Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10878 articles
Browse latest View live

MAMA WA PROF JAY AFARIKI KWA AJALI YA GARI MBEZI MWISHO

$
0
0



Mama Rosemary Majanjala ambaye ni mama mzazi wa Msani wa Muziki wa Kizaz kipya Joseph Haule maarufu PROF JAY aliyefarika jana usiku kwa ajali ya kugongwa na gari wakati akijaribu kuvuka barabara akitokea dukani majira ya saa 1 za usiku huko Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam.
 
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Prof Jay Mbezi Mwisho baada ya stendi mpya ya mabasi mbele kidogo utaona njia yakushoto inamagari mengi ndipo msiba ulipo.jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA DKT. JUDITH KAHAMA

$
0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya Msiba wa marehemu Dkt, Judith Kahama, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es salaam, leo Julai 11, 2013
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano w a Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji baadhi ya ndugu wa marehemu Dkt. Judith Kahama, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, leo Julai 11, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt. Judith Kahama, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam leo Julai 11, 2013. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,sambamba na viongozi wengine wakijadiliana, wakati walipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam leo Julai 11, 2013.

AIRTEL INAWATAKIA KHERI NA BARAKA KATIKA MWEZI HUU MTUKUFU.

African Lyon yapata hasara ya milioni 180.3

$
0
0
Meneja wa Fedha wa Timu ya Afrikan Lyon, Rahim Kangezi akifafanua jambo kuhusiana na mapato na matumizi ya klabu hiyo, kushoto ni Ibrahim Salim ambaye ni meneja wa fedha wa timu hiyo.
 
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya soka ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam imetangaza hasara ya sh. milioni 180.3 kutokana na ushiriki wake katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Lyon ni miongoni mwa timu tatu zilizoshuka daraja kutoka katuika ligi hiyo kubwa ya soka nchini, nyingine ni Toto African na Polisi Moro.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Meneja wa Fedha wa Lyon, Ibrahim Salim, alisema timu yao imetumia zaidi ya sh. 388,614,500 kwa ajili ya maandalizi hadi michezo yake.

Salim alisema katika makusanya na matumizi yao, walilazimika kutumia kiasi cha sh. milioni 268.09 katika mzunguko wa kwanza, kabla ya kutumia sh. 123.6.

"Katika matumizi yote haya, fedha ambayo tumeiingiza kama klabu kupitia viingilio na vyanzo vingine ni sh. milioni 207.6, na hapo ndipo unapopata tofauti ya sh. milioni 180.3, ambayo ni hasara," alisema Salim.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Lyon, Rahim Kangezi, alisema soka ya Tanzania inaendeshwa kwa hasara huku wenye dhamana ya kusaidia wakiwa hawatendi haki kwa baadhi ya vipengele.

Kangezi alisema timu yake imeingia katika hasara ya sh. milioni 180.3 kutokana na uendeshaji, lakini bado wameshuka daraja, huku akisisitiza kuwa hakuna anayeshutumiwa kwa kushuka kwa timu hiyo.

"Unaweza kuona changamoto ambayo tunakumbana nayo katika uendeshaji wa taasisi kamam a hizi, tunapopiga kelele kwa wadhamini kutuwahishia fedha tunamaanisha.

"Angalieni mfano mdogo kwa fedha za wadhamini (Vodacom), ambazo awamu ya mwisho zimetufikia Mei mwaka huu, tukiwa tumebakiza mechi moja ya Ligi Kuu, sasa zingetusaidia katika nini? Alihoji mmiliki huyo.

Akizungumzia kuhusu uendeshwaji wa Ligi Kuu na changamoto walizokutana nazo, Kangezi alisema bado hakujakuwa na usimamizi mzuri katika kuhakikisha kuwa ligi hiyo inakuwa bora.

Katika hatua nyingine, Kangezi alisema timu yake inajivunia mafanikio waliyochangia kusogeza maendeleo ya soka nchini kutokana na kutoa nafasi kwa Mrisho Ngassa kwenda kujaribu soka ya kulipwa na kucheza katika kikosi cha Seattke Soundowns dhidi ya Manchester United.

"Tulifanikiwa pia kuileta timu kubwa ya Ligi Kuu ya Brazil (Atletico Parenese) kwa ziara ya kimichezo nchini, tulitoa wachezaji watano kwa ajili ya kujaribu soka ya kulipwa sambamba na kufanya semina mbili juu ya uongozi wa michezo," aliongeza.

AIRTEL YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA MIKOA MINNE

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa  habari (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya makabidhiano  ya vyakula  vya kufuturisha watoto yatima atika vitu vilivyopo mikoa ya Dar es  salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  iliyofanyika  katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa  na meneja wa huduma za Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi.
Meneja  Uhusiano wa Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi  akimkabidhi  mwakilishi wa Bakwata Ustadh Hassan Malangali vyakula vya kufuturisha  katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  vilivyotolewa kwa vituo vitatu  vya watoto yatima Dar es Salaam (hawapo pichani)  vituo  vitakavyofaidika zaidi ni vya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Arusha  hafla ya makabidhiano iliyofanyika  katika ofisi za Airtel  Morocco  jijini Dar Es Salam .
 
