Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10656 articles
Browse latest View live

MNAOSAKA AJIRA SOMENI TANGAZO HILI LA NAFASI ZA KAZI

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

  TANGAZO KWA UMMA
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Tangazo lake kwenye Gazeti la Habari Leo la tarehe20 Aprili, 2013 siku ya Jumamosi na la tarehe 23 Aprili, 2013 siku ya Jumanne na kwenye tovuti ya Wizara, ilitangaza nafasi mbalimbali  za kazi za Kada ya Afya zikiwemo za Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii Wasaidizi, Walezi wa Watoto, Maafisa Lishe na Maafisa Lishe Wasaidizi.
Wizara inapenda kuwajulisha waombaji wa nafasi za Kada tajwa hapo juu zitashughulikiwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira.
Hivyo, waombaji wote waliotuma maombi yao Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wanajulishwa kuwa maombi yao yatapelekwa Sekretarieti ya Ajira kwa ajili ya uchambuzi na usaili.
Tangazo hili halihusu waombaji walioomba Kada mbalimbali za Afya ambazo zitashughulikiwa moja kwa moja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
  
Kaimu Katibu Mkuu
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
22 Mei, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONYESHO YA NANE YA KAMISHENI YA VYUO VIKUU MBALIMBALI JIJINI DAR

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere, Africa Junior, kuhusu Kituo cha utafiti wa Usafirishaji, wakati alipotembelea kwenye banda la Chuo Kikuu cha Makerere kwenye Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali, yatakayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yamefunguliwa leo. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR
Baadhi ya washiriki  wa maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya kufungua rasmi maonyesho hayo ya siku tatu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Maofisa wa mfuko wa PPF, kutoka (kushoto) ni Meneja wa Kanda ya Ilala, Evans Musiba, Meneja Uhusiano, Lulu Mengele na Ofisa Masoko, Sereki Michael, wakati alipotembelea katika banda la maonyesho la PPF, leo kwenye maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa, Ofisa Udahiri Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Hilder Kawiche, wakati alipotembelea Banda hilo kwenye Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa, Makamu Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha United African-Tanzania, Jo, Do Hyun, kuhusu matumizi ya gari ndogo inayotumia Chaji ya Umeme wakati alipotembelea katikia Banda hilo,kwenye Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Sakina Taki (kushoto) na Tannaz Naseri, kutoka 'University of the Future' , Kuala Lumpur, wakati alipotembelea Banda hilo kwenye Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa, Msimamizi Mkuu wa Teknolojia wa Chuo Kikuu cha SUA, Gaudencia Donati, wakati alipotembelea Banda hilo kwenye Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Akitembelea katika Mabanda ya maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo.

KUTOKA MAGAZETINI HII LEO

MWINYI ATAKA NOVEMBA 30 KUWA MAPUMZIKO AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha ripoti ya utafiti juu ya ushirikishwaji wa raia katika mchakato wa uanzishwaji wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika jan a jijini Dar es Salaam. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Dira ya Afrika Mashariki (VEAF),  ambao ndio waliofanya utafiti huo,Dr. Azaveli Lwaitama.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (katikati) akizindua kitabu cha ripoti ya utafiti juu ya ushirikishwaji wa raia katika mchakato wa uanzishwaji wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC). Pamoja nae ni Katibu Mkuu wa zamani wa EAC, Balozi Dk. Juma Mwapachu (kulia) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Dira ya Afrika Mashariki (VEAF),  ambao ndio waliofanya utafiti huo,Dr. Azaveli Lwaitama.
 Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (walioketi katikati) akiwa pamoja na washiri wa Kongamano hilo. ******  *******

Na Mtuwa Salira wa EANA
Rais wa zamani wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi amependekeza kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutangaza Novemba 30 kuwa siku ya mapumziko kwa nchi zote za jumuiya hiyo ili kuongeza uelewa wa wananchi wake juu ya masuala ya mtangamano.

