarifa muhimu yanayowasaidia kutoa huduma bora kwa wateja ambazo zinaleta maendeleo makubwa na kuonesha utofauti katika soko la ushindani la mawasiliano ya simu.

TUSKER LITE LAUNCH - LAKE ZONE

$
0
0
Wakizundua rasmi bia ya Tusker Lite kanda ya ziwa katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Golden Crest jijini Mwanza, kutoka kulia ni Meneja mipango na masuala ya habari wa Kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombella, Meneja wa vinywaji vya Tusker Sialuoise Shayo, Meneja mipango na Ugavi wa SBL kanda ya ziwa Dilip Chudasama na Meneja mauzo wa kanda Octavian Migire(wa kwanza kushoto).
Baadhi ya viongozi wa idara ya masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti wakiwaonesha wageni waalikwa(hawapo kwenye picha) chupa ya bia ya Tusker Lite  katika hafla ya uziduzi wa bia hiyo kanda ya ziwa iliyofanyika katika hoteli ya Golden Crest jijini Mwanza, kutoka kulia ni Meneja mipango na masuala ya habari wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bi Nandi Mwiyombella, Meneja wa vinywaji vya Tusker, Bi Sialuoise Shayo, Meneja mipango na Ugavi wa SBL kanda ya ziwa na Meneja mauzo wa kanda Octavian Migire(wa kwanza kushoto).

MCHAKATO WA TUSKER PROJECT FAME 6 WAANZA KWA KISHINDO

$
0
0
 Vijana wakitoa burudani wakati wa amsha amsha hiyo ya kusaka washiriki wa Tusker Project Fame.


Baada ya ya Shangwe za Tusker Project Fame kurindima katika mikoa ya  Arusha, Mbeya, Mwanza juzi Septemba Mosi ilikuwa zamu ya jiji la Dar es Salaam kupata shangwe hizo .

Shangwe hizo ni katika amsha amsha ya kupata wawakilishi ambao watafanyiwa usaili na baade kupata mwakilishi mmoja au wawili ambao wataiwakilisha nchi katika mashimndano ya uaimbaji wa Afrika Mashariki.

usahili utakaofanyika hivi karibuni wa nani ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kusaka kipaji bora cha kuimba Afrika Mashariki ambao unategemewa kufanyika tarehe 7 na 8 mwezi huu, kampuni ya bia ya Serengeti imewaburudisha watanzania wa mikoni na kuwapa fursa ya kushiriki usahili huo kwa kuwapa nafasi ya kuonesha uwezo wao wa kuimba na mshindi kujipatia tiketi ya kusafiri mpaka Dar es salaam ili kushiriki katika usahili huo.

 Wateja wa kampuni hiyo mkoani Arusha walijipatia tisheti, bia za bure na washindi wa kipaji cha kuimba walipata tiketi za bure za kushiriki usaili  mkoanidar es salaam.

Washindi hao ni pamoja na David Jamal,Bartazal Kauki na wengine wengi. pia mkoani mbeya mashindano hayo yalifanyika katika baa za Rombo Bar, Mama Land Bar na Airport Bar ambapo kila bar ilitoa mshindi na kujipatia tiketi ya kushiriki usaili.

CHEKA APOKELEWA KWA SHANGWE MOROGORO

$
0
0
Bondia Francis Cheka akiwa sambamba na Mkanda wake aliokabidhiwa Agost 30 baada ya kumtwanga Mmarekani Phil William  mwishoni mwa wiki ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar,pichani bondia huyo akiwa na mashabiki wake wakati alipokuwa akiwasili mkoani Morogoro anakoishi mapema jana jioni.
                 Msafara kuelekea katikatika ya mji ukiendelea

