Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10644 articles
Browse latest View live

RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA MAONYESHO YA MFUMO WA MATOKEO MAKUBWA 'SASA' AWAMU YA KWANZA

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wakati wa Ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa 'Sasa' Awamu ya Kwanza leo Mei 24, 2013
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Mtafiti Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Shetto, wakati walipokuwa wakitembelea Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa Awamu ya Kwanza, baada ya kuyafungua rasmi leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mchambuzi Sera Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mipango, Lorah Madete, wakati walipokuwa wakitembelea Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa Awamu ya Kwanza, baada ya kuyafungua rasmi leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam.
 
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwasili kwenye Ukumbi wa Jumba la Makumbusho ya Taifa, leo Mei 24, 2013 kwa ajili ya Kufungua rasmi Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa 'Sasa' Awamu ya kwanza.
 Msanii maarufu wa kughani, Mrisho Mpoto, wakibinjuka Sarakasi, wakati kikundi chake na Bendi yake ya Mjomba ilipokuwa ikitoa burudani katika Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa 'Sasa' Awamu ya Kwanza, yaliyofunguliwa na Rais Jakaya Kikwete, leo Mei 24, 2013. 
Wanamuziki wa Bendi ya Mjomba, wakiimba kutoa burudani katika Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa 'Sasa' Awamu ya Kwanza, yaliyofunguliwa na Rais Jakaya Kikwete, leo Mei 24, 2013

JK AWASILI ADDIS ABABA KUHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 50 ZA UMOJA WA NCHI ZA AFRIKA (AU)

$
0
0
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipata maelezo ya maandalizi ya sherehe hizo toka kwa balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Profesa Joram Biswaro mara baada ya kuwasili Addis Ababa.
*********
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni miongomi mwa marais wa bara la Afrika watakaohudhuria Sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Umoja  wa  nchi za Afrika (AU) zinazo fanyika rasmi leo Jumamosi Mei 25, 2013 katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia. 

 Shamrashamra zimetawala kila pembe ya jiji la Addis, wakati viongozi wa nchi za Afrika wakiwasili mmoja baada ya mwingine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole. 

 Muungano wa Afrika wakati huo ukijulikana kama OAU, ulizaliwa Mnamo Mei 25, 1963 jijini Addis Ababa, ukianza na nchi za 32 na baadaye nchi 21 zikajiunga miaka ilivyozidi kwenda, huku Afrika ya kusini ikijiunga kuwa mwanachama wa 53 mwaka 1994. 

Mwaka 2001 OAU iligeuzwa kuwa AU katika mkutano uliofanyika Lusaka, Zambia. Jumamosi hii kutakuwa na sherehe za kilele kuadhimisha miaka hiyo 50 ya AU na kuhudhuriwa na marais karibia wote wa Afrika. 

 Kauli mbiu ya sherehe za hapo kesho ni mjadala mkuu kuhusu ushirikiano wa nchi za Afrika na kuimarishwa kwa muungano huo. Mwenyekiti wa tume ya muungano huo, Dr Nkosazana Dlamini Zuma, anaseme kuwa hii itakuwa fursa kwa AU kujadili kuhusu uwezo wa bara hili na ambacho kinaweza kufikiwa katika miaka 50 ijayo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa alipowasili Ijumaa usiku  tayari kujiunga na viongozi wenzie wa nchi za Afrika katika sherehe za miaka 50  tangu kuanzishwa kwa Umoja  wa  nchi za Afrika (AU) zinazofanyika leo katika makao makuu ya umoja huo
Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete wakiwasili Addis Ababa.

KIBONZO CHA MARCO TIBASIMA HII LEO

RAIS WA ZANZIBAR AMTEMBELEA SHEHA ALIYEMWAGIWA TINDIKALI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein akimuangalia Sheha wa Shehia ya Tomodo wilaya ya Magharibi Unguja, Mohammed Said Kidevu (kulia) jinsi alivyoathirika na tindikali aliyomwagiwa na mtu asiyefahamika. Bw. Kidevu alimwagiwa tindikali hiyo juzi alipokuwa akirudi nyumbani kwake kutoka kuchota maji; amelazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar. Kushoto ni Dkt. Salim Mohammed.
Bw. Mohammed Kidevu, Sheha wa Shehia ya Tomondo, Zanzibar (kulia) akimuelezea Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein jinsi alivyomwagiwa tindikali hiyo. Bw. Kidevu alimwagiwa tindikali hiyo juzi na mtu asiyefahamika akielekea nyumbani kwake akitoka kuchota maji. Wa pili kulia ni kaka wa Bw. Kidevu, Sudu Mgeni Said.

TAMKO LA CUF JUU YA GHASIA ZA MTWARA

$
0
0
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti wa Taifa CUF.
Chama Cha Wananchi (CUF) kimesikitishwa sana na vurugu zilizotokea Mtwara tarehe 22 Mei 2013 na uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa na polisi tarehe 23 Mei 2013. Chimbuko la mgogoro wa gesi wa mikoa ya Lindi na Mtwara ni kushindwa kwa serikali ya CCM kutekeleza ahadi zaka za miradi ya kutumia gesi ya Msimbati na Mnazi Bay mkoani Mtwara na hasa ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa MW 300 na kuiunganisha Mtwara, Lindi na Ruvuma katika gridi ya taifa.

CUF inalaani vikali vitendo vya kihalifu vya kuchomea nyumba ya mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Kassim Mikongolo, na nyumba za baadhi ya viongozi wa CCM. Vile vile tunalaani vikali vitendo vya kuhujumu miundombinu muhimu likiwemo daraja la Mikindani linalounganisha Mkoa Mtwara na Mikoa ya Lindi, Pwani na Dar es Salaam.

CUF imesikitishwa sana na taarifa za vifo vya askari wanne wa JWTZ kwa ajali ya gari iliyotokea Kilimahewa wakati askari hao wakisafirishwa toka Nachingwea kwenda Mtwara kusaidia kudhibiti vurugu.Tumepeleka salamu za pole kwa CDF Jenerali Mwamunyange na kupitia kwake kwa familia za marehemu. Tunawapa pole askari wote waliojeruhiwa na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka na waweze kurejea katika ulinzi wa taifa letu.

Vilevile tumesikitishwa na kifo cha raia wawili kwa kupigwa risasi akiwemo mama mjamzito na raia wengi kujeruhiwa. Tunawapa pole familia za marehemu na kuwaombea wote waloumia wapone haraka na waendelee na shughuli zao.

Taarifa za vyombo vya habari vinaeleza kuwa ghasia hizi zilianza baada ya hotuba ya bajeti ya Waziri wa Nishati na Madini iliyosomwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusisitiza ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi toka Mtwara kwenda Dar es Salaam.

Taarifa tulizozipata toka Mtwara zinaeleza kuwa jana kuanzia asubuhi, wakati Waziri Nchimbi akisoma tamko la serikali bungeni kwa niaba ya Waziri Mkuu kuwa hali ya Mtwara sasa ni shwari askari wa Jeshi la Polisi walifanya vitendo vya kinyama kwa raia wasio na hatia.

 Polisi walipita katika nyumba za wananchi na kuwachomoa vijana, kuwapiga na kuwachukua kuwapeleka kituo cha Polisi. Mabomu ya machozi na risasi za moto zilipigwa hovyo hovyo.

Aidha katika maeneo ambayo vijana hawakuwepo waliwapiga wake zao, watoto wadogo na hata wazee kwa madai kwamba vijana wao wanasumbua. Binti mjamzito aitwae Fatuma alipigwa risasi na kufariki. Katika eneo la Mkana Read, Polisi walichoma moto soko la wananchi, nyumba nyingi za raia zimechomwa moto na polisi wamepora mali za watu zikiwemo za maduka ya wafanyabiashara. Wananchi wengi wakiwemo wanawake wamelazimika kukimbia nyumba zao. Taarifa tulizopata zinaeleza vitendo vya kinyama vya polisi vilisita baada ya maafisa wa juu wa Jeshi la Polisi kufika Mtwara.