Novemba 30, 1993 ilikuwa ndiyo siku ambapo Kamisheni ya Utatu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilizinduliwa na hatimaye kuzaliwa upya kwa jumuiya hiyo iliyokufa mwaka 1977. Hivi sasa tarehe hiyo inaadhimishwa kama Siku ya EAC lakini siyo siku ya mapumziko katika nchi wananchama.

Mwinyi alitoa mapendekezo hayo Jumatano jijini Dar es Salaam alipozindua ripoti ya  utafiti wa kwanza wa Afrika Mashariki juu ya ushiriki wa raia katika mchakato wa ushirikiano wa EAC, uliyofanywa na Jukwaa la Dira ya Afrika Mashariki (VEAF) ambayo imebaini kwamba upo ushiki hafifu wa raia katika mwenendo mzima wa mchakato huo.

''Nitakuwa na furaha zaidi kutoa mchango wangu wa kuwashawishi marais waliopo sasa ili kutangaza Novemba 30, 1993, siku ambayo Tume ya Utatu ya Afrika Mashariki ilipozinduliwa mjini Arusha, marehemu Mwalimu Nyerere akiwepo, kuwa Siku ya Afrika Mashariki,'' alisema Mwinyi ambaye wakati huo alikuwa Rais wa Tanzania.

Alisema, siku kama hiyo wananchi pamoja na mambo mengine wanaweza kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na maonyesho ya utamaduni na bidhaa za kilimo na viwanda katika majiji yote na mipakani, ambapo alisema, mwisho wa siku vitaongeza uelewa wa wananchi juu ya jumuiya yao ya Afrikia Mashariki. 

Sehemu ya ripoti hiyo ilisema ingawa kuanzsihwa upya kwa jumuiya hiyo kulilenga iwe na misingi yake kwa wananchi, matokeo ya u

Dar Stock Event- Triniti bar

GHANA YAIBUKA MSHINDI WANUSU FAINALI YA GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™, KENYA MSHINDI WA PILI

$
0
0
Washindi wa pili wa nusu fainali ya kwanza ya Guiness Football Challenge Francis Wangari(kushoto) na  Kepha Kimani(kulia) kutoka Kenya  katika picha ya pamoja na waendeshaji wa kipindi cha Pan-Africa Guinness Football Challenge Larry Asego na Mimi Kalinda.
Washindi wa kwanza wa nusu fainali ya kwanza ya Guiness Football Challengekutoka Ghana Naab Jonathan Baan(kushoto) na Desmond Odaano(kulia) katika picha ya pamoja na waendeshaji wa kipindi cha Pan-Africa Guinness Football Challenge Larry Asego na Mimi Kalinda.

******   *******
Jana usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV nusu fainali ya kwanza kabisa ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ ilirushwa hewani na katika runinga Afrika nzima   ambapo timu ya Ghana ilionesha ni kwanini  ni timu bora ambayo ndiyo imejishindia pesa nyingi mpaka sasa.

Jonathan Nabb na Desmond Odaano walionesha  uwezo na  ujasiri wao walipoibuka washindi zidi ya wapinzani wao timu kutoka Kenya katika mchezo wa jana. Katika hatua ya pesa ukutani walifanikiwa kulenga lango namba nne na hivyo kupata dola za kimarekani 12,000 wanazoziongeza katika dola 8,500 walizokuwa nazo awali katika hatua ya robo fainali.

Wakenya Francis Ngigi na Kepha Kimani ambao ni washindi wa pili katika nusu fainali hii wataungana na Ghana katika fainali.Ingawa waliikosakosa hatua ya ukuta wa pesa wa Guinness  bado wana nafasi ya kuwa mabingwa katika fainali.

Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness football challenge wanaweza kupima maarifa yao katika soka kupitia GUINNESS® VIP™.  Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi.  

Usikose kufuatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania

Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.

BARAZA LA HABARI LA TOA TAMKO KULAANI MASHAMBULIO YA WAANDISHI MTWARA

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MABALOZI WANNE NA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA SHERIA IKULU LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Kiwete akimwapisha Balozi Modest Mero kuwa Balozi mpya wa Kidumu Umoja wa Mataifa (UN), nchini Geneva Uswis. Jumla ya Mabolizi wanne waliapishwa na Rais kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali za nje pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha sheria.

