Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10583 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA NISHATI NAMADINI PROF. MUHONGO AKAGUA MAENDELEO YA UTANDAZAJI MABOMBA YA GESI MTWARA-DAR

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na Balozi wa China nchini, Lu Youqing walipokuwa wakikagua mitambo ya kisasa ya kuunganisha mabomba ya kusafirishia gesi, katika karakana namba tano  ya Kampuni ya kichina ya CPTDC ya Ikwiriri, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani .Profesa Muhongo alifanya ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa  Kampuni ya kichina ya CPTDC iliyopewa tenda ya kutandaza mabomba ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, alipokuwa katika ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi, juzi eneo la Somanga Fungu, wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi.

 Sehemu ya mabomba ya gesi yakiwa eneo la kuhifadhia la Nyamwage, Rufiji
 Profesa Muhongo akiangalia kipenyo cha bomba ambacho ni mita moja
 Profesa Muhongo akioneshwa sehemu ya bomba itakayounganishwa na bomba lingine
 Watalaamu wa ubora wa ufungaji mabomba ya gesi kutoka Afrika Kusini wakimueleza Waziri Muhongo kuhusu umakini wakati wa kuunganisha mabomba hayo
 Profesa Muhongo akiwa eneo la kuhifadhia mabaomba, Nyamwage, wilayani Rufiji. Mabomba hayo yalianza kuunganishwa jana.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia), akizungumza na baadhi ya vibarua  wa kitanzania wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ya kichina katika kambi ya kuhifadhia mabomba ya Nyamwage, wilayani Rufiji, Pwani.
 Waziri Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kamapuni hiyo ya kichina.
 Mmiliki wa blogu hii, Kamanda Richard Mwaikenda naye akiwa katika ziara hiyo eneo la Nyamwage, Rufiji.
 Kambi ya wafanyakazi wa kamapouni ya kichina eneo la Mkuranga, Dar es Salaam
 Waandishi wa habari walioambatana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (amezibwa), wakiangalia nyaya za mkongo zitakazotandazwa sambamba na mabomba ya gesi kwa ajili ya usalama, zilizokuwa kwenye lori katika ghala la kampuni hiyo ya kichina wilayani Mkuranga, Pwani
Baadhi ya mitambo ikiwa imefungwa wilayani Mkuranga, Pwani, kwa ajili ya kuongezea unene wa mabomba maalumu ya gesi yatakayotandazwa baharini. Picha na KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

REDD'S MISS TEMEKE ATOA MSAADA WA VITABU VYA SH. 300,000 SHULE YA MSINGI GULUKA KWALALA,UKONGA,DAR

$
0
0


Malkia wa Redd's Miss Ilala 2013, Doris Mollel akiwa na wanafunzi baada ya kukabidhi msaada wa vitabu  30 vyenye thamani ya sh. 300,000 kwa Shule ya msingi Guluka Kwalala, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Malkia wa Redd's Miss Ilala 2013, Doris Mollel amkimkabidhi  vitabu mwanafunzi Charles Costantino ambaye alipokea msaada huo kwa niaba ya Shule ya Msingi Guluka Kwalala, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mollel alikabidhi vitabu 30 vyenye thamani ya sh. 300,000. Wanaoshuhudia ni Miss Ilala namba mbili Alice Issack (wa tatu kushoto), mshindi wa tatu Clara Bayo (wa pili kushoto) na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Rehema Mketo.

 Wanafunzi wakifurahi pamoja na wanafunzi
 Mshindi namba tatu Clara Bayo akizungumza na mmoja wa wanafunzi.
 Mollel akimkabidhi zawadi shs. 5000 mwanafunzi aliyejibu swali walililoulizwa wanafunzi
 Mamis wakiwa katika piacha ya pamoja na wanafunzi pamoja na Mwalimu Mkuu
 Warembo wakiwa na mwalimu wa shule hiyo, Lugano Mwaikambo ambaye aliwahi shiriki Miss Morogoro mwaka 2000.
 Warembo wakicheza michezo mbalimbali na wanafunzi wa shule hiyo



Warembo wakiondoka shuleni hapoPICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

LB DRESSES MISS JAMAICA UNIVERSE CHANTAL ZAKY AT ATLANTA FASHION NIGHT OUT ON SUNDAY AUG 25th 2013

$
0
0
WE ARE VERY HAPPY AND FORTUNATE TO DRESS MISS JAMAICA UNIVERSE 2012 CHANTAL ZAKY FOR THE ATLANTA FASHION NIGHT OUT ON AUG 25th 2013. CHANTAL WAS ONE OF THE HOSTS FOR THE NIGHT.
The Boss of LB Apparel Madam Linda Bezuidenhout (Middle) with Miss Jamaica Universe Chantal Zaky (Left) and LB Model Taelor Moore (Right) in the LB Galactic Dress. Taelor was one of the greeters at the Fashion Night Out ATL on Aug 25. This dress has lights more pictures to come.

