Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10583 articles
Browse latest View live

MDAU BEN MWANYIKA ALAMBA CHUO CHA NONDO USIU NAIROBI

$
0
0
1187141_10151862610225879_247673981_n Mdau Ben Mwanyika na wazazi wake baada ya kuchukua nondoz katika Chuo cha USIU Nairobi jana Jumamosi.

DK. STERGOMENA TAX WA TANZANIA AWA KATIBU MTENDAJI WA SADC

$
0
0
Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamemteua Dkt. Stergomena Tax wa Tanzania kuwa Katibu Mtendaji mpya wa Jumuia hiyo.

 Wakuu hao wamemteua Dkt. Tax jioni ya leo, Jumamosi, Agosti 17, 2013, mwishoni mwa kikao chao cha siku ya kwanza cha mkutano wa 33 wa wakuu hao unaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Bingu wa Mutharika kwenye mji mkuu wa Malawi wa Lilongwe.

Uteuzi huo unafuatia mapendekezo ya Baraza la Mawaziri wa SADC ambao walifanya tathmini ya wagombea wawili wa nafasi hiyo ambako Dkt. Tax alipatiwa wastani wa alama 79 wakati mgombea mwingine wa nafasi hiyo, MheshimiwaPeter G. Sinon, Waziri wa Serikali ya Shelisheli alipata alama 72.

Dkt. Tax ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki anachukua nafasi ya Dkt. Tomaz Augusto Salamao wa Mozambique ambaye amemaliza muda wake baada ya kutumikia nafasi hiyo kwa miaka minane.

RAIS BANDA WA MALAWI AMFAGILIA RAIS KIKWETE KWA KUDUMISHA AMANI NCHI ZA SADC

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Malawi, Mheshimiwa Joyce Banda (pichani kulia) amemwelezea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kama mwanademokrasia na kiongozi hodari anayepigania amani na  utawala bora.

Aidha, Rais Banda amewaelezea wanawake maarufu wa Tanzania, Mama Gertude Mongella na Dkt. Asha Rose Mingiro kama baadhi ya matunda ya juhudi za Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuleta usawa wa kijinsia katika eneo la Kusini mwa Afrika.

Rais Banda ametoa sifa hizo kwa Rais Kikwete na Watanzania hao wawili leo, Jumamosi, Agosti 17, 2013 wakati alipozungumza kwenye hotuba ya kupokea uongozi wa SADC kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa SADC kwenye Kituo cha Mikutano cha Bingu wa Mutharika mjini Lilongwe, mji mkuu wa Malawi. Mkutano huo wa 33 wa wakuu wa nchi SADC ni wa siku mbili.


Akizungumza baada ya kuwa amepokea Uenyekiti wa SADC kutoka kwa Rais Armando Emilio Guebuza wa Mozambique, Rais Banda amesema kuwa uongozi wa Rais Kikwete wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC umethibitisha na kuonyesha dhahiri kuwa kiongozi huyo wa Tanzania ni mwanademokrasia anayepigania amani na utawala bora wakati wote.

“Wakati wa uongozi wake wa SADC-Troika, Rais Kikwete amejihusisha kwa karibu sana na ujenzi na utetezi wa demokrasia, utafutaji amani na jitihada za kuongeza kiwango cha utawala bora katika eneo letu la Afrika,” Mama Banda amewaambia mamia ya wasikilizaji kwenye ukumbi huo wa Bingu wa Mutharika.

Kuhusu Mama Mongella na Dkt. Asha Rose Mingiro, Rais Banda amesema kuwa Watanzania hao wawili ni sehemu ya wanawake kadhaa katika eneo la SDAC ambao wamefanikiwa kupata nafasi kubwa za uongozi  kipindi ambako SADC imeelekeza nguvu zake katika kuleta usawa wa kijinsia.

Wakati wa uongozi wake wa SADC-Troika, Rais Kikwete amejihusisha sana na kutafuta suluhu na utatuzi wa migogoro ya kisiasa katika nchi za Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Madagascar.

Rais Kikwete amemaliza muda wake wa uongozi wa Troika leo na nafasi yake inachukuliwa na Rais Hifikepunye Phohamba wa Namibia.

Mbali na Marais Kikwete, Banda na Guebuza, viongozi wengine ambao wamehudhuria mkutano na shughuli za leo ni pamoja na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Rais Joseph Kabila Kabange wa DRC, Rais Khama Ian Khama wa Botswana, Dkt. Tom Thabane ambaye ni Waziri Mkuu wa Lesotho, Waziri Mkuu wa Mauritius na Makamu wa Rais wa Zambia, Mheshimiwa guy Scott.

Jumla ya nchi 14 zinawakilishwa katika Mkutano wa mwaka huu wa wakuu wa nchi wanachama wa SADC kati ya nchi 15 wanachama wa Jumuia hiyo. Madagascar haishiriki Mkutano huo kwa sababu ya kusimamishwa uanachama kwa sababu ya mgogoro wa kisiasa nchini humo.

MAAZIMIO 22 YA MAFUNZO YA KAMATI ZA BUNGE ZINAZOSIMAMIA FEDHA ZA UMMA NA BAJETI (PAC, LAAC NA BC)

$
0
0
1)      Kutokana na kutokuwepo na taarifa sahihi kuhusu deni la Taifa kuna umuhimu wa kukutanisha wadau wakuu wanaohusika hususani BOT, HAZINA, Kamati za Bunge na CAG ili kuweza kujua kwa usahihi zaidi ukubwa wa deni hilo.  Vile vile imeamuliwa kuwa Serikali ishauriwe kuunda chombo huru kitakachosimamia deni la taifa.

2)      Baada ya kuanzisha mfumo mpya wa bajeti ya Serikali mwaka huu kuna umuhimu wa kuandaa mkutano wa kutathimini mafanikio na changamoto za mfumo huu na kujadili mambo ya kuboresha zaidi mfumo mzuri wa bajeti ya Serikali.