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel, Hawa Bayumi  akimkabidhi tende Saida Makope ambaye ni mwakilishi wa vituo vitatu vya watoto yatima Dar es Salaam  katika  hafla ya makabidhiano  ya vyakula vya kufuturisha katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani  vilivyotolewa katika ofisi za Airtel, Dar es Salaam  jana. Anayeshuhudia ni mwakilishi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Ustaadh Hassan Malangali.
Na Mwandishi wetu.
KAMPUNI za simu za mkononi za Airtel Tanzania kupitia Kitengo chake cha huduma kwa Jamii wametoa msaada kwa vituo vitatu jijini Dar Es Salaam vya watoto yatima katika mwezi mtukufu wa Ramadhani vikifuatiwa na vituo vingine katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya ili kusaidia watoto wanaolelewa kwenye vituo hivyo.
Msaada huo umetolewa kwa lengo la kuwalenga watoto kutoka mikoa minne ambayo ni Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya kwa watoto hawa wanaohitaji upendo  hususani katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani. Baadhi ya vitu vilivyotolewa ni Mchele,Sukari, maharagwe,unga, mafuta ya kupikia,maziwa, juice, majani ya chai na sabuni vyenye dhamani ya shilingi milioni tano na nusu.

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyoandaliwa katika makao makuu ya  Airtel jijini Dar Es Salaam, Meneja uhusiano wa huduma kwa Jamii bi Hawa Bayumi alisema "kwa kutambua umuhimu wa Jamii tunayofanya nayo biashara kampuni ya Airtel tumeamua turudishe kiasi cha faida tunayopata kwa wananchi ili iwasaidie.

Akifafanua alisema kwa muda wa miaka 11 iliyopita tumeweza kusaidia Jamii mbalimbali ya watanzania ndani ya mfungo wa Ramadhani na bila kuacha nyanja za elimu, michezo kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kukosa huduma mbalimbali za kijamii.

Kwa mwaka huu kupitia Kitengo chake cha huduma kwa Jamii tutarudisha tulichokipata na tutaweza kufikia watoto zaidi ya 300 wa mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha , Mwanza na Mbeya na mpaka sasa  kwa mwaka huu Airtel imegharamia zaidi ya shilingi millini 150 katika kukuza kiwango cha elimu kwa watoto wetu hapa Tanzania," alisema Bayumi.

Bayumi aliongeza kwa kusema kwamba Airtel inapenda kuwatakia kheri na Baraka katika mwezi huu mtukufu na tangu kuanza kwa Mwezi mtukufu wa Ramadhan, wateja wa Airtel wanaweza kufurahia huduma maalumu ya Ramadhani kwa kutuma neno RAMADHANI kwenda namba 15322 kwa shilingi 153 tu kwa siku. Katika huduma hii mteja atapokea dua, nukuu za
qurani, mawaidha na taraweh salat moja kwa moja kwenye simu yake, kila siku.

Naye katibu mkuu wa Bakwata Sheikh Suleiman Lolila  ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema mbali ya hafla hiyo makabidhiano ya chakula imetoa fursa kwa waislam kutoka maeneo mbalimbali kukutana pamoja na kukumbushana juu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Aidha Lolila licha ya kuishukuru Airtel Tanzania kwa misaada inayotoa kwa Jamii alisema jambo hilo linahitaji pongezi na kutaka liungwe mkono na kuigwa na kampuni zingine hapa nchini.
 

WANAFUNZI SOMENI MASUALA YA AFYA, UALIMU MIFUGO NA KILIMO AJIRA ZIPO NJE NJE

$
0
0
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini,Ofisi ya Rais Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham (kushoto) akizungumza na vyombo vya habari nchini juu ya Uendeshaji wa Mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma, kwenye mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO)Jijini Dar es Salaam,kulia ni Katibu Msaidizi Idara ya Ajira kutoka Ofisi hiyo Bw. Malimi Muya.
**********
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29 (1).

Jukumu la msingi la Sekretarieti ya Ajira ni kuendesha mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma.  Hapa ina maana  kuwa jukumu la kuajiri, kuthibitisha watumishi kazini pamoja na masuala ya nidhamu ya Watumishi yanabaki kwa Watendaji Wakuu wa Wizara na Taasisi katika Utumishi wa Umma  mitarafu ya Kifungu cha 6(1) (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma no 8 ya mwaka 2002.

 Ambapo katika kuendesha mchakato huo, Sekretarieti ya Ajira inapaswa kuzingatia Sheria, Kanuni, na Taratibu zilizopo ili kuhakikisha Utumishi wa Umma unapata Watumishi weledi na wenye maadili mema. Hadi sasa jumla ya waombaji 4891 tumeshaendesha mchakato wao wa ajira na kuwapangia vituo vya kazi.