Vurugu zilizotokea Mtwara tarehe 22 Mei hazihalalishi Jeshi la Polisi kupiga watu, kuua, kuchoma moto nyumba na vibanda vya biashara na kupora mali za watu wasio na hatia. Vitendo hivi vya polisi kupora mali na kuchoma vibanda vilitokea Tandahimba mwaka jana.

Weledi ndani ya Jeshi la Polisi uko chini sana. Tunalaani vikali vitendo vya Jeshi la Polisi la kupiga watu, kuchoma nyumba na kupora. Uongozi wa Jeshi la Polisi uchukue hatua za kinidhamu na kisheria dhidi ya polisi waliohusika na vitendo hivyo. Tunatoa wito kwa asasi za haki za binadamu na wanaotoa misaada ya kisheria kuwasaidia wahanga wa Mtwara kudai haki zao.


Pamoja na kulaani vitendo hivi vya kihalifu na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale waliohusika na vitendo hivyo, Serikali itafanya makosa makubwa na kuingiza nchi katika mgogoro wa muda mrefu na wananchi wa mikoa ya kusini ikiwa itafumbia macho chimbuko la mgogoro huu na kushikilia hoja nyepesi kuwa mgogoro huu ni matokeo ya uchochezi wa wanasiasa wachache wanaojitafutia umaarufu.

Narudia Chimbuko la mgogoro wa gesi wa mikoa ya Lindi na Mtwara ni kushindwa kwa serikali ya CCM kutekeleza ahadi za miradi ya kutumia gesi ya Msimbati na Mnazi Bay mkoani Mtwara na hasa ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa MW 300 na kuiunganisha Mtwara, Lindi na Ruvuma katika gridi ya taifa.

 Mradi mwingine ni kuanzisha kiwanda cha mbolea kitakachotumia gesi kama malighafi kama ilivyopendekezwa na Wentworth resources wanaomiliki visima vya gesi ya Mnazi Bay na Msimbati. Kama miradi hii ingeanza kutekelezwa nina uhakika wananchi wengi wa mikoa ya kusini hawatapinga gesi ya ziada kusafirishwa Dar es Salaam.

Kauli ya Waziri Nchimbi Bungeni kuwa serikali itawasaka waasisi wa vurugu hizi ndani na nje ya Mtwara ni juhudi za kutafuta mchawi badala ya kutathmini kwa nini wananchi wa Mtwara hawaiamini kabisa serikali ya CCM. Tumepata taarifa kuwa pana mpango kabambe wa kuwakamata viongozi mbalimbali wa CUF na kuuaminisha umma kuwa wanaohusika na kuchochea, kupanga na kutekeleza vurugu za Mtwara ni viongozi na wafuasi wa CUF.

Serikali ya CCM imekubuu katika kubambikia kesi nzito watu wasiokuwa na hatia. CUF inafanya siasa kwa kujenga hoja. Katika suala la gesi tumejenga hoja za kiuchumi na maendeleo na uwajibikaji wa kisiasa kuhusu utekelezaji wa miradi ambayo CCM na serikali yake iliahidi kuitekeleza. Viongozi wa CUF hawajachochea vurugu wametumia majukwaa ya mikutano ya hadhara na maandamano ya amani kujenga hoja za kimsingi.

Mimi binafsi nilienda Mtwara mwaka jana nikazuwiwa kufanya mkutano wa hadhara Mtwara mjini kwa madai kuwa hali siyo shwari wilaya ya Tandahimba. Wananchi wa Mtwara walitaka nifanye mkutano huo pamoja na kuwa umezuwiwa na polisi, nikawasihi tusifanye hivyo na wakakubali. Tarehe 14 Aprili 2013 nilikuwa Mtwara nikazuwiwa kufanya mkutano wa hadhara sikukaidi nikafanya mkutano wa ndani. Maalim Seif, Katibu Mkuu wa CUF na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alitaka kufanya ziara ya mkoa wa Mtwara akaambiwa hana ruhusa ya kufanya mikutano ya hadhara mkoa wa Mtwara na hivyo akasitisha ziara yake.

Kuwakamata viongozi wa CUF wa wilaya za Mtwara na Lindi na wa kitaifa hakutamaliza mgogoro kati ya serikali na wananchi wa Mtwara ikiwa serikali itaendelea kuwabeza, kuwadharau na kutowasikiliza. Badala yake itaongeza chuki dhidi ya serikali.

Wakati wananchi wa Mtwara wamepoteza imani kwa uongozi wa CCM na serikali yake, Serikali imezuia vyama vingine vya siasa na asasi za kiraia kufanya shughuli za kuwasiliana na wananchi wa Mtwara na kwa hiyo kuunyima umma miongozo ya kisiasa za demokrasia. Umma uliokata tamaa na unaoamini unabezwa, kudharauliwa na kudanganywa na watawala unaweza kuchukua hatua zenye madhara hata kwa maslahi yao wenyewe.

Serikali imekuwa inapotosha kwa makusudi madai ya msingi ya wananchi wa Mtwara ambayo ni kuwa serikali itekeleze miradi ya gesi iliyoahidi wananchi wa Mtwara. Badala yake wananchi wa mikoa mingine wanalishwa sumu kuwa Wananchi wa Mtwara hawataki raslimali ya gesi iwanufaishe Watanzania wengine. Umeme ukifuliwa Mtwara na kuunganishwa katika gridi ya taifa utatumiwa na wote waliounganishwa na gridi ya taifa. Kiwanda cha mbolea cha Mtwara kitazalisha mbolea itakayotumiwa nchi nzima. Wananchi wa Mtwara hawajasema Watanzania wengine hawana haki ya kwenda Mtwara kupata ajira au kufanya shughuli za kibiashara.

 Wanaobomoa umoja na mshikamano wa kitaifa ni wale wanaowabeza, kuwadharau na kuendelea kuwadanganya wananchi wa Mtwara na kupandikiza sumu kwa Watanzania wengine kwa kupotosha madai ya msingi ya wananchi wa Mtwara na kushindwa kwa serikali kuwajibika kisiasa kwa ahadi ambazo viongozi akiwemo Rais alizitoa kwa wananchi wa Mtwara.

Wananchi wa Mtwara zaidi ya elfu 24 wameweka sahihi na kupeleka ombi (petition) kupitia Mhe. Habibu Mnyaa, Mbunge wa Mkanyageni kujadili kutekelezwa kwa miradi ya gesi ya Mtwara. Spika Anna Makinda kazuwia ombi hilo kujadiliwa.

Bunge limeshindwa kuisimamia serikali na kuhoji kwa nini mradi wa kufua umeme MW 300 ambao katika mwaka wa bajeti wa 2011/12 ulitengewa na kutumia shilingi 540 milioni umesitishwa. Mpaka hivi sasa hakuna kamati ya Bunge iliyoenda kusikiliza kilio cha Wananchi wa Mtwara badala yake Spika amekuwa mstari wa mbele kuunga mkono vitendo vya serikali badala ya kuhakikisha kuwa Bunge linaisisimamia serikali.

Katika hotuba ya bajeti ya mwaka huu, Waziri kaeleza serikali kupitia TANESCO kwa kwa kushirikiana na kampuni ya Symbion itajenga kituo cha kufua umeme cha MW 400 na kuunganisha Mtwara na gridi ya taifa kupitia Songea.