SAMAKI SAMAKI YATEKETEA KWA MOTO WAKATI WA UBOMOAJI

$
0
0
Hivi ndivyo ilivyo sasa Bar maarufu ya SAMAKI SAMAKI iliyokuwa ikivuma sana jijini Dar es Salaam. Bar hii iliyokuwa maeneo ya Mbezi Beach jijini imefikwa na janga la moto hii leo majira ya saa 3:15 asubuhi wakati moja ya makarandinga yaliyokuwa yakibomoa nyumba zilizopo kando ya barabara ya Bagamoyo (mkono wa kushoto ukitokea Mwenge) kupisha mradi wa maji wa DAWASCO.
 
Kwa mujibu wa Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa chanzo cha moto huo ni Buldoza lililokuwa likivunja kusababisha moto kupitia bomba lake la moshi ambalo lilikuwa limeshika katika makuti na kushika moto.

BONDIA WA DUNIA FRANCOIS BOTHA ATUA JIJINI DAR

$
0
0
Bondia wa Dunia wa uzito wa juu  Francois Botha akionyesha jinsi ya kupambana kulia ni Yasini Abdalla Rais wa Shirikisho la ndondi nchini ,kushoto ni mdau wa ndondi , uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere  leo  jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya  Michezo Bi.Juliana Yassoda akiwa na  Bondia wa Dunia   wa uzito wa juu Francois Botha alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  leo  jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya  mchezo wa ndondi utakaofanyika  30 Agosti mwaka huu katika ukumbi wa Diamond.
 Bondia wa Dunia wa uzito wa juu  Francois Botha  akionyesha mmoja ya mkanda alioishinda kwa   muuandaaji wa pambano hilo J Msangi,kushoto ni Rais wa  Shirikisho la Ndondi  Howard Goldberg katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  leo  jijini Dar es salaam
Bondia wa Dunia  Francois Botha akiwa na muuandaaji wa pambano hilo J Msangi,kushoto ni Rais wa  Shirikisho la Ndondi  Howard Goldberg katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere  leo  jijini Dar es salaam.

BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka bungeni mjini Dodoma leo
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambaye pia ni Mbunge wa Songwe, Philipo Mulugo kwenye viwanja vya bunge Mjini Dodoma leo.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Mbinga Magharibi Capt. John Komba, bungeni mjini Dodoma leo.

KUTOKA TFF HII LEO

$
0
0
MAANDALIZI MKUTANO WA UCHAGUZI TFF
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaendelea na maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 26 na 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Awali mkutano wa uchaguzi ulikuwa ufanyike Februari 23 na 24 mwaka huu lakini tukauahirisha kusubiri maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), hivyo tayari wajumbe wana taarifa rasmi kuhusu mkutano huo.

Orodha ya wajumbe iliyotumwa awali kwa ajili ya Mkutano tunayo, isipokuwa kama kuna wanachama wetu wana mabadiliko ya majina ya wajumbe watakaohudhuria wanatakiwa kutuma majina hayo kabla ya Septemba 30 mwaka huu.

Wanachama wa TFF ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu 14 za Ligi Kuu ya Vodacom.


WAWILI WAPINGWA UCHAGUZI WA TFF
Wanamichezo wawili walioomba kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu wamewekewa pingamizi.

Waliopingwa ni Wallace John Karia anayeomba kupitishwa kuwania urais na Vedastus Kalwizira Lufano anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda Namba Mbili ambayo ni mikoa ya Mara na Mwanza. Anyempinga Karia ni Shamsi Rashid Kazumari wa Dar es Salaam wakati Lufano anapingwa wa Samwel Nyalla wa Mwanza.