Rais Jakaya Kiwete Rais Jakaya Kiwete akimwapisha Jaji Aloysius Mujulizi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, mbali na Mwenyekiti huyo wa Tume pia Rais aliwaapisha Mabolizi wanne kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali za nje.
Rais Jakaya Kiwete akimwapisha Balozi Modest Mero kuwa Balozi Wilson Masilingi anaekwenda Uholanzi.
Rais Jakaya Kiwete akimwapisha Balozi Modest Mero kuwa Balozi Wilson Masilingi.
Rais Jakaya Kiwete akimwapisha Balozi Modest Mero kuwa Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.
 Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Balozi Modest Mero.
 Rais Jakaya Kikwete akipiga picha ya pamoja na ndugu na jamaa wa Balozi Modest Mero Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuapishwa.
 Balozi Mero akiwa na ndugu zake Dalas (kushoto) na Mzirai.
 Balozi Modest Mero (kulia) akiwa na Michael Ley.
 Balozi Mero akipongezwa na Mpambe wa Rais (ADC to President) Kanali Kimario.
Balozi Mero akiwa na jamaa yake Richard Kasesela.

RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA TIMU YA TAIFA LEO.

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
*******
 Na. Veronica Kazimoto na Aron Msigwa–MAELEZO.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na timu ya Taifa (Taifa stars) kwa lengo la kuitia moyo katika mechi ijayo kati yake na timu ya Moroco ikiwa ni harakati za Tanzania kutafuta tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2014.

Rais Kikwete ameiambia timu hiyo kuwa ina uwezo mkubwa wa kusonga mbele kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha katika mchezo wao dhidi ya Gambia ambapo walifanikiwa kupata ushindi wa bao 2-0.

“Maadamu mara ya kwanza mliwashinda Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi dhidi ya Moroco, mkishinda tunafurahi sana na mkishindwa tunanyong’onyea sana,” amesema Rais Kikwete.

Aidha amempongeza kocha wa timu hiyo Kim Poulsen pamoja na Kamati ya Taifa ya ushindi ya Taifa stars kwa kuisaidia timu hiyo kiasi cha shilingi milioni 30 ikiwa ni mkakati wa kuiongezea nguvu kwa hatua iliyofikia na kuwataka wachezaji kujituma ili kuwafurahisha watanzania ambao hivi sasa wanaipenda timu yao ya Taifa.

Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fenera Mukangara amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo nchini ili kuondoa changamoto zinazoikabili timu hiyo.

Kwa upande wake Kocha Poulsen, amemshukuru Rais Kikwete kwa kuwakaribisha na kuwatia moyo ambapo ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo ili kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake kaptaini wa timu hiyo Juma Kaseja amemshukuru Rais Kikwete na kuahidi kujituma kwenye mazoezi na hatimaye kuibuka washindi kwenye mechi zijazo.

Taifa stars ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi C inatarajia kucheza ugenini na Morocco mnamo Juni 7 mwaka huu.

NAMASTE INDIA KWA AIRTEL PEKEE YATOSHA!!

$
0
0
India inajulikana kwa lipi zaidi? Movies(Bollywood), shule bora au matibabu??
Sasa Airtel ya kuwezesha kulonga zaidi na walio india kwa bei nafuu,Kwa tsh 3000 tu utapata dakika 25, za kuwasiliana wiki nzima.
kujiunga piga*149*13# upate kuwasiliana kwa bei poa ya shilingi 2 kwa sekunde
 Airtel Yatosha!!

KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI CCM ZIARANI BERLIN, UJERUMANI

$
0
0
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye (katikati) akikaribishwa na baadhi ya viongozi wa chama cha SPD mjini Berlin, Ujerumani alipowasili jana kuhudhuria sherehe za miaka 150 ya kuzaliwa kwa chama hicho cha SPD.