3)      Kamati za Bunge zinazoshughulikia usimamizi wa fedha na rasilimali za taifa zishughulikie zaidi Maafisa Masuuli hatarishi (risk based) ili kuleta thamani ya fedha katika utendaji wao.  Kamati zishirikiane na CAG katika kuamua ni Afisa Masuuli yupi aitwe kukutana na Kamati.


4)      Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge na TAMISEMI waanzishe utaratibu wa kuratibu mikutano na mafunzo ya Wakurugenzi wa Halmashauri kwa pamoja kuliko kila Wizara kuwaita watendaji hao katika sehemu mbalimbali kwa muda tofauti na kuwafanya kutokuwepo ofisini kwa kipindi kirefu.

5)      Mfumo wa kutunza kumbukumbu za hesabu na nyaraka mbalimbali katika Serikali Kuu na Halmashauri uboreshwe ili zinapohitajika zipatikane kwa wakati muafaka bila kisingizio cha aina yoyote.

6)      Kuhusu ukaguzi wa ufanisi CAG asisubiri mpaka asikie malalamiko kutoka kwa wananchi au kwenye magazeti bali akague mara kwa mara sehemu zote zenye matatizo.

7)      Taarifa za mwaka za Kamati za Bunge ziwe na kipengele cha kiwango cha utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati yaliyotolewa awali. Kamati ziwezeshwe kifedha ili ziweze kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yao. Kanuni za Bunge zieleze utaratibu wa ufuatiliaji wa Maazimio ya Bunge na namna utekelezaji wake utavyowasilishwa Bungeni.  Vile vile Bunge litenge siku ya kujadili Serikali ilivyoshughulikia hoja za Kamati za Bunge.  Spika ashauriwe kuhusu umuhimu wa kuunda Kamati ya Bunge ya kufuatilia ahadi za Serikali.

8)      Mikataba katika ngazi ya Serikali za Mitaa iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

9)      Serikali inatakiwa kufanya jitihada za ziada kuzalisha wataalam wa fani ya manunuzi.  Kuna umuhimu wa PPRA kuongezewa nguvu za ziada za kiutendaji ikiwa ni pamoja na fedha na wafanyakazi.
10)  Bajeti ya Bunge iongezwe kupitia Mfuko wa Bunge na iwasilishwe Bungeni na Naibu Spika na sio Ofisi ya Waziri Mkuu.

11)  Serikali iandae mjadala wa kitaifa wa kutafuta ufumbuzi wa kukabiliana na vitendo vya rushwa na mmomonyoko wa maadili vinavyoongezeka kwa kasi hapa nchini. Vilevile viongozi wa umma na watendaji waongoze kwa mfano kwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika kutekeleza majukumu yao.

12)  Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma haiweki uwazi wa kutangaza umiliki wa mali za viongozi.  Hii inapelekea viongozi kutoweka wazi mali wanazomiliki na ni rahisi mtu kuzushiwa umiliki usio wa ukweli.  Ni vyema Sekretarieti wakafanya utafiti wa umiliki wa mali kwa viongozi wa Umma na kuweka taarifa hizo katika tovuti ya Sekretariati ili kuwawezesha wananchi kuweza kuona mali zinazomilikiwa na viongozi wao; na pale ambapo kiongozi hatakuwa ametoa taarifa ya umiliki huo basi taarifa hiyo itolewe kwa Tume.

13)  Kwa kuwa leseni za udereva za sasa zinaweza kuweka kumbukumbu za makosa ya usalama barabarani, basi TRA ikishirikiana na  Wizara ya Mambo ya Ndani zihakikishe ya kuwa Askari wa Usalama Barabarani wanatumia utaratibu huu wa kisasa wa kutoa  “notification” na kutoa risiti za malipo za elektroniki.

14)  Maduhuli ya Serikali sasa yakusanywe kwa kutumia risiti za elektroniki.  Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma yaanze kutumia risiti za eletroniki mara moja ili kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali yanayotokea hivi sasa katika kutumia risiti zinazoandikwa kwa mkono. Pia ofisi za serikali zifanye manunuzi yake kwa wafanyabiashara wanaotumia mashine za kielektroniki.

15)  TRA ihamasishe wananchi na wafanya biashara umuhimu wa matumizi ya risiti za elektroniki, wafanyabiashara waelimishwe umuhimu wa kutoa risiti hizo na wananchi waelimishwe umuhimu wa kudai risiti kila wanapofanya manunuzi. Elimu na uhamasishaji huo unaweza kufanywa kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo sanaa, timu za michezo, bendi za muziki, redio, TV, mbao za matangazo n.k.

16)  Serikali idhibiti makampuni ya uwakala wa kupakia na kupakua mizigo (clearing and forwarding) yaliyopo Bandarini ili kudhibiti mapato ya forodha.

17)  Sheria ya “Anti Money Laundering” ya 2006 irekebishwe ili iweke viwango vya fedha ambazo mtu anaweza kuingia au kutoka nazo nchini bila kuzitaja  (declare). Kuna umuhimu wa Waziri wa Fedha kutengeneza kanuni za kutekeleza Sheria hiyo.

18)  Benki Kuu iandae mfumo thabiti wa usimamizi wa Maduka ya Fedha (Foreign Bureau de Change), na kuhakikisha kutungwa kwa sheria inayozuia matumizi ya fedha za kigeni katika shughuli za kibiashara hapa nchini.

19)  The Proceeds of Crime Act, 1991” ifanyiwe marekebisho na kuweka kifungu kinachomwezesha AG/DPP kuwa na mamlaka ya kuomba mahakama kufungua kesi ya madai (Civil Forfeiture) kwa watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

20)  Imesisitizwa kwamba CAG akague misamaha ya kodi na kuweka taarifa hiyo kwenye taarifa za kila mwaka.

21)  Serikali iimarishe Taasisi zinazoshughulikia maadili utawala bora na uwajibikaji kama vile Sekretariati ya Maadili ya Viongozi, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Takukuru, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Kamati ya Maadili ya Bunge ili ziweze kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizoanzisha Taasisi hizo.