Pamoja na mambo mengine, Kazumari anampinga Karia kwa madai kuwa akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, aliwashawishi wajumbe wenzake kuingia mkataba na Azam Tv wakati akijua kamati hiyo ni ya muda, hivyo haina nguvu za kisheria kusaini mkataba huo.
Naye Nyalla ambaye pia ni mmoja wa wanamichezo waliojitokeza kuwania ujumbe kupitia Kanda hiyo anampinga Lufano kwa madai hana uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbezeleni itakutana kesho (Agosti 28 mwaka huu) saa 4 kamili asubuhi kusikiliza pingamizi hizo ambapo wawekaji pingamizi na waliopingwa wanatakiwa kufika wenyewe ndani ya muda kwa vile uwakilishi hautakiwi.

YANGA, COASTAL UNION KUUMANA VPL
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi ya pili kesho (Agosti 28 mwaka huu) kwa timu zote 14 kuwa viwanjani huku macho na masikio ya washabiki wengi yakielekezwa kwenye mechi kati ya Yanga na Coastal Union.

Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro ndiye atakayepuliza filimbi wakati Kamishna atakuwa Omari Walii kutoka Arusha.

Mtibwa Sugar itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro wakati Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora utakuwa mwenyeji wa pambano kati ya wenyeji Rhino Rangers na Azam.

Vumbi lingine litatimka kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati maafande wa JKT Ruvu watakapokwaruzana na wenzao wa Tanzania Prisons kutoka Mbeya. Mbeya City na Ruvu Shooting zitacheza kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Jiji la Tanga litakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Ashanti United itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Oljoro JKT itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.

RATIBA COPA U15 KUPANGWA ALHAMISI
Ratiba ya michuano ya U15 Copa Coca-Cola ngazi ya kanda mwaka huu itapangwa keshokutwa (Agosti 29 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Michuano hiyo ya kanda itaanza Septemba Mosi mwaka huu wakati mikoa inakumbushwa kuwa inatakiwa iwe imewasilisha usajili wa wachezaji wao kufikia Agosti 28 mwaka huu kupitia email ya TFF ambayo ni tanfootball@tff.or.tz na nakala kwa madadi_salum@ yahoo.com

Pia mikoa inakumbushwa kutowajumuisha wanafunzi wa darasa la saba katika timu zao katika ngazi ya kanda na fainali itakayochezwa Dar es Salaam kuanzia Septemba 7 mwaka huu kwa vile watakuwa katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi. Timu zinatakiwa kufika vituoni Agosti 30 mwaka huu.

Kanda hizo ni Mwanza itakayokuwa na timu za mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Tabora. Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida inaunda Kanda ya Arusha.

Zanzibar itakuwa na Kaskazini Pemba, Kusini Pemba na mikoa miwili ya Unguja wakati Kanda ya Dar es Salaam ina Ilala, Kinondoni, Lindi, Mtwara, Temeke na mkoa mmoja wa Unguja.

Kanda ya Mbeya inaundwa na Iringa, Katavi, Mbeya, Njombe, Rukwa na Ruvuma wakati Dodoma, Morogoro, Pwani na Tanga zinaunda Kanda ya Morogoro.

Mwanza itatoa timu nne kucheza hatua ya fainali wakati kanda nyingine za Arusha timu mbili, Zanzibar (2), Mbeya (3) na Kanda ya Morogoro itaingiza timu mbili.

NEC YA CCM YAMALIZA MGOGORO WA MADIWANI BUKOBA

$
0
0

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa kamati kuu wa kubatilisha kufukuzwa kwa madiwani wa Bukoba nje ya ukumbi wa NEC.
****
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imejadili na kutolea maamuzi pamoja na mambo mengine suala la Madiwani wanane waliotangazwa kufukuzwa uanachama na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera.

Katika maamuzi yake, Kamati Kuu imebatilisha uamuzi uliofanywa na Halmashauri Kuu CCM ya Mkoa wa Kagera Agosti 13, 2013 wa kuwafukuza uanachama Madiwani hao. Hivyo Madiwani hao wanane ni wanachama halali wa CCM.

Kamati Kuu imetoa uamuzi huo, baada ya kubaini kuwa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera haikuzingatia Katiba ya CCM ya 1977 Toleo la 2012 Ibara ya 93 (15). Ibara hiyo inasomeka kuwa moja ya kazi ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ni:-

“Kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa, isipokuwa kwa suala la kumvua uanachama au uongozi Diwani lisifanyike hadi Kamati Kuu imearifiwa na kutoa maelekezo”.

Aidha, Kamati Kuu imewaonya Madiwani wa CCM wa Manispaa ya Bukoba, Mbunge wa Bukoba Mjini na Meya kwa kusababisha kukosekana kwa utulivu, mshikamano na amani katika Manispaa na Chama.

