Quantcast
Channel: Father Kidevu
Viewing all 10583 articles
Browse latest View live

PONDA AFIKISHWA MAHAKAMANI MOROGORO HII LEO ASOMEWA MASHITAKA 3.

$
0
0


Sheikh Issa Ponda Akiwa mahakamani mkoani Morogoro asubuhi ya leo Sheikh Ponda Amesomewa Mashtaka Matatu katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro Likiwemo la uchochezi alilolitoa Kwenye  Mkutano wa Hadhara Tarehe 10 mwezi huu Ambapo Inadaiwa alisema kwamba ''Ndugu waislamu Msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za Misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa Serikali ''katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege Mkoani Morogoro.Baada ya kusomewa Mashitaka hayo Mahakama imesema Upelelezi Umekamilikaa Dhamana Imefungwa  na Amerudishwa Rumande Mpaka tarehe 28 mwezi huu ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro.
Sheikh Issa Ponda Akiondoka mahakamani mara baada ya kusomewa mashtaka matatu na kesi yake imehairishwa Hadi  tarehe 28.08.2013.
Ulinzi Ukiwa umeimarishwa mahakamani leo.Picha Na MATUKIO NA MICHAPO BLOG

MAMA SALMA KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA KIMATAIFA

$
0
0
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi Tuzo ya Ben TV Diplomatic Awards-2012  Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ofisini kwake tarehe 19.8.2013. Tuzo hiyo ilitolewa kwa Mama Salma baada ya kuibuka mshindi miongoni mwa mataifa ya bara la Afrika, Caribean, Asia na Pacific kutokana na kazi za kuendeleza rasilimai watu hapa Tanzania.
************
Na Anna Nkinda – Maelezo
19/8/2013 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametunukiwa tuzo ya kimataifa  ya jitihada za kuendeleza rasilimali watu katika taifa kwa mwaka 2012 na Taasisi ya Bright Entertainment Network (BEN) ya nchini Uingereza.
 
Tuzo hizo pamoja na cheti amekabidhiwa leo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) zilizopo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
Waziri Dk. Mukangara alikabidhiwa tuzo hiyo na Taasisi ya BEN mwezi wa sita mwaka huu alipokuwa nchini Uingereza kwa shughuli za kikazi ili aifikishe kwa  Mama Kikwete.
 
Dk. Mukangara  alisema kuwa tuzo hiyo ambayo inafahamika kwa jina la “Country Human Development – 2012 Award” inatolewa kwa mshindi anayeteuliwa na Taasisi ya BEN ikiwa ni miongoni mwa waliowania kutoka nchi za Bara la Afrika , Carribbia, Asia na Pasifiki.
 
“Ushindi huu wa kimataifa Mama Kikwete umeupata kutokana na juhudi na harakati zako za kuwainua kimaendeleo wananchi wa matabaka mbalimbali hapa nchini hasa wasichana na kina mama kupitia Taasisi uliyoiasisi na kuendelea kuiendesha ya WAMA.
 
Sote tunakubalina kutokana na kazi tunazozishuhudia ambazo Taasisi yako chini ya uongozi wako inazifanya, hakika umestahili kutunukiwa tuzo hii ya jitihada za kuendeleza rasilimali  watu katika taifa hongera sana”, alisema Waziri Dk. Mukangara.
 
Kwa upande wake Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa WAMA alimshukuru waziri Dk. Mukangara kwa kuchukua dhamana ya kupokea tuzo hiyo na kuifikisha kwake pia aliishukuru Taasisi ya BEN kwa kuona umuhimu wa kazi anazozifanya na kumchagua kuwa mmoja wa washindi wa tuzo hiyo kwa mwaka 2012 kwani watu walioshiriki ni wengi kutoka ndani na n je ya bara la Afrika.
 
“Ninashukuru sana kwa tuzo hii niliyoipata ambayo inazidi kunipa moyo na ninaahidi nitaendelea kufanya kazi kwa kujituma kadri Mwenyezi Mungu atakavyoniwezesha na sintarudi nyuma kuwasaidia watanzania eti kwa kuwa nimepata tuzo kwani  sikutegemea kuwa ipo siku nitapata tuzo kutokana na kazi ninazozifanya za kuisaidia jamii”.
 
Hii tuzo ni kwa ajili ya  watanzania wote na wafanyakazi wa taasisi ya WAMA kwani bila ya watanzania nisingeweza kupata tuzo kama hii”, alisema Mama Kikwete.  
 
Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema taasisi zote za maendeleo zitaendelea kufanya kazi kwa bidii ili ziweze kutimiza malengo ya Maendeleo ya Milinia kwa wakati uliokusudiwa.
 
Kazi zinazofanywa na Taasisi ya WAMA zilizopelekea Mwenyekiti wa Taasisi hiyo kupewa tuzo ni uraghibishi wa kuboresha hali ya maisha kwa watoto, wasichana na wanawake hasa kwa upande wa afya, elimu na uchumi na kuwasaidia mitaji kinamama wajasiriamali.
 