MINJA ASHINDA MILIONI 1 YA WINDA NA USHINDE YA BIA YA SERENGETI

$
0
0
 Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo, akiongea na mshindi wa droo ya kwanza ya Winda na Ushinde kwa njia ya simu iliyochezeshwa leo katika ofisi za Kampuni ya bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam
 Meneja mauzo na masoko wa kampuni ya Push Mobile Media Rugambo Rodney(katikati) akiwaonesha kitu Afisa mwandamizi wa PWC Tumainieli Malisa(kushoto) na kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo.
Meneja wa Bia ya Serengeti Allan Chonjo (katikati) akizungumza kwa njia ya simu na mshindi wa 1,000,000 wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya Winda na Ushinde leo katika ofisi za Kampuni ya bia ya Serengeti, akiwa pamoja na Meneja mauzo na masoko Rugambo Rodney(kulia) na Afisa mwandamizi wa PWC Tumainieli Malisa(kushoto). 
Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo, akimtangaza Honest Minja(38) mshindi wa Tsh 1,000,000 wa droo ya kwanza ya Winda na Ushinde kwa wana habari katika droo iliyochezeshwa leo katika ofisi za Kampuni ya bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam.

KUTOKA MAGAZETI YA TANZANIA HII LEO MEI 24,2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA UTOKOMEZAJI WA UGONJWA WA FISTULA, JIJINI DAR

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baba wa mtoto, Elizabeth Nora kutoka Dodoma aliyelazwa katika Hospitali ya CCBRT, wakati Makamu alipofika hospitalini hapo leo Mei 23, 2013 kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dokta wa Hospitali ya CCBRT, wakati alipokuwa akitembelea katika wodi za wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo, alipofika hospitalini hapo leo, kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula. Kulia ni Mtoto Boniface Patrick akiwa na Baba yake, Patrick Luwao, Wakazi wa Dodoma, akiwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji na kuongezewa sehemu ya mguu uliokuwa mfupi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Stellah Nzyemba, ambaye awali alikuwa mgonjwa na baada ya kutibiwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT na kupona ameajiriwa ili kuwasaidia wagonjwa wa Fistula. Makamu alifika hospitalini hapo leo kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika Wodi ya wagonjwa wa Fistula, wakati Makamu alipofika hospitalini hapo leo kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.
 Makamu wa Rais Dkt Bilal, akimjulia hali mtoto mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT
 Baadhi ya wasichana waliokuwa wakiugua ugonjwa huo na kutibiwa katika Hospitali ya CCBRT, ambao kwa sasa wanapewa mafunzo ya kufanya kazi za mikono.
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwasili katika eneo lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kufanyia shughuli za maadhimisho hayo

TAARIFA ZA SOKA KUTOKA TFF HII LEO

$
0
0
WENYEVITI WA FA NDIYO WASIMAMIZI RCL
Wakati mechi za kwanza za raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zinachezwa wikiendi hii, Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesisitiza kuwa wasimamizi wa mechi za ligi hiyo ni wenyeviti wa mikoa wa vyama vya mpira wa miguu.

Kamati hiyo chini ya uenyekiti wa Ramadhan Nassib ilikutana jana (Mei 23 mwaka huu) kupitia ripoti za makamishna kwa mechi za raundi ya kwanza ya RCL iliyomalizika wikiendi ya Mei 18 na 19 mwaka huu.

Kuhusu viwanja vinavyotumika kwa ligi hiyo, Kamati imesema vitaendelea kuwa vile vya makao makuu ya mikoa, na kwa vile vilivyokuwa vimeombwa vifanyiwe marekebisho ili viweze kukaguliwa kwa ajili ya RCL msimu ujao. Pia imeitaka mikoa kuendelea kuboresha viwanja vinavyotumika sasa, lakini vina upungufu.

Vilevile Kamati imebaini kuwa zimekuwepo pingamizi kuhusu usajili wa wachezaji ambapo imesema haiwezi kujadili pingamizi hizo kwa vile mikoa yote haikuwasilisha usajili wa wachezaji wa klabu husika uliofanyika mikoani kama ilivyoagizwa na kuelekezwa na TFF.