22)  PCCB na vyombo vingine vinavyohusiana na kushughulikia masuala ya jinai wawe waalikwa kwenye vikao vya Kamati za Bunge ili waweze kutoa ushauri kwenye kamati hizo.

LEAH SIMBA ASHUSHA 'JINSI ULIVYO' NDANI YA BONGO FLEVA

$
0
0
MWANA dada machachari  kutoka visiwani Zanzibar ambaye ameamua kuingia katika anga ya muziki wa Kizazi kipya, Leah Simba ameshusha mtaani wimbo wake wa kwanza na mpya unaoenda kwa jina la Jinsi ulivyo.

Wimbo huo ambao umepigwa na midundo ya staili mpya ambayo imetokea kushika nchini ya Kwaito umeimba na mwana dada huyo akishirikiana na chipukizi mwingine Joseph Mwingira a.k.a King Pozza kutoka kundi la Zeetown Sojaz kutoka Zanzibar.

Akiongea na Father Kidevu Blog, Msanii huyo Leah Simba amesema kuwa wimbo huo amerekodiwa katika studio ya Jupiter Records chindi ya mtayarishaji mziki Aloneym.

“Hii ni kazi yangu ya kwanza ambayo nimeifanya kwa muda mrefu na kuhakikisha ikitoka inashika vilivyo na kunitambulisha katika anga ya bongo fleva Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania, nikiwa nimesmhirikisha King Pozza ambao nao kupitia kundi lao ndio kwanza wameachia wimbo wao wa Chinjachinja,” alisema Leah.


Aidha Leah amesema kuwa anataraji kufanya kazi nyingi zaidi za mziki hivyo anaomba saport ya mashabiki maana mziki ni kazi nayeye ameamua kuifanya kazi hiyo kwanguvu na uwezo wake wote.

“Mziki ni Kazi name nimeamua kuifanya hivyo nataraji mengi sana kupitia mziki na mashabiki wa tasnia hii ya burudani nao wakae mkao wakula nimekuja kuwapa burudani ili name nipate kipato kupitia kazi hii,” alisema Leah.

Leah amesema niimani yake kuwa lengo lake la kufika levo za juu ambazo wamefikia wasanii wakubwa wa hasa wa kike katika mziki zitatimia endapo kazi yake hiyo itapata mashabiki wengi.

MAJAMBAZI YADAKWA TAZARA HII LEO

$
0
0
Majambazi wakamatwa hii leo mchana Tazara wakikimbia baada ya kupora fedha Milioni kadhaa.

BI SITI HAMAD KHAMIS ANAOMBA MSAADA ATIBIWE FIGO

$
0
0
BIBI Siti Hamad Khamis ambaye anasumbuliwa na ugojwa wa figo ambazo zimeshindwa kufanyakazi  anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema utakaomuwezesha kutibiwa.
 
Amelazimika kuomba msaada wa hali na mali ili kuokoa maisha yake kutokana na gharama kubwa za matibabu zinazoendelea kuikabili familia yake kwa muda mrefu sasa.
 
Kwa mfano kila wiki anatakiwa kwenda hospitali mara tatu ambapo kwa siku hulipa sh. 350,000.
Matibabu anayopatiwa ni kusafishwa damu ili kupunguza sumu mwilini, kupimwa na chanjo.
 
Anaomba kwa wale watakaoguswa na tatizo linalomsumbua, wamsaidie matibau ndani na nje ya nchi au wamchangie kupitia AC 2011601674 Benki ya NMB, tawi la Bank House.
 
Au wawasiliane na mumewe kwa simu 0774215217.

KATIBU MTENDAJI MPYA WA SADC DKT.STERGOMENA TAX APONGEZWA

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza katibu Mtendaji mpya wa SADC Dkt.Stergomena Tax wakati wa kikao cha 33 cha wakuu wa nchi za SADC kilichofanyika jijini Lllongwe Malawi leo kikao hicho kimeisha leo. Kushoto ni Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Rais wa  Dkt. Joyce Banda(wa pili kushoto) Jaji Mkuu wa Malawi Mhe. Anastazia Msosa,na Mwenyekiti wa Umoja wa Africa (AU) Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma wakimpongeza  katibu Mtendaji mpya wa SADC Dkt.Stergomena Tax baada ya kula kiapo wakati wa kikao cha 33 cha wakuu wa nchi za SADC kilichofanyika jijini Lllongwe Malawi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

IGP MWEMA AKABIDHI UENYEKITI WA SARPCCO NCHINI NAMIBIA.

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Said Mwema akimkabidhi kitara Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga kama ishara ya kumkabidhi uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) baada ya Tanzania kumaliza uongozi wake kwa kipindi cha mwaka mmoja.Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa mkutano maalumu wa wakuu hao uliofanyika nchini Namibia.
Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Said Mwema akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga baada ya kumkabidhi uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO). 
*********

Habari na picha na Frank Geofray,Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia
Inspekta Jenerali wa Polisi wa Tanzania IGP Said Mwema amekabidhi uenyekiti wa Umoja wa wakuu wa majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika SARPCCO baada ya kumaliza kipindi chake cha mwaka mmoja cha kuongoza umoja huo.
IGP Mwema amekabidhi uongozi huo kwa Inspekta Jenerali wa Polisi wa Nchi ya Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga wakati wa mkutano mkuu maalumu wa viongozi hao uliofanyika jana katika jiji la Windhoek na kuhudhuriwa na Wakuu wa Polisi kutoka nchi wanachama pamoja na viongozi mbalimbali kutoka INTERPOL na SADC.
Akizungumza katika mkutano huo IGP Mwema alisema katika kipindi cha uenyekiti wake walifanikiwa kufanya Operesheni kubwa iliyojulikana kama Operesheni Usalama ambayo ilijumuisha umoja wa SARPCCO na ule wa Afrika Mashariki EAPCCO,operesheni ambayo ililitea manufaa makubwa katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka.
Alisema Nchi wanachama wanapaswa kuendeleza ushirikiano wao ili kuhakikisha kuwa ukanda wa kusini mwa Afrika unakuwa salama kwa kukabiliana na uhalifu hasa kwa kupeana taarifa za uhalifu na wahalifu.
Aidha alisema katika kipindi hicho Tanzania iliweza kuandaa mikutano yote ya kamati tendaji za SARPCCO ambazo ziliweza kuibua maazimio mbalimbali ya kupambana na uhalifu ambayo yaliweza kupitishwa na kuwa mikakati endelevu katika kukabiliana na uhalifu.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga alisema atahakikisha umoja huo unakuwa imara na kupambana na uhalifu unaovuka mipaka kama vile wizi wa magari, wahamiaji haramu, usafirishaji wa fedha haramu na binadamu, wizi wa mitandao pamoja na madawa ya kulevya.
Naye Mgeni rasmi katika mkutano huo Waziri wa Usalama na ulinzi wa Namibia Immanuel Ngatjizeko alisema serikali ya Namibia itaendelea kushirikiana na umoja huo kwa kila hali ili kuhakikisha Nchi wanachama na Afrika kwa ujumla zinakuwa salama.
IGP Mwema alikabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO mwezi Septemba mwaka 2012 mjini Zanzibar kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Afrika kusini ambapo kutokana na uenyekiti huo mikutano yote ya umoja huo ilikuwa ikifanyikia nchini Tanzania.