Zingine ni kupambana na mimba za utotoni hasa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari  na kuendesha  mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa kina mama, hususani kupunguza maambukiziya Virusi vya Ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

MSTAHIKI MEYA WA ILALA MH. SILAA ATOA SOMO KWA VIJANA JINSI WANAVYOWEZA KUISHI NDOTO ZAO.

$
0
0
20130818_161729_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chimbo School of Thought ambaye pia ni mtangazaji wa redio Clouds na TV Harris Kapiga wakati alipofika kwenye chimbo hilo kuzungumza na vijana baada ya kuitikia mwaliko kutoka kwa Mwenyekiti huyo.
20130818_162938_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mwenyekiti wa Chimbo School of Thought ambaye pia ni mtangazaji wa redio Clouds na TV Harris Kapiga.
20130818_164446_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akitema cheche kwa vijana na kuwatia moyo.
20130818_175056_resized
Mmoja wa vijana akimuuliza maswali Mstahiki Meya Jerry Silaa.
 
Na.Mwandishi wetu.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akiwa katika ya nchi ya Ahadi Sinza Kamanyola amefunguka kuhusiana na namna gani kijana anaweza kuishi ndoto zake.
 
Moja ya mambo aliyoyazungumzia ni pamoja na kijana kujitambua na kujua nini hasa anataka na anapata vipi kwa maandalizi ya kutimiza nia yake.
 
Mh. Jerry pia amechambua mada hiyo kwa marefu na vijana kuonekana kumuelewa ipasavyo na hivyo kubaki kazi kwao kutekeleza na kuyafanyia kazi yale aliyoyazungumza, ikiwemo kujua lengo lao hasa ni nini na kujipima wanautayari wa kiasi gani katika kutekeleza hilo lengo na kubwa zaidi ni uthubutu wa kufanya jambo lenyewe.
 
Katika mazungumzo yake kilichowavutia vijana wengi zaidi ni pale alipowaeleza kuwa yeye Mstahiki alithubutu kugombea udiwani ndani ya kata ya Ukonga akiwa na umri wa miaka 23 na kufanikiwa kushinda.
 
Ni jambo la kujivujia kuwa na vijana hasa kama mstahiki Jerry Silaa ambaye pamoja na kuwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya Chama tawala cha CCM Taifa.
 
Pamoja na hayo Mh. Jerry Silaa amewaeleza vijana kutambua hizo ndoto ni za nani hasa na ni nani wakuzifanikisha kama si wenyewe.
 
Aidha, zaidi ya hapo amewaasa vijana kuwa na majibu ama matokeo ya kila wanalofanyia kazi "being result oriented" na kupata kile wanachokitaka kwa kuzingatia lengo pamoja na muda kiutendaji.
20130818_183833_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa katika picha ya pamoja na vijana waliojitokeza kumsikiliza wakati akifunguka kuhusuiana na namna gani kijana anaweza kuishi ndoto yake.

SERIKALI KUANZISHA MKAKATI KABAMBE WA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Serikali  imeanzisha mkakati  wa  kutokomeza wimbi la tatizo la dawa za kulevya nchini kwa kudhibiti viwanja vya ndege na  sehemu mbalimbali za mipakani  zinazotuhumiwa kupitisha dawa za kulevya.
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene (pichani juu)  leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo.
“Kwa yeyote aliyekuwa anafikiria kufanya biashara ya dawa za kulevya ajue muda wake umekwisha” alisema Mwambene.
Mwambene alisema kuwa tatizo hili litakuwa historia  kwani ulinzi umeimarishwa, hivyo ametoa rai kwa mtu yeyote mwenye  nia ya kufanya biashara hiyo aache mara moja.
Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa Serikali imeweka jitihada kubwa ya kutoa elimu kwa watumiaji na waathirika wa dawa za kuelevya ili waweze kubadili tabia zao za kutumia dawa hizo na kuwa watu wema katika jamii.
Aidha Mkurugenzi Mwambene amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa “twitter” kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana.
“Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete”, ameongeza Mwambene.
Assah Mwambene amefafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha Umma na si kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote. Ameripoti Eleuteri Mangi – MAELEZO.

RAIS ATUNUKU HATI IDHINI KWA VYUO NANE NCHINI.

$
0
0




Na Immaculate  Makilika- Maelezo.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ametunuku hati Idhini kwa vyuo vikuu na vyuo vishiriki 8 baada ya vyuo hivyo kutimiza taratibu zote za uanzishwaji wake hapa nchini.

Vyuo vilivyotunukiwa hati  baada ya kutimiza taratibu zote ni Chuo Kikuu cha Tumaini(TUMA),Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT),Chuo  Kikuu Kishiriki  cha Ruaha(RUCo),Chuo Kikuu  cha Mount Meru(MMU),pamoja na Chuo Kikuu cha Arusha(UoA).

Vyuo vingine vilivyotunukiwa hati hiyo ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini Dar es salaam(TUDARCo) ,Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi  na Teknolojia Arusha (NM-AIST) na Chuo Kikuu cha Sayansi  na Teknolojia Mbeya(MUST).