Hata hivyo bajeti ya maendeleo haijautaja mradi huu wala kutenga hata shilingi 1 kwenye mradi. Wananchi wa Mtwara wanaona wanaendelea kudanganywa na serikali ya CCM. Mikogo, majigambo na kauli za kejeli za Waziri wa Nishati kuhusu uelewa mdogo wa wananchi wa Mtwara katika masuala ya gesi zinazidi kuongeza chuki na jazba za wananchi.

Mpaka hivi sasa serikali imekataa kuweka wazi mkataba wa ujenzi wa bomba na upembuzi yakinifu wa mradi huu. Hotuba ya bajeti ya Waziri wa Nishati haielezi kama Wentworth Resources wanaoendesha visima vya gesi wataweza kuzalisha gesi kukidhi ukubwa wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam na ahadi mpya za miradi ya kutumia gesi mkoani Mtwara.

Linalonistusha na kunitisha ni kwa nini viongozi wa juu wa serikali hawataki kuwa wawazi kuhusu mradi huu na wako tayari kupotosha, kuwagawa wananchi na kudanganya alimuradi mradi huu utekelezwe na usihojiwe?

Gesi ya Mnazi Bay, Mtwara iligunduliwa toka mwaka 1982 lakini mpaka hivi sasa haijatumiwa kikamilifu. Kampuni ya Artumas ilianza utaratibu wa kuichimba gesi mwaka 2006 na kuitumia kufua umeme wa Megawati 18. Tarehe 17 Oktoba 2007 kampuni ya Artumas ilitoa taarifa ya mpango wake wa kujenga kituo cha kufua umeme wa MW 300. Mpango huu ulitarajiwa kugharamiwa toka Mfuko wa Maendeleo wa Uholanzi - Netherlands Development Finance Company. Gharama za mradi wa kufua umeme zilikadiriwa kuwa dola za Marekani 225.

Kampuni maalum ya kuendesha mradi huu ya Tanzania Generation Company Ltd (TANGEN) ilisajiliwa ili kujenga na kuendesha mradi huu. Kampuni hii ingekopa dola milioni 160 na dola milioni 65 zingechangiwa kama hisa na kampuni nyingine zikiwemo mifuko ya pensheni ya Tanzania na kampuni ya madini ya Barrick International.

Kampuni nyingine maalum ilitarajiwa kuanzishwa ili ijenge msongo wa umeme (nguzo za nyaya za kusambaza umeme) na kuunganisha umeme wa Mnazi Bay kwenye gridi ya taifa. Mradi huu ungegharimu dola milioni 400. Mradi huu ulitarajiwa kugharamiwa na mifuko ya pensheni ya Tanzania na wawekezaji kutoka Mashariki ya Kati. Mpango huu ulikubaliwa na serikali na ukaingizwa katika Mpango Kabambe wa Taifa wa kufua na kusambaza umeme (National Power Development Master Plan). Mradi huu wa kufua umeme MW 300 Mtwara ulipangwa uwe umekamilika mwaka wa 2012. Tovuti ya Tanesco inaueleza mpango huu kuwa ni wa muda wa kati. Bila shaka serikali iliukabali mradi huu baada ya kuufanyia utafiti na upembuzi yakinifu.

Mtikisiko wa sekta ya fedha na uchumi wa dunia wa mwaka 2008 uliathiri kampuni ya Artumas. Thamani ya hisa moja ya Artumas iliporomoka toka dola za Marekani 10.80 mwezi wa Aprili 2008 na kufikia dola 0.12 mwezi wa Machi 2009. Kampuni ilipata matatizo makubwa ya ukata na ilibidi serikali iisaidie dola milioni 7 ili iweze kuendelea na ufuaji wa umeme wa MW 18 Mtwara. Barrick International ilijitoa katika mradi wa TANGEN. Katika kujiunda upya Kampuni ya Artumas Group Inc. iliamua kubadilisha jina lake na kuwa Wentworth Resources Limited na kuteua menejimenti mpya.

Tarehe 10 Juni 2009 Rais Kikwete alipokuwa anawahutubia Wabunge na Wananchi katika Ukumbi wa Kilimani Dodoma kuhusu athari za mtikisiko wa uchumi duniani alieleza “Kwa sababu ya matatizo ya uchumi uwekezaji wa vitega uchumi kutoka nje umepungua.

Wawekezaji wamekuwa wanakosa fedha kutoka mabenki na masoko ya mitaji. Matokeo yake ni kuchelewa au kukosa kabisa au kuahirishwa miradi mikubwa ambayo ingetoa mchango muhimu kwa ukuaji wa uchumi wetu na ajira. Kwa mfano: Mradi wa umeme wa MW 300 kule Mtwara kwa sababu ya Barrick Gold Ltd. kujitoa na Artumas peke yake haina uwezo wa kifedha; mradi wa nickel Kabanga, mradi wa aluminium smelter, Mtwara; mradi wa usambazaji umeme mkoani Mtwara, miradi ya viwanda vya saruji na mbolea Mtwara.”

 Kwa kauli ya Rais ambayo wananchi wa Mtwara na Watanzania kwa ujumla waliisikia kwani hotuba hii ilirushwa live na Shirika la Utangazaji la Tanzania – Radio na Televisheni na vyombo vingine vya habari.

 Miradi ya kutumia gesi ni pamoja na kufua umeme MW 300, kutengeneza mbolea inayotumia gesi kama malighafi, aluminium smelter inayohitaji umeme mwingi, na kiwanda cha saruji ambacho kinatumia umeme na kinu chake kinaweza kutumia gesi. Wananchi wakamuamini Rais wetu na wakaelewa kuwa miradi hii imekwama kwa sababu ya mtikisiko wa uchumi na kwamba serikali inajitahidi kutafuta njia mbadala ya kujikwamua ili miradi hiyo iendelee.

Wakati wa kampeni ya uchaguzi wa 2010, Rais Kikwete aliwaeleza wananchi wa Mtwara akichaguliwa ataendeleza miradi ya Mtwara itakayotumia gesi ya Mnazi Bay. Maelezo ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi wa 2010, ibara ya 63 kifungu (j) Kuzalisha umeme (300MW) kutokana na gesi asili ya Mnazi Bay (k) Kupanua mitambo ya kusafisha gesi na bomba la kusafirisha gesi kutoka Songo Songo hadi Dar es Salaam.

Mitambo ya kufua umeme ya Dar es Salaam ilitegemewa itumie gesi ya Songosongo kwani bomba la kutoka Songosongo hadi Somanga mpaka Dar es Salaam lingepanuliwa. Toka mwaka 2010 kampuni ya Globeleq- Songas ilijiandaa kutekeleza mradi wa kuongeza uwezo wa bomba la gesi kutoka Songosongo – Somanga – Dar es Salaam ili likidhi mahitaji ya gesi ya vituo vya kufua umeme Dar es Salaam kikiwemo kituo cha Kinyerezi. Serikali iliisitisha kampuni hiyo isiendelee na mradi huo ambao hivi sasa ungekuwa umekamilika na kuongeza uwezo wa kufua umeme kwa kutumia gesi kwa alau MW 200.

Rais Kikwete alipoenda Mtwara kuhudhuria sherehe ya Mashujaa tarehe 25 Julai 2011 alizungumza na wananchi wa Mtwara na kueleza miradi ya maendeleo itakayotekelezwa kwa kutumia gesi ya Mnazi Bay ikiwemo ufuaji wa umeme wa MW 300 na kupanua bandari ya Mtwara.