CASTLE LAGER KULETA MAKOCHA KUTOKA KWA WAKALI WA KATALUNYA, FC BARCELONA!!

$
0
0
IMG_1698Balozi wa Hispania nchini, Luis Manuel Ceuesta Civis (kushoto), Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Robin Goetzsche wakigonganisha glasi kuashiria uzinduzi wa bia ya Castle Lager kwa klabu ya FC Barcelona ya Hispania katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika jijini Dar es salaam jana usiku.
IMG_1710Meneja wa bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo akimkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara zawadi kwenye uzinduzi uzinduzi wa bia ya Castle Lager kwa klabu ya FC Barcelona ya Hispania katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika jijini Dar es salaam jana usiku. Wengine kwenye picha ni Balozi wa Hispania nchini, Luis Manuel Ceuesta Civis (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Robin Goetzsche.

 **********
Na Ibrahim Kyaruzi-Executive Solutions
Bia ya Castle Lager imepanga kuandaa kliniki za soka ambazo zitaongozwa na makocha kutoka Klabu ya Barcelona inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga.

Hayo yalidhibitishwa Agosti 17 mwaka huu katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Castle Lager na Klabu ya Barcelona.

Goetzsche alisema ushirikiano huo utahusisha shughuli za soka ambazo zitashirikisha zaidi ya timu 120 nchini kote huku wakijitahidi mradi huo kufikia jamii katika mikoa yote.

“Kutakwepo na kliniki za soka ambazo zitaongozwa na makocha kutoka Klabu ya Barcelona na kuna uwezekano timu itakayoibuka bingwa katika mchezo wa soka itakayoandaliwa na bia ya Castle kusafiri kwenda Camp Nou nchini Hispania kucheza mechi ya kirafiki,” alisema.

Goetzsche alisema bia ya Castle Lager imeingia mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano na Klabu ya Barcelona Julai 26 mwaka huu ambapo bia hiyo bora Afrika ndiyo mdhamini mkuu wa vigogo hao wa Ulaya na duniani barani Afrika.

Alisema ushirikiano huo haulengi tu biashara na wateja wao mbali jamii yote ambayo bidhaa yao inawafikia lengo likiwa ni kukuza soka.

Mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara ambaye alisifu bia ya Castle Lager kwa kupiga hatua moja mbele kutokana na kushirikiana na Klabu ya FC Barcelona kuendeleza soka la humu nchini.

Dk Mukangara alisema ushirikiano huo umekuja wakati mwafaka ambao Tanzania imekuwa ikitilia mkazo kukuza na kuendeleza vipaji vya soka katika taasisi mbalimbali na akademi chache ambazo hazina miundombinu stahiki.

“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, napenda kuwashukuru Castle Lager kwa kutusaidia na ninaamini hii itasaidia kuendeleza soka la humu nchini,” alisema.

Dk Mukangara aliongeza kuwa ushirikiano kati ya Castle Lager na Klabu ya FC Barcelona iliyosheheni wachezaji nyota kama vile Lionel Messi, Neymar na Andres Iniesta itakuwa changamoto katika kubadilisha maisha ya wachezaji wa soka Tanzania.

Waziri huyo alihakikisha kufanya kazi kwa karibu na Castle Lager kuwawezesha jamii nchini kote kupitia mchezo wa soka.

“Napenda kutoa wito kwa wanasoka wote Watanzania na wataalamu wa soka kukumbatia fursa hii inayotolewa kwa ushirikiano wa Castle Lager na Klabu ya Barcelona kutimiza programu zilizoainishwa kwenye mkataba kwa manufaa ya soka letu,” alisema Dk Mukangara.

Miongoni mwa walikwa katika uzinduzi huo walikuwa Balozi wa Hispania nchini Tanzania, Luis Manuel Ceuesta Civis, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik, Meya wa Ilala Jerry Slaa na Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo.

TUSKER PROJECT FAME IMERUDI TENA!

$
0
0
2Meneja wa bia ya Tusker Lager Sialouise Shayo akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya New Africa  wakati wa uazinduzi wa Tuker Project Fame 6 uliofanyika leo jijini Dar es salaam kutoka kulia ni Aneth Kushaba Mwanamziki na mshiriki wa TPF 2010 na katikati ni  Mwanamuziki Zahir Zoro na jaji wa TPF mwaka huu .
 3Mwanamuziki Zahir Zoro na jaji wa TPF mwaka huu  akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo kulia ni Janeth Kushaba mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka 2010.