Kamati Kuu pia imeitaka Serikali kumwagiza mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali(CAG) kufanya ukaguzi maalum wa haraka wa mambo yanayolalamikiwa dhidi ya Meya ili ukweli ujulikane na matokeo ya uchunguzi huo yasilishwe kwenye baraza la madiwani ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazoongoza Serikali za Mitaa.

Wakati tuhuma hizo dhidi ya Meya zikichunguzwa; Kamati Kuu inawataka Madiwani wa CCM  kurejesha utulivu kwenye Manispaa na Chama kwa ujumla ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwaletea maendeleo wananchi wa Bukoba.
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM
ITIKADI NA UENEZI
27/08/2013

VIFAA VYA LIGI KUU KUKABIDHIWA LEO

$
0
0

MDHAMINI Mkuu wa Ligi Kuu ya Zanzibar, Kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, maarufu kama ‘Grand Malt Premier League’ leo wanatarajia kukabidhi vifaa kwa timu shiriki za ligi hiyo katika hafla itakayofanyika hoteli ya Bwawani, mjini Zanzibar.
 
Katika hafla hiyo maalumu inayotarajiwa kuanza saa 4 asubuhi, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Saidi Ali Mbarouk.
 
Akithibitisha hilo, Meneja Masoko wa Grand Malt, Fimbo Butallah alisema, hiyo ni kuashiria kukaribia kuanza rasmi kwa msimu wa Ligi Kuu ya Zanzibar wa 2013/3014.
 
“Kama tulivyoahidi kipindi tunaingia mkataba wa kudhamini ligi hii, kesho (leo) tutakabidhi zawadi kwa timu zote zishiriki za ligi hiyo, ambavyo vitakuwa ni vifaa bora kabisa.
 
“Pia tutatoa mipira itakayotumika katika ligi hiyo pamoja na jezi maalumu kwa waamuzi, kwani tunachotaka ni kuwa na ligi bora na iliyo na ushindani,” alisema.
 
Naye Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam alisema, watahakikisha wanaendelea kutoa udhamini uliotukuka kwa ajili ya kukuza michezo ndani ya Zanzibar.
 
“Ligi Kuu ya Grand Malt ndio inatarajiwa kuanza wiki ijayo na sisi tuko kwa ajili ya kuhakikisha inaafanikiwa zaidi,” alisema.
 
KMKM ndio waliofanikiwa kutwaa ubingwa huo msimu uliopita, wakiwa ni mabingwa wa kwanza kabisa toka kuanza kwa udhamini wa Grand Malt.
Kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ndio walioingia mkataba wa kudhamini ligi hiyo hivyo kujulikana kama Ligi Kuu ya Grand Malt.

KAMPUNI YA CHLORIDE EXIDE YASAIDIA KITENGO CHA EMERGENCY CHA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

$
0
0

Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo kulia na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakikabidhi Betri za kampuni hiyo kwa  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dharura  'EmerGency Medicine Profesa, Victor Mwifongo kwa ajili ya magari ya kitengo hicho Dar es salaam leo kushoto ni Kaimu Dereva Mkuu Sultan Kitanga na Mkuu wa Idara ya Ufundi ENG,Leonard Elizeus
Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo kushoto na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakishusha betri walizopeLeka Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Kwaajili ya Msaada katika Kitengo Cha Dharura.
 
Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo kulia na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakishusha betri walizopeleka Muhimbili kwaajili ya msaada katika kitengo cha Dharura
Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo kushoto na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya maofisa wa kitengo hicho
Mkuu wa Madereva wa Kitengo cha Emergency Medicine Bw. Kafuru Rashidi akikagua betri hizo baada ya kukabidhiwa
Baadhi ya Madereva wa kitengo hicho wakikagua
Baadhi ya wahudumu wakiendelea na shughuli zao katika gari la wagojwa kushoto ni Nikijaeli Ngareni na Josephine Lazaro
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dharurua  'Emergency Medicine Profesa, Victor Mwifongo kushoto akibadilishana namba za mawasiliano na  Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza Na Mwandishi Wetu MRATIBU wa Masoko wa Kampuni ya Chloride Exide Bw, Robert Hiza leo ametoa msaada wa Betri mbili katika kitengo cha Emergency Medicine ya hospitali ya Taifa Muhimbili .
 
Msaada huo wa kwanza kutoa inaendana na miaka 50 ya kampuni hiyo ambapo watatoa viti mbalimbali katika hospital za Serikali vikiwemo Sola kwa ajili ya umeme wa jua .
 