Rais  Kikwete  alivitunuku  vyuo hivyo kwenye hafla fupi iliyofanyika  leo Ikulu jijini  Dar es Salaam , ambapo  alisema  vimepiga hatua kubwa ya  kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiandikisha hadi kufikia  laki moja sitini na sita elfu mwaka 2013 ,ukilinganisha na idadi ya wanafunzi elfu arobaini ya mwaka 2005.

 “Idadi kubwa ya wanafunzi pekee haitoshi,ubora wa elimu uzingatiwe . Ikiwemo kupata wakufunzi wengi na wenye sifa  ni lazima sisi wenyewe tuwekeze ndani ili kupata wakufunzi wakutosha katika vyuo vyetu ,” alisema Rais Kikwete.

Aidha Rais  Kikwete  alivitaka vyuo hivyo kutekeleza  mkakati wa elimu wa  Matokeo  Makubwa Sasa (Big results now)  ipasavyo  ili kuboresha elimu nchini kwa kuimarisha miundombinu  ya  vyuo vikuu nchini.

Aliongeza kuwa  lazima viwe na mahitaji yote muhimu kwa kutoa elimu bora ikiwemo vifaa vya kutosha,maabara,vyuo vya zamani viwekwe kwenye viwango  ili kukidhi utoaji wa elimu bora, na kusisitiza vyuo vikuu vyetu vishirikiane na vyuo vikuu vya nje na kuvishauri   vitafute vyanzo vingine vya mapato ili  kukidhi uendeshaji badala ya kutegemea ada.

 Utoaji wa hati Idhini kwa vyuo vikuu  ni zoezi endelevu linalolenga  kuboresha  kiwango cha utoaji elimu  ya juu nchini  ili kuwezesha wahitimu  kukabiliana na changamoto  za maendeleo  ya taifa letu kwa ujumla. Kwa mara ya mwisho zoezi hili lilifanyika  tarehe 18 Agosti,2010 ambapo jumla ya vyuo vikuu na vyuo vishiriki  13 vilitunukiwa hati Idhini.

24 WAITWA TAIFA STARS KUIVAA GAMBIA, TFF 'YAMREJESHA' KASEJA SIMBA

$
0
0
LICHA ya kuwa mlinda mlango wa namba moja wa Tanzania na nahodha wa timu ya Taifa, Taifa Stars Juma Kaseja kuwa ni mchezaji huru kwa sasa na bado hajapata timu ya ndani au ya nje ya nchi kulisakata Kabumbu baada ya kutem,wa katika usajili wa mwaka huu wa timu hiyo, TFF bado inamtambua kuwa kua ni mchezaji wa timu ya Simba.
 
Hilo lina kuja baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu  Tanzania (TFF) kutoa orodha ya majina ya wachezaji 24 walioitwa kujiandaa na maandalizi ya kukabiliana na Gambia katika mchuo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia.
 
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameita kambini wachezaji 24 kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini humo.
 

Wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 29 mwaka huu kabla ya saa 1 kamili usiku. Kambi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa kwenye hoteli ya Accommondia jijini Dar es Salaam.
 
Makipa walioitwa katika timu hiyo Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar) na David Luhende (Yanga).
 
Viungo Khamis Mcha (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Amir Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga), John Boko (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo) na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).
 
RAMBIRAMBI MSIBA WA BARAKA KITENGE
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Yanga na Taifa Stars, Baraka Kitenge (74) kilichotokea leo mchana (Agosti 20 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
 
Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Kitenge akiwa mchezaji, alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
 
Kitenge amefia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alikuwa amelazwa akisumbuliwa na kansa ya uti wa mgongo. Enzi zake katika Yanga na Taifa Stas alicheza na wachezaji kama akina Athuman Kilambo na Abdulrahman Juma.
 
TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kitenge, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Yanga na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
 
Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu, Yombo Vituka (Jet) jijini Dar es Salaam. Mungu aiweke roho ya marehemu Kitenge mahali pema peponi. Amina

OPERESHENI YA KUONDOA WAHAMIJAI HARAMU KUANZA GHAFLA

$
0
0
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
SERIKALI imesema kwamba operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu katika Kanda ya Ziwa itaanza kwa ghafla, huku  ikiendelea kusisitiza kwamba  watu wanoaishi nchini bila taratibu za kisheria kuondoka kwa hiari na mali zao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (pichani juu) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wahamiaji haramu waliorejea kwao baada ya agizo la Rais Jakaya Kiwete   alilolitoa Juni 29, mwaka huu katika ziara yake ya mkoa wa Kagera.

“Nimeshapewa maelekezo  rasmi na Rais Jakaya Kikwete ya kuwaondoa wahamiaji haramu nitakapoona inafaa. Operesheni itaanza ghafla haiko mbali. Muda mwuafaka wa kutekeleza vyombo vya dola vitasema.