Hata hivyo, Sekretarieti ya Ajira kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ilipeleka Mswada Bungeni unaopendekeza kukasimu madaraka ya kuendesha mchakato wa Ajira ili baadhi ya Waajiri wakasimiwe madaraka hayo ili kurahisisha utendaji kazi katika kushughulikia  mchakato wa ajira kwa baadhi ya kada.

Huku Sekretarieti ya Ajira ikiendelea kuhakikisha kuwa jukumu hilo linaendelea kutekelezwa kwa ufanisi. Tunapoongelea suala la ufanisi hapa Kitengo cha Udhibiti na Ubora kinasimamia suala zima la uhakiki wa taarifa za mhusika, uhakiki wav yeti na uadilifu wake kwa ujumla.

 Ambapo hadi sasa tumeshakamata  jumla ya vyeti vya kughushi 677 ambavyo wahusika wanadai wamevipata kutoka RITA, VETA na NECTA.

Nafasi  wazi za kazi zitakazokuwa zikitangazwa na mchakato wake kuweza kukasimiwa ni pamoja na Kada ya Wasaidizi wa ofisi, Wahudumu wa afya, Madereva, Maafisa Watendaji wa Kata, Mtaa, Kijiji, Wapishi, Walinzi, Madobi, Wasaidizi watunza kumbukumbu pamoja na Makatibu Muhtasi (walio chini ya cheo cha mwandishi mwendesha ofisi)  au Kada zingine ambazo Katibu wa Sekretarieti ataona inafaa kukasimu.

Aidha, nitoe ushauri kwa wanafunzi walioko shuleni na wanaotarajia kuingia vyuoni kuchukua masomo ama kozi za fani ya Afya, Elimu, Mifugo na Kilimo maana ni maeneo ambayo bado yana fursa nyingi za ajira Serikalini na wahitimu wake pindi wamalizapo wanapangiwa vituo vya kazi moja kwa moja bila ya kupitia mchakato wetu wa ajira kutokana na uhaba wa Wataalam wa fani hizo katika soko la ajira hivi sasa.

Sekretarieti ya Ajira katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa  kwa haraka zaidi zinazohusu  mchakato wa ajira katika Utumishi  wa Umma na ili kuweza kuendana na mabadiliko ya sayansi na  teknolojia ya habari na mawasiliano nchini na duniani kwa ujumla, iliamua kuanzisha tovuti yake (www.ajira.go.tz) ambayo imerahisisha  kwa kiasi kikubwa utoaji na upokeaji wa taarifa mbalimbali  hususani  za matangazo ya fursa za ajira taarifa nyingine zinazohusu masuala ya ajira Serikalini na matangazo mengine yanayohusu shughuli za Sekretarieti ya Ajira. Tangu kuzinduliwa mwezi Aprili, 2013 imeweza kutembelewa na  wadau zaidi ya 2,900,000.

Pamoja na tovuti Sekretarieti ya Ajira imeanzisha KANZIDATA (DATABASE)  za aina tatu (3) ambazo ni Kanzidata ya Wahitimu wa Vyuo, Kanzidata ya waliofaulu usaili na Kanzidata ya waliopangiwa vituo vya kazi.

Jambo lingine ambalo ningependa mkalifahamu ni kuwa, Sekretarieti ya Ajira iko katika hatua za awali za mchakato wa kuwawezesha waombaji wa fursa za ajira kuwasilisha maombi ya kazi kwa mfumo wa kielektroniki (e-application) kwa nafasi wazi zitakazokuwa zikitangazwa katika Utumishi wa Umma ili kurahisisha kupunguza mlolongo wa uendeshaji mchakato wa ajira ulivyo hivi sasa.

Mwisho nimalizie kwa kuwataka waombaji wa fursa za ajira kutokuchagua maeneo ya kufanyia kazi, hususani wale wanaopangiwa vituo vya kazi na Sekretarieti ya ajira na hawaendi kuripoti bila ya kutoa sababu za msingi maana Sekretarieti ya Ajira inaona hili ni kosa na inaandaa utaratibu wa kutowaruhusu kufanya usaili mwingine waombaji kama hao.                   

Imetolewa na Riziki V.  Abraham, Msemaji na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma  +255-687624975

MAZISHI YA MGANGA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM DKT JUDITH KAHAMA MARO KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR

$
0
0
Gari lililobeba mwili wa marehemu likiwasili katika makaburi ya Kinondoni kwa mazishi
Mume wa marehemu Profesa Maro akiwa katika gari hilo na watoto wake
Profesas Maro akiwasili makaburini
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii akitoa mkono wa pole kwa Profesa Maro
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa mfiwa
Mama Salma Kikwete akitoa mkono wa pole
Mama Salma Kikwete akimpa pole binti wa marehemu
Rais Kikwete akitoa pole kwa mtoto wa marehemu
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa pole kwa wafiwa
Pole kwa wafiwa
Pole kwa wafiwa
Sehemu ya waombolezaji
Rais Kikwete akiongea na Profesa Maro, mume wa marehemu
Waombolezaji wakiwa mazishini
Sehemu ya waombolezaji
Watoto na ndugu wa marehemu
Sala ya mazishi
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa na ndugu wa marehemu
Padri Paul Haule akiongoza mazishi
Profesa Maro akiweka udongo kaburini
Wazazi wa marehemu wakiweka udongo kaburini
Mama Anna Mkapa akiweka udongo kaburini
Rais Kikwete na Mama Salma wakiweka udongo kaburini
Fred Maro akiweka udongo kaburini
Babu na bibi wakiweka udongo kaburini
Ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu mazishini
Padri Paul Haule akiongoza mazishi
Profesa Maro akiweka shada la maua kaburini
Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua
Wazazi wa marehemu wakiweka shada la maua
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua kaburini
Mama Anna Mkapa akiweka shada la maua Kaburini
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Said Meck Sadick akitoa heshima baada ya kuweka shada la maua kaburini
Babu na bibi wakiweka shada la maua kaburini
Sehemu ya waombolezaji
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt Hussein Mwinyi akiweka shada
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akiweka saha la maua
Ndugu wa marehemu wakiweka shada la maua
Kaka na dada wa marehemu wakiweka shada
Kaka wa marehemu wakiweka shada la maua
Kaka wa mume wa marehemu na mkewe wakiweka shada la maua
Kaka wa marehemu na mkewe wakiweka shada
Kaka wa muwe wa marehemu na familia yake wakiweka shada
Kaka wa marehemu na mkewe wakiweka shada la maua
Kaka na mkwe wa marehemu wakiweka shada la maua
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiweka shada la maua
Ndugu wa marehemu wakiweka shada la maua
Mkuu wa hospitali ya Hindu Mandal Dkt Kaushik akiweka shada la maua
Madaktari wenzie marehemu wakiweka shada la maua kaburini
Dada wa marehemu akiweka shada la maua
Ndugu wa marehemu wakiweka shada la maua
madaktari ambao ni wana kwaya wakipeleka shada lao la maua kaburini
Msemaji wa familia akitoa shukrani zake baada ya zoezi la kuweka mashada ya maua kaburini. PICHA NA IKULU

BENDERA ATEMBELEA KIWANDA CHA KIBUKU CHA DARBREW, DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia), akizungumza alipotembelea hivi karibuni Kiwanda cha Kibuku cha Darbrew, kilichopo Ubungo Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Kirowi Suma. Kulia ni Akoli Mbilinyi ambaye ni Ofisa Rasilimali Watu wa kiwanda hicho.
 Joel Bendera (kulia) akitembelea kiwanda hicho. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho. Kirowi Suma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kibuku cha Darbrew Limited, Kirowi Suma (kushoto), akielezea mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera kuhusu utendaji wa kiwanda hicho. Bendera alitembelea hivi karibuni kiwanda hicho kilichopo Ubungo Dar es Salaam.
 Bendera akipata maelezo kuhusu uzalishaji bora wa kinywaji cha asili cha kibuku kiwandani hapo
 Bendera akiwa ndani ya kiwanda hicho kilichopo Ubungo karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi
 Bendera akiwa na baadhi ya viongozi wa kiwanda hicho alipotembelea kiwanda hicho
Bendera akiondoka baada ya kumaziza ziara kiwandani hapo

TAIFA STARS SASA MMEIVA KUPAMBANA- TENGA

$
0
0
 Rais wa TFF, Leodogar  Tenga akizungumza na Waandishi wa Habari
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzana (TFF), Leodegar Tenga amesema kikosi cha Taifa Stars sasa kina uwezo wa kushindana katika mashindano yoyote, kwani tayari kimeiva.
 
Akizungumza na wachezaji wa timu hiyo kambini kwao hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam, Rais Tenga aliwaambia kuwa kiwango walichoonesha kwenye mechi zilizopita za mchujo za Kombe la Dunia dhidi ya Morocco na Ivory Coast kimethibitisha hilo.
 
“Kiwango mlichoonyesha katika mechi hizo kila Mtanzania anayewafuatilia amekiona, hivyo hatuna shaka kuwa mtatuwakilisha vizuri kwenye mechi ya kesho dhidi ya Uganda,” amesema Rais Tenga na kuwataka kupigana kwa ajili ya Tanzania.
 
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kesho (Julai 13 mwaka huu) saa 9 kamili alasiri Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itacheza na Uganda (The Cranes) katika mechi ya kwanza ya raundi ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
 
Rais Tenga amesema TFF, mdhamini Kilimanjaro Premium Lager, Kamati ya Ushindi na Watanzania kwa ujumla wanawaunga mkono kwani wamekuwa wakiboresha kiwango chao kila wanavyozidi kucheza mechi tangu wake chini ya Kocha Kim Poulsen, Mei mwaka jana.
 
Wakati huo huo, Rais Tenga ameahidi kumpatia tiketi ya kwenda Uganda kwenye mechi ya marudiano mshabiki Wiseman Mwakyusa Luvanda anayetembea kwa miguu kutoka Mbeya kuja Dar es Salaam kushuhudia mechi ya kesho.
 