Tarehe 12 Oktoba 2011, Ikulu ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa “Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Oktoba 12, 2011, amepokea ripoti kutoka makampuni mawili ya kimataifa kuhusu Mpango Kabambe ya mradi mkubwa wa umeme ambao utaunganisha kwenye Gridi ya Taifa mikoa yote sita ambayo kwa sasa haiko kwenye gridi hiyo. Rais Kikwete amepokea ripoti hiyo kutoka makampuni ya China National Machinery&Equipment Import&Export Corporation (CMEC) ya China na Siemens ya Ujerumani ambayo kwa pamoja yanatarajia kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kutokana na gesi katika eneo la Mnazi Bay, mjini Mtwara na pia kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kilomita 1,100 kutoka Mtwara hadi Singida. Mradi huo mkubwa wa umeme wa megawati 300 utakaogharimu karibu dola za Marekani milioni 684 na utakaozalisha umeme wa moja kwa moja na wenye nguvu kubwa ya 300 kV (300 kV High Voltage Direct Current – HVDC) utagharimiwa kwa pamoja na mkopo kutoka Benki ya Exim ya China na Serikali ya Tanzania.”

Mikoa sita ambayo bado haijaunganishwa na gridi ya taifa ni Lindi, Mtwara, Ruvuma, Rukwa, Kigoma na Kagera. Mradi huu pamoja na kufua umeme wa MW 300 Mtwara ungekamilisha kuunganisha mikoa yote ya Tanzania kwenye gridi ya taifa. Taarifa iliendelea kueleza “Kuunganisha mikoa yote ya Tanzania kwenye Gridi ya Taifa ilikuwa moja ya ahadi kubwa zilizotolewa na Serikali ya Rais Kikwete wakati anaingia maradakani na kwa kuuunganisha mikoa hiyo sita kwenye Gridi hiyo, Serikali hiyo itakuwa imetimimiza ahadi hiyo.”

Maelezo haya yametolewa na Ikulu na vyombo vya habari vikayatangaza na wananchi wa Mtwara wakasikia. Kutekeleza mradi wa kufua umeme kutaifanya Mtwara iwe na umeme wa kutosha kushawishi kampuni kuanzisha viwanda hasa ukizingatia ahadi ya Rais Kikwete ya kupanua bandari ya Mtwara. Mwaka wa fedha wa 2011/12 serikali ilitenga na kutumia shilingi 540 milioni fedha za maendeleo za mradi wa Mnazi Bay 300MW Development Project. Baada ya hapo mradi huu haukutengewa fedha tena. Badala ya mradi huu kuendelezwa kama Rais alivyowaahidi wananchi wa Mtwara na Watanzania kwa ujumla badala yake wanasikia serikali imezindua mradi wa kujenga bomba la kusafirisha gesi toka Mtwara kuja Dar es Salaam.

Kwa taarifa ya Ikulu gharama za mradi wa kufua umeme wa MW 300 Mtwara na kuiunganisha mikoa sita katika gridi ya taifa gharama yake ni dola milioni 684. Mradi wa kutandaza bomba la gesi unagharimiwa na mkopo wa dola milioni 1220 kutoka Benki ya Export Import Bank ya China. Ni wazi gharama za kufua umeme Mtwara na kuunganisha mikoa sita kwenye gridi ya taifa ni ndogo zaidi kuliko gharama za kutandaza bomba la gesi.

Msongo wa umeme za kV 400 unajengwa kuunganisha Iringa – Dodoma – Singida na Shinyanga. Mradi huu unatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika. Nyaraka ya mradi unaonyesha gharama za kujenga umeme za kV 400 ni dola za Marekani  600,000 kwa kilomita 1. Gharama za kujenga bomba la gesi lenye kipenyo (upana wa nchi 36) ni dola 1,309,636 kwa kilomita 1. Kwa madhumuni ya kufua umeme, gharama ya kujenga bomba la gesi ni zaidi ya mara mbili ya gharama za kunganisha Mtwara na Dar es Salaam. Isitoshe unaweza kuongeza ufuaji wa umeme Mtwara na kusamabaza kwa msongo huo huo.

Ujenzi wa bomba la Dar es Salaam Mtwara umeanza bila kuwa na mipango ya kuhakikisha kuwa kutakuwepo na gesi ya kutosha kuisafirisha hadi Dar es Salaam. Bomba hili litakuwa na uwezo wa kusafirisha futi za ujazo bilioni 200. Uwezo wa gesi ya Mnazi Bay na Msimbati kwa hivi sasa ni futi za ujazo bilioni 80. Hakuna mpango unaoeleweka wa kupata futi za ujazo bilioni 120 ili bomba la gesi liweze kutumiwa kikamilifu.

Mpaka hivi sasa gesi kiasi cha futi za ujazo trilioni 33.7 imegunduliwa katika bahari yenye kina kirefu. Uchimbaji wa gesi hii bado haujaanza. Inaweza kuchukukua miaka 7 – 10 kabla ya shughuli ya uchimbaji wa gesi kukamilika. Kampuni zilizogundua gesi bahari kuu bado hazijafanya uamuzi wa utaratibu wa kuichimba na kuisafirisha gesi hadi nchi kavu. Kwa kuwa gharama za kujenga bomba la gesi chini ya bahari ni za juu sana, kampuni hizi zitapendelea kutandaza bomba kwenda nchi kavu kwenye eneo lililo fupi kuliko yote.

Statoil imegundua gesi nyingi eneo la Zafarani bahari kuu eneo la mkoa wa Lindi. Hivi sasa wanatazama maeneo ya Kilwa kuweza kuweka kituo cha nchi kavu. Bandari ya Lushungu kata ya Limalyao, wilaya ya Kilwa ambayo ina kina kirefu cha bahari yaelekea kuwavutia. Kwa hivi sasa hakuna uhakika gesi iliyogunduliwa bahari kuu itapelekwa Mtwara. Uamuzi wa kujenga bomba kubwa umefanywa haraka haraka bila kutathmini kikamilifu faida zake kiuchumi. Jambo la kujiuliza kwa nini uamuzi huu umechukuliwa na kuacha kutekeleza mradi wa kufua umeme Mtwara wenye mantiki kiuchumi, kijamii na uwajibikaji wa kisiasa?

Wentworth Resources wamefanya upembuzi yakinifu (feasibility study) na kubaini kwamba njia nzuri ya kibiashara na kiuchumi ya kutumia gas wanayoweza kuzalisha Mnazi bay hivi sasa ni kuanzisha kiwanda cha kutengeneza mbolea na kemikali nyingine Mtwara. Kiwanda cha mbolea chenye faida kubwa kinaweza kuanzishwa na kuendeshwa hata kama akiba ya gesi iliyogunduliwa siyo kubwa sana kama ilivyo Mnazi Bay. Mradi wa kujenga kiwanda unaweza kukamilishwa kwa muda mfupi. Pamoja na mbolea kiwanda kitazalisha methanol yenye soko kubwa duniani. Kiwanda kitatumia hewa ukaa (carbondioxide) na kwa hiyo kuweza kupata fidia ya kuboresha mazingira. Uongozi wa Wentworth Resources una uzoefu wa miaka mingi katika miradi ya kutumia gesi. Wanajua wanalolieleza. Hata hivyo serikali imewamrisha kupeleka gesi watakayozalisha kwenye bomba la gesi la kwenda Dar es Salaam.

Serikali imeanzisha mgogoro wa gesi kwa kuanza kutekeleza mradi mkubwa wa kutandaza bomba la mafuta na kuacha miradi yenye manufaa makubwa kiuchumi na kijamii kwa taifa letu. Uchunguzi huru na wa kina ufanyike kubaini sababu za serikali kuacha miradi ya kutumia gesi Mtwara na kukumbatia mradi wa kutandaza bomba. Ripoti aliyopewa Rais ya mradi wa kufua umeme Mtwara na kuunganisha mikoa 6 katika gridi ya taifa itolewe ili Watanzania waweze kuelewa mantiki ya mradi huu. Mkataba wa mkopo na utekelezaji wa mradi wa kutandaza bomba la gesi uwekwe wazi. Serikali iruhusu kampuni ya Wentworth resources kuendelea na mradi wa kiwanda cha mbolea. Rais aende Mtwara kuwaeleza wananchi kuwa ahadi alizoeleza za kutumia gesi Mtwara zitatekelezwa.