“Tunatoa wito waondoke wenyewe na mali zao bila kunyang’nywa. Wenye mali nyingi wanatakiwa kutoa taarifa katika vituo vya polisi ili waweze kusindikizwa. Hatutawavumilia wahamiaji haramu,” alisema Waziri Nchimbi.

 Aliongeza kuwa wahamiaji hao  wanaotaka kuishi nchini wanatakiwa kurudi nchini kwao kwanza na kufuata taratibu za kisheria kama ambavyo nchi nyingine zinavyofanya mtu akitaka kuishi nchi yoyote anatakiwa kufuata taratibu hizo.

Waziri alitoa onyo kwa viongozi wa vijiji wanaoshirikiana na wahamiaji hao kuwatunza na kusema jambo hilo ni makosa kisheria , hivyo watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

 Akizungumzia kuhusu takwimu za wahamiaji hao waliorejea nchini kwao mpaka sasa ni 10,672 kati ya  hao Wanyarwanda ni  6,088, Warundi 4000 na Waganda 269  ambao wametoka mkoa wa Kagera. Kwa wa mkoa wa Kigoma  ni  Warundi 142, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nane na katika mkoa wa Geita Wanyarwanda  126 na Warundi 39.

 Hata hivyo Waziri Nchimbi alisema  kuna wahamiaji  14 wamerejea nchini tena baada ya kurudi makwao na kuwataka wasilione jambo hilo kuwa ni mzaha.

 Aidha Waziri Nchimbi alisema Serikali ya Tanzania inashukuru ushirikiano unaotolewa na nchi wanazotoka wahamiaji hao kwa kuwapokea vizuri.

 Alifafanua kuwa suala la kuwarudisha wahamiaji  hao si la mara ya kwanza, lilishawahi kutokea. Huku akisisitiza kwamba tatizo linatokana na sababu mipaka yetu mikubwa na kuna watu wasio  wazalendo  ambao wanawapokea na kuwakaribisha kwa kupatiwa zawadi. Hivyo Serikali inalifanyia kazi jambo hilo.

Airtel money, Hakatwi Mtu kuingia mtaani kwa kishindo

$
0
0
Wafanyakazi wa Airtel wanategemea  kuiingiza rasmi promosheni ya Airtel money, Hakatwi mtu hapa kwenye mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kuanzia jumatano wiki hii.
wafanyakazi wa kampuni ya mitandao ya simu za mkononi Airtel wanafanya hivyo kwa dhumuni la kuelimisha na kuikaribisha rasmi promosheni ya Airtel money, Hakatwi mtu hapa kwa watanzania.
Airtel imechukua maamuzi hayo katika muendelezo wa kuhakikisha inajenga mahusiano mazuri kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na wateja wake na kuwapatia huduma bora kwa kuwatembelea maeneo walipo.
Akizungumza juu ya ziara hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema dhumuni la ziara hiyo ni kuhamasisha na kuwaelewesha wateja mbalimbali wa Airtel juu ya huduma mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na kampuni hiyo ya mitandao ya simu za mkononi hususani promosheni mpya ya Airtel money, hakatwi mtu hapa.
“Tumeamua kuingia mtaani kuwahamasisha wateja wetu juu ya huduma ya Airtel Money Yatosha kwamba inamuwezesha mteja yeyote wa Airtel kutuma na kupokea pesa bure katika Mtandao wowote hapa Tanzania,” alisema Mmbando.
Kwa mwaka huu ziara hii inakuwa ni ziara ya tatu kufanywa na kampuni hiyo ya simu za mkononi baada ya ziara nyingine mbili zilizofanywa hapo awali mwaka huu kuwa na mafanikio makubwa sana kwa kuweza kupata nafasi ya kuweza kukutana na wateja wao kwa kutoa Elimu  na kuweza kuwasaidia katika  maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

TANGAZO LA MSIBA WA VICKY KITOSI (DOTTO)

$
0
0


FAMILIA ya Mzee Augustino Mgonja wa Pugu Kajiungeni Dar es Salaam na Familia ya Marehemu Bwana na Bibi Henry Kitosi (Mwakitosi) wa Iringa zinasikitika kutangaza kifo cha Mtoto wao, VICTORIA KITOSI  (DOTTO) kilichotokea Alfajiri ya leo Agosti 22, 2013 katika Hopitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam alikolazwa baada ya kuugua ghafla.

Mipango ya Mazishi inafanyika Pugu Kajiungeni nyumbani kwa Mjomba wake Agustino Mgonja.

Habari ziwafikie, Mama Mdogo wa Marehemu, Mary Nathan wa Kinyenze Kipera Mkoani Morogoro, Kaka wa Marehemu Bosco Kitosi wa Mwanza,Doris KitosiA wa Iringa, Bibi wa Marehemu,Balozi  Christina Shogholo wa Kisiwani Same-Kilimanjaro, Mjomba John Mgonja wa Kabuku Tanga, Ukoo wote wa Mwakitosi na Shogholo, Ndugu Jamaa na Marafiki popote pale walipo.

Marehemu ameacha Mume na watoto wawili, Sanden na Sabri.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. AMEN.