“Kama ni kweli anakuja kwa kutembea, huyu ameonyesha kiwango kikubwa cha uzalendo kwa timu ya Taifa, nitampatia tiketi ya kwenda Kampala kuishangilia Taifa Stars kwenye mechi ya marudiano,” amesema Rais Tenga.
 
…POULSEN, MICHO WATABIRI MECHI KALI
Makocha wa timu hizo Kim Poulsen wa Taifa Stars na Sredojvic Micho wa The Cranes wamesema mechi ya kesho itakuwa ngumu kwa vile kila mmoja amejiandaa kuhakikisha anafanya vizuri.
 
Wakizungumza na Waandishi wa Habari leo, makocha wote waliezea ubora wa wapinzani wao, lakini wakasisitiza kuwa wanaingia uwanjani kuhakikisha wanashinda ili kujiweka katika mazingira mazuri kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayochezwa Kampala wiki mbili zijazo.
 
Kim alisema Uganda ndiyo inayoongoza kwa ubora wa viwango vya FIFA katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati, hivyo ni changamoto kwao ingawa wachezaji wake tayari wamejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.
 
Naye Micho aliyefuatana na nahodha wake Hassan Wasswa alisema Taifa Stars imekuwa ikifanya vizuri tangu iwe chini ya Kim, na itakuwa na wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza kinachocheza mechi za mchujo za Kombe la Dunia wakati kwa upande wake atakuwa na wachezaji wawili tu.

MWANAFUNZI IFM AFA MAJI AKIOGELEA KIGAMBONI

$
0
0

Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza Uhandisi wa Kompyuta wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Wendy Habakuki Lwendo amefariki dunia katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kipepeo Kigamboni akiogelea na wenzake watatu jana jioni.

Akizungumza na Father Kidevu Blog, kaka wa Marehemu, Sammy Lwendo amesema mdogo wao alipatwa na maswahibu hayo akiwa na rafiki zake hao watatu wakiogelea baharini na wakati wanaogelea walikuwa katika eneo la kina kifupi cha maji yaliyokupwa na mara maji hayo yaka jaa na walipokuwa wakijaribu kutoka ndipo Wendy akazidiwa na maji.

Lwendo amesema kuwa wenzake walifanikiwa kumtoa majini lakini hali yake tayari ilikuwa mbaya na kwakuwa hawakuwa na ujuzi wa kutosha wa kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyezama majini walihangaika kwa zaidi ya dakika 40 kumsaidia ndipo wakapata msaada wa Polisi  kumkimbiza kituo cha afya Kibaoni huko Kigamboni lakini jitihada za kuokoa maisha yake ziligonga mwamba.

Aidha alisema kuwa mwili wa Marehemu ulihamishiwa katika Hospitali ya Wilaya Vijibweni na sasa ndugu wamefika na kuhamishia mwili huo Hospitali ya jeshi Lugalo.

Msiba kwa sasa upo Kinondoni nyuma ya Vijana, huku wakisubiriwa wazazi wa marehemu pamoja na ndugu wengine ili kujua taratibu kamili za maziko.

Wazazi wa Wendy, Mchungaji Habakuki Lwendo ni mwalimu wa Chuo cha Uchungaji Makumira mkoani Arusha.

Emirates hosts Iftar celebrations in Tanzania

$
0
0


Emirates Country Manager for Tanzania Abdulaziz Al Hai speaking to the Media during the Iftar dinner last evening in honour of its trade partners and the Media at the Hyatt Regency Dar es Salaam, the Kilimanjaro.

Emirates, one of the world’s fastest growing airlines, hosted Iftardinner last evening in honour of its trade partners and the media at the Marquee Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kiimanjaro.

Speaking at the event, Emirates Country Manager for Tanzania Abdulaziz Al Hai thanked the Government of Tanzania, trade partners and the media for their outstanding and continuous support to the airline.


“Ramadan is a period of sharing and we are pleased that each one of you found time to join us as we celebrate Iftar,” said Al Hai. “Our services in Tanzania have gone from strength to strength over the last 15 years and we owe our success to the very important partnerships we have with our trade partners, our loyal customers, as well as the media. This event is an amicable opportunity for us to show our appreciation for your vital role in the growth of Emirates in Tanzania. I am confident we can always count on your assistance going forward.”

He noted that the provision of excellent in-flight service and entertainment, ongoing network expansion and focus on developing innovative ways to improve customer comfort and convenience have been key in driving  success for Emirates in Tanzania.

“Our modern and convenient Dubai hub enables our customers to seamlessly connect to our ever-expanding global network,” Al Hai said. 

Emirates established operations in Tanzania in 1997. Currently, the airline flies daily from Julius Nyerere International Airport (JNIA) to Dubai, connecting passengers to 134 destinations in 77 countries across six continents.

EK 725 departs Dubai International Airport every day at 1015hrs and arrives at the Julius Nyerere International Airport (JNIA) in Dar es Salaam at 1455hrs. The return flight leaves JNIA at 1645hrs and lands in Dubai at 2320hrs every day.  