Vyama vya siasa na asasi za kiraia viruhusiwe kufanya mikutano ya hadhara kueleza njia za kidemokrasia za kudai haki za kiuchumi za wananchi wa Mtwara. Bunge liunde kamati teule ya kuchunguza kwa nini Mradi wa Kufua umeme MW 300 umesitishwa na serikali, upembuzi yakinifu wa mradi wa bomba la gesi na mikataba yote inayohusiana na mradi huu.

Sakata hili la gesi ya Mtwara linaonyesha wazi kuwa hatuna sera muafaka na mkakati wa kuendeleza sekta ya gesi kwa manufaa ya taifa letu na Wananchi wa kawaida. Badala ya gesi kuwa neema inaelekea kuwa itakuwa balaa na laana. Sera ya gesi inapaswa kuweka taratibu zitakazohakikisha kuwepo kwa uwekezaji wa kutosha katika sekta hii na utakaolinufaisha taifa letu bila kuathiri motisha kwa wawekezaji wenye teknolojia ya kutafuta na kuchimba gesi. Wananchi wa Mtwara wanahitaji kushirikishwa. Serikali iwe wazi na kutoa taarifa sahihi kuhusu miradi ya gesi.

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti wa Taifa, Mei 24 2013

RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA AU JIJINI ADDIS ABABA LEO

$
0
0
 
Muono wa jicho la samaki katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013
Marais Wastaafu wakiwa katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013
Viongoi AU wakiwakumbuka waliotangulia mbele ya haki.

ISSERE SPORTS YATOA JEZI, MIPIRA KWA VIJANA KONDOA

$
0
0
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally Isere (kulia) akimkabidhi jezi seti moja mwakilishi, Dige Shaaban Nkusa kwa ajili ya timu ya vijana wa kijiji cha Mwembeni wilayani Kondoa ili kuimarisha michezo vijijini.

 Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Isere Sports imetoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. mil. 1.7 kwa ajili ya kuendeleza vijana katika wilaya ya Kondoa.

Akikabidhi vifaa hivyo jana, Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Isere alisema ametoa vifaa hivyo ili kuwasaidia vijana kupenda michezo ili kujenga afya na kujikinga na vitengo cha kihalifu.


Abbas alisema vifaa alivyotoa ni kwa ajili ya vijiji vya Changaa kwa Mafunchi ambako wamepewa jezi, mipira na soksi, katika kijiji cha Mwembeni kata ya Hondomairo wilayani Kondoa wamekabidhiwa vifaa kama hivyo.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya vijana wa Changaa, Issa Lubuva alisema umefika wakati kwa wananchi waishio mijini kuwakumbuka vijana waliobaki nyumbani kwa kuwapatia vifaa vya michezo.

Naye Dige Shaaban aliyepokea vifaa kwa niaba ya kijiji cha Mwembeni alisema wachezaji wengi wapo vijijini lakini hawajapata fursa ya kuonesha vipaji vyao hivyo vifaa hivyo vitasaidia kutoa wachezaji kutoka wilaya ya Kondoa.

MADABIDA MGENI RASMI TAMASHA LA WASANII CHIPUKIZI LA MTANDAO WA WASANII TANZANIA (SHIWATA)

$
0
0
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida atakuwa mgeni rasmi katika tamasha la Mastaa chipukizi zaidi ya 320 litafanyika Jumapili 26, 2013 katika ukumbi wa Starlight Hotel kuanzia saa 4 asubuhi.

Mwenyekiti wa Shiwata, Caasim Taalib alisema Madabida ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) atapata nafasi ya kuona vikundi mbalimbali vya sanaa kikiwepo kikundi cha  Kaole, Splendid, Super Shine Taarab pa moja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na Sarakasi nao wamethibitisha kushiriki.

Taalib alisema wasanii wakongwe wa bongo flava walioalikwa ni Stara Thomas, Safi Theatre Group, Ommy G na waigizaji wakongwe wa Kaole na Splendid wataonesha umahiri wao katika fani ya sanaa Kauli Mbiu ikiwa ni Kilio cha Msanii .

Vikundi vingine vitakavyonesha vipaji vyao ni Kepteni  Shaibu, Tanzania Disabled, Uyoga Boga Village, Ndafu Arts Group, CGC, Magengistar Crew, Dodo Arts Group, Culture Arts Group, Wachapa Kazi Academy, Soweto Picture, Shiwata Commedy, Mwavionelachi, Manuari Arts Group, Tandale Morden Taarab na Begeja Wushu.

 Taalib alisema tamasha hilo ambalo limepata kibali cha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pia wamealikwa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania,Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Shirikisho la Muziki Tanzania na Shirikisho la Sanaa za maonesho Tanzania.

Mwenyekiti aliwaomba viongozi wengine wa bendi za muziki, taarab, vikundi vya sanaa,mapromota,maprodusa na wadau wote kushiriki katika tamasha hilo ili kujenga ushirikiano wa pamoja.

MISS TANZANIA 1999, AWAFUNDA REDD'S MISS KIGAMBONI

$
0
0


 Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akizungumza na warembo wanao wania taji la Redd's Miss Kigamboni 2013 wakati malikia huyo wa miaka 14 iliyopita alipo zuru kambi ya warembo hao jijini Dar es Salaam na kuwapa nasaha na mbinu mbalimbali za ushindi wa taji hilo na lile na Miss temeke na baade Redd's Miss Tanzania 2013. Picha ya chini ni Hoyce ambaye sasa ni Mfanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania na mwandaaji wa Kipindi cha Televisheni cha Mimi  na Tanzania akiwa na wartembo katika picha ya pamoja.


Na Mwandishi Wetu
MREMBO wa Tanzania mwaka 1999, Hoyce Temu, amewataka warembo hapa nchini kuwa na nidhamu na kutotumia mashindano hayo kama sehemu ya kujitafutia umaarufu.

Hoyce aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipotembelea kambi ya warembo wanaoshiriki wa shindano la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Redd's Miss Kigamboni 2013' litakalofanyika Ijumaa Juni 7 kwenye ukumbi wa Navy Beach, Kigamboni.

Akizungumza na washiriki hao, Hoyce, aliwataka warembo kujiamini, kujiheshimu na kuwa mabalozi wema kwa jamii inayowazunguka hapa nchini kabla na baada ya kumaliza mashindano.

Hoyce aliwataka warembo hao kuwa na mawazo ya kujiendeleza na kamwe wasiridhike na elimu waliyonayo sana kwani urembo walionao hivi sasa una mwisho.

"Nawaomba mfahamu kuwa nyie ni madalali (mabalozi) wa jamii inayowazunguka na kila mara mfikiri kujiendelea, urembo sio kichaka cha wahalifu, wezi au kutumia miili  yenu kufanya mambo yasiyokubalika na jamii," Hoyce alimaliza.

Naye mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa maandalizi ya kinyang'anyiro hicho yanaendelea vizuri na kuongeza kwamba anaridhishwa na nidhamu na warembo.

Alisema kwamba kamati ya shindano hilo imejipanga kufanya shoo nzuri zaidi mwaka huu na kuwaambia wadau wa sanaa ya urembo kufika kushuhuria safari ya kumtoa mshindi wa taifa ikianzia kwenye kitongoji hicho.

Aliwataja warembo wanaoendelea na mazoezi kuwania taji hilo ni pamoja na Rogathe Michael, Irene Rajab, Magdalena Olotu, Latifa Mohammed, Axsaritha Vedastus, Angella Lutataza, Sara Makembo, Amina Mussa,  Ellen Sulle, Rachel Reuben, Margareth Gerald na Zuhura Masoud.