WAKULIMA WA SHAYIRI BABATI WANUFAIKA NA MSAADA WA PEMBEJEO ZA TBL

$
0
0
 Mhasibu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Octaty Minja (kushoto), akioneshwa na mkurugenzi wa kampuni ya Agric Evolution inayomiliki shamba la kuzalisha shayiri katika Kijijicha Sigino, Kata ya Sigino, , wilayani Babati, Manyara, .David Bagereza  (wa pili kushoto), ubora wa shayiri ambayo amekuwa akiilima katika shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 3000.Kulia ni mwandishi wa habari,Eliya Mbonea. Maofisa wa TBL na wageni wengine wakiwemo waandishi wa habari walitembelea hivi karibuni shamba hilo la shayiri inayotumika kutengenezea bia katika viwanda vya TBL nchini.TBL imekuwa ikiwasaidia pembejeo wakulima  zao hilo.

 Mhasibu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Octaty Minja (kushoto), akioneshwa na mkurugenzi wa kampuni ya Agric Evolution inayomiliki shamba la kuzalisha shayiri katika Kijiji cha Sigino, Kata ya Sigino, , wilayani Babati, Manyara, .David Bagereza  (wa pili kushoto), ubora wa shayiri ambayo amekuwa akiilima katika shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 3000. Maofisa wa TBL na wageni wengine wakiwemo waandishi wa habari walitembelea hivi karibuni shamba hilo la shayiri inayotumika kutengenezea bia katika viwanda vya TBL nchini.TBL imekuwa ikiwasaidia pembejeo wakulima  zao hilo.
 Machine ya kuvuna shayiri ikimwaga shayiri iliyokwishavunwa hivi karibuni katika shamba lenye ekari 3000 la David Bagereza lililopo katika Kijiji cha Sigino, Kata ya Sigino, , wilayani Babati, Manyara, kabla ya kupakiwa kwenye magunia na kusafirishwa kwenda viwanda vya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)  kutengeneza bia. Kampuni ya TBL imekuwa ikiwasaidia pembejeo  wakulima zao hilo.
Wafanyakazi wa shamba la kampuni ya Agric Evolution lililoko katika Kata ya Sigino, Kijiji cha Sigino, wilayani Babati, Manyara,wakiweka shayiri iliyokwisha vunwa kwenye magunia tayari kusafirishwa kwenda kiwanda cha biacha TBL jijini Arusha hivi karibuni.

KAMATI KUU YA CCM KUKUTANA KESHO

$
0
0

Kamati Kuu ya CCM Taifa itakutana tarehe 23.8.2013 ikifuatiwa na Halmashauri Kuu keshokutwa asubuhi  ambapo itakuwa kwa siku mbili.

Ajenda Kuu ya Kamati Kuu itakuwa  kujadili maoni ya wana CCM juu ya rasimu ya Katiba, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa White House,Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema mpaka sasa CCM na wanachama wake wameshirikiana vya kutosha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Pia Kikao hicho kitajadili hali ya kisiasa na hatma ya madiwani Bukoba na Masuala Utumishi
Alisema siku ya Jumamosi asubuhi tarehe 24,kutakuwa na sherehe fupi za kuzindua Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM kabla ya kikao cha halmashauri.

Baraza hilo linaundwa na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wastaafu wote wa CCM Taifa.


GURUMO ASEMA KUIMBA SASA BASI

$
0
0


Na Jennifer Chamila, Maelezo.
MWANAMUZIKI mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Mzee Muhidin Gurumo amestaafu rasimi kazi ya muziki alioifanya kwa muda wa miaka 53.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mzee  Gurumo mwenye umri wa miaka 73 amesema ameamua kustaafu kazi hiyo kwa hiari yake mwenyewe kutokana na umri wake kuwa mkubwa.

“Muziki kwangu umekuwa kama asili yangu na kazi yangu lakini nimeamua kustaafu kutokana na umri wangu na nitabaki kuwa mshauri tu kwa mwanamuziki yeyote atakayetaka ushauri wangu,”alisema  Mzee Gurumo.


Pamoja na kufanya kazi ya muziki Gurumo alisema kuwa hakupata mafanikio makubwa zaidi ya kujenga nyumba anayoishi na familia yake.

 “Mimi  nimeimba kwa muda mrefu sana lakini hata baiskeli sina,”alisema Mzee Ngurumo. Hata hivyo alisema  nashukuru kuwa ana nyumba ya kuishi na familia.

Vilevile Mzee Gurumo amewaasa vijana kuwa wabunifu na kuupenda mziki wa zamani kwani ndio chimbuko la bongofleva na kuwashauri wanamuziki wa sasa kuwa wavumilivu kukaa muda mrefu kwenye bendi moja ili hata wanapoondoka mchango wao uthaminiwe.

 Mzee   Gurumo  ambaye ana mke na watoto wanne alisema kuwa katika maisha yake ya muziki alifanikiwa kutunga nyimbo 60,000 na anavutiwa zaidi na mwanamziki Hussein Jumbe na Hassani Lehan Bichuka na kwa wanamuziki wa kizazi kipya anavutiwa na Nassibu Abdul ’Diamond’.