Cheka akizungumza na umati mkubwa wa watu uliofurika kwenye ukumbi wa Old Vai jana majira ya saa 12 jioni kwenye mapokezi hayo ya Cheka kulikuwa na vituko kibao kikiwemo cha Mlemavu wa miguu aliyenusurika kugongwa na gari alipotaka kumshika mkono Cheka baada ya kuona tukuio hilo Cheka alisimamisha msafara huo na kumshika mkono Mlemavu huyo kwa habari na picha za tukio hilo la kuhudhunisha zitawajia hivi punde

PICHA ZOTE NA KWA HISANI YA DUSTAN SHEKIDELE,MOROGORO-

HAPPINESS WATIMANYWA NDIYE REDDS MISS TANZANIA PHOTOGENIC 2013

$
0
0

Redd’s Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa (19) akipozi kwa p[icxha mara baada ya kuibuka mshindi wa taji hilo na kuwa mrembo wa kwanza kutinga nusu fainali za Miss Tanzania 2013 baada ya kuwashinda warembo wenzake 29 katika shindano hilo dogo kuelekea fainali za Redd’s Miss Tanzania 2013. 
********   ********
Mrembo wa Mkoa wa Dodoma,  na mwakilishi wa Kanda ya Kati, Happiness Watimanywa, juzi amenyakua taji la Redds Miss Tanzania Photogenic 2013 na kuwa  mrembo wa kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ya shindano la Redds Miss Tanzania 2013. 


Happiness amefanikiwa kuingia hatua hiyo ambayo itaingiza warembo 15 bora na kuwashinda warembo wenzake 29 ambao wapo katika kambi ya Redds Miss Tanzania 2013.

Shindano hilo dogo la Haiba ya Picha “Miss Photogenic” alipatikana baada ya jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha mashuhuri nchini Tanzania wakiongozwa na Jaji Mkuu Mroki Mroki kutoka magazeti ya Serkali Daily News, Habarileo na Spotileo.

Mapema akitaja majina ya warembo walioingia hatua ya tano bora Mroki aliwataja mamaji wengine aliyoshirikiana nao kuwa ni Mpigapicha wa Jambo Leo Richard Mwaikenda na Mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Aika Kimaro.

Dalili za kuonesha kuwa Happiness amekubalika hata kwa washiriki wenzake katika shindano hilo ziliibuka wakati Mroki akitaja majina ya warembo waliofanikiwa kuingia hatua hiyo na lilipotajwa jina lake katika Hoteli ya Giraffe Ocean View warembo ulilipuka kwa kwashangwe.

Warembo watano walifanikiwa kuingia katika mchujo huo ni pamoja na Anastazia Donald ,Latifa Mohamed, Clara Bayo na Jacline Luvanda na Happiness Watimanywa aliyeibuka mshindi.

Warembo wa Redds Miss Tanzania watashindana tena katika shindano la Miss Top Model linalotaraji kufanyika Septemba 7 mwaka huu, katika Hotel ya Naura Spring jijini Arusha.

Mataji mengine yatakayo waniwa na warembo hao na washindi kuingia moja kwa moja klatika hatua ya Nusu fainali ni Miss Talent, Miss Personality na Miss Sports Woman.

Taji la Miss Photogenic lilikuwa linashikiliwa na mrembo Lucy Stephano kutoka Manyara na Kanda ya Kaskazini, kutoka Shinyanga na Kanda ya Ziwa. 

Fainali za mwaka huu za Redds Miss Tanzania zinataraji kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City  jijini Dar es Salaam Septemba 21,2013.
Mrembo Happiness Watimanywa akiwa amekubwa na butwaa baada ya kutajwa Mshindi wa Redd's Miss Photogenic 2013. 

Redd’s Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa (katikati) akipozi kwa picha na warembo wengine walioingia hatua ya tano bora ya kumsaka mshindi wa taji la Miss Photogenic 2013. Kutoka kulia ni Anastazia Donald ,Latifa Mohamed, Clara Bayo na Jacline Luvanda.(
Warembo wengine Walioshiriki shindano hilo wakifuatilia utangazwaji wa matokeo hayo katika Hoteli ya Giraffe Ocean View katika kambi yao. 
Viewing all 10588 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>