Akipokea msaada huo.Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dharura  'Emergency Medicine Profesa, Victor Mwifongo amewashukuru kampuni ya Chloride Exide kwa kuliona hilo kwani ni mara ya kwanza katika kitengo chao kupokea msaada kama huo, na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia vitu mbalimbali ikiwemo hata magari kama yapo tunaomba msaada maana hapa kitengo chetu ni cha mambo ya dharura na kinategemewa sana kama mnavyojua alisema Prof Victor Mwifongo Nae  Mkuu wa Madereva wa Kitengo cha Emergency Medicine Bw. Kafuru Rashidi amendelea kutoa shukrani kwa kampuni hiyo kwa kuliona hilo kwani yeye kama Dereva ameona ni jambo bora sana

WANAHABARI KUKUTANA NA REDD'S MISS TANZANIA 2013 KESHO

$
0
0
 WAREMBO 30 wanaowania taji la Redd’s Miss Tanzania 2013, leo wanatarajiwa kukutana rasmi na waandishi wa habari, ili kila mmoja kutoa mtazamo wake shughuli itakayofanyika katika hoteli ya Giraffe iliyopo Kunduchi, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, ambao ni waandaaji wa shindano la Redd’s Miss Tanzania 2013, Hashim Lundenga alisema, mkutano kati ya waandishi wa habari na warembo ni muhimu kuwajengea uwezo zaidi wa kujiamini.
“Washiriki  wataulizwa maswali mbalimbali na waandishi wa habari na wao wataeleza mtazamo wao kuhusu Redd’s Miss Tanzania, hatutawafunga, wao waandishi watakuwa huru kila mmoja kumuuliza mshiriki yoyote swali analotaka,” alisema.
 Leo washiriki hao walikuwa na semina maalumu kati ya washiriki hao na waandaaji wa mashindano haya ambao ni Kampuni ya Lino International Agency Limited.
Baada ya kukutana na waandishi wa habari kesho, warembo hao wanatarajiwa kuanza ziara maalumu ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa lengo la kuhamasisha utalii wa ndani.
Warembo hao watakuwa kambini kwa muda wa siku 30 wakipata mafunzo  mbalimbali yatakayotolewa na wataalamu kutoka katika sekta mbalimbali kama vile afya, ajira, ujasiriamali, uwekezaji na sekta ya utalii.
Brigitte Alfred ndiye anayeshikilia taji hilo kwa sasa, baada ya kufanikiwa kulitwaa mwishoni mwa mwaka jana.
Meneja wa Redd’s, Victoria Kimaro naye alisema kama wadhamini wapo tayari kuhakikisha shindano hilo linafanikiwa zaidi mwaka huu kuliko kipindi chote kile.
Kinywaji cha Redd’s Original kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

 Warembo wakitoka katika ukumbi wa JETI 1 Hoteli ya Giraffe ambako leo walikuwa na semina.
 Warembo wakiwa katika pozi la picha
Mwalimu wa warembo hao Magdalena Roy ambaye ndiye anashikilia taji la Redd’s Miss Tanzania Top Model 2012,akizungumza jambo na washiriki wa Redd's Miss Tanzania 2013.

REDD'S MISS TANZANIA 2012 AAGWA TAYARI KUSHIRIKII MISS WORLD NCHINI INDONESIA

$
0
0
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa,Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred Lymo (katikati) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2013).Kushoto ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.

REDD'S MISS TANZANIA 2012 AAGWA TAYARI KUSHIRIKII MISS WORLD NCHINI INDONESIA

$
0
0
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa,Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (katikati) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2013).Kushoto ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.

Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa,Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (katikati) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2013).Kushoto ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko na Kulia ni Mkurugenzi wa Utamaduni, Prof. Herman Mwasoko.
Brigitte Aflred Lymo akipongezwa na mama yake huku Mlezi wa Miss Tanzania, Emmanuel Ole Naiko akishuhudia.
Mgeni rasmi Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara (kulia) Redd's Miss Tanzania 2012/13, Brigitte Alfred (katikati) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2013) pamoja na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania, Emmanuel Ole Naiko.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kulia) akizungumza wakati wa hafla hiyo  na wengine pichani ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara (wapili kushoto) Redd's Miss Tanzania 2012/13, Brigitte Alfred (kushoto) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2013) na  Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasok.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akimkabidhi Bendera ya Taifa,Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (pili kushoto) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2013).Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko (pili kulia),Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kulia) pamoja na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
Warembo mbalimbali wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Tanzania 2013 wakifuatilia tukio hilo la kuagwa kwa Miss Tanzania 2012 katika Hoteli ya Giraffe.
Hapa ni katika kutafuta taswira tu!!
Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakifuatilia tukio.
Wageni waalikwa
Picha ya pamoja na warembo wapya ilipigwa.