Mwanamuziki huyo mkongwe alianza kufahamika katika tasnia ya muziki wa dansi kwenye miaka ya 1960 ambapo mwaka 1964 alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa bendi ya ya N

Alidumu na Mlimani Park mpaka mwaka 1985 na kuhamia Safari Sound aliyofanya nayo kazi mpaka mwaka 1990 na kujiunga na Msondo Ngoma mpaka sasa anaamua kustaafu Muziki.

TWANGA PEPETA,ROMA MKATOLIKI KUPAMBA TAMASHA LA WAFANYA MAZOEZI LA VITA MALT KESHO.

$
0
0
Mkufunzi wa kimataifa wa maswa ya mazoezi ya viungo bwana SAAS akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya tamasha kubwa linalowakutanisha wafanya mazoezi kote nchini na familia zao linalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar Es Salaa ambapo watu mbalimbali watapata fursa ya kujumuika pamoja na kufanya mazoezi ya pamoja sambamba na hilo pia burudani toka kwa bendi ya Twanga pepeta na Roma Mkatoliki na baa za kisuma na Fyatanga zitakuwepo kuchoma nyama kwa kipindi chote,Katikakati ni Meneja wa Vitamalt Plus Consolata Adam na Meneja mawasiliano na mahusiano wa TBL Edith Mushi
 
************
Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuhakikisha Watanzania wanakuwa na afya bora, kinywaji kisicho na kilevi cha Vita Malt, kimeandaa bonanza maalumu litakalowashirikisha wafanya mazoezi na litakalofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Vinywaji visivyo na Vileo katika Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Consolata Adam alisema, wameamua kuandaa bonanza hilo ili kuwakutanisha pamoja wafanya mazoezi wote, ambao mara nyingi wanafanyia katika vituo maalumu (gym).

Consolata alisema, bonanza hilo la aina yake kwa Dar es Salaam litafanyika katika Viwanja vya Posta vilivyopo Kijitonyama kuanzia saa 12 asubuhi hapo kesho (Jumamosi).

“Tumeamua kuandaa bonanza linalowakutanisha wanamichezo mbalimbali hasa wafanya mazoezi ili kuweza kukutana na kufanya mazoezi kwa pamoja.

“Siku hiyo katika Viwanja vya Posta kutakuwa na gym kumi na mbili zilizo maarufu ambazo zitashiriki na kutakuwa na wakufunzi kumi ambao wataongozwa na mkufunzi wa kimataifa SAAS,” alisema, huku akidai mtu anatakiwa kwenda tu kwani mazoezi hayo yatakuwa bure.

Alisema, lengo kuu kuu la bonanza  ni kuhamasisha jamii nzima kutambua umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujenga afya bora za miili yao na pia kujenga umoja imara wa gym zilizopo nchini.

Consolata alisema, katika kuhakikisha bonanza hilo linakuwa bora na la kufana jumla ya gym kumi na mbili zitashiriki ambazo ni Better Life, Genessis ya Kijitonyama, Segerea Gym, Rio Gym,Genessis ya Kimara, Azula ya Mikocheni na Serena Gym.

Alisema pia baa zilizoshinda katika kuchoma nyama katika mashindano yaliyofanyika hivi karibuni za Fyatanga ya Tegeta na Kisuma Bar ya Temeke, zitaonyeshana umwamba kwa kuchoma nyama bomba kwa kipindi chote hicho.

“Tumeweka burudani za kila aina kwani kutakuwa na michezo mbalimbali ya kufurahisha kama soka, netiboli, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, Sehemu za watoto kuchezea pia na zawadi nyingi toka Vita Malt zitakuwepo.”

NaYe Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TBL, Edith Mushi alisema mbali na hayo kutakuwa na burudani mbalimbali toka kwa bendi African Stars ‘Twanga Pepeta’ na msanii mkali wa Hip hop, Roma Mkatoliki sambamba na burudani nyingine nyingi kwa kipindi chote cha tamasha.

“Hii ni siku ya familia napenda kuwajulisha watanzania wote na wapenda michezo kote nchini kuwa waje mapema na familia zao siku ya Jumamosi, hakutakuwa na kiingilio chochote na vinywaji vyote toka TBL vitakuwepo.

“Lakini pia watu wa kawaida na wa rika zote siku hiyo hakutakuwa na kikwazo chochote cha kufanya mazoezi, kwani ni bure kabisa, hivyo nawashauri tufike kwa pamoja ili tuweze kupata pia ushauri mbalimbali juu ya kupunguza uzito na aina ya mazoezi yanayotakiwa,” alisema.