Hata hivyo, Kamati imeitaka mikoa ambayo klabu zao zimefanikiwa kuingia raundi ya pili kuwasilisha usajili huo haraka.

Pia Kamati imebaini kuwa zipo baadhi ya klabu ambazo zimekata rufani kuhusu usajili wa baadhi ya wachezaji, na kusisitiza kilichowasilishwa ni pingamizi kwa vile kwa mujibu wa kanuni masuala ya uwanjani hayakatiwi rufani. Hivyo, Kamati imeshauri klabu zilizokata rufani zilirejeshewe ada zilizolipa kwa ajili hiyo.

Makamishna na waamuzi wanaosimamia mechi za RCL wamekumbushwa kuwa ili mchezaji aruhusiwe kucheza mechi ni lazima awe na leseni yake (kadi ya usajili), vinginevyo asiruhusiwe kucheza mechi husika.
Mechi za RCL zinaendelea wikiendi hii ambapo zote zitachezwa Jumapili (Mei 26 mwaka huu) isipokuwa mechi kati ya Friends Rangers ya Dar es Salaam na African Sports ya Tanga itakayochezwa Jumamosi (Mei 25 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi.

Nayo mechi kati ya Abajalo ya Dar es Salaam na Kariakoo ya Lindi iliyokuwa ichezwe Jumamosi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam sasa itachezwa Jumapili kwa vile siku hiyo uwanja huo utatumika kwa mazoezi ya Taifa Stars.

Mechi nyingine za RCL zitakazochezwa Mei 26 mwaka huu ni Machava FC ya Kilimanjaro dhidi ya Mpwapwa Stars ya Dodoma kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.

Polisi Jamii ya Bunda mkoani Mara na Biharamulo FC ya Kagera zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma. Mjini Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika ni kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi Warriors ya Katavi.

Nayo Kimondo SC ya Mbeya itakuwa mgeni wa Njombe Mji ya Njombe katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe. Mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.

Timu zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.

SEMINA YA USAJILI- TMS KUFANYIKA MEI 25
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa semina ya usajili kwa njia ya mtandao (Transfer Matching System-TMS) kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom kwa ajili ya msimu wa 2013/2014.

Semina hiyo itafanyika Jumamosi (Mei 25 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF saa 3 kamili asubuhi ikishirikisha watu wawili kutoka kila klabu ambao ni TMS Manager, na ofisa mwingine wa klabu.

Klabu za ligi hiyo zinazotakiwa kuhudhuria semina ya usajili ni Ashanti United, Azam, Coastal Union, JKT Ruvu, Kagera Sugar, Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Oljoro JKT, Rhino Rangers, Ruvu Shooting, Simba, Tanzania Prisons na Yanga.

DC BAHI AKAGUA MRADI WA MAJI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Betty Mkwasa (nguo nyekundu) akitoka katika kukagua mitambo ya kusukumua maji iliyopo katika vyanzo vya maji vya Kijiji cha Chipanga B wilayani humo ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya kuanza kuweka mabomba mapya ambayo yanatakiwa kufika kwenye tanki ambalo mwisho wa kuingia maji humo ilikuwa mwaka 1970. Vijiji 5 vitafaidikia na mradi huo.