SEREEE CO YAJA NA MEN'S WEAR KINONDONI TX

$
0
0
 WADAU mbalimbali mnakaribishwa SEREEE CO, Kinondoni jirani na Soko la TX. Ndani ya SEREEE CO utakutana na huduma mbalimbali nzuri za kuvutia pamoja na mambo mazuri kibao kama vile MEN'S WEAR SHOP, DECORATION SERVICES, CAKE SHOP, EVENT ORGANIZING, BEAUTY SALON, CATERING SERVICES, KIDS GAME & MANY MORE!!!
 Hili ndilo jengo ambalo Duka la Nguo za Kiumela SEREEE pamoja na Salon vinapatikana Duka lipo chini na juu ni Salon matata na yakisasa. Linatazamana kabisa na soko la TX kinondoni.

 SALON pia ipo na huduma za kila namna
 Viatu vizuri na imara vinapatikana.
 Mashati na fulana za kila namna zipo SEREEE Co.

Ukiingia ndani hutatoka bila kitu kikupendezacho na kesho utarudi tena.
 Kule ndani kabisa pia viwalo vyake vipo swaaafi kabisa.
 Manukato ya uhakika
 Walet za nguvu kuweka Shilingi au dola..

 Mikanda ya ngozi za Ukweli na tai za uhakika kwa bei nafuu kabisa.
 Mambo ndio kama hayo...Soksi za pamba







KUREJESHWA KWA URUSHAJI MATANGAZO RADIO IMAAN FM NA KWA NEEMA FM RADIO

$
0
0


KUREJESHWA KWA URUSHAJI MATANGAZO RADIO IMAAN FM NA KWA NEEMA FM RADIO

1.0 Utangulizi:

Mnamo tarehe 26/02/2013 Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilitoa uamuzi wa kuvifungia vituo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kukiuka Sheria na Kanuni za Utangazaji.

Kamati ya Maudhui iliuita uongozi wa vituo hivyo tarehe 11/02/2013 na tarehe 14/02/2013 ili kujitetea na vyote vilikiri kosa. Baada ya kutafakari utetezi wa Radio Imaan na Radio ya Kwa Neema FM na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utangazaji, Kamati iliamua kutoa adhabu kwa vituo vyote viliwi kama ifuatavyo:-


a)   Vituo vyote vilipewa  onyo pamoja na kufungiwa kurusha matangazo kwa kipindi cha miezi sita kuanzia tarehe 26/02/2013;

b)  Vituo vyote vilitakiwa kuithibitishia Mamlaka ya Mawasiliano na Kamati ya Maudhui kwa maandishi kuwa hawatarejea kutenda kosa la aina hiyo au linalofanana na hilo. Ikiwa vitarudia Kamati ya Maudhui haitasita kuvifutia leseni zao za utangazaji.

2.0 Kutekeleza adhabu na hatua zilizochukuliwa na vituo hivyo
      na Mamlaka ya Mawasiliano:   

Baada ya Uamuzi huo kusomwa, vituo vyote viwili vilianza kutekeleza adhabu mara moja kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utangazaji. Mamlaka ya Mawasiliano ilipokea barua ya udhibitisho wa kutofanya kosa tena yaani “Commitment letter” pamoja na sera ya uhariri (Editorial Policy) na ratiba ya vipindi kutoka kwa vituo vyote viwili.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilifanya ukaguzi kwa vituo vyote viwili ili kujiridhisha na kuzipitia sera za uhariri pamoja na mwongozo wa vipindi kabla ya kuvifungulia.

3.0 Kurejeshwa kwa Matangazo

Kamati ya Maudhui iliandika barua tarehe 27/08/2013 kuhusu kuvifungulia vituo hivyo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kutumikia adhabu kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utangazaji. Vituo hivi vimeanza kurusha matangazo yake kuanzia leo tarehe 28/08/2013 baada ya muda wa adhabu kuisha.

Kamati ya Maudhui inapenda kutumia fursa hii kuvionya vyombo vya habari vya utangazaji vya redio na televisheni kuwa makini katika kutekeleza masharti ya leseni pamoja na kufuata Sheria na Kanuni za Utangazaji. Kamati ya Maudhui haitasita kutoa adhabu kali au kuvifungia vituo vitakavyokiuka Masharti ya leseni, Sheria pamoja na Kanuni za Utangazaji au hata kuvifutia leseni zao.