Aliyataka makampuni na taasisi mbalimbali zinakaribishwa kudhamini shindano hilo ambalo mwaka jana lilitoa mshindi katika kinyang'anyiro cha Kanda ya Temeke ambaye ni Edda Sylivester.
Warembo watano watakaoshika nafasi za juu kwenye shindano hilo watapata nafasi ya kushiriki kinyang'anyiro cha Redd's Miss Temeke baadaye mwaka huu.

Wadhamini ambao wamethibitisha kusaidia shindano hilo ni pamoja na kampuni ya bia Tanzania kupitia kinywaji cha Redd's Premium Original,Dodoma Wine, Montage Limited, Clouds Media Group, Papa Z, Logitik, Glolab Agency Limited, Cyn Henjewele na Wasemaje Blog.

Taji la Redd's Miss Tanzania linashikiliwa na Brigitte Alfred wakati Edda alishika alifanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye fainali hizo za taifa mwaka jana.

MARTHA GEWE ANYAKUA TAJI LA REDD'S MISS UKONGA 2013

$
0
0
 
Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Ukonga 2013, Martha Gewe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili, Diana Joachim (kushoto) pamoja na mrembo aliyeshika nafasi ya tatu, Natasha Mohamed mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa ndio washindi wa shindano hilo Usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Ukumbi wa Wenge Garden Ukonga Mombasa jijini Dar es Salaam. Martha aliwashinda warembo wengine 12 katika shindano hilo.
Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Redd’s Miss Ukonga 2013 wakiwa katika picha ya pamoja kutoka kushoto ni Vanesa Magile, Matha Gewe, Diana Joachim, Natasha Mohamed na Nancy Abasy shindano lilifanyika Ukumbi wa Wenge Garden Ukonga Mombasa jijini Dar es Salaam. Martha.
 
Baadhi ya washiriki wa Shindano la Redd’s Miss Ukonga 2013 wakicheza show ya ufunguzi wa shindano lao lililofanyika usiku wa kuamkia jana katika ukumbi wa Wenge Garden Ukonga jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya majaji wa shindano hilo wakiongozwa na William Malecela 'Le Mutuz' (mwenye kofia) wakifuatilia shindano hilo kwa umakini.
 Gwiji wa Mipasho nchini Tanzania, Malkia Hadija Omar Kopa aliongoza upande wa Burudani na kukonga nyoyo za mashabiki wake na wa sanaa ya urembo katika eneo la Ukonga na viunga vyake.
 Baadhi ya warembo wa Ukonga walioshiriki shindano hilo 2012 na katikati ndiye aliyevua taji jana Elizabeth.
 Warembo mbalimbal;i walioshiriki Redd's Miss Ukonga wakijinadi na vazi la ubunifu jukwaani.
 Martha Gewe akijinadi na kivazi cha Ufukweni
 Annatolia Raphael nae alirusha kete yake jukwaani na vazi la ufukweni.
 B Band ikiongozwa na Mtanashati, Banana Zahiri Ali Zoro nayo ilikuwepo ndani ya Wenge Garden Ukonga Mombasa kusindikiza vilivyo show hiyo.
 Redd's Miss Tanzania aliyeshika nafasi ya pili 2012, Eugenia (kushoto) nawashiriki wenzake wa shindano hilo mwaka jana walikuwepo Ukonga.
 Redd's Miss Tabata 2013 nao walifika kujitambulisha na kuwakaribisha wana Ukonga katika onesho lao litakalofanyika Ijumaa katika ukumbu wa DarWest Park Tabata. Warembo hawa muda huu wapo Mikumi kwa ziara ya kutalii.
 Baada ya kupita jukwaani na vazi la usiku washiriki wote wa Redd's Miss Ukonga 2013 walijipanga jukwaani.
 Mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa (katikati), Mdau wa Miss Ukonga  Daud Mambya (kushoto) pamoja na Regina Ogwal wakifuatilia matukio katika shindano hilo.
 Jaji Mkuu wa Shindano hilo William Malecela akitangaza majina ya washindi.
 Mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa (katikati), Mdau wa Miss Ukonga  Daud Mambya (kushoto) pamoja na mmoja wa wadhamini wa Shindano hilo, Kampuni ya Mambya Insurance, John Mambya wakifuatilia shindano.
 Ofisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania, Hidan Ricco (kulia) akiwa pamoja na Mwandaaji wa Miss Tabata, Fredy Ogot na Mwandaaji wa Miss Moshi, Jacqueline Chuwa.

NCHI 22 ZA AFRIKA ZAPATA DARASA JUU YA AMANI YA MTU BINAFSI JANA

$
0
0

Mtaalam na mkufunzi wa masuala ya amani ya mtu binafsi kwa njia ya kutafakari kutoka taasisi ya Art of Living, Chandrika Magaraja akitoa maelezo juu ya amani ya mtu binafsi inavyoweza kupatikana kwa kutafakari wakati wa kushiriki Mafunzo hayo yalifanyika jana kwa njia ya video na kufanyika kwa wakati mmoja kwa nchi 22 za Afrika na yaliongozwa na Kiongozi wa Art of Living Duniani ambaye pia ni Balozi wa Amani Sri Sri Ravi Shankar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Umoja wa Afrika (AU).


Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam walioshiriki katika katika kutafakari ambayo ni njia bora na yapekee ya kuleta amani ya mtu binafsi. Mafunzo hayo yalifanyika jana kwa njia ya video na kufanyika kwa wakati mmoja kwa nchi 22 za Afrika na yaliongozwa na Kiongozi wa Art of Living Duniani ambaye pia ni Balozi wa Amani Sri Sri Ravi Shankar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Umoja wa Afrika (AU). 

Balozi wa Jamhuri ya Djbout nchini Tanzania, Saidi Amin Shamo (kushoto) na Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw wakishiriki katika kutafakari ambayo ni njia bora na yapekee ya kuleta amani ya mtu binafsi. Mafunzo hayo yalifanyika jana kwa njia ya video na kufanyika kwa wakati mmoja kwa nchi 22 za Afrika na yaliongozwa na Kiongozi wa Art of Living Duniani ambaye pia ni Balozi wa Amani Sri Sri Ravi Shankar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Umoja wa Afrika (AU). 
 Balozi wa Jamhuri ya Djbout nchini Tanzania, Saidi Amin Shamo (kushoto) Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw (katikati) na Mwakilishi na Mtaalam na mkufunzi wa masuala ya Kutafakari kutoka Taasisi ya Art of Living, Chandrika Magaraja wakishiriki katika kutafakari ambayo ni njia bora na yapekee ya kuleta amani ya mtu binafsi. Mafunzo hayo yalifanyika jana kwa njia ya video na kufanyika kwa wakati mmoja kwa nchi 22 za Afrika na yaliongozwa na Kiongozi wa Art of Living Duniani ambaye pia ni Balozi wa Amani Sri Sri Ravi Shankar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Umoja wa Afrika (AU). 
Wageni maalum katika mafunzo maalum ya ya amani ya Mtu bianfsi kwa njia ya kutafakari kutoka kulia Mwakilishi na Mtaalam na mkufunzi wa masuala ya Kutafakari kutoka Taasisi ya Art of Living, Chandrika Magaraja,  Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw, Balozi wa Jamhuri ya Djbout nchini, Saidi Amin Shamo, Mke wa Balozi Shamo, Mariam Shamo, Mke wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) Theresa Gannon na Mkurugenzi wa SBL, Steven Gannon,  wakishiriki katika kutafakari ambayo ni njia bora na yapekee ya kuleta amani ya mtu binafsi. Mafunzo hayo yalifanyika jana kwa njia ya video na kufanyika kwa wakati mmoja kwa nchi 22 za Afrika na yaliongozwa na Kiongozi wa Art of Living Duniani ambaye pia ni Balozi wa Amani Sri Sri Ravi Shankar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Umoja wa Afrika (AU). 