Chilly Willy, Dodoma Wine, CXC Africa kudhamini Redds Miss Sinza 2013

$
0
0
WAKATI jumla ya warembo 13 wamejitokeza kuwania taji la Redds Mid Sinza 2013 iliyopangwa kufanyika Juni 7, kwenye ukumbi wa Meeda Club, kampuni ya Tanzania Distillers Limited (TDL),  kinywaji cha Chilly Willy na kampuni ya  CXC Africa zimejitokeza kudhamini mashindano ya Redds Miss Sinza 2013 yaliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi w Meeda Club Juni 7.
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema jana kuwa TDL imedhamini mashindano hayo kupitia kinywaji chake cha Dodoma Wine ambao pia mwaka jana walidhamini mashindano hayo.
Majuto alisema kuwa wamepata faraja kubwa mwaka huu baada ya idadi ya warembo kuongezeka sambamba na wadhamini. Wadhamini wengine ni kampuni ya TBL kupitia Redds Original, Clouds FM, Fredito Entertainment,  Sufiani Mafoto Blog na Saluti5.
Alisema kuwa warembo wameitikia wito katika mashindano hayo kwani wanataka kutwaa taji la Miss Redds Miss Tanzania ambalo Sinza ni watetezi kupitia mrembo wake Brigitte Alfred.
“Bado tunahitaji warembo zaidi ili kupamba shoo yetu ambayo ni ya mwisho kwa kanda ya Kinondoni. Pia tunawaomba wadhamini wengine kujitokeza kwani Miss Sinza 2013 ni zaidi ya promosheni na burudani,” alisema Majuto.
Mpaka sasa warembo 13 wamejitokeza katika mashindano hayo na wapo mazoezini chini ya Miss Tanzania Top Model, Mwajabu Juma.

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mh Samuel Sitta akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2013/14 Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria,Mh Mathias Chikawe (kushoto), Mbunge wa Sengerema,Mh William Ngeleja na Mbunge wa Peramio, Mh Jenister Mhagama wakifurahi jambo wakati wakitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana. Picha zote na Zawadi Msalla wa MAELEZO.

RATIBA YA SHEREHE ZA AU KESHO - KARIMJEE HALL

$
0
0
TENTATIVE PROGRAMME FOR THE CELEBRATIONS OF THE OAU/AU GOLDEN JUBILEE ON 25th MAY, 2013
Venue                  -        Karimjee Hall
Guest of Honour  -        Hon. Bernard Kamillius Membe (MP)
Minister for Foreign Affairs and International Cooperation
TIME
EVENT
RESPONSIBLEINSTITUTION
8.00
Arrival at the Ministry
All
8.30
Lighting of the OAU/AU Torch
Hon. Membe-Minister for Foreign Affairs and International Cooperation
8.35
Festive Procession led by Brass Band
Invitees
8.45
Arrival at the Karimjee Hall
Invitees
8.50-9.10
Folk Dances
Dance Troupes
9.15-9.25
Playing of the AU and the Tanzania Anthems
Brass Band
9.30-10.00
Opening Remarks
Guest of Honour (Hon. Membe)
10.10-11.20
Panel Discussion-Pan Africanism and African Renaissance
Key Speakers: Amb. W. M. Mangachi & Mme Tonia Kandiero
Moderator: Prof. A. Mhina
11.40-12.50
Panel Discussion-OAU/AU’s Role in the Liberation Struggle and Self-determination
Key Speakers: Amb. A. Kiwanuka & Amb. T.H. Chiliza
Moderator: Amb. M. Maundi
12.50
Closing Remarks
Dean of the African Diplomatic Group
12.50
Folk Dances
Dance Troupes
13.00
Luncheon
Caterer

YANGA WAMPIGA PINI NIYOZIMA ASIENDE SIMBA

$
0
0
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KIUONGO wa Yanga, Haruna Niyonzima leo ameongeza mkataba ndani ya klabu yake kwa kujifunga kwa miaka miwili zaidi na kuwafurahisha wapenzi na wanachama wa timu yake.
 
Haruna Niyonzima wa pili kutoka kushoto, wakati anatambulishwa na uongozi wa Yanga, baada ya kupigwa pini kwa miaka miwili zaidi.

Wakati Niyonzima anazungumza na wanahabari leo Makao Makuu ya Yanga, nje kulikuwa kumezunguukwa na mashabiki na wanachama wa Yanga waliokwenda kusikiliza kinachoendelea.

Niyonzima aliishukuru Yanga na kuahidi kufanya kazi ya maana zaidi katika kuhakikisha kuwa anaitumikia timu yake kwa mafanikio makubwa zaidi.

Mchezaji huyo alizua gumzo kwa siku kadhaa baada ya mkataba wake kumalizika, hivyo timu kadhaa ikiwamo Simba kuonyesha nia ya kutaka kumnyakua akipige kwenye klabu zao.
Viewing all 10656 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>