1 
Meneja Masoko wa Tusker Lager Anitha Msangi akifafanua jambo kwa  waandishi wa habari kwenye hoteli ya New Africa leo wakati wa uazinduzi wa Tuker Project Fame 6 uliofanyika leo jijini Dar es salaam kutoka kulia ni Aneth Kushaba Mwanamziki na mshiriki wa TPF 2010, Mwanamuziki Zahir Zoro na Meneja wa bia ya Tusker Lager Sia Shayo.
**********
Kwa miaka 7 sasa TUSKER PROJECT FAME imeendelea kuwapagawisha mashabiki wake Afrika Mashariki huku ikiwa na washiriki wengi kutoka Tanzania ambao hufanya vizuri mashindano hayo. TUSKER PROJECT FAME imerudi tena kwa kishindo na mwaka huu ikiwa ni msimu wa 6 wenye muonekano wa kipekee kwani mashindano haya yameboreshwa na kupanua wigo wake ambapo washindi katika usaili wataweza kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa la Tusker project  fame  nchini Kenya, na mshindi wa mwaka huu atapata kitita cha shilingi milioni 100.000.000 na kuingia mkataba mnono  wa kurekodi kwa shilingi 200.000.000.

Akiongea na wana habari, Meneja wa bia ya Tusker Lager Sialouise Shayo  amesema “Tunawakaribisha watanzania wote ambao wanaamini wanakipaji na wanaweza kudhihirisha kuwa kweli wao ni nyota katika muziki. Ili waweze kujipatia nafasi ya kushiriki watanzania wanaweza kuudhuria usaili utakaofanyika tarehe 7 na tarehe 8 Septemba katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Posta  jijini Dar es salaam. Vigezo na masharti vitazingatiwa na wanachotakiwa kufanya ni kuwapagawisha majaji na kuwaonyesha kuwa kweli mshiriki anaweza kuipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano”.

Mashindano haya yatatikisa zaidi kwani Mwanamuziki mahiri Zahira Zorro atakuwa jaji katika mashindano haya.   Yeye na majaji wenzake  wataanza katika usaili. Tanzania mwaka huu itapata nafasi ya kuwakilishwa na washiriki wenye uwezo wa kujiamini kwa hali ya juu. Mashindano hayo yataoneshwa katika televisheni inayoongoza  kwa burudani Afrika Mashariki,  East Afrika Television (EATV).

“Najivunia na najiona mwenye bahati kuwa miongoni mwa majaji watakaohakikisha vipaji stahiki vinang`ara na kuiwakilisha nchi yetu. Kwangu hii ni fursa kwa kuhakikisha vipaji vipya vinaendelea kuinuliwa na nawaahidi watanzania kusimamia haki. Ninachokiomba kutoka kwa watanzania ni kujiamini na kuonesha vipaji vyao kwani ukweli ni kwamba vipaji tunavyo na tunaweza.” Alisema Zahiri Zorro.

Katika mkutano huo na wanahabari miongoni mwa washiriki wa Tusker Project Fame miaka ya nyuma alikuwepo, Aneth Kushaba. Alisisitiza suala la kujiamini kama nguzo ya mafanikio katika kuhakikisha mshiriki anarudi na ushindi.

HUDUMAYAMAWASILIANOYA VODACOM YAREJESHWA.

$
0
0
Baada ya kukosekana kwa huduma za mtandao wa Vodacom kwa takribani masaa 16, huduma hizo zimerejeshwa katika hali yake ya kawaida asubuhi  ya Jumamosi ya Agosti 17.
 
Akizungumzia tatizo lililosababisha kukosekana kwa huduma za mawasiliano kwa watumiaji wa mtandao huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (pichani juu) amesema chanzo cha kukatika kwa mawasiliano nchi nzima siku ya Ijumaa ni moto uliotokea katika mtambo mkuu wa kuendeshea mtandao (Main Switch) uliyoko Dar es Salaam.

 “Kufuatia hatua hiyo, hatukuwa tena na uwezo wa kutoa huduma kwa watu wote kuanzia siku ya Ijumaa jioni hadi Jumamosi asubuhi, hali hii iliathiri wateja wetu wote kwa ujumla kwani walishindwa kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki ambao wote ni wateja wetu, alisema Meza.


Aidha aliomba radhi kwa jamii ya Watanzania na wateja wa Mtandao wa Vodacom kwa kukosa mawasiliano katika kipindi hicho, na kusema kuwa wateja wote wa mtandao wa Vodacom watarudishiwa gharama zote kwa huduma yoyote walionunua na kuhitaji kuitumia wakati ambapo mtandao  haukuwa unapatikana, “Fidia hizi kwa wateja wetu wote zitatolewa siku ya jumatatu ya Agosti 19, 2013 alisema Meza.

 “Tunaishi katika dunia ambayo mawasiliano ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku hivyo tunaelewa kuwa tatizo hili limekuwa kikwazo kikubwa kwa wateja wetu, Na tunawashukuru kwa kuwa waelewa na wavumilivu katika kipindi chote ambacho tumekuwa tukikabiliana na tatizo hili, alisema Meza.

Meza alihitimisha kwa kuhakakikishia Watanzania na wateja wa Vodacom kwa ujumla kuwa Vodacom imedhamiria kuendelea kutoa huduma zenye viwango vya hali ya juu nchini.

 “Ninapenda kuwashukuru wafanyakazi wetu wote na washirika wetu ambao kwa pamoja wamefanya kazi bila kuchoka katika kuhakikisha huduma zote zinarejea hadi katika hali ya kawaida hadi kufikia Jumamosi asubuhi, Jitihada zao na kazi kubwa waliyoifanya imewezesha huduma zote kurejea katika hali ya kawaida, alihitimisha Meza.

AIRTEL YAKABIDHI FUNGUO YA NYUMBA YA KWANZA IRINGA

$
0
0
Meneja  wa Airtel mikoa ya  kusini Beda Kinunda (kulia) akimkabidhi funguo ya nyumba mshindi wa  nyumba ya kwanza  ya Airtel Yatosha mkazi wa Frelimo mjini Iringa, Sylivanus Wanga  wanaoshuhudia  wakati wa makabidhiano hayo jana mjini Iringa ni mke wa mshindi, Veronica  Wanga na Meneja  uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando . 
MSHINDI wa nyumba ya kwanza ya Airtel Yatosha, yenye thamani ya Sh milioni 65, amekabidhiwa rasmi funguo yake mwishoni mwa wiki hii.