STELLA MWANGI A.K.A STL KUTUMBUIZA UZINDUZI WA BIG BROTHER JIJINI JO’BURG AFRIKA KUSINI LEO

$
0
0
IMG_0004
Mmoja wa wasanii watakaotumbuiza jioni hii kwenye uzinduzi wa show ya Big Brother-The Chase Stella Mwangi a.k.a STL kutoka Kenya akifanya mahojiano na Tsholofelo Mothibi wa Vuzu Tv ya nchini Afrika Kusini kwenye mkutano wa kutambulisha wasanii watakaotoa burudani kwenye uzinduzi huo leo. Kaa tayari kushuhudia uzinduzi huo Live kupitia DStv channel 197 na 198 kuanzia saa moja jioni usiku wa leo. Unaweza pia kutazama Live Stream kupitia www.bigbrotherafrica.com
IMG_0001
Senior PR Manager wa Multichoice Africa Sandhya Singh akibadilisha mawazo na baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi mbambali watakaoshuhudia Live uzinduzi wa Show ya Big Brother The Chase wakati wa kutambulisha wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza usiku wa leo jijini Johannesburg Afrika Kusini.

IMG_9975
Mwandishi wa Daily Monitor Uganda Henry Ssali na Faith wa Nairobi Star wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa mkutano huo.
IMG_9972
M-Net Africa Managing Director Biola Alabi.
IMG_9977
Baadhi ya waandishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakati wa mkutano huo.
IMG_9983
Stella Mwangi a.k.a STL na wasanii wenzake wakifuatilia jambo kwenye mkutano huo.
IMG_0025
M-Net Africa Managing Director Biola Alabi (wa pili kulia) na Group Brand Assets Manager Airtel Africa Andrew Masitsa ambao ndio washamini wakuu wa shindano la Big Brother The Chase kwa mwaka huu wakiwa kwenye pozi na Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Kenya Churchill (kushoto) na Msanii wa Hip Hop kutoka Kenya Stella Mwangi a.k.a STL (wa pili kushoto).
SAMSUNG DIGITAL CAMERA
Operation Manager wa Mo Blog Zainul Mzige akipozi na Stella Mwangi STL.
IMG_0030
Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Kenya Churchill ambaye pia ni miongoni mwa waburudishaji kwenye uzinduzi huo akiteta jambo na M-Net Africa Managing Director Biola Alabi wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Sandton Sun jijini Johannesburg.
IMG_0035
Managing Director Channel O Afrika Leslie Kasumba katika picha ya pamoja na msanii maarufu wa Hip Hop nchini Kenya Stella Mwangi a.k.a STL.
IMG_9986
Big Brother Crew wakati wa mkutano na waandishi wa habari mapema leo asubuhi.
IMG_0041
Final Touches......M-Net Africa Managing Director Biola Alabi akipitia ratiba ya uzinduzi wa Big Brother The Chase. Kulia ni Senior PR Manager wa Multichoice Africa Sandhya Singh.

MARTIN FUNDI NDIYE MSHINDI WA THE MIC KING 2013

$
0
0
...Akiliwasha gari lake.Meneja wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akimkabidhi ufunguo wa gari mshindi wa The Vodacom Mic King 2013, Martin Fundi. Katikati ni Meneja Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho. Martin Fundi akifungia mlango wa gari lake.

...Akiingia.
Mashabiki wakiwa wamelizunguka gari la Martin Fundi.Martin Fundi kutoka Kimara usiku wa kuamkia leo ameibuka kidedea katika shindano la The Vodacom Mic King 2013 na kujinyakulia gari jipya aina ya Toyota Funcargo (new model). Shindano hilo lililokuwa likidhaminiwa na Kampuni ya simu ya Vodacom lilidumu kwa takribani miezi sita na usiku wa kuamkia leo ndiyo limefika tamati.

FEDHA KESSY NA NANDO WAIWAKILISHA TANZANIA KWENYE SHINDANO LA BIG BROTHER-THE CHASE 2013

$
0
0
IMG_0226
Mwakilishi wa Tanzania Fedha Kessy akiwasalimu mashabiki wake kwa kuwapungia bendera ya Tanzania. Kulia ni mtangazaji wa Shindano la Big Brother The Chase 2013 Ik.
IMG_0156
Kundi la Mafikizolo la nchini Afrika Kusini likitoa burudani wakati wa uzinduzi wa show ya Big Brother-The Chase iliyorushwa Live na Channel za DStv 197 na 198 jijini Johannesburg usiku huu. Shindano la Big Brother-The Chase limedhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.

IMG_0140
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo waandishi wa habari kutoka nchin mbalimbali za Afrika kushuhudia Live uzinduzi huo.
IMG_0209
Mwakilishi kutoka Tanzania Nando akihojiwa na Mtangazaji wa kipindi hicho Ik wakati wa uzinduzi wa show hiyo.Kushoto patna wa Nando Mshiriki kutoka Namibia Cleo.
IMG_0231
Mtangazaji IK akifanya mahojiano na Patna wa Mwakilishi wa Tanzania Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa Shindano la Big Brother The Chase lililozinduliwa rasmi leo jijini Johannesburg Afrika Kusini ambapo washiriki watakaa ndani ya jumba hilo kwa siku 90 na mshindi kujinyakulia kitita cha Usd 300,000. Kulia ni Fedha Kessy mshiriki kutoka Tanzania.
IMG_0235
Mtangazaji IK akimtambulisha rasmi mshiriki kutoka Tanzania Fedha Kessy kwa Patna wake Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa shindano hilo leo jijini Johannesburg.
IMG_0108
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliopata mwaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa shindano hilo Live kutoka Kampuni ya Multichoice Africa. Wa pili kulia ni Operations Manager wa Mo Blog Zainul Mzige aliyeiwakilisha Tanzania.
IMG_0081
Kutoka kushoto ni Mwandishi wa habari kutoka Afrika Kusini Munya, Buhle na Thato kutoka Ofisi za Multichoice Afrika Kusini wakishow love back stage wakati wa uzinduzi wa shindano la Big Brother The Chase.
IMG_0083
Wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali mbele ya camera yetu.
IMG_0098
Mini Bar iliyondaliwa maalum kwa wageni waalikwa.
IMG_0220
Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka nchini Kenya Stella Mwangi a.k.a STL akitoa burudani huku akipewa sapoti na Manager wake.
IMG_0218
More pictures to come. (Picha na Dewji Blog)

KINANA NAPE WATUA IRINGA, KUANZA ZIARA NJOMBE LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakisalimia baadhi ya viongozi, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Iringa asubuhi hii, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku saba, mkoani Njombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  akiwa na viongozi wa mkoa wa Iringa. Nyuma ni Nape Nape naye akiwa na wenyeji.

 Kinana akisaini kitabu cha wageni Uwanja wa Ndege wa Iringa baada ya kuwasili uwanjani hapo asubuhi hii. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Joyce Msavatavangu
Nape akisaini kitabu cha wageni.

KIMTWARA MTWARA NA MARCO TIBASIMA HII LEO

BARCLAYS YATANGAZA WADHAMINI WA MATEMBEZI YA HISANI YA 'STEP AHEAD'

$
0
0
Meneja wa Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays, Tunu Kavishe (kushoto) akizungumza na waandishi wakati wa kutangaza wadhamini wa Matembezi ya Hisani ya ‘Step Ahead’ ambayo yamelenga kukusanya fedha kwaajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto na yanataraji kufanyika Juni 8 mwaka huu jijini Dar es salaam. Pamoja na ni Meneja masoko wa benki hiyo, Sara Munema. Wadhamini hao ni Montage Ltd, ITV/Radio One na Capital TV, Clouds Media Group, Cocacola, Golden Tulip, Mwananchi Communications, Serena Hotels na Ultimate Security.