More information on offering conditions and bookings can be obtained fromwww.emirates.com/tz

Mfuko wa Starkey Hearing watoa huduma za kutibu masikio kwa wakazi wa Dar

$
0
0
Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing William Austin akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu ya huduma ya vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
Baadhi ya wakazi na watoto kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam wakiwa katika foleni ya kupatiwa matibabu ya huduma ya vifaa vya kuwasaidia kusikia kutoka Mfuko wa Starkey Hearing leo jijini Dar es salaam. Mfuko huo umeweka kambi katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambapo wanatarajia kutoa huduma hiyo bure kwa watu zaidi ya 2000 kwa kipindi cha nne.
Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing William Austin (kulia) akisaidiana na Mkewe Tani Austin(kushoto) kumuvalisha kifaa cha kumwezesha kusikia mtoto Lilian Vincent (leo) jijini Dar es salaam wakati Mfuko huo ulipoendesha huduma ya kutoa vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing William Austin (kulia) akisaidiana na Mkewe Tani Austin(kushoto) kumuvalisha kifaa cha kumwezesha kusikia mtoto Malechela Juma (katikati) leo jijini Dar es salaam wakati Mfuko huo ulipoendesha huduma ya kutoa vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing William Austin (wa tatu kutoka kulia) akiwa amemkumbatia Mkewe Tani Austin leo jijini Dar es salaanm katika picha ya pamoja na Teddy Mapunda (wa pili kutoka kulia) wakati wa zoezi la utoaji wa vifaa vya kuwasaidia kusikia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia wa jiji la Dar es salaam ambayo itatolewa kwa wakazi zaidi ya 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hoteli ya Serena wakishirikiana na wafanyakazi wa Mfuko wa Starkey Hearing kuwavisha vifaa cha kuwawezesha kusikia wakazi mbalimbali wa jijini Dar es salaam leo wakati Mfuko huo ulipoendesha huduma ya kutoa vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne.
 
Mtalaam wa kusafisha masikio Dkt. Leigh Kassneo akimsafisha sikio mtoto Rashid Said leo jijini Dar es salaam kabla ya kupata huduma ya kuchunguzwa na kupatiwa vifaa vya kumwezesha kusikia wakati Mfuko wa Starkey Hearing ulipoendesha zoezi la kusaidia vifaa watu wenye matatizo ya kusikia ambapo wanatarajia kutoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi ya 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.Picha na MAELEZO_ Dar es salaam.

MWANAFUNZI IFM KUZIKWA KESHO MAKABURI YA KINONDONI, NI WENDE LWENDO ALIYEKUFA MAJI

$
0
0
Na Father Kidevu Blog
MAZISHI ya Mwanafunzi na Rais wa Taasisi ya wanafunzi AIESEC- IFM, Wende Lwendo wa Mwaka wa Kwanza Uhandisi Kompyuta wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) aliyefariki juzi kwa kufa maji baharini yanafanyika kesho.

Wende , alifariki katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kipepeo Kigamboni jijini Dar es Salaam akiogelea na wenzake watatu majira ya jioni baada ya kumaliza mitihani yao ya kufunga mwaka wa masomo.

Kaka wa marehemu, Sammy Lwendo ameiambia Father Kidevu Blog leo kuwa marehemu anataraji kuzikwa kesho alasiri katika makaburi ya Kinondoni na mipango yote ya mazishi inaendelea vizuri.

Lwendo amesema kuwa mipango ya mazishi ilikuwa ikisubiri wazazi wa marehu ambao waliwasili juzi usiku wakitoakea mkoani Arusha na kutaarifu ndugu kuwa mazishi yatafanyika Dar es Salaam.


"Marehemu Wende, anataraji kuzikwa Makaburi ya Kinondoni kesho  lakini kabla ya mazishi kutakuwa na ibada itakayofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kinondoni, "alisema Lwendo.

Lwendo amesema ibada hiyo itaanza majira ya saa 8:00 mchana ambapo pia ndugu jamaa na marafiki watapata wasaa wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Wende.

Mmmoja wa wanafunzi wa IFM, Ester Boswell, ambaye walikuwa wakishi chumba kimoja na marehremu huko Kigamboni ameelezea msiba huo kuwa ni pigo chuoni kwao na kwake kwani Marehemu alikuwa ni rafiki yake mkubwa si chuoni lakini hata kabla hawaja jiunga na chuo hicho.

Boswell amesema kuwa Marehemu alikuwa ni Rais wa taaasisi ya Wanafunzi wa IFM ijulikanayo kama AIESEC na alikuwa mhim,ili mkubwa wa taasisi hiyo.

Aidha amesema kuwa hadi sasa binafsi haamini kifo cha Wendi, huku akielezea kuwa Marehemu alikuwa ni mtu mcheshi na kuogelea ilikuwa ni moja ya vitu vikubwa anavyo vipenda.