Nyumba hiyo imekabidhiwa kwa mshindi huyo, Silvanus Juma,  na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel,  baada ya kuibuka mshindi kupitia promosheni maalumu ya Airtel yatosha, shinda nyumba tatu.


Alikabidhiwa funguo zake mkoani Iringa pamoja na cheti kinachoonesha kwamba yeye ni mshindi wa kwanza wa nyumba katika nyumba tatu zinazoshindaniwa kupitia promosheni hiyo.


Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando, akizungumza katika makabidhiano hayo, alisema; “makabidhiano ya funguo hizi ni ya awali, lakini Alhamisi ya wiki hii  Juma atakabidhiwa rasmi nyumba yake iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.”

Alisema Airtel inayo furaha kumkabidhi mshindi wao huyo zawadi hiyo, na itaendelea kutoa zawadi zilizo bora kwa wateja wake nchi nzima, kupitia promosheni mbalimbali zinazoendeshwa na kampuni hiyo.

“Kama alivyo na furaha mshindi wetu, ndivyo na sisi tunavyofurahi na hii sio kikomo, bado kuna zawadi mbalimbali kwa wateja wa Airtel nchi nzima na cha muhimu ni wao kujiunga na vifurushi mbalimbali vinavyopatikana kwenye promosheni hii  ya Airtel Yatosha Shinda Nyumba Tatu ili kushinda,” alisema Mmbando.

Mmbando alisema ili mteja wa Airtel ajiunge na vifurushi hivyo, anapaswa kupiga *149*99# na kuchagua 1 au 2, kisha ajiunge na kifurushi chochote cha wiki, siku au mwenzi.

Mpaka sasa  Airtel imeshatoa zawadi mbalimbali kwa wateja wake nchi nzima, ikiwemo Sh milioni 37 kwa washindi 37 na inaendelea na promosheni hiyo ya siku 90. Sambamba na hilo nyumba mbili kati ya tatu zilizopo Kigamboni, bado zinashindaniwa kupitia promosheni hiyo.

Akielezea furaha yake, Juma alisema zawadi hiyo ya nyumba ni bahati ya kipekee ambayo hakuitarajia hapo awali, na hata alipopigiwa simu hakuamini kwa sababu alijua kitu kama hicho hakiwezekani, na hawezi kupata nyumba katika msimu kama huo.

“Nilipopigiwa kwanza nilijua ni utani, pengine mtu amejisikia tu kunitania lakini nilipigiwa tena na hapo ndipo nilipoanza kuamini.

Nawashukuru sana Airtel kwa zawadi hii na ni kielelezo cha wazi kuwa Airtel ni mtandao unaojali na kuthamini wateja wake,” alisema Juma.

Juma alipatikana baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kwanza katika Makao Makuu ya Airtel Dar es Salaam, mwisho wa mwenzi wa saba mwaka huu.
 Viongozi wa Airtel wakiongea na familia ya mshindi hyo nyumbani kwake Frelimo Iringa.



USAILI WA KUTAFUTA MODELS WATAKAOSHIRIKI KWENYE ALLY REHMTULLAH 2014 COLLECTION FASHION SHOW WAFANYIKA JIJINI DAR.

$
0
0
DSC_0049DSC_0037
Meza kuu ya Majaji walioshiriki katika Usaili ya kutafuta Models watakaoshiriki kwenye Ally Rehmtullah 2014 Collection Fashion show kutoka kushoto ni Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja, Ally Hassan, Mrembo na mwigizaji maarufu nchini Wema Sepetu, Mwandaaji wa Onyesho hilo ambaye pia ni Mbunifu wa Mavazi nchini Ally Rehmtullah, Mwanamitindo Jamillah Nyangasa, Sarah Raqey.
 
Mwanamitindo maarufu hapa nchini Ally Rehmtullah amefanya maandalizi ya awali ya fashion show yake itayofanyika 30th August mwaka huu katika Hoteli ya Serena ambapo zaidi ya wanamitindo 30 wasichana na wavulana watashiriki katika maonyesho hayo kabambe.
 
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi kwenye mahojiano maalum Rehmtullah amesema kwenye onyesho la mwaka huu wasichana watashiriki 20 na wavulana 10 ambao watavaa mavazi mbalimbali yaliotengezwa na kubuniwa na Rehmtullah mwenyewe kwa kuzingatia mila na desturi za Kiafrika.
 
Katika mchujo huo majaji watano watashiriki kuchagua warembo wenye mvuto, kujiamini na wenye kuwa na muonekano mzuri kwenye jukwaa ili kuwavutia wageni waalikwa ambao watakuwa ni wabunge, mawaziri na viongozi mbalimbali.
 
Rehmtullah alilisitiza mwaka huu kwamba onyesho la mitindo ya mavazi yatafana baada ya kudhamini wa makampuni kadhaa makubwa hapa nchini.
DSC_0050 
Pichani juu na chini ni Models wa kike wakipita mbele ya majaji wakati wa Audition ya kutafuta washiriki watakaonyesha mavazi kwenye Onyesho la Mavazi la Ally Rehmtullah 2014 Collection.
DSC_0053
DSC_0082
Pichani juu na chini ni Models wa kiume wakipita mbele ya majaji kwa ajili ya kuchaguliwa kushiriki kwenye Ally Rehmtullah 2014 Collection Fashion Show.
DSC_0080
DSC_0069
DSC_0071

WARSHA YA WIKI MOJA KWA REDIO ZA JAMII NCHINI KATIKA KUTEKEKELEZA MRADI WA DEMOKRASIA NA AMANI WA UNESCO UNAOFADHILIWA NA UNDP YAMALIZIKA WILAYANI SENGEREMA.