*****  ******

Every year, Barclays Bank Tanzania organises a fund-raising walk christened ‘Step-Ahead’. Barclays Tanzania held its first Step-Ahead event in the year 2008 through which funds were raised and donated towards cancer treatment for children at the Ocean Road Cancer Institute (ORCI). Introduced globally in 2004, Step-Aheadis a signature Barclays initiative which aims to create awareness and resources in support of community needs.  

Speaking at the press conference today, Ms. Tunu Kavishe, the Barclays Tanzania Communications and Community Investment Managersaid “Barclays Bank takes its Citizenship role seriously and recognizes it as one of our key business deliverables.

Taking on maternal and infant health as our flagship cause in Tanzania springs from our need to play a role in addressing the march towards achieving the 2015 MDG goals on maternal and infant health. 

We are pleased that our partners CCBRT and AMREF have joined us once again in this initiative. This exciting event will be held on the 8th June, 2013 at the Golden Tulip Hotel and will include a 5km walk in which all members of the public are invited to participate. Step Ahead Walk 2013 welcomes the support of all partners and the community at large.

Today we are pleased to announce our sponsors for this year’s Event and these are Montage Ltd, ITV/Radio One and Capital TV, Clouds Media Group, Cocacola, Golden Tulip, Mwananchi Communications, Serena Hotels and Ultimate Security she added…

The funds raised will go towards supporting theCapacity building for midwives, Fistula treatment and Reconstructive surgery for children born with correctible birth defects.

Tickets cost Tshs 5,000/- each and will be available at any Barclays Bank branch, Montage Limited offices – Ada Estate, Golden Tulip, Serena Hotels and Slipways 

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NA KUMPA POLE KUFUATIA VIFO VYA ASKARI

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkuu wa jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kwa mazungumzo leo Mei 27, 2013.
****** ********
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amekutana na Mkuu wa jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Said Mwema ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Mei 27, 2013. 

Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais ametumia nafasi hiyo kumpa pole Mkuu wa Polisi kufuatia ajali ya gari la iliyosababisha vifo vya askari wanne wa Jeshi hilo, waliokuwa njiani kutoka Nachingwea kuelekea Mkoani Mtwara kwa kazi maalum ya kudhibiti vurugu zilizojitokeza Mkoani humo juma lililopita.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema, askari hao watazidi kukumbukwa kwa kuwa walikuwa mstari wa mbele kuhakikisha majukumu yao kwa Taifa hili yanafanikiwa. Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema pia kuwa, serikali inathamini sana mchango wa Jeshi la Polisi sambamba na majeshi mengine kutokana na kufanya kazi kwa kujitolea na kwa kutambua kuwa ulinzi na usalama wa Taifa ni jambo muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Mkuu wa Polisi kuwa, kazi inayofanywa na jeshi lake ni kubwa na kwamba Watanzania wanaithamini sana. Pia aliongeza kuwa katika nchi zote wananchi wanaojitolea kufanya kazi katika vyombo vya usalama, ni miongoni mwa wazalendo wakubwa wanaopaswa kuenziwa kwa kuwa wamekubali kuweka maisha yao kwa ajili ya nchi na watu wake.

Katika mkutano huo, Makamu wa Rais alitumia nafasi hiyo kupata taarifa kuhusu hali ya usalama mkoani Mtwara na pia kubadilishana mawazo kuhusu kuhakikisha maeneo ya nchi yetu kubakia salama wakati wote. 

Na Boniphace Makene, Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais.

BBA: First Kiss has Been Recorded!

$
0
0
Barely a day into Big Brother The Chase, the first kiss of the Season has been recorded in the Ruby House.
 
A casual game of spin the bottle in the garden resulted in Ghana’s Selly reaching over to Angola’s Biguesas for a passionate kiss much to the amusement and applause of her fellow Housemates. This was in between the Housemates’ first Nominations session in the game. 

South Africa’s Koketso could not match up to Selly’s antics when it was her turn to kiss Zambia’sSulu. Koketso simply hugged the dreadlocked Zambian and gave him a perk on the cheek.

However, it seemed to be Sulu ‘s lucky day as the green bottle pointed to Selly to give him a warm smooch, almost to make up for Koketso’s shortcomings.

After Koketso’s ‘cheating’, one Housemate was heard suggesting that; “from now on it’s either we French kiss or we stop playing the game.” From then on, it was kissing galore – on the lips too.


We know the House is red but it seems as though blood is already racing in the Ruby House. What a way to get to know each other though.

Our eyes are wide open as we wait in anticipation of what these kisses will turn into. It’s Big Brother The Chase and clearly, The Chase is on.

KINANA: CCM IMEDHAMIRIA KUZOA KATA ZOTE 25

$
0
0
NA BASHIR NKOROMO, IRINGA
CHAMA Cha Mapindizi (CCM) kimesema kimedhamiria kushinda kwenye kata zote 25 katika uchaguzi mdogo wa madiwani ambao kampeni zake zinaendelea katika kata mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa leo  na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati akizungumza na wananchi katika kata ya Mbalamaziwa, wilayani Mufindi mkoani Iringa, ambako zinaendelea kampeni za udiwani katika kata hiyo. Katika Kata hiyo bendera ya CCM inapeperushwa na  Zuberi Nyamoleo.

"Kutokana na jeshi kubwa na wafuasi tulio nao na imani inayoendelea kuonyeshwa na wananchi kuiunga mkono CCM, tuna imani dhamira hii itafanikiwa bila shaka yoyote", alisema Kinana na kuongeza;"Pale Mbinga katika Kata ya Lokindo CCM imeshapita bila kupigwa, wapinzani wenyewe wametuachia kwa sababu wameridhika kuwa tunafaa kiuwaongoza, na pele Iramba Vijijini, Chadema walijaribu kuchacharika lakini wameambulia matupu vijiji vinane vyote vimeenda CCM".

Kinana aliwapongeza wagombea wengine waliokuwa katika mhakato na  Nyamoleo kwa kuamua kuuga mkono mgombea wa CCM katika 'vita' hiyo ya kuwania udiwani katika kata ya Mbalamaziwa.

"Ninyi ni watu wa kuheshimika sana ndani ya CCM, mmefanya uamuzi wa busara kuamua kumsaidia mgombea wa CCM aliyejipita kwenye kura za maoni. Huu ndiyo ustaarabu na moyo wa dhati unaotakiwa kwa kila mwana-CCM", alisema Kinana.

Kinana alisema, wanachama walio bora ndani ya CCM ni wale wasio na ubinafsi kwa kung'ang'ania kila wanachotaka wapate na wanapokosa inakowa nongwa.

"Mwanachama lazima uelewe kwamba unapogombea nafasi yoyote inayowaniwa na wengi huwa kuna kushinda au kushindwa, sasa inapotokea umeshindwa ni lazima uendelee kuwa mwaminifu kwa chama ili kuhakikisha kinashinda", alisema.

Kinana alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kutwaa kata zote, lazima wagombea watakaposhinda wawe watumishi wenye kujinyenyekeza kwa wananchi siyo kujinyayua mabega kana kwamba wao ndiyo bora kuliko wanaowaongoza.

"Tafadhalini sana, Chama hiki ni cha wananchi, diwani atakayeshinda ahakikishe  ushindi aliopata haugeuzi kuwa utukufu kwake kabla ya utumishi, huyo tutamshughulikia mara moja", alisema Kinana.

Kinana alipita katika kata hiyo akiwa njiani kwenda wilayani Njombe ambako anaanza ziara ya siku saba akifuatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Viewing all 10644 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>