Vita Malt ni kinyaji kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

WAREMBO WA REDD'S MISS TANZANIA 2013 WAINGIA KAMBINI HII LEO

$
0
0
Warembo 30 wa Redd's Miss Tz wakiwasili katika kambi ya Taifa ya warembi hao kwenye Hotel Ya Giraffe Ocean View jijini Dar Es Salaam ambapo warembo 30 wataanza kambi hiyo Leo,Katikati ni Mkurugenzi wa LINO Hashimu Lundenga na meneja wa Kinywahji cha Redd's Original Victoria Kimaro


Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akiwa pamoja na Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original ambao ndio wadhamini wakuu wa Shindano la Redd's Miss Tanzania,Victoria Kimaro wakiwapokea Warembo wanaoshiriki shindano hilo wakati wakiwasili kwenye Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam leo tayari kwa kuanza rasmi Kambi yao.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akizungumza machache wakati wa kuwakaribisha Warembo hao wa Redd's Miss Tanzania 2013/14 walioanza kambi yao rasmi leo kwenye Hoteli ya Giraffe,jijini Dar es Salaam.
 
Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original ambao ndio wadhamini wakuu wa Shindano la Redd's Miss Tanzania,Victoria Kimaro akizungumza machache wakati wa kuwakaribisha Warembo hao wa Redd's Miss Tanzania 2013/14 walioanza kambi yao rasmi leo kwenye Hoteli ya Giraffe,jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Warembo hao akizngumza namna walivyojipanga kwa mashindano.
Mkuu wa Itifaki kwa Kamati ya Miss Tanzania,Albert Makoye akitoa maelekezi kwa Warembo hao.

BIG BROTHER: THE CHASE IS OVER AS DILLISH TAKES HOME USD300 000

$
0
0
Namibia’s Dillish emerged victorious on Big Brother: The Chase tonight (25 August) after 91 days in the Big Brother house. She won more viewer votes than Beverley, Melvin, Elikem and Cleo in the final week, to scoop the USD300 000 prize and become the 3rd woman to win a season of Big Brother Africa.

She emerged on stage, tearful, to be greeted by her four fellow finalists and her man, Steven, who crowned her with a tiara. “Dillish, it’s official, you’re rich!” proclaimed Big Brother Africa host IK as fireworks and streamers signaled the end of 91 days of drama and intrigue.

The stunning 2-hour Finale, which was screended live on Africa Magic Entertainment and Channel 197 and 198 on DStv, kept viewers enthralled and amazed, with some of the continent’s hottest entertainers lighting up the stage as the tension built.

TANZANIA NATIONAL FAMILY PLANNING CONFERENCE

HALMASHAURI KUU YA CCM YAMALIZA KIKAO LEO

$
0
0
 Katibu wa NEC Uchumi na Fedha  Zakhia Megji akibadilishana mawazo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa  Mama Salma Kikwete katika ukumbi wa NEC, kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu Dodoma leo, 26 Agosti 2013.

 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa taarifa za misiba iliyojiri, kabla ya kikao akijaanza cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu wakiwa wamesimama kwa dakika moja kwa ajili ya kumuombea mjumbe mwenzao aliyefariki ndugu Meja Jenerali Haji Makame Rashid.

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo mjini Dodoma.



CCM YAZIDI KUWA IMARA ZAIDI
Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kimemalizika jioni ya leo huku kukiwa na mabadiliko mbali mbali makubwa kwenye chama hicho.
Kikao hicho ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wake wa Taifa Jakaya Mrisho Kikwete kimemalizika kukiwa na mabadiliko na mapendekezo mbali mbali, kikao hicho ambacho kimekaa kwa siku tatu mfululizo kikitumia siku mbili nzika kujadili Rasimu ya Katiba na maoni ya wana CCM 
Halmashauri hiyo pia imeridhia uamuzi wa kufukuzwa uanachama Mansour Yussuf Himid kwa tuhuma za Kushindwa kusimamia malengo na madhumuni ya chama na kutekeleza masharti ya uanachama, kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka maadili ya Kiongozi wa CCM,Kuikana Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010-2015 na kukisaliti chama.
Mansour alianza uanachama tarehe 7/4/1988 na ni mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki,wilaya ya Damani,Mkoa wa Magharibi Unguja.
 katika hatua nyingine ya Kimaadili sula la madiwani wa Bukoba bado halijafikiwa uamuzi ingawa Kamati Kuu itakaa tena kesho tarehe 27 Agosti 2013 kufanya maamuzi ya suala la Bukoba.
Kamati Kuu pia imependekeza  majina ya Makatibu wa Jumuiya,Ikiwemo Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi, Umoja wa Vijana  CCM  Ndugu Sixtus Mapunda, Wazazi Seif Shaaban Mohamed .
 Makatibu wapya wa Mikoa walioteuliwa ni Romuli Rojas John, Kaskazini Pemba Kassim Mabrouk Mbarak na Geita Mary Maziku.