Kamati ya Maudhui inatoa wito kwa vyombo vya habari vya utangazaji kuzingatia Sheria, Kanuni na Masharti ya leseni ilikuboresha Sekta ya Utangazaji na kudumisha amani nchini.

 Eng. Margaret Munyagi
Mwenyekiti,
Kamati ya Maudhui Ya TCRA,
S.L.P. 474,
DAR ES SALAAM.
28/08/2013

ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia takriban dakika 25 zilizopita.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika  kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.

BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe. SOURCE: http://gospelkitaa.blogspot.com

MJUE MTUMISHI WA MUNGU ASKOFU MOSES KULOLA

$
0
0
Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.

Ni mume wa Elizabeth na wamezaa watoto10 ambapo saba bado hai.alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa.

Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.

Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.

Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzishaa makanisa Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuna makanisa yapatayo 4000 katika nchi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo Askofu Moses Kulola anayeongoza makanisa elfu nne, Askofu Msaidizi wake ni Mwaisabila.
Askofu Kulola aliyeketi akiwa na waimbaji wa injili nchini Mwinjilisti Faustin Munishi mkono wa kushoto pamoja na Emmanuel Mwasota. mwanzoni mwa mwaka 1970
Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo yasiyopungua 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake. 
 
Nampenda sana Askofu Moses Kulola maana anafanya kazi ya MUNGU kwa moyo na kwa mujibu wa kitabu cha historia yake Askofu Kulola amezunguka Tanzania nzima tena wakati mwingine kwa kutembea kwa miguu na kwenye mazingira magumu sana kiasi kwamba ni wito mkuu wa MUNGU mkuu alionao Askofu Kulola na kwa miaka zaidi ya 60 amekuwa akihubiri neno la MUNGU na hadi sasa MUNGU anamtumia sana, katika mkutano uliopita wa askofu Kulola pale viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam maelfu ya watu walihudhulia na wengi sana kufunguliwa na injili anayohubiri askofu Kulola ni injili iliyonyooka na akiwataka wanadamu kumpa YESU KRISTO maisha yao ili wapate uzima wa milele bure.

Ukiacha mengi ambayo Mungu anaendelea kumtumia mtumishi wake huyu, kuna suala la nywele zake, askofu Kulola kama tulivyowahi kuandika siku zilizopita, hajanyoa nywele zake kwa takribani miaka 47 sasa, kwakuwa hakupendezwa na suala la kwenda salon kunyoa nywele zake hivyo akamwambia Mungu nywele alizokuwa nazo kwa wakati huo zisikue zaidi au kupungua, na ndivyo ilivyo mpaka sasa wembe haujapita kichwani mwake.
Askofu Kulola akipeana mkono na mwanae Daniel Kulola ambaye ni mchungaji. 

EDWARD LOWASSA ASHEHEREKEA MIAKA YAKE 60 YA KUZALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli mkoani Arusha, Edward Lowassa akilishwa kipande cha keki na mkewe wakati wa maadhimisho ya siku yake ya Kuzaliwa ambapo kiongozi huyo alitimiza miaka 60 Agosti 26, mwaka huu. Tafrija hiyo ambayo alijumuika na wajukuu zake ilifanyika nyumbani kwake Monduli.
 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli mkoani Arusha, Edward Lowassa akimlisha keki mkewe wakati wa maadhimisho ya siku yake ya Kuzaliwa ambapo kiongozi huyo alitimiza miaka 60 Agosti 26, mwaka huu. Tafrija hiyo ambayo alijumuika na wajukuu zake ilifanyika nyumbani kwake Monduli.  
 waziri mkuu mstaafu na mbunge wa monduli Mh Edward Lowassa akiwa na wajukuu zake tayari kukata keki ya sherehe ya kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake tarehe 26 aliyoandaliwa na mkewe mama Regina Lowassa huko Hekima Garden mikocheni.
 Wajukuu wakimwimbia Babu Happy Birthday!!
 Mishumaa iliwashwa

 babu kata kekiii tuleeeeeee
 Bibi alisaidia kukata keki hiyo...
 Makamanda wakiisubiri kwa hamu....
 kumbato la pongezi kutoika kwa mkewe.

 Mzee Lowassa akilishwa keki na mtoto wake Freddy Lowassa.
 Freddy nae akilishwa keki na baba.