$
0
0
IMG_2735
Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph Al-Amin asikiliza maoni wakati akiendesha mjadala wa namna ya ku-brand mradi wa Demokrasi na Amani (DEP) kuelekea uchaguzi 2015 kwa Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii 25 nchini zilizohudhuria siku ya kufunga warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na shirika la UNESCO na kufadhiliwa na UNDP.
IMG_2789
Meneja wa mradi wa Amani na Demokrasi (DEP ) kutoka UNESCO Courtney Ivins akizungumza na Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii kupata tathmini ya warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa Juma wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
IMG_2743
Washiriki wakijadiliana katika makundi mambo mbalimbali ya kuboresha kwenye redio jamii zao katika utekelezaji wa mradi wa DEP kuelekea uchaguzi 2015 wakati wa kuhitimisha warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa Juma.
IMG_2741
IMG_2739
Mkufunzi na Mshauri wa redio za jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo kwa Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph Al-Amin wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja wa redio za jamii katika kuziandaa kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
IMG_2763
Msafiri Andrew kutoka Mpanda FM akiwasilisha maoni ya kikundi chake nini kifanyike katika utekelezaji wa mradi wa Demokrasia na Amani kwa redio za jamii kuelekea uchaguzi 2015.
IMG_2718
Meneja wa Triple A FM Borry Mbaraka akichangia maoni wakati wa kufunga warsha ya wiki moja kwa Wakurugenzi na Mameneja wa Redio za jamii nchini iliyomalizika mwishoni mwa wiki wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
IMG_2798
Meneja Mawasiliano wa Pangani FM Abdullah Mfuruki akichukua matukio mbalimbali ya kumbukumbu wakati wa kuhitimisha warsha warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO na kufadhiliwa na UNDP iliyowakutanisha Mameneja na Wakurugenzi wa radio za jamii 25 nchini kwa ajili ya kuwaandaa kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
IMG_2714
Sehemu ya washiriki ambao ni Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha hiyo ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa Juma kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre wilayani Sengerema mkoani Mwanza iliyoandaliwa na shirika la UNESCO na kufadhiliwa na UNDP.
IMG_2813
Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre SengeremaFM mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye akitamka kufunga rasmi warsha ya wiki moja kwa redio za jamii katika kutekeleza mradi wa Demokrasia na Amani kuelekea uchaguzi 2015.
IMG_2823
Mshauri wa Redio za Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu akigana na Meneja wa Mradi wa DEP kutoka UNESCO Courtney Ivins mara baada ya kuhitimisha warsha ya wiki moja iliyokuwa ikifanyika kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza mwishoni Juma.
IMG_2825
Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii nchini kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji mara baada ya kumalizika kwa warsha ya wiki moja kwa ajili ya kuwaanda redio za jamii kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasi kuelekea uchaguzi 2015 iliyoandaliwa na shirika la UNESCO na kufadhiliwa na UNDP.

Mpango wa Taifa wa Damu salama wavuka lengo

$
0
0
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Bw. Rajab Mwenda akizungumza na waandishi wa habari jana kutoa takwimu za makusanyo ya damu kwa mwezi Aprili mpaka Juni mwaka huu ambapo ulivuka malengo kwa asilimia 111 kutoka chupa 36,278 mpaka 38,948. Kulia ni Ofisa Msaidizi wa Masoko na Uhusiano Bi. Rayah Hamad.
****************
MPANGO wa Taifa wa Damu Salama umevuka lengo la makusanyo ya damu katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu kwa kukusanya chupa za damu 38,948 ambazo ni asilimia 111 ikilinganishwa na chupa 36,278 zilizokusanywa kutoka Januari hadi Machi mwaka huu.

Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Damu Salama, Bw. Rajab Mwenda akizungumza jana Dar es Salaam alisema kanda inayongoza kwa uchangiaji ni Mashariki na Kanda ya Ziwa.

Alisema mafanikio hayo yametokana na uanzishajiwa mpango wa damu salama wa  kampeni ya kuhamasisha uchangiaji damu kwa hiari  katika jamii na kushirikisha wadau.

 Bw. Mwenda alisema maadhimisho ya siku ya wachangia Damu duniani ambapo lengo la kukusanya chupa za Damu 8,500 kutoka kanda sita za mpango wa Taifa wa damu salama liliwekwa na mpango ulifanikiwa kukusanya jumla ya chupa 8,683

Alisema Mpango wa Damu salama kushirikiana na wadau mbalimbali kama asasi za kiraia  nayo imeongeza makusanyo ya damu toka vituo vidogo vya kuchangia damu Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,  Morogoro na Dodoma kutoka chupa za damu 2,560 mpaka chupa 3,151 kufikia Aprili hadi Juni mwaka huu.

 Aliwaomba wadau kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari kwa kutumia vyombo vya habari, mitandao ya jamii na vipeperushi.

Bw. Mwenda alisema ushirikiano ni mdogo kati ya wahamasishaji wa Mpango  wa damu salama na viongozi wa Taasisi mbalimbali, matumizi mabaya ya damu kidogo inayopatikana katika hospitali zetu na miundo mbinu hafifu hususan barabara mbovu wakati wa ukusanyaji  na usambazaji wa damu.

Alisema changamoto nyingine ni uuzwaji wa chupa za damu kunakofanywa na baadhi ya watumishi wa hospital ambao si waaminifu hivyo kukatisha tamaa wachangia damu kwa hiari.

Bw. Mwenda alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilianzisha Mpango wa Taifa wa Damu Salama mwaka 2005 ili kuhakikisha uwepo wa damu salama na ya kutosha kwa wote wanaohitaji.

Alisema shughuli za mpango ni pamoja na uhamasishaji jamii kuhusu uchangiaji damu wa hiari, ukusanyaji upimaji na usambazaji wa damu salama mahospitalini.

 “Mpango wa Taifa wa Damu salama unafanya kazi kwa kushirikianana kitengo cha kuzuia magonjwa (CDC)  na wadau wengine wa Chama cha Msalaba Mwekundu na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)” alisema Bw. Mwenda.