KUTOKA VIKAO VYA CCM DODOMA: SIXTUS MAPUNDA ACHUKUA MIKOBA YA SHIGELA UVCCM, MANSOUR AULA ZANZIBAR

$
0
0
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC, leo Agosti 26, 2013 mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikaocha NEC, mjini Dodoma leo mchana. Kushoto ni Katibu Mkuuwa CCM  Abdulrahman Kinana.
 *********
BASHIR NKOROMO, Dodoma
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo imemamliza kikao chake cha siku tatu chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete ikiwa imeridhia mapendekezo kadhaa ya Kamati Kuu ya CCM, ikiwemo kumfuta uongozi Mbunge wa jimbo la Mjini Magharibi, Zanzibar,  Mansor Yusuf Himid.

Kikao hicho pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuia za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Katika uteuzi huo mapendekezo hayo yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM, na kuridhiwa na NEC, kwa upande wa Umoja wa Vijana wa CCM ameteuliwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa NEC kutoka Pemba, Seif Shabani Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa Katibu Mkuu wa sasa, Amina Makilagi.

Mapunda atachukua nafasi iliyokuwa imneshikiwa na Martine Shigela ambaye ameongoza UVCCM kwa miaka mitano sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka Pemba akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi ambaye pia amekuwa katika wadhifa kwa miaka mitano sasa.

Pia, NEC imeridhia mapendekezo  ya Kamati Kuu kwa ajili ya kuziba nafasi Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu ya Morogoro,  Kaskazini Pemba na Geita ambayo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imekuwa wazi kwa muda mrefu sasa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.

Kufuatia mapendekezo hayo ya Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha  Uchaguzi, CCM Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Romuli Rojas John (Morogoro), aliyekuwa Katibu wa wilaya ya Mkinga, Kassim Mabrouk Mbarak (Kaskazini Pemba) na aliyekuwa Katibu wa CCM Igunga, Mary Maziku (Geita).

Kuhusu sakata la madiwani wa Bukoba mjini, CCM imesema suala hilo, linaendelea kushughulikiwa ambapo baada ya kikao hicho cha NEC, Kamati kuu iliendelea kukutana na viongozi wa wilaya ya Bukoba, Mwenyekiti wa CCM na Katibu wa wilaya hiyo.

Mapema kabla ya kikao cha NEC, Kamati Kuu ilikutana na Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba mjini na kuwahoji, wakati jana Kamati Kuu ilikutana na  Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utangulizi kabla ya Mwenyekiti wa CCm Rais Jakaya Kikwete (kushoto) kufungua kikao cha NEC, Agosti 26, 2013
 Baadhi ya wajumbe wa NEC, ukumbini. Kulia mstari wa mbele ni Mjumbe wa Kamati ya Ushauri ya Viongozi wastaafu wa CCM, John Malecela ambaye ni mwalikwa kwenye kikao hicho.
 Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Zakiah Meghji kabla ya kikao cha NEC kuanza, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Mjumbe wa NEC, Dk. Fenela Mkangala na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro wakijadili jambo kabla ya kikao cha NEC kuanza leo Agosti 26, 2013, Makamo Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Wajumbe wa NEC kutoka Pemba wakiwa nje ya ukumbi kabla ya kikao kuanza. Kutoka Kushoto ni Hamadi Bakari Ali, Mwinyi Fakih Hassan, Ali Issa Ali,  Masoud Mohammed Abdallah, Seif Shaaban Mohammed na Mussa Fumu Mussa.

MISS ILALA 2013 ADHAMIRIA KUNYANYUA ELIMU NCHINI, AKABIDHI VITABU SHULE YA MSINGI TABATA JIKA

$
0
0
3
Miss Ilala 2013 Doris Mollel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Tabata Jika baada ya kukabidhi Vitabu shule hapo.
4
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Tabata Jika wakiwa katika picha ya pamoja na Miss Ilala 2013 Doris Mollel, huku wakiwa na baadhi ya vitabu vilivyokabidhiwa shuleni hapo na mrembo huyo.

1
Miss Ilala 2013 Doris Mollel akitia saini kitabu cha wageni katika shule ya msingi Tabata Jika wakati alipotembelea shuleni hapo na kukabidhi vitabu vya maandalizi ya mtihani wa Darasa la 7.
2Doris Mollel, Miss Ilala 2013 akimkabidhi baadhi ya Vitabu mkuu wa shule ya msingi Tabata Jika Bwana Kiwia. Kushoto ni katibu wa kamati ya Miss Tabata 2013 Bw. Adili.

RAIS KIKWETE WA TANZANIA AMUAPISHA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA IKULU LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Msajili wa Vyama vya Siasa mpya Jaji Francis Mutungi Ikulu jijini Dar es salaam leo. Jaji Mutungi ameapishwa baada ya kuteuliwa na Rais hivi karibuni kushika nafasi hiyo iliyo kuwa ikishikiliwa na John Tendwa kustaafu kwa mujibu wa sheria.


 Jaji Mutungi akisaini hati ya kiapo.
 Rais Jakaya KLikwete akitia saini hati ya kiapo ya Jaji Mutungi.
 Rais Kikwete akikabidhi vitendea kazi Jaji Mutungi.
 Pongezi...
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na  Msajili wa Vyama vya Siasa mpya Jaji Francis Mutungi na viongozi wa vyama vya siasa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Viewing all 10583 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>