"Marehemu alikuwa mpenzi kumbwa sana wa kuogelea na siku zote alikuwa anapenda kwqenda kuogelea na hata anapokuwa mpweke hosteli huamua kwenda Beach kuogelea na siku ya tukio aliniaga kuwa anaenda kuogelea na wanafunzi wengine wakiwapo wazungu ambao wapo katika kubadilishana uzoefu wa kimasomo," alisema Boswell.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam ukisubiri maziko.

RAIS KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WA JWTZ CHUO CHA MAFUNZI YA KIJESHO MONDULI

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Ofisa Kadet Ngodoke kwa kuibuka mwanafunzi bora wa jumla mwaka huu katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Ofisa Kadet D.G.L. Wong- Pool toka Visiwa vya Ushelisheli kwa kuibuka mwanafunzi bora wa kigeni wa jumla mwaka huu katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
 
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maafisa katika Chuo cha Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
Meza kuu wakati wa sherehe za kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange baada ya sherehe za kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.PICHA NA IKULU

MAMA WA PROF JAY AAGWA NA KUZIKWA JIONI HII KINONDONI

$
0
0
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Joseph Haule akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehem,u Mamayake aliyefariki dunia hivi karibuni kwa ajali ya gari Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam. Mazishi yanafanyika jioni hii Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam. Zoezi hilo lililofanyika nyumbani kwa Mwanae, lilihudhuriwa pia na wasanii mbalimbali wakiwepo wanasiasa.
 
 
 
   

 
 
 
 
 

MECHI YA TAIFA STARS, UGANDA YAINGIZA MIL 113/-; TAIFA STARS YAINGIA KAMBINI MWANZA

$
0
0
 Mshambuliaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars),John Boko (14) akiwa na mpira mbele ya Beki wa timu ya Uganda ( The Cranes) katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Kombe la mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN),uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imekubali kipigo cha Bao 1-0 kutoka kwa Uganda.
********* 
Mechi ya kwanza mchujo ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) iliyochezwa jana (Julai 13 mwaka huu) imeingiza sh. 113,268,000 kutokana na watazamaji 17,121.

Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 17,278,169.49 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.

Asilimia 15 ya uwanja sh. 13,227,108.98, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 17,636,145.30 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 4,409,036.33.


Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 52,908,435.91 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,645,421.80 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.

TAIFA STARS KAMBINI TENA JULAI 14
Timu ya Taifa (Taifa Stars) imeondoka leo asubuhi (Julai 14 mwaka huu) kwenda Mwanza ambapo itapiga kambi ya siku kumi kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Uganda (The Cranes) kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeondoka kwa ndege ya PrecisionAir na itafikia hoteli ya La Kairo wakati mazoezi yatafanyika Uwanja wa CCM Kirumba kulingana na programu ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.

Wachezaji walioko katika kikosi hicho ni Juma Kaseja, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vincent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd na Haruni Chanongo.

Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Julai 26 na 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nelson Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala. Tarehe rasmi itapangwa na Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu vya Uganda (FUFA) siku kumi kabla ya mechi.

TENGA AWASHUKURU WAJUMBE WA MKUTANO MKUU TFF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa michango yao, na utulivu waliouonesha katika kupitisha marekebisho ya Katiba ya TFF ya 2013.

Amesema marekebisho hayo yatawasilishwa kesho (Julai 15 mwaka huu) kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo kwa ajili ya kupitishwa ili mchakato wa uchaguzi uweze kuanza mara moja.

“Tutamuomba Msajili atusaidie kusajili haraka Katiba yetu ya 2013 ili tuingie katika mchakato wa uchaguzi. Kama tulivyotangaza awali tumepanga kufanya uchaguzi Septemba 29 mwaka huu, na tusingependa tarehe hiyo ipite,” amesema Rais Tenga wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji.

Katika kikao chake, Kamati ya Utendaji  imepitisha Kanuni za Maadili, Kanuni za Nidhamu, na marekebisho kwenye Kanuni za Uchaguzi yanayotokana na kuundwa kwa Kamati ya Maadili.

MAMIA WAMZIKA WENDE LWENDO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam leo wameungana na Familia ya Mchungaji, Habakuki Lwendo na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika mazishi ya Binti yao Wende Lwendo aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Uhandisi Kompyuta katika mazishi yaliyofanyika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Wende alifariki Ijumaa ya Julai 12, 2013 wakati akijumuika na rafiki zake kuogelea Bahari ya Hindi eneo la Ufukwe wa Kipepeo Kigamboni kilometa chache kutoka eneo alilokuwa akishi. 

Mazishi hayo mbali na wanafamilia na wanafunzi wa IFM kuhudhuria pia yalihudhuriwa na Askofu Mkuu wa KKKT Tanzania, Askofu, Dk Alex Malasusa, Makamu Mkuu wa Chuo cha Tumaini Makumira, Prof. Parsalaw pamoja na wachungaji mbalimbali na Wafanyakazi wa Chuo cha Makumira anakofanyia kazi Mchungaji, Habakuki Lwendo ambaye ni baba wa Marehemu Wende.



 Wazazi wa Marehemu, Mch. Habakuki Lwendo na mkewe wakiwa ni wenye majonzi.
















 Makamu Mkuu wa Chuo cha Tumaini Makumira, Prof. Parsalaw akiongea nenoa.
 Askofu Mkuu wa KKKT. Ask.Dr. Alex Malasusa akitoa salamu za Kanisa.








 Ni vilio tu kwa waombolezaji


 Rachel Fute na Vaileth Lwendo ambao ni Dada wa Marehemu wakipita
 Mama wa Marehemu akisaidiwa kutoa heshima kwa Binti yake.
 Baba wa Marehemu, Mchungaji Habakuki Lwendo akimuaga Binti yake.




 Vilio vilitawala kanisani
 Sanduku lililouhifadhi mwili wa Marehemu Wende likiwa tayari kushushwa kaburini.




RAIS KIKWETE KATIKA SHUGHULI YA UTOAJI VIFAA VYA KUONGEZA USIKIVU KWA WALEMAVU WA KUSIKIA JIJINI DAR LEO

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mmoja wa wanafunzi wa shule ya walemavu wa kusikia ya  Buguruni akiwa na  mwanzilishi na mkuu wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation Bw. Bill Austin alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mwanzilishi na mkuu wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation Bw. Bill Austin alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013

 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza wanafunzi wa shule ya walemavu wa kusikia ya  Buguruni baada ya kupatiwa vifaa na  mwanzilishi na mkuu wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation Bw. Bill Austin alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wanafunzi wa shule ya walemavu wa kusikia ya  Buguruni  alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Chief.  Shogholo Challi, katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa mstaafu,  alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013.

WANAJESHI WALIOUWAWA DAFUR KATIKA SHAMBULIO KUREJESHWA NCHINI

$
0
0
The African Union – United Nations Mission in Darfur (UNAMID), held a memorial ceremony, in Nyala, the capital of South Darfur, to honor the seven fallen peacekeepers who lost their lives in the 13 July attack in South Darfur. The bodies are scheduled to be repatriated to Tanzania, the home country of the fallen peacekeepers. In addition to the seven killed, 17 military and police personnel were wounded, among them two female Police Advisors, all of whom are recovering from their injuries in UNAMID’s hospital in Nyala, South Darfur. Photo by Saidi Msonda, UNAMID.






 On 14 July 2013, following a 13 July attack in which seven military peacekeepers of the African Union - United Nations Mission in Darfur (UNAMID) were killed and 17 military and Police personnel wounded, among them two female Police Advisers, Joint Special Representative Mohamed Ibn Chambas visited the wounded peacekeepers at UNAMID’s hospital in Nyala to provide encouragement and support. Photos by Albert González Farran, UNAMID.


JK AZUNDUA HUDUMA YA BENKI YA POSTA POPOTE LEO

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete akizindua huduma mpya ya Benki ya Posta iitwayo TPB POPOTE mapema leo mchana kwenye hotel ya Serena jijini Dar ,hafla hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wa mambo ya kibenki na wengineo, lengo kuu ya uzinduzi wa huduma hiyo ikiwa ni kuweka na kutoa  fedha kupitia Mawakala wa Benki ya Posta nchini Tanzania.Kushoto ni Waziri wa Fedha Dkt.William Mgimwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya na kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw.Moshingi wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa.

Rais Jakaya Kikwete akijaza fomu yake ya huduma hiyo mpya ya TPB POPOTE iliyozinduliwa na Benki ya Posta mapema leo mchana kwenye hotel ya Serena jijini Dar ,hafla hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wa mambo ya kibenki na wengineo, lengo kuu ya uzinduzi wa huduma hiyo ikiwa ni kuweka na kutoa  fedha kupitia Mawakala wa Benki ya Posta nchini Tanzania.Pichani kulia ni Waziri wa Fedha Dkt.William Mgimwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya na kushto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw.Moshingi wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa.
 Rais Kikwete akipewa maelezo mafupi namna ya kuitumia huduma hiyo ya TPB POPOTE kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya Posta.
  Rais Jakaya Kikwete akikabidhiwa kadi yake mpya ya huduma mpya TPB POPOTE  na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki  ya Posta Bw.Moshingi ,mara baada ya huduma hiyo kuzinduliwa rasmi mapema leo .
  Mgeni rasmi,Rais Kikwete akikabidhiwa zawadi kut0ka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya 

Picha pamoja.
Rais Jakaya Kikwete akiondoka mara baada ya kuzindua huduma mpya ya TPB POPOTE iliyozinduliwa na Benki ya Posta mapema leo mchana kwenye hotel ya Serena jijini Dar ,hafla hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wa mambo ya kibenki na wengineo, lengo kuu ya uzinduzi wa huduma hiyo ikiwa ni kuweka na kutoa  fedha kupitia Mawakala wa Benki ya Posta nchini Tanzania.
Viewing all 10878 articles
Browse latest View live