Alisema Mpango wa Taifa wa Damu salama uliweka lengo la kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) katika damu iliyokusanywa asilimia 1.1 kwa kipindi Aprili- Juni ikilinganishwa na asilimia 1.2 kipindi cha Januari hadi Machi baada ya kujikita katika suala la uhamasishaji na kutoa damu toka kwa jamii ambayo ni salama, kuboresha dodoso la wachangiam damu na kuendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu na wachangiaji kujiepusha na tabia hatarishi ili wawe wachangiaji wa kujirudia.

BONDIA IDDY MNYEKE AMTWANGA MWALIMU ALONI KWA POINTI

$
0
0
Bondia Sadick Momba kushoto akipambana na Amos Mwamakula wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa taifa momba alishinda K,O raundi ya kumi.
Mabondia Mwalimu Alon kushoto na Iddy Mnyeke wakioneshana uwezo wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao wa kirafiki uliofanyika manzese mwishoni mwa wiki iliyopita

Bondia Iddy Mnyeke kushoto akimshambulia Mwalimu Alon wakati wa mpambano wao uliofanyika Manzese Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita MNyeke alishinda kwa pointi
Bondia Lucas Mkenya kushoto akipambana na Adamu Yahaya wakati wa mpambanbo wao wa upingwa wa Taifa uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita 
Lucas Mkenya akivalishwa mkana baada ya kumdunda mwenzi
Bondia Sadick Momba kulia akipambana na Amos Mwamakula wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa taifa momba alishinda K,O raundi ya kumi Picha na  BLOG YA SUPER D

FORTUNATA MASHINJI AHEHEREKEA SIKU YA KUZALIWA NA WAFANYAKAZI WENZAKE.

$
0
0
Fortunata akimlisha keki rafiki yake Scola
 Keki ya Fortunata ambayo ilikuwa maalumu kwenye siku yake ya kuzaliwa ambayo alikula pamoja na wafanyakazi wenzake wa LAPF ,Dodoma.
 Wakati wa kugonga glasi kama ishara ya kumpongeza Fortunata kwa kuongeza umri zaidi katika sherehe ndogo iliyofanyika kwennye Pub maarufu ya Ngonyani , Dodoma.
Fortunata akimimina champaigne kwa wafanyakazi wenzake wa LAPF waliojumuika nae siku ya kuzaliwa kwake iliyofanyika hivi karibuni,Dodoma.

TAMASHA LA KILI MUSIC AWARD WINNERS TOUR MWANZA

$
0
0

Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Fleva),Nassib Abdul a.k.a Diamond akiwajibika jukwaani sambamba na madansa wake wakati wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza na mikoa ya Jirani waliokataa kupitwa na Onyesho hilo kabambe.
Diamond akiwa amenyanyuliwa juu na madansa wake wakati wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza

Mkali wa Ryms afahamikae kama Joseph Haule au ukipenda waweza muita Profesa Jay wa Mitulinga akiwapagawisha vilivyo wakazi wa Jiji la Mwanza waliofurika kwa wingi ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba kwenye Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza.


Wanamuziki wakongwe katika medani ya muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee na Joseph Haule au ukipenda waweza muita Profesa Jay wakiburudisha maelfu ya mashabiki wa muziki waliofurika katika Uiwanja wa Ushirika mjini Moshi mwishoni mwa wiki katika muendelezo wa Maonyesho ya Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.
Mwanadada nguli katika tasnia ya Muziki hapa nchini,Muite Bint Komando au Lady Jaydee akifanya vitu vyake ndani ya jukwaa moja la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Wakongwe katika medani ya muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee na Joseph Haule a.k.a Profesa Jay wakionyesha uhodari wao kwa kulishambulia jukwaa mbele ya maelfu ya mashabiki wa muziki waliofurika kwa wingi katika Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Mwanamuziki bora wa Hip Hop hapa nchini kwa mwaka 2013, Kala Jeremiah akiwarusha mashabiki wake waliofurika kwa wingi katika Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Kala Jeremiah akiendelea kufanya vitu vyake jukwaani.
Msanii Bob Junior akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa muendelezo wa awamu ya pili ya Onyesho la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Bob Junior na madansa wake. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

VIONGOZI DECI JELA MIAKA 3 AU FAINI MILIONI 21 KILA MMOJA

$
0
0
SHERIA imewatia hatiani viongozi 4 kati ya 5 wa kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) iliyokuwa ikijihusisha na shughuli za kuvuna na kupanda fedha nchini kinyume cha sheria.

Hayo yalibainika hii leo wakati wa hukumu ya kesi hiyo iliyodumu kwa miaka kadhaa huku mtuhumiwa mmoja katika kesi hiyo akiachiw huru baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa yake.

Akisoma hukumu hiyo iliyo andikwa na Hakimu Mwenzake, Stuart Sanga, Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Aloyce Katemana alitafsiri sheria kadhaa zilizowatia hatiani watuhumiwa hao.


Vigogo hao waliotiwa hatiani ni pamoja na Jackson Sifael Mtares, Dominick Kigendi, Timotheo Saigaran ole Loitginye, Samwel Sifael Mtares,Samwel Mtalis huku sheria ikimwachia huru Arbogast Francis Kipilimba baada ya kushindwa kumtia hatiani.

Miongoni mwa makosa yaliyokuwa yakiwakabili ni kuendesha na kusimamia mradi wa upatu kinyume na kifungu 111A(1,3) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 na Mahakama iliwatia hatiani kwa maosa mawili ambayo yote mawili yaliwatia hatiani na adhabu ya kifungo cha miaka 3 kila mmoja au faini ya milioni 3 na milioni 18 (21 Milioni). 

Kati yao washitakiwa wawili walifanikiwa kulipa faini ya Milioni 21 kila mmoja huku wengine wawili wakienda jela. 

Washtakiwa hao walipatikana na kesi ya kujibu Julai 16 mwaka jana , hivyo kutakiwa kujitetea baada ya mashahidi 16 wa Jamhuri kutoa ushahidi wao.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya mwaka 2007 na Machi 2009 katika Makao Makuu ya DECI, Mabibo, Dar es Salaam walikusanya fedha kutoka kwa wananchi wakiwaahidi kuwa watapata faida ya riba kubwa (kupanda na kuvuna).
Viewing all 10583 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>