STAND UP FOR AFRICAN MOTHERS CAMPAIGN – FUNDRAISING GALA DINNER

$
0
0
Montage Managing Director Ms.Teddy Mapunda speaks to the media during press conference of announcing the date for Fundraising Gala Dinner which will be on 11th October,2013  at  Dar es Salaam Serena Hotel with the aim of raising funds  for the campaign dubbed “Stand Up for African Mothers”, Hon.Jakaya Kikwete  will be the Guest of Honour.

AMREF Country Director Dr. Festus Ilako speaks to the media during press conference of announcing the date for Fundraising Gala Dinner which will be on 11th October, 2013 at Dar es Salaam Serena Hotel with the aim of raising funds for the campaign dubbed “Stand Up for African Mothers”, Hon.Jakaya Kikwete will be Guest the of Honour,on the left side is  Montage Managing Director Ms.Teddy Mapunda and AMREF Deputy Country Director Dr.Rita Noronha(R).
 
 ********
AMREF Tanzania today announced the date for the Fundraising Gala Dinner which will be on 11th October, 2013 at the Dar Es Salaam Serena Hotel.  The aim of the Gala Dinner is to raise funds for the campaign dubbed “Stand up for African Mothers”. 

Speaking at the press conference today, Dr Festus Ilako, AMREF Country Director said “we are playing our part in helping the Country meet its health related millennium development goals (MDGs) targets, by strengthening the national health care system and contributing to the improvement of the current state of maternal health.Tanzania has done well in meeting the other MDG goals but the one that is critical and important for the future of our country is improving the quality of care for maternal health.  

Enhancing the skills of our existing nurse midwives and training others is critical and that is the reason we appeal to you.   The funds raised since the launch of the campaign have so far supported the training of 10 nurse midwives from Tanga (Kilindi) and 70 more are expected to be enrolled from Kilindi, Mtwara and Simiyu regions.  The training will be expanded to cover all regions of Tanzania mainland and Zanzibar, if we can mobilise adequate resources”.
Contributions to support this initiative will be received using the following channels: 

  • Mpesa number +255 752 167286 or,
  • Deposit your contribution in our National Bank of Commerce (NBC), Corporate Branch, account number 0111030004548
  • Purchase a table of 10 at USD 1,500 at the fundraising event
“The expected guest of honour will be His Excellency Dr Jakaya Mrisho Kikwete the President of the United Republic of Tanzania. The event is expected to bring together senior government officials, development partners, Corporates, interested public and the media. All proceeds from this event will go towards supporting the aforementioned objective”, he added.

AMREF has been active for the last 57 years striving to create a healthy generation.  Last year in May 15th2012, we launched the Stand Up for African Mothers campaign and rallied all to join hands to improve the quality of maternal and child health care services .  To achieve this, we need to upgrade the skills of 2,800 existing health workers using eLearning and an additional 1,000 nurse midwives through pre-service training by 2015.

This will contribute to the country’s efforts to achieve MDG5 by increasing the number of skilled birth attendants.  We are appealing to all Tanzanians, to join in the various fundraising activities that will kick off starting with the major one that will be held on 11thOctober at the Serena Hotel.  

For further enquiries, please call Montage Limited on 0685701269/270/298/289 or email info@montaget.com

MDAU BOKHE ASHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA KWAKE

$
0
0
1 
Bokhe akipozi kwa picha katika hafla ya kuzaliwa kwake iliyofanyika jana32 
Bokhe akikata keki kama ishara ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake katika hafla fupi ya chakula cha jioni iliyofanyika Kebbys Hotel Mwenge jijini Dar es salaam jana ambapo alijumuika na marafiki zake pamoja na baadhi ya ndugu zake.5 
Hapa akimlisha keki rafiki yake Sinta4 
Hapa akimlisha keki ndugu yake GetuAkimlisha keki ndugu yake Winnie
15 
Akimlisha keki rafiki yake Sauda wa Nguvu14 
Getu akipozi kwa picha13 
Story kidogo kabla ya kukata keki12 
Sauda akiwa na Box yake ya Juice tayari kwa kuondoka11 
Sauda wa Nguvu akipozi kwa picha10 
Bokhe akiwa na Winnie kushoto na Sauda katika picha9 
Bokhe kulia Winnie Kushoto na Getu wakipozi kwa picha8 
Bokhe na Getu wakipuzi kwa picha7 
Bokhe na rafiki yake Sinta wakipozi kwa picha6 
Bokhe akifurahi na marafiki zake
Viewing all